Mzee Mwanakijiji,
Wapi mie nimekuambia Mohamed Said ndiyo wa kwanza kumtaja Sheikh Suleiman Takadir.
Nimecheka sana na maneno yako mpaka mtoto wangu kashangaa, wewe ulivyokuwa nyuma kufahamu historia ya Tanganyika unadhani wote kama wewe kwa taarifa yako vitabu vya histori ya Tanganyika nimevikuta nyumbani mzee wangu alikuanavyo ngoja nikutajie.
1. Macpherson Fergus, Kenneth Kaunda of Zambia.
2. Pratt Cranford, The Critical in Tanzania.
3. Hatch John, Two African Statesmen.
4. John Iliffe, A Modern history of Tanganyika.
5. Listowel Judith, The Making of Tanganyika.
Niambie wapi Listowel kamtaja Sheikh Takadir ndie mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Wazee wa TANU ambalo lilikuwa na wajumbe 170. Kama siyo Mohamed Said.
Wewe leo ndiyo umenunua vitabu AMAZON kuwasoma kina Listowel Judith, John Iliffe, haa haaa ha.
Vitabu vipo vingi bahati nzuri mzee wangu alikuwa anaeleza baadhi ya makosa ya vitabu vya Tanganyika.
Wewe unanichukulia poa unajidanganya ujiulizi kwa nini Ritz ameganda kwenye huu uzi muda mwingi kuna vitu najua vingi nimeadithiwa na Wazee wetu siyo kutoka kwa wazungu ambao nao wameadithiwa na wazee wetu, ambao wewe leo hii ndiyo unaanza kuwasoma na kutaka kuifahamisha mimi.
Endelea kusoma vitabu vyako.