Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Ndugu yangu gombesugu, sijui ulitaka kusema nini hapo nilipo weka red!Kama ulighadhibishwa na matusi ya Gwalihenzi na ukaomba jamii hapa JF iyakemee basi na upande wa pili yaani matusi ya Zali la Mentali yalipaswa kukemewa na wewe muungwana. Ajabu ulikaa kimya kana kwamba hukuyaona! hapo ndipo unaposhangaza!
 

Nadhani hata wewe ni muungwana ulipaswa kukemea matusi aliyokuwa anatukwanwa Mohamed Said, na wanaukumbi wengine lakini ulikaa kimya bila kuonyesha chochote.

Au mwenye jukumu la kukemea matusi jamvini ni Sharrif gombesugu, tu.

Tuendelee kusemezana kwa lugha ya ushui Inshaaalah.
 
Last edited by a moderator:

Maulaga,

Kama ujuavyo mimi ni Mgeni mno hapa Jamvini na Jamii Forum kwa Ujumla.

Na pia mimi kwa kuwa ni Mswahili nikatumia ule msemo yakuwa "Uingiapo mji wa vipofu nawe fumba lako jicho".

Kwa kifupi ulitakiwa unisifu japo kiduchu,kwa sababu pamoja na ule ugeni wangu nilijaribu ku-highlight hiyo issue kwa wenyeji wangu/Senior Members.

Na kuanzia sasa sitatumia hilo neno Nyerere wako asilan. Lakini na hili pia nilishawahi kulalama hapo awali;yaani hapa jamvini pana baadhi ya watu wanajiona yakuwa Nyerere ni kama vile wana hati miliki nae...na sisi wengine hatutakiwi asilan kumjadili au hata kumtaja bila kunasibishwa na chuki ya Ukatoliki au chuki binafsi dhidi ya "Mwalimu"!?

Ndo maana nilipoanza kutumia hiyo Nyerere wao/wako.

Nina mengi ya kukwambia ndugu yangu Maulaga,lakini nakuomba utulie na upitie posts zangu kwa utuvu. Maana hicho ndicho kitu pekee kitachoni-exonarate mimi dhidi ya hizo allegations zako.

Katika ile hoja yako nyingine ulidai yakuwa Nyerere anaonewa na hayupo hapa kujitetea,kwa hili yawezekana ni kweli. Lakini ukadai yakuwa Allah na Mtume Muhammad wanaweza kujitetea!? Hili si kweli abadan!....Mtume Muhammad hawezi asilan kuja hapa kujitetea dhidi ya kashfa na matusi ya Gwalihenzi...maana naye pia alikua ni mwana-Adam wala hakuwa na hatakuwa Mungu asilan!

Nakushukuru mno ndugu yangu Maulaga kwa ustaarabu wako wa kunirekebisha japo kiduchu.

Shukran.
 
Swadakta nimeiweka Vatican makusudi nisikie tunashukuru kama Vatican siyo nchi basi nitaitoa kwenye hiyo orodha.

gombesugu, Jasusi, Mdondoaji,

RITZ,
Umemshika Yericko pabaya! naona sasa unataka Mwanakijiji aje hapa kukanusha ya Yericko kuwa Vatikan ni nchi! halafu Yericko huyu huyu ndie alikuwa akishirikiana na Mwanakijiji kusisitiza Vatikan ni nchi! labda kwa kuwa leo ni weekend jamaa kasahau kuwa Vatikan ni nchi! hembu tungoje labda jumatatu baada ya mastarehe ya weekend huenda akaja kukanusha!
 
Matusi ni matusi tu, yanatakiwa kukemewa bila kujali anayetukanwa ni nani! sasa unapoona Mohamed anatukanwa ukaumia lakini Nyerere akitukanwa unapongeza hapo kuna hitilafu! Tuwe wakweli na kweli itatuweka huru.
 
Last edited by a moderator:
Swadakta nimeiweka Vatican makusudi nisikie tunashukuru kama Vatican siyo nchi basi nitaitoa kwenye hiyo orodha.

gombesugu, Jasusi, Mdondoaji,

mbona katika yale mambo yao ya kidini vatican wanasema nchi sawa sawa na iran leo hii wanaikana ama kweli njia ya muongo ni fupi
 
Last edited by a moderator:


Mzee MS; Sina budi kuuliza. Haya hapa juu ni maelezo mazuri sana ya kilichotokea. Mimi nikisoma ni kuwa wazee hawa wa Lindi walimfanyia Nyerere mpaka ibada ya kiislamu kwa vile WAZEE hawa walikuwa ni waislamu. Naamini kama angealikwa na Makalasinga wanaounga mkono TANU pia wangeendesha masuala haya kama wenzao waislamu kule Lindi. Sasa nakusihi kuwa CREDIT pia mpe na mpokeaji (NYERERE)kwa ule uelewa na TOLERANCE YA DINI ZA WENZAKE KUWA HAIKUMPA SHIDA YEYE KAMA MKATOLIKI KUCHANGANYIKA NA WATANGANYIKA WENZIE WAISLAMU, WAKIRISTO, WAHINDU HATUJUI NA DINI ZIPI TENA KUFANYIWA KARAMU, KULA NAO, NA HATA DUA ZAO. Mimi naliona taifa lilikuwa na mwelekeo wa kuvumiliana tangu wakati huo. Au sijaelewa agenda???
 
Kwa wanajamvi;

Nimeona kunapengine jitihada za makusudi za kupotosha wasomaji juu ya bango nililoweka siku za awali juu ya mpasuko EAMWS na aliyekuwa anaiongoza wakati ule ambaye pia alikuwa mufti wa Tanzania. Japokuwa nilionyesha vipande vya paper ya Dr. Iddy Ziddy vilivyoelezea kilichomkumba na kuikumba EAMS lakini nimesoma posting fulani humu ambazo zina lego la kuwapotosha wasomaji.

Ile paper nii hapa na unaweza kuisoma online.

JSTOR: An Error Occurred Setting Your User Cookie

Ukifanikiwa kuipata, sasa pitia hiyo paper kisha mkono kwa mkono kagua ile posting niliyoifanya wakati ule.
 
Matusi ni matusi tu, yanatakiwa kukemewa bila kujali anayetukanwa ni nani! sasa unapoona Mohamed anatukanwa ukaumia lakini Nyerere akitukanwa unapongeza hapo kuna hitilafu! Tuwe wakweli na kweli itatuweka huru.

maulaga,

Ukinisoma vizuri humu ukumbini sijawahi kumpongeza yeyote anayemtukana Nyerere.

Mara nyingi ninachofanya humu jamvini ni kuwatetea wazee wetu pamoja na Masheikh wetu wanaokejeliwa na kufanyiwa dhihaka.

Nadhani wewe umeshuhudia wanavyoitwa wazee wetu.

Bahati mbaya hata wewe upo kimya matusi yanapotolewa dhidi ya wazee wetu.
 
Last edited by a moderator:
gombesugu,

..naomba ufafanuzi kidogo.

..umesema ktk shughuli zako za kila siku unamtetea sana Mwalimu Nyerere.

..sasa kwanini hapa JF unapojumuika na wa-Tanzania wenzako unatumia msamiati "Nyerere wenu" au "Nyerere wako"??
 
Last edited by a moderator:
Mag3,

Kwa faida ya wanajamvi tufahamishe waafrika wa Zanzibar ni kina nani, halafu nyie Chadema mnamchukuliaje mfadhili wenu Mustafa Sabodo, wa chama chenu Chadema ni Muhindi au Mwafrika.



Naona hapa umeamua kupambana mpaka dakika za mwisho hili kiongozi wako wamlipe pesa nyingi pamoja na kukopa milioni 150 bado hazimtoshi, siku mkija kuchukuwa nchi walaahi sijui itakuaje ndiyo mtalipana mamalioni ya mishahara.

Hapa kama kawaida yako baada ya kuchakachuwa na kuficha source ya majedwali yako hili utimize lengo lako la kuwadanganya wanaukumbi wanaofutilia huu mnakasha basi mie kwa faida ya wanaukumbi nawawekea ulipoyatoa hayo majedwali kisha ukayachakachuwa haya hapa chini.
[TABLE="class: wikitable"]
[TR]
[TH]Party[/TH]
[TH]Votes[/TH]
[TH]%[/TH]
[TH]Seats[/TH]
[TH]+/-[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Afro-Shirazi Party[/TD]
[TD]87,085[/TD]
[TD]54.2[/TD]
[TD]13[/TD]
[TD]+3[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Zanzibar Nationalist Party[/TD]
[TD]47,950[/TD]
[TD]29.9[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD]+2[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Zanzibar and Pemba People's Party[/TD]
[TD]25,609[/TD]
[TD]15.9[/TD]
[TD]6[/TD]
[TD]+3[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Invalid/blank votes[/TD]
[TD]2,866[/TD]
[TD]-[/TD]
[TD]-[/TD]
[TD]-[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Total[/TD]
[TD]163,510[/TD]
[TD]100[/TD]
[TD]31[/TD]
[TD]+8[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 5, align: left"]Source: Nohlen et al.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
References


  • ^ Nohlen, D, Krennerich, M & Thibaut, B (1999) Elections in Africa: A data handbook, p880.

[TABLE="class: wikitable"]
[TR]
[TH]Party[/TH]
[TH]Votes[/TH]
[TH]%[/TH]
[TH]Seats[/TH]
[TH]+/-[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Afro-Shirazi Party[/TD]
[TD]36,698[/TD]
[TD]43.2[/TD]
[TD]10[/TD]
[TD]+5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Zanzibar Nationalist Party[/TD]
[TD]32,724[/TD]
[TD]38.5[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD]New[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Zanzibar and Pemba People's Party[/TD]
[TD]15,541[/TD]
[TD]18.3[/TD]
[TD]3[/TD]
[TD]New[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"]Total[/TD]
[TD]84,963[/TD]
[TD]100[/TD]
[TD]22[/TD]
[TD]+16[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 5, align: left"]Source: Nohlen et al.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
madhila waliyofanyiwa ndugu zake hayafikii yale waliyofanyiwa waafrika wa Zanzibar chini ya wakoloni kutoka Oman kwa karne nenda rudi.
Kwa faida ya wanaukumbi tufahimishe uafrika ni nini? hapa chini huyu anayewapa cheki viongozi wa Chadema ni mwafrika au muhindi?
 

Wickama,
Hilo ulisemalo la Nyerere wala halina ubishi hata kidogo.

Labda la kujiuliza.

Wakatoliki wa Peramiho walikuwa wapi wakati akina Sheikh
Badi wanapambana na Mwingereza?

Nadhani agenda sasa iko hadhir.
 
Wickama,
Hilo ulisemalo la Nyerere wala halina ubishi hata kidogo.

Labda la kujiuliza.

Wakatoliki wa Peramiho walikuwa wapi wakati akina Sheikh
Badi wanapambana na Mwingereza?

Nadhani agenda sasa iko hadhir.

Kazi ya kasisi Maranta ilihusu maeneo yote ya kihuduma Tanganyika ikiwemo Peramiho,

Sasa sijui unatazamaje juu ya hilo?
 
Wickama,
Hilo ulisemalo la Nyerere wala halina ubishi hata kidogo.

Labda la kujiuliza.

Wakatoliki wa Peramiho walikuwa wapi wakati akina Sheikh
Badi wanapambana na Mwingereza?

Nadhani agenda sasa iko hadhir.

Ok I get your point. Will you blame catholics for the defeat that Abdulwahid Sykes suffered at the hands of Nyerere at Arnatoglu Hall as well?
 
Ritz,

..Sabodo ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi.
 
Last edited by a moderator:
Ok I get your point. Will you blame catholics for the defeat that Abdulwahid Sykes suffered at the hands of Nyerere at Arnatoglu Hall as well?

Wickama,
Nimeeleza huko nyuma kuwa wazo la kumpata kiongozi mmoja kuwaunganisha
Watanganyika wote alikuwanalo Abdu Sykes siku nyingi na 1950 alijaribu sana
kumshawishi Chief David Kidaha Makwaia ajiunge na TAA ili wamchague kuwa
rais wa chama.

Chief Kidaha hakutaka.

Ilipofika 1952 Abdu alipokutana na Nyerere akampa fikra ile na Nyerere akakubali.
1953 Nyerere akachaguliwa kuwa rais wa TAA na 1954 TANU ikaundwa.

Abdu hakuwa mtu wa kupenda madaraka.
Hawezi kulaumiwa mtu kwa Abdu kumleta Nyerere pale New Street na kumjulisha
kwa wanamji.

Katika historia hii yake ndipo unapomsoma Abdu anapendeza.

Enzi hizo akiendesha Mercedes Benz na kijana mdogo akijiweza sana.
Vijana wenzake wakimuheshimu sana pamoja na Nyerere.

Yapo mengi lakini ya nini hayo yote?
 
Ritz,

..Sabodo ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi.

Jokakuu,
Chadema kupokea Takrima toka kwa kada wa CCM tafsiri yake nini? ni kichekesho kwa Chama kinachodai ni Wapinzani huku wanapokea Takrima toka kwa kada wa Chama tawala! Sabodo ni kada wa CCM au CDM? haingii akilini kada 1 kupenda vyama 2 tofauti! hapa kuna usiri fulani tunaomba akina Jokakuu watufichulie!
 
Gombesugu nami nakuamkua huko ughaibuni ulipo. Je, kulikoni?

Naona umeguswa sana na suala la rangi. Nikufahamishe kuwa suala la rangi kwa ZNZ ni jambo ambalo huwezi kuliepuka katika siasa zake. Nadhani unajua kuwa hivi karibuni wapo viongozi waliotoa kauli za kuonyesha wazi urangi ulivyotamalaki visiwani.

Ni suala la historia na litabaki kama lilivyo kwasababu uwezo wa kupindua historia haupo isipokuwa kwa wachache waliojaaliwa. Ili kuipindua historia inabidi ujivike joho la uongo, fitna al maarifa kwa kutumia CD,paper au vitabu. Vyovyote iwavyo historia inabaki kama ilivyo na huko visiwani Urangi ni sehemu yake.

Kuna mahali umemgusa Mwanakijiji kuhusu masuala aliyoongelea ingawa umepindisha kidogo ili kutoa taswira unayoitaka na siyo iliyoongelewa.

Nalazimika kuingia hapa kwasababu katika nyuzi hiyo aliyochangia Mwanakijiji nami pia nilichangia.
Na hapa naweka rekodi sawa.

Aliyeleta hoja ya kugawana kila kitu pasu kwa pasu ni mzanzibar.
Mzanzibar huyo alidai kuwa muungano ukivunjika itabidi kugawana kila kitu kwa kuzingatia kuwa BoT ina mtaji wa 12.5%.

Katika majibu na langu likiwemo, tulisema kuwa hiyo haina taabu lakini basi kila kitu kiwekwe mezani.
Kwamba znz haijawahi kuwa na bajeti ya ulinzi na usalama, elimu ya juu, imekuwa inapata 7% zamani 4% ya pato la taifa, huduma za bure kama umeme, mishahara ya wastaafu, mishahara ya wafanyakazi wa SMZ hadi masheikh, kuziba nakisi ya bajeti ambayo ni pengo mara 3 kuliko pato la znz n.k.

Pesa zote hizo zinatoka Tanganyika na kwa Watanganyika kwasababu znz haina uwezo.
Haina uwezo kwa kuzingatia kuwa pato lake la mwaka ni bilioni 120 ambazo haziwezi kuendesha wizara ya mambo ya ndani ya muungano au basi hata vikosi viwili vya jeshi.

Kwa mantiki hiyo, 12.5 ya znz itawekwa mezani, lakini haitaishia hapo itabidi na makando kando mengine yawekwe mezani pia ili haki itamalaki. Kwa msingi huo znz itajikuta inalazimika kulipa na si kulipwa.

Hapo ndipo inaposemwa kuwa znz waondoke katika muungano salama salimini hawana kitu cha kudai, vinginevyo watakuwa wanakaribisha matatizo. Ili kuondoa Gubu wao waende zao taratibu.

Hapo hakuna suala la fiscal activist ni suala la ukweli na kama ni uongo, basi hebu tufahamiane wapi unapodhani kuna wahka ulioleta staftashi katika kiwango ulichoonyesha.

Kuhusu znz kutumika pale penye ''mafao''kwa Watanganyika, nadhani hilo halina ukweli.
ZNZ haina mafao na Mtanganyika ya aina yoyote.

Suala la muungano lipo wazi kuwa kama wamechoka na wanaona wanaonewa, basi wao kwa pamoja na viongozi wao waondoke Tanganyika warudi kwenye nchi yenye neema.
Ingawa wzn wengi wasingependa muungano uvunjike kwa manufaa wanayoyapa, hilo halizuii wao kuamua hatima yao wakitaka.

Lakini pia usisahau kuwa suala la Urangi linakuzwa sana na wzn wenyewe. Wanapomwita Karume Mnyasa, Mwinyi Mndengereko n.k. maana yake wanawagawa watu wao.

Kwamba ili uwe mznz halisi lazima uwe na nywele za ''katani'' midevu ya nguvu at least kuonyesha una unasaba mwingine na si wandengereko au Wanyasa.

Hapo ndipo ftina al maarufu ilipo kwahiyo kumlaumu Mag3 kwa kuweka anayoyafahamu kuhusu historia si kumtendea haki.Unapaswa uwasote vidole wzn ambao hutambuana kwa rangi kwanza.

Na mwisho, pengine uwaase wznz wenzako kuwa hizi habari za mkafir n.k. ndizo zinazozaa hisia za urangi.
Kwamba ukitoka bara ni chogo, na kama umezaliwa visiwani ni chogo mdogo.
Asiye chogo lazima awe na yale niliyoyasema hapo, ikiwa ni pamoja na karangi ka kiarabu japo kwa kuibia.

Khair Inshallah basi mjulie hali ahli wako na vijana.

cc. Al-akhyi wote,waungwana,wanajamvi na 'makafir'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…