Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Usikonde; Jaribisha hii, simu nyingi zinaipata, imem-cover JOHN OKELLO vizuri sana. Kuna mahali anazichapa kavukavu (hahahahahaha) Mimi nimeifurahia Good nite

Top 100 Goals of the Year 2012 - YouTube



cc Gombesugu

ha haa haaa!! naangalia fainal ya Copa del Rey, Real Madrid na Atletico Madrid huku nacheka peke yangu.

Hiyo YouTube ya Okello imerekodiwa mwaka 1964?

Hollywood Cinema wamekushikia akili... Ha haa haaa! unajua video za Okello zipo ngapi?

Jipange siyo unakurupuka.

Cc.. Barubaru, gombesugu,
 
Last edited by a moderator:
In the name of jah!
We trust!

Karibu kwenye ibada ya kirasta fari kesho mkuu,

Kanisa la RastaFarian lipo Kigamboni Mbutu, nyimbo bora kabisa za rege zitatumbuizwa kumsifu jah,

Pia weed ya kutosha itatolewa kama sehemu ya sakramenti kuu

Mkuu Yericko nashukuru sana ningependa tujumuike pamoja...
Jah bless you...
 

RITZ; NIMEKUKUBALI MSHIKAJI; WEE BURUDIKA, MBONA NI MGENI WANGU? LAZIMA NIKUKARIMU. NDIO MWENDO MDUNDO HIVYO

https://www.youtube.com/watch?v=YXb7kdnDsEU

CC GOMBESUGU
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Yericko nashukuru sana ningependa tujumuike pamoja...
Jah bless you...

Mkuu wa Chuo,
nawewe umejiunga na dini inayoruhusu uvutaji wa midaharati! ndio maana ulikiri kuwa wewe ni Mkuu wa ....!!! haa, haa, haa.
 
Kadogoo,

..U r not going to fool me na maneno matamu.

..mimi siyo Mchaga, lakini nafahamu vita wanayopigwa Wachaga, na kwamba kampeni za kuinasabisha CDM na Wachaga ni jitihada za kukiua chama hicho.

..hata CUF nao zilifanyika kila juhudi kukinasabisha chama hicho na Wapemba na Waislamu, na madhara ya kampeni hiyo sote tunayajua.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa Chuo,
nawewe umejiunga na dini inayoruhusu uvutaji wa midaharati! ndio maana ulikiri kuwa wewe ni Mkuu wa ....!!! haa, haa, haa.

Kadogoo
Mihadarati ni mirungi ambayo mimi situmii na huwa haivutwi
 
Last edited by a moderator:
Wickama, unajua kuna watu ambao wapo tayari kuridhika na udanganyifu hata kama fikra zao hazikubaliani.

Jasusi #15050 kaweka dhahiri shahir kuhusu watoto wa Nyerere, sasa Barubaru aje akanushe kama si kweli.

Baada ya jitihada za kumshambulia Nyerere kwa masimulizi, ngano na mikoba kushindwa sasa wanamgeukia kuhusu watoto wake.
Tumesikia kuhusu Virago vya mwalimu, mtaa na chumba alichoishi. Tena tukatajiwa hata siku tumbo lilipochafuka!
Hizo zote ni hila na mbinu chafu walizofuzu kutoka kwa mzee kwa ubani wa ''kufyonza ilm''

Kuhusu mapigano ya wakurya, nimempa challenge moja tu. Kwamba, anitajie taifa moja tu duniani ambalo jamii zake hazina migongano! ninataka taifa moja tu.

Anasema Nyerere hakuwa mzalendo, basi kama ni hivyo taifa hili halijawahi kuwa na kiongozi mzalendo!
 

Nguruvi3 umechuja sana,umechooka na kunyong'onyea kabisaa,ungelog out kwa sasa na kubakia as a GUEST ungekuwa umejitendea haki sana...
Kila napokuona na bandiko lako nazid kuingiwa na mshangao wa hali ya juu,kimekusibu nini??
 
Last edited by a moderator:

Nashukuru sana mkuu kwakuamua kulijibu swali hili,

Niliamua kujiepusha nisimjibu lakini nimefurahishwa sana najinsi ulivyojibu kwa ufasaha kabisa!

Zaidi ya mara tatu huyu bwana Barubaru analirudia tena kwa dhihaka sana,

Kuna watu hapa huishi kwa hisia tu!

Asante sana mkuu!
 

Kwa sababu Musoma makabila wanauwana kwa kuchinjana unataka kulazimisha kila nchi zina ugomvi wa kikabali mie nakutajia kwa uchache nchi ambazo hazina migogoro ya kikabila.

1) Tuwalu

2) Nauru

3) Vatican

4) Brueni

5) Luxembourg

Kama hutaitaji zingine takutajia wewe umeita moja mie nimekupa tano.
 

Nguruvi; Shukran. Kwanza hata kama Nyerere asingefikisha watoto vyuo vikuu, what has this got to do with the liberation ya watu weusi wa Zenj waliokuwa wanaitwa WAKATA MAJI? au wanaambiwa watamke HALUA ili wajulikane kama ni wenyeji? (yaani neno HALUA ndio ID!!!!!)Waone watu wametulia, wanauwezo wa kunyanyasa wenzao utashangaa.
 
gombesugu, sikupendezwa na lugha ya Gwalihenzi, lakini niwewe huyohuyo gombesugu uliyemuunga mkono mtukanaji mwingine aliyejiita Zali la Mentali aliyekuwa anashusha matusi ya nguoni dhidi ya Nyerere bila hata chembe ya aibu mpaka alipopigwa ban!Allah na mtume wana nguvu ya kujitetea na kutoa adhabu kwa Gwalihenzi! lakini Nyerere aliyetukanwa na Zali la Mentali kwa jina la kuutetea uislam atasaidiwa na nani? gombesugu ndugu yangu acha hiyo double standard.
 

Unajua maana ya nchi?

Vatican ni nchi?
 

Muheshimiwa Mag3,

Nashukuru kwa kunitumia salaam kupitia kwa ndugu yetu JokaKuu,nami nimekuja mwenyewe ili tuamkuane uzuri.

Kwa kifupi hiyo Historia ya Zanzibar nami pia naijua kwa kina na kiundani mno kwa minajil ya uwezo nilojaaliwa nao. Japo hii haina maana yakuwa ati wewe nawe hujui kitu,hasha mwandani wangu!

Tatizo ni yakuwa tuna mitazamo tafauti,ambalo pia ni jambo jema sana khasa kitaaluma.

Lakini tatizo jingine linipalo dhiki na madhila mengi,ni yakuwa nakuhisi wewe ndugu yangu Mag3 ni Mbaguzi wa rangi. Jambo ambalo ni hatari na khasara kwa Taifa letu changa.

Hayo majedwali yako hapo juu mimi binafsi na wewe ndugu yangu twajua yakuwa hizo informations/statistics ni fake na ni upotoshwaji wa Historia mkubwa mno!

Lakini napenda fursa kwa leo nirejee kiduchu kwenye huo ubaguzi wako wa rangi. Hivi Mag3 na wenzio woote hapa jamvini tangia lini mmeanza kuwa na Imani,huruma,majonzi,empathy,sympathy,sikitiko na labda pia kufikia kilio cha "ndugu zenu WaZanzibary Weusi"!? Halafu hizi definitions zenu za "Arabs","Africans","Bantu","Comorians" na mengineyo mengi,ndio mwanzo wa machochezi na kuhatarisha amani ya nchi.

Kuna baadhi ya Thread humu ndani nimeona ati huyo Mwanakijiji,amefikia hadi ya kujipa dhamana na authority ati ya kujua ni kiwango gani cha senti,hao WaZanzibary walipwe ili watolewe kwenye muungano!? Yaani imefikia huyo Mwanakijiji anajifanya yeye ni Fiscal Activist na kupangia Taifa/WaZanzibary kiasi gani cha senti wapewe ili waondoshe "gubu lao" kwa WaTanganyika!? Ama kweli hapa JF pana viroja vingi mno!

Ndo maana mimi binafsi,huwa nakuoneni yakuwa wengi wenu ni Wazandik tu. Yaani mnakuwa upande wa WaZanzibary pale tu inapo-suit matakwa na vigezo vyenu vya kibaguzi!? Sisi watu wa Madrassa hiyo tunaita Fitnatil Al Maaarifa.

Haya si ndo mambo mlokua mkimfanyia kebehi Sheikh Mohammed hapa jamvini,alipokua akitaja baadhi ya Makabila ya wenye mji/Wazee wetu hapo Mzizizma!?

Kama nilivywahi kunena hapo awali,haya majambo ya Race Issue ni very complex subject. Inalazim muwe waangalifu japo kiduchu,khasa mnapokua kwenye Public Forum kama hapa.

Mimi nina personal experience kutokana na family background yangu,kwa hiyo nazungumza kitu ninachokifahamu kwa undani na khatari zake kwenye Family au Taifa letu.

Nipo huku nje ya nchi kwa miaka mingi mno,tangia nakaribia "Alamatu'l Bulugh". Na nimetembea pahala na nchi nyingi mno kutokana na kibarua/Taaluma yangu. Nimekutana na watu na Historia nyingi zisizo mipaka na nimeona athari nyingi saana zitokanazo na huo ubaguzi wa rangi na ukabila ulokuingia kichwani.

Nilialikwa kupitia hapa kibaruani pangu,kwenye zile sherehe za ule "Uhuru wa South Sudan". Yaani nilitokwa na machozi mengi. Niliona vituko na mambo mengi kwa zile siku chache nilizokuwapo pale. Nilithibitisha zaidi jinsi gani Wazungu/Wakoloni walivyo mahiri na mastadi kwenye kutumia "Government machines" zao,influences na massive contacts walizonazo...ili kuendeleza madhila kutugombanisha WaAfrika,na wao wakiendela kuchota hizo rasilimali zilizopo hapo. Hii nayo pia ni topic ndefu mno,na bila ya shaka wewe mwenzangu itakuwa waijua uzuri zaidi yangu kutokana na huo umri wako ulowahi kukutajia hapa jamvini!?

Kwa kumalizia napenda kama kipata fursa japo kiduchu,rejea baadhi ya bayana zangu za awali khasa ile niliyokua nikijadiliana na ndugu yangu Nyambala,na nilijaribu kuweka tahadhari kwa Taifa letu WaTanzania,kwa kutumia kigezo/mfano wa nchi ya Sudan.

Nakuheshimu saana ndugu yangu,na pia napenda kuchukua fursa hii kukupa mwaliko rasmi katika Thread yetu mimi na ndugu yangu JokaKuu itakapokua tayari. Itahusu na kunyambua kiundani Nyerere na Mozambique,walakin tumekubaliana yakuwa ndani yake tutaweka na vikorombwezo vingi,khasa hiyo khabari ya Race Relation/Issue.


Lazim leo ninene hapa barazani;yaani kuna wakti nafikira kama siku tukijaaliwa kukutana popote pale basi hata mimi pia waweza kuniona au kuniita yakuwa sio MTanzania/MTanganyika, khasa kutokana na hizo definitions zenu za urangi na Makabila. Jana nilikua nawasomea wanangu/wajukuu zako ambao ni viduchu mno khadith za kulalia/bed time reading. Basi ghafla nikakukumbuka wewe Babu yao Mag3,je utakubali kuwa wao nao pia ni WaAfrika/WaTanzania siku ukiwaona/wakija kukuamkua!?

Kaa chini kwa utuvu ufikirie haya majambo kwa kina...huna haja ya kujilazimisha kujibu kwa pupa na zogo. Tumia busara nyingi ulonazo kwa utaratibu na madhubuti.

Insha Allah tuendelee na mnakasha,na nakutakia w'end njema.

Ahsnata.

Cc;Ritz
 

Maulaga,

Naomba uonyeshe hapa hadhwaran,pahala gani nilipompa LIKE huyo "mtukanaji". Au umechanganya yale majibizano ya kisiasa na hoja dhidi ya Nyerere na matusi!?

Tafadhali,mimi niko karibu mno na huyo Nyerere kuliko unavyofikiri na namtetea huku nje na kumlindia hishma yake kila kukicha kwa niyajuayo mema alofanza na nilikua nakubaliana nae. Kuna vitu mambo mengine/facts nijuazo sitaweza asilan kuyaweka hapa jamvini hata iweje. Kama vile asemavyo Sheikh Mohammed,yakuwa hawa ni Wazee wetu na wajibu wetu kuwastiri.

Kipata fursa kiduchu pitia bayana zangu za awali kwa Ihsan yako ndugu yangu Maulaga.

Kwa kifupi kwa hapa jamvini,zaidi ya huyo Jasusi labda na Andrew Nyerere ambae sijamuona kuchangia tangia nimefika hapa;basi hakuna mwengine ambae anaweza kunishinda kwa kumjua na ukaribu nilokua nae huyo Nyerere wako.

Hicho ni kwa kifupi tu ndugu yangu,na nimependa mno jinsi ulivyonikanya nami natumai utafurahia majibu yangu kwako.

Ahsanta na tuendelee nam mnakasha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…