Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said,

Naomba utupe darsa habari za hawa jamaa wawili kwenye TANU.

1. Andrew Tindegebage

2. Germano Pacha.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo umekiri alichokisema Mohamed Said kule Ibadan kuwa balozi wa Marekani ndiyo aliwahotubia wabunge wa Tanzania wakapitisha sheria ya ugaidi.

Halafu Mohamed Said anavyokuambia pinda mgongo usome siyo dhihaka kiwango chako cha elimu bado.

Mohamed Said anakufundisha mengi sana.
Mzee Mohamed Said anayo meeengi ya kumfundisha huyo kijana pamoja na wengine wengi humu jamvini na nje ya jamvi. Lakini tunakosa uhondo huo kwa kuwa "Wanafunzi" wanafanya fujo darasani, hawampi mwalimu fursa ya kufundisha. Ukiwadadisi kwa nini wanafanya fujo? Wengi wao itakuwa wanataka Darsa lifundishe wanavyotaka wao kama walivyozoea kusikia na si vinginevyo.
Na wengine wana chuki binafsi tu. akisema fulani, hata Kama ni maneno ya kijinga, ni sawa, lakini fulani akisema...hawamuamini.
Hapo ndipo kwenye kasoro ingawa hawatathubutu kusema hivyo.
 
Zali; Nakushukuru kwa majibu yako. Unayoyasema kuhusu kina Bush na Ukatoliki pia yanawezekana. Ila Bush sio Mkatoliki na Marekani sio a catholic country. Kwa CIA, nia ya kuiunganisha tanganyika na Zanzibar ilikuwa inainufaisha Marekani kuizuia Umma party (ikichukuliwa kama a communist party)isiwe na influence. Hata huyo mwandishi anapomhoji Babu anahoji jinsi gani Wakomunisti walimsadia. Hamu ya kuwakomoa wakomunisti wa zenj toka Marekani ilijitokeza pia walipopata fursa ya kumpigia Dr Salim kura ya veto asipate ukatibu mkuu wa UN, kwa kule yeye kuwa "rafiki" na China, japo bado ndio walikuwa wanawakomoa makomredi. Kwa hiyo hauko mbali na ukweli ukisema Marekani walitaka Zanzibar ithibitiwe. Kuwasilimisha Wazenj wote SIJUI. Sijalisoma.

Nachosema, ni kuwa angalia hizo silaha za hao askari wa Okello kwenye hiyo video, hizi sio bunduki za watu kuomba toka nchi nyingine kama Algeria. Na kama bunduki ni 850 kama video ya pili (hiyo ya rangi) inavyosema kuwa walipewa na Nyerere, haiwezekani Meli toka Algeria ilete bunduki 850 tena hizo nazoziona hapo.

Mi nadhani hii dhana ya kuwa kulikuwa na mapinduzi mengine yanasubiriwa (ya Afro-shiraz) na yangefanyika wiki moja kabla ya haya kina okello kama anavyo-eleza huyu mwandishi kwenye video ya kwanza huenda yakawa na ukweli. Aina hiyo ya mapinduzi ndio yangetumia silaha nzuri toka bara sio za kupora kituo cha polisi na magereza (sio hizi nazoona)na yangekuwa na kuratibiwa. Kwenye Kitabu cha Dr Ghassany sikumbuki kumsoma Okello akiwa Kipumbwi-Pangani kwenye mazoezi Iwe itakavyokuwa lakini ni dhahiri kuwa mshikamano kama jamii katika jumuiya hii ulishayumba hadi matatizo haya yanakuja.

Ni kweli kwamba suala la Marekani hasa lilikuwa ni Kuudhibiti Ukomunist. Lakini ajenda ya Bush ya Crusade dhidi ya Uaislamu inafahamika hivyo huwezi kutenganisha ajenda yake ya udini na ile ajenda mama ya kuudhibiti Ukomunist. Kama ni suala tu la kuudhibiti Ukomunist basi hata Muislamu wangeweza kumtumia kwani walishafanya hivyo sehemu nyingi tu including kumtumia Osama kule Afghanistan.

Wamarekani mpaka leo wameweka Plan B ya kuhakikisha kwamba Wazanzibari hawapati nchi yao kwa kutumia harakati zozote zile ziwe za kisiasa au vinginevyo. Dola la Urusi limeshaporomoka mda sasa. Kwa nini Plan B bado ipo na inafanya kazi mpaka leo kama sio suala la kuudhibiti Uislam?
 
Mzee Mohamed Said anayo meeengi ya kumfundisha huyo kijana pamoja na wengine wengi humu jamvini na nje ya jamvi. Lakini tunakosa uhondo huo kwa kuwa "Wanafunzi" wanafanya fujo darasani, hawampi mwalimu fursa ya kufundisha. Ukiwadadisi kwa nini wanafanya fujo? Wengi wao itakuwa wanataka Darsa lifundishe wanavyotaka wao kama walivyozoea kusikia na si vinginevyo.
Na wengine wana chuki binafsi tu. akisema fulani, hata Kama ni maneno ya kijinga, ni sawa, lakini fulani akisema...hawamuamini.
Hapo ndipo kwenye kasoro ingawa hawatathubutu kusema hivyo.

NGUVUMOJA,

Unachosema ni kweli raha ya mijadala hata kama hamtakubaliana lakini bado mnaendelea kueheshimiana.

Chochote atakachosema Mohamed Said hata kama ni cha kweli watu wanapinga kutokana imani tu.

Mohamed Said ana mambo ya kutufundisha humu jamvini tatizo ndiyo hilo.
 
Last edited by a moderator:
Wickama,
Nimekaa miaka mingi sana na Bwana Ally na katika kipindi hicho kila
nilipokuwa na nafasi nilikuwa ''nikimchokoza'' anieleze maisha yake na
mimi nikawa nachukua ''notes.''

Ana mengi kaniachia.

Shukran Mzee MS; Leo unaongelea "kakuachia mengi". Binafsi ningependelea sana mtu aandike his own story kama ile ya Museveni "Sowing the Mustard Seed" (hopefully nimeitamka sawa) au vitabu vya Obama nk. Kina POwell, Clinton. Au hata vitabu vya fani husika basi, Lakini nenda kwenye vyuo vyetu, takriban vitabu vyote wanafunzi wanavyopewa kama references huwa waandishi ni wa nje. Nimesoma SUA, kitabu kimoja cha fani kama ya Veterinary, kwa sasa usishangae kuambiwa lipa 150,000, sijui fani zingine, ilimradi tuu mlango huu upo wazi na ni mara chache kukuta ma-professa wazawa wanaandika vitabu kulijaza soko hili. Sasa tabia hii ndio unaikuta karibu maafisa wote waandamizi wanastaafu bila hata kuandika memoirs zao (labda tatizo ni soko, au publishers hawataki sijui). Ni tatizo ambalo kila anayejaribu kulivuka sharti apewe nguvu na pongezi.
 
Zali la Mentali,
Me naona hili punching bag ungelipa nafasi kidogo lisije likapasuka na haya mapigo yako,
Lipumzishe na tuendelee na mengineyo,ukiamua kuendelea kulipiga piga mie sina neno,Ahalan wasa'lani...

Ha ha ha ha ha "shit list" kama vile kuna kitu unajua....

Ni "Big Show" wala si utani
 
Last edited by a moderator:
Kadogoo,Ahsante sana.Mzee Nasib Siwa.Wanae ni umri wangu.Nikifika Moshi lazima nifike pale kwao kwenye barza.
Mohamed,Bila shaka rika lako ni Ali Nasibu, kwani nadhani ndie mkubwa ktk familia ya Mzee Nasibu, lakini Mzee Nasibu alikuwa na kaka ake akifanya kazi ofisi ya Tanu mkoani Kilimanjaro, alikuwa dereva wa miaka mingi ktk ofisi ya Tanu. Baadae Wazee wa Moshi hasa akina mama wakiongozwa na Marehemu Juma Ngoma, Mama Halima Selengia, Yusuf Ngozi na wengine walichangishana fedha nyumba hadi nyumba na kujenga ofisi kubwa na ya kisasa kwa ajili ya CCM! MS, amini usiamini ofisi hii sehemu kubwa ya fedha zimetolewa na akina Mama wa Kiswahili wauza vitumbua na mama ntilie!Baada ya kumtaja Mzee Nasibu siwa nimeamini kweli wewe mtoto wa Mjini! halafu kumbe watoto wa mjini mtandao wao si mdogo!
 
Ni kweli kwamba suala la Marekani hasa lilikuwa ni Kuudhibiti Ukomunist. Lakini ajenda ya Bush ya Crusade dhidi ya Uaislamu inafahamika hivyo huwezi kutenganisha ajenda yake ya udini na ile ajenda mama ya kuudhibiti Ukomunist. Kama ni suala tu la kuudhibiti Ukomunist basi hata Muislamu wangeweza kumtumia kwani walishafanya hivyo sehemu nyingi tu including kumtumia Osama kule Afghanistan.

Wamarekani mpaka leo wameweka Plan B ya kuhakikisha kwamba Wazanzibari hawapati nchi yao kwa kutumia harakati zozote zile ziwe za kisiasa au vinginevyo. Dola la Urusi limeshaporomoka mda sasa. Kwa nini Plan B bado ipo na inafanya kazi mpaka leo kama sio suala la kuudhibiti Uislam?

Kama utataka mawazo na msimamo wangu kama mimi, kesho wakina Waryoba wakiweka kipengele cha kupiga kura kuhusu fate ya muungano uwe na uhakika nitawatema wa-zenj. Hii sio kwa sababu ya dini hapana. Ila kama wao wanaamini ndio njia iliyobaki ya kuwaletea masikizano na maendeleo, why NOT? Mashindano ya dini kuu mbili duniani (ukiristo na uislamu) yamepitia historia nyingi na ngumu na humu sio mahala pake. Unaweza ukaanza na kufika kwa wareno na wao walikaa 200 years mwambao huu wa afrika mashariki hadi zanzibar kuokolewa na wa-oman. Haya ya Plan B unayosema ni ya zama hizi za leo. Siasa hazina adui wa kudumu. Ni maslahi. Subiri utaona, Zipo dalili kuwa huenda mwambao wa zenj ukawa na mafuta, sasa kwa kuanzia zipo kelele tele 'jamani hatutaki mafuta kuwa suala la muungano'. Yaani kama vile huku tanganyika ni marufuku kupata mafuta. Sasa subiri uone kama wakuu hao unaowasema wataongelea Plan B zenj wakipata oil au wataongelea kupata mafuta kwenye jamhuri huru ya zenj. Refer case ya Savimbi na Angola. Walim-support for so many years, lakini ilipokuwa wazi kuwa sasa wanaweza kupata mafuta ya kule Cabinda and other parts? You will know how the war ended. Mimi navyoona (hapa na mimi ni mawazo yangu pia) Marekani (of course na nchi nyingi) hata vita zao ni masuala ya resources. Ingekuwa ni dini tuu basi leo Japan baada ya kumeza yale mabomu ya atomic, au Iraq, au Vietnam wote wangekuwa Protestant-Christians.
Hao kina Bush ndio kwanza wanahusishwa sana Freemasonry, Atheism, Bone and Skull society etc. Mwisho wa siku inakuwa kila mtu achague pa kupita. Nashukuru kwa majibu yako yana fikra nzuri.
 
Umeongea jambo moja muhimu sana mkuu,

Na mimi naungana na wewe kuwa USA hujihusisha na raslimali ghafi na sio dini!

Sera ya nje ya USA inajieleza wazi!
 
Mzee Mwanakijiji,

Wapi mie nimekuambia Mohamed Said ndiyo wa kwanza kumtaja Sheikh Suleiman Takadir.

Nimecheka sana na maneno yako mpaka mtoto wangu kashangaa, wewe ulivyokuwa nyuma kufahamu historia ya Tanganyika unadhani wote kama wewe kwa taarifa yako vitabu vya histori ya Tanganyika nimevikuta nyumbani mzee wangu alikuanavyo ngoja nikutajie.

1. Macpherson Fergus, Kenneth Kaunda of Zambia.

2. Pratt Cranford, The Critical in Tanzania.

3. Hatch John, Two African Statesmen.

4. John Iliffe, A Modern history of Tanganyika.

5. Listowel Judith, The Making of Tanganyika.

Niambie wapi Listowel kamtaja Sheikh Takadir ndie mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Wazee wa TANU ambalo lilikuwa na wajumbe 170. Kama siyo Mohamed Said.

Wewe leo ndiyo umenunua vitabu AMAZON kuwasoma kina Listowel Judith, John Iliffe, haa haaa ha.

Vitabu vipo vingi bahati nzuri mzee wangu alikuwa anaeleza baadhi ya makosa ya vitabu vya Tanganyika.

Wewe unanichukulia poa unajidanganya ujiulizi kwa nini Ritz ameganda kwenye huu uzi muda mwingi kuna vitu najua vingi nimeadithiwa na Wazee wetu siyo kutoka kwa wazungu ambao nao wameadithiwa na wazee wetu, ambao wewe leo hii ndiyo unaanza kuwasoma na kutaka kuifahamisha mimi.

Endelea kusoma vitabu vyako.

Ritz,
Judith Listowell amemtaja Takadir kama mwenyekiti wa kwanza wa baraza la wazee wa TANU.
 
Mohamed,Bila shaka rika lako ni Ali Nasibu, kwani nadhani ndie mkubwa ktk familia ya Mzee Nasibu, lakini Mzee Nasibu alikuwa na kaka ake akifanya kazi ofisi ya Tanu mkoani Kilimanjaro, alikuwa dereva wa miaka mingi ktk ofisi ya Tanu. Baadae Wazee wa Moshi hasa akina mama wakiongozwa na Marehemu Juma Ngoma, Mama Halima Selengia, Yusuf Ngozi na wengine walichangishana fedha nyumba hadi nyumba na kujenga ofisi kubwa na ya kisasa kwa ajili ya CCM! MS, amini usiamini ofisi hii sehemu kubwa ya fedha zimetolewa na akina Mama wa Kiswahili wauza vitumbua na mama ntilie!Baada ya kumtaja Mzee Nasibu siwa nimeamini kweli wewe mtoto wa Mjini! halafu kumbe watoto wa mjini mtandao wao si mdogo!

Kadogoo,
Ali Nasibu katanguliwa na dada yake Asina.

Ali tumecheza sote udogo na tumeanza wote chuoni kwa Maalim Mussa
hapo Msikiti wa Ijumaa Mtaa Chini.

Hao wazee wote uliowataja ni kama nawaona vile.
Naifahami vyema historia ya TANU hapo Moshi.
 
Ritz,
Judith Listowell amemtaja Takadir kama mwenyekiti wa kwanza wa baraza la wazee wa TANU.

Judith Listowell, kamtaja Sheikh Takadir "Makarios" kijuu juu tu.

Mohamed Said ndiyo kaenda mbali zaidi kumuelezea Sheikh Takadir.

Vipi ameeleza ugomvi wake na Nyerere jinsi ulivyokuwa.
 
Shukran Mzee MS; Leo unaongelea "kakuachia mengi". Binafsi ningependelea sana mtu aandike his own story kama ile ya Museveni "Sowing the Mustard Seed" (hopefully nimeitamka sawa) au vitabu vya Obama nk. Kina POwell, Clinton. Au hata vitabu vya fani husika basi, Lakini nenda kwenye vyuo vyetu, takriban vitabu vyote wanafunzi wanavyopewa kama references huwa waandishi ni wa nje. Nimesoma SUA, kitabu kimoja cha fani kama ya Veterinary, kwa sasa usishangae kuambiwa lipa 150,000, sijui fani zingine, ilimradi tuu mlango huu upo wazi na ni mara chache kukuta ma-professa wazawa wanaandika vitabu kulijaza soko hili. Sasa tabia hii ndio unaikuta karibu maafisa wote waandamizi wanastaafu bila hata kuandika memoirs zao (labda tatizo ni soko, au publishers hawataki sijui). Ni tatizo ambalo kila anayejaribu kulivuka sharti apewe nguvu na pongezi.

Wickama,
Kitabu cha Ally Sykes kipo.

Yeye hakushika kalamu kwa maana yake halisi lakini MS alikuwapo...na tape
yake na note book yake...

Nimejifunza kitu kimoja hawa ''celebrities'' ukitaka wafunguke wachukue kama
vile mko jamvini mnazungumza hapo utashangaa na hakika utastaajabu.

Lakini kwenye ''formal interview'' hupati kitu kizuri.

Miaka michache ilopita nilikuwa naandika maisha ya Sal Davis (Shariff Salim
Abdallah) kijana wa Kimombasa aliepiga muziki Ulaya katika 1960s.

''One on one'' hupati kitu lakini mkute barazani kisha mchokoze...
Utashangaa.
 
Judith Listowell, kamtaja Sheikh Takadir "Makarios" kijuu juu tu.

Mohamed Said ndiyo kaenda mbali zaidi kumuelezea Sheikh Takadir.

Vipi ameeleza ugomvi wake na Nyerere jinsi ulivyokuwa.

Ritz,
Katika historia ya TANU kuna mambo TANU yenyewe ilikuwa wanayaogopa
na hili limekuja kurithiwa na CCM.

Sheikh Suleiman Takadir anaogopwa kama vile anavyoogopwa Abdu Sykes.
TANU haikuipenda kueleza michango ya wazalendo hao.
 
Abdul Sykes anaogopwa na TANU?

Asingetajwa katika kitabu cha TANU cha Kivukoni
 
Abdul Sykes anaogopwa na TANU?

Asingetajwa katika kitabu cha TANU cha Kivukoni

Jana ulituambia Abdulwahid Sykes katajwa sana kwenye kitabu cha Kivukoni.

Ukatoa ahadi kuwa utatuwekea mabandiko kwa faida ya wanajamvi tuwekee hicho kitabu cha TANU.
 
Wickama,
Kitabu cha Ally Sykes kipo.

Yeye hakushika kalamu kwa maana yake halisi lakini MS alikuwapo...na tape
yake na note book yake...

Nimejifunza kitu kimoja hawa ''celebrities'' ukitaka wafunguke wachukue kama
vile mko jamvini mnazungumza hapo utashangaa na hakika utastaajabu.

Lakini kwenye ''formal interview'' hupati kitu kizuri.

Miaka michache ilopita nilikuwa naandika maisha ya Sal Davis (Shariff Salim
Abdallah) kijana wa Kimombasa aliepiga muziki Ulaya katika 1960s.

''One on one'' hupati kitu lakini mkute barazani kisha mchokoze...
Utashangaa.

MS heshima yako. Nadhani uko sawa kabisa 100%. Wajua kuandika na haswa kitabu au vitabu ni kipaji pamoja na bidii. Hawa celebrities na pengine hata hawa viongozi tunaosema, vipaji vyao vipo kwenye kuhamasisha watu na kama haya. Lakini kushika kalamu na kuyaandika waliyoyafanya ni kazi kweli kweli. Haitofautiani na ule usemi wa kuwa ukiwakuta wale "vipanga" wa ma AAAAAAA-shuleni basi wasubiri in real life utashangaa zile AAAA zimeenda wapi. Duniani hupewi vyote. Pengine kulikuwa na haja ya kutumia njia kama hiyo ya uliyotumia kwa Ally ili angalau ile squad yote ya founders wa TANU wakawa na vitabu vyao japo kupitia migongo ya hao waliowaacha. Vingenevyo ndio imetoka.
 
Mkuu Wickama:

Nadharia nzima ya mapinduzi ya Zanzibar inabebwa na Okello,

Japokuwa inaelezwa kuwa Okello aliwazidi kete wahafidhina wa ASP ambao inaelezwa kuwa walishapanga kufanya mapinduzi wiki moja mbele ya yale ya Okello,

Mkanganyiko kwangu unakuja kutuama kwa Mzee Karume,

Je Karume alikuwa kwenye jeshi la Okello ama alikuwa kwenye kundi la mapinduzi la ya ASP ambayo yalipangwa kufanyika wiki moja mbele ya Okello?

Hebu tupeane elimu hapa mkuu!
 
Yericko,

Okello kama walivyokuwa wale mamluki wa Kimakonde kutoka Sakura na Kipumbwi
hawakuwa na lolote katika mapinduzi yale.

Wala hao Umma Party hawakuwa na mkono katika mapinduzi.

Nakuwekea hapa habari kiduchu sana ya Mkuu wa Mapinduzi - Abdallah Kassim Hanga.

Maneno haya niliandika kiasi cha kama miaka mitano hivi iliyopita na chanzo chake kwa
hakika ilikuwa mazungumzo ya simu kati yangu na Dk Harith Ghassany mwandishi wa kitabu
maarufu cha mapinduzi ya Zanzibar Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.

Wakati tukizungumza yeya alikuwa akinirekodi kutoka Washington na baada ya mazungumzo
aliniomba ayatie maneno yangu katika kitabu chake.

Na wakati ule mimi nilikuwa mtafiti msaidizi katika maradi huo wa kitabu.

Staladhi na hayo niliyosema:

Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa Mapinduzi ya Zanzibar hili si jambo lenye utata tena. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika mapinduzi hayo. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa umauti uliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa. Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho kwa hiyo kutangulia mbele ya haki yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma wakihangaika kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha mapinduzi kuuliwa kwao kulikuwa muujuza wa aina yake, uchawi usioelezeka nani fundi wake. Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kutoka katika mikono ya maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo. Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa waume na babazao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa mapinduzi aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa kifo tu bali kifo cha kishenzi. Fikra ya Hanga ilikuwaje alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison…usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa kikipitika katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali aikijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake. Fikra yake ilikwenda wapi? Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah na kwa Masultani wengi waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu za raia waoau kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde wakata mkonge kutoka Sakura na Kipumbwi? Fikra ya Hanga ilielekea wapi? Kwa Nyerere aliyemsaliti au kwa wale mbwa mwitu wakali mbele yake ambao midomo yao ilikuwa ikichuruzika udenda mwepesi wa uchu wa kuua? Hakika ni wazi hakutegemea mapinduzi aliyoyasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga na kufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya mapinduzi aliyokusudia ingeongoza Zanzibar. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume. Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, "Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale walipinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui." Halikudondoka chozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnong'ono wa kuuliwa kwake alikuwa kimya kama vile ile taarifa ile ya kifo haimuhusu.
 
Back
Top Bottom