Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


UONGO usiokifani,

Tumeshaeleza sana juu ya uongo wako usiojua hata kuutetea,

Nyerere ameanza kuhudumu katika siasa tangu mwaka 1945 ndani ya AA, Abdul kaibukia TAA mwaka 1948, sasa hapo nani mkongwe wa siasa za Tanganyika?

Unadanganya watu kuwa Abdul Sykes hakupenda kuwa kiongozi ilihali alishindana na Nyerere marambili? 1953 katika TAA, na 1954 katika TANU

Nachukia sana nikimuona mzee ni muongo
 


Haiwezekani,haingii akilini hata kidogo,
Mtu mzima na akili zake atoke zake kuoga na kuingia nyumba ya bui bui kubadilishia nguo zake huku akitaraji wapita njia na jirani zake wasiione aibu yake,hilo haliwezekani hata kidogo...

Kwenye bandiko lako hili kwa mtu mwenye akili timamu anang'amua wazi wazi mantiq yako..!

Pole sana...
 

Waache hao wa pembeni, je unaweza nitajia mmoja tu ambaye kabla kifo chake alikuwa na Degree kama hu msema kweli?. Kumbuka nawafahamu vizuri sana na nilikuwa nao karibu sana nilipokuwa Mwanza.

Na ninapozungumza mambo ya mkoa Mara jua naujua vizuri sana nimewahi kukaimu mara nyingi sana wakti akiwa madarakani niambie ni wakti gani ulitulia? au zilikuwa kuna siri kubwa na kuminywa kwa habari ndiko kulikoleta amani.

Uzizungumze jambo ambalo huna uhakika nalo kumbuka ninachoandika nakijua na naweza yakinisha hata kwa muumba.

Kuhusu Ilmu ni popote pale kwani wazazi wangu walikuwa walipa kodi wazuri sana kutokana na biashara zao, hivyo mi sikubahatika kusoma bure bali Wazazi wangu walinisomesha kwa kodi walizokuwa wanalipa Serikalini na walilipa pesa nyingi sana nami nikasoma toka darsa la nne mpaka UDSM bila mushkirah.

POLE SANA.

cc😡Jasusi, Mag3, Wickama, Kadogoo, Ritz, Nguruvi3

 
Yericko,
Sheikh Badi alikuwa mpigania uhuru.

Mbona hutulii kwenye hoja?

Hoja yako yamsingi ilikuwa kwanini wakristu wa Peramiho hawakupambana na Muingereza?

Mimi nikakujibu kuwa Kazi ya kasisi Maranta katika kuhudumu kwa harakati za ukombozi Tanganyika, na Peramiho ilikuwa ni wajibu wake!
 
Ritz,

..Sabodo ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi.

Nashukuru kwa jibu lako murua.

Na Nyerere je asili yake ilikuwa wapi?

Hata mbunge wenu wa Chadema Mwanza Nyamagani Wenje ni Mtanzania mwenye asili ya Kenya.

Sabodo ni mwafrika au siyo mwafrika hapa ndiyo nataka kujua.
 
Last edited by a moderator:

nGURUVI3,

Si vizuri kuongelea jambo usilokuwa na ujuzi nalo. Mimi ni mmoja niliyewahi kukupambanualia kwa kina sana huo mgao ukoje na nikakupa mpaka reference na wapi unaweza kuzipata lakin naona umekuwa mvivu kufanyia kazi.

Kwa sababu umegusa katika eneo langu la uchumi kuhusu huo mgao. Kwa leo nakupa reference hii kwa faida ya wana ukumbi wote. Katika BOT kuna kuna kitengo katika Serikali hizi mbili kinachoshughulikia na kuangalia maslahi ya nchi hizi mbili yaangi Tz bara (Tanganyika na Znz kinaitwa JOINT FINANCE COMMISSION (JFC) na afisi zao zipo pale Sukari house Dar es salaam.
Nakusihi fuatilia taarifa zao zitakupa mwanga mzuri sana kuhusu gawiwo hilo la BOT na sio kuleta maneno ya Sunday school.



Kuhusu hiyo kuitwa chogo mbona jambo la kawaida sana. Hata mimi nilipokuwa nafanya kazi bara nilikuwa naitwa MPEMBA. Je na mimi nichukie hilo. Kama umekaa Mwanza na wasukuma kuna mambo kama hayo pia kuna wasukuma halisi na wengine wakuja wakiitwa wadahama. sasa jua utani ni sehemu ya kukuza mahusiano kama mtatumia vizuri lakin vile vile ni sehemu ya kuvunja mahusiano kama mtatumia vibaya. sasa maamuzi ni yenu kusuka au kunyoa.

Pole sana ahali yangu.

wasalimie wapendwa wote, wanajamvi wote.
 

Nguruvi3,

Awali ya yote nimesikitika sana timu yangu Simba kufungwa na Yanga 2-0. lakin yote ndio mpira kuna kufunga na kufungwa. Ni wakti wa Malkia wa Nyuki na Ismail Aden Rage kujipanga upya kwa ajili ya ligi.

Mimi binafsi kama mchumi naweza kumchambua Nyerere kiuchumi zaidi kuwa ALIFELI vibaya sana na hali zote mlizonazo pamoja na rasilimali zote mumezidi kuwa masikini sababu ni SIASA za Nyerere.

Nitakupa ushuhuda nikiwa wizara ya fedha kuna fedha alikuwa analazimishwa zipelekwe kwa wapigania uhuru wa Swapo na ANC wakti wananchi wa Tz wakiwa wanakula unga wa yanga. kwa hiyo utaona alipenda sana kujipendekeza kwa nchi za nje na kulaza wananchi yake na njaa na majanga.

Alikuwa TAJIRI wa siasa lakin masikini wa uchumi na hivyo kukosa uzalendo wa kuweza kuinua uchumi wa nchi yake.

Ni yeye aliasisi Rushwa na Ulanguzi kutokana na siasa zake kiasi cha kufanya raia wake waishi kwa taabu na dhiki kubwa kukesha kwenye foleni za hata sabuni zakufulia na kuogea achilia mbali unga, mchele na maharage.

Alipiganisha vita vya Uganda kwa nia ya kumrejesha Rafiki yake Obote madarakani na kuuwa kabisa uchumi wa nchi yake na kuwaongpea mfunge mikanda ya kiuchumi kwa miezi 18 jambo ambalo ameshindwa kuwaeleza mfungue mikanda hiyo mpaka anakwenda kaburini.

Kwa vigezo hivyo nashawishika kusema kuwa hakuwa MZALENDO kwa taifa lake bali alipenda kupewa sifa binafsi.

sasa naomba uniainishie uzalendo wake uko wapi

 
i

Hao wanajeshi je unajua wote walifukuzwa. Huyo wa Air force ngerengere alifukuzwa na wa china japo alikuwa mahiri sana kuongea kichina.Uliza utaelezwa.

Na hao wengine wote kama walipata degree basi wamepata degree zao baada ya baba yao kuondoka madarakani.Lakin jiulize je walisoma skuli gani za Sc na kama yupo aliyewahi kwenda High sch skuli gani?

Naomba uchunguze hilo kisha nikosoe kama nitakuwa nimenena uwongo

usitake niseme meng

 
Nimezungumza kama mtanzania yeyote yule anaekereka na uchochezi wa Mohamed Said,Sijabeba undugu damu katika hili.

naona huna la ziada...watu wanakuletea na evidence..we unapiga porojo tuu...huna unachojua zaidi ya umbeya wa kisiasa...! Mohamed Said ni Shujaa wa Kiihistoria...! tunasubiri kitabu chako cha UGAIDI naona hiko kitakuwa ni NGANO za VULI kabisa....maana utangulizi wake tu waonyesha kijana unapenda kudandia hoja....u know nothing
 


Ukisikia kuweweseka ndiyo huku, Mag3 kaleta jedwali lenye data ulizotuhumu kuwa si za kweli. Sasa wewe ilibidi uje na jedwali lako lenye data za kweli kupinga hoja kwa hoja. Badala yake umekurupukia name calling na accusations zisizo na mashiko. Let me tell u something openly inaonekana unasumbuliwa na kaugonjwa ambako ni mix ya ulimbukeni na inferiority complex. I could be wrong but that is the way I see it. Ndiyo maanna badala ya kujibu hoja kwa hoja lazima ulete ngoonjera ndefu ya historia ya maisha yako, familia yako which is just a b.l shyt. Lakini nadhani hiyo ndiyo namna unafikiri itafanya hoja zako ziaminike and there goes my point. You are the very person who claim to be ridiculed kwa sababu ya dini yako kwamba oooh wanywa kahawa, madrassa, na upuuzimwingine. Cha kushangaza wewe mwenyewe ni bingwa wa kuridicule others almost in every post unayotuma. Jibu hoja kwa hoja usilete vioja.


Halafu jingine naona mbonyezo like huwa unakuwewesesha mno, anyway utazoea taratibu. Demokrasia ya JF inaruhusu mtu yeyote ku-like post yeyote and they are entitled to their own reasoning.
 



Tehe tehe tehe!!!!!! hivi hizo nchi Tuwalu, Brueni, Luxembourg ziko wapi hopefully hutawaambia wanajamvi ni typo. (if u know the meaning of it anyways)

Hoja ni kuwa taja nchi ambayo haina migogoro ya kijamii wewe umeleta yako kuhusu migogoro ya kikabila. Where did u pulll that one from?
 

Sawa Mzee MS; Nakukumbusha ni WEWE ULIMWONYESHA Abdul Sykes akimsengenya Nyerere kwa Swahiba wake (Mwapachu) kuwa WANGEMWACHIAJE CHAMA MTU WASIYEMJUA. Then Abdul anagombea. Then, mtoto wa mjini mwenye Benz na heshima ya wana Dar, LOST (Labda; check orodha ya voters, for Catholics!!!) Wapo wengine pia hapo awali walimwomba Nyerere kugombea kwa kumuona anafaa na kwa kuona tangu Vedasto Kyaruzi aondoke, chama kilikuwa kinadorora (Msome Seaton-wewe hujaandika). Soma yule meneja wa Arnatoglu Hall (Phombe???) anavyohaha chama kiongozwe na Julius.

Mzee MS,somewhere in life you must face it; that your Abdul was not only a backbiter but also a bad loser. No president would have kept a backbiter and double dealer in his cabinet (as you have shown him yourself!!!!) If he was any good and trustworthy as you have trumpeted in this forum, he could have not fallen from grace for others. That is the bottom line.
 
Si kweli! Hapa ndipo hoja ya Mag3 inapokuwa na nguvu sana.
Mag3 ameweka wazi jinsi Nyerere alivyokuja mwaka 1946 (kama mwaka ni sawa) na akauliza wakati huo Abdul alikuwa na sifa gani katika siasa?

Nyerere alikutana na Dosa Aziz kabla ya kukutana na Abdul. Kwa uchache alikuwa ameshaanza kufahamiana na wanamji

Ama kuendesha Benz kama hilo lilitokea basi kwa nyakati hizo ilikuwa ni heshima kwasababu Watanganyika wengi hawakumudu kiatu sembuse Benz. Sasa kuheshimiwa ikiwa ni pamoja na Nyerere hayo ni maneno yako kwasababu hakuna mahali pamenukuliwa akisema hayo. Tunaheshimu sana mawazo yako binafsi na si ya kihistoria.

Wazee wote waliopigania uhuru wa nchi hii wanapaswa kupewa heshima.
Hakuna mwenye heshima kubwa au ndogo, heshima ni heshima.

Jitihada za kumpandisha Abdul awe Rais wa TAA na TANU kisha Tanganyika haziwezi kuzaa matunda kwa werevu.
Abdul atabaki kuwa na mchango wake na kuheshimiwa kwa hilo.

Jitihada za kumdhalilisha Nyerere ili kusafisha nyota ya Abdul hazitazaa matunda asilani.
Nyerere atabaki kuwa kiongozi wa TAA,TANU, Rais wa kwanza wa Tanganyika huru, mwenyekiti wa kwanza wa CCM.

Na hapa umetusadia sana kutambua kuwa kumbe hata Abdul alifahamu kuwa ipo haja ya kuwa na mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha Watanganyika. Kidaha alikataa, Nyerere akakubali. Swali ni kuwa je, lengo la Abdul kuwaunganisha Watanganyika kwa kumtumia Nyerere lilifanikiwa au la?
 
Mkuu Jausi, Barubaru anasema watoto wa Nyerere hawakusoma highschool.
Ana mashaka na degree walizopata na anasema kama zilipatikana ni baada ya baba yao kufariki.
Mkuu, busara zako tafadhali
 
Thanks Bro!
 
Kinachonitia nguvu zaidi ni kuwa hoja zangu zinasimama kama zilivyo na zinabaki kuwa uchochoro wa personal attack. Nafahamu wazi kuwa kejeli, matusi na dharau huwa ni silaha za mwisho kabisa kutumika pale ambapo ghala silaha linapkuwa halina kitu.
 
Barubaru, wewe ni fundi sana wa kukimbia hoja.

Kwanza, ile ya Nyerere Mkuu Jasusi atakapoamka atakuja na zana, huwa sina shaka na maudhui yake. Tuliweke kiporo

Pili, nimekuuliza taifa moja tu duniani ambalo jamii zake hazina migogoro. Umekaa kimya.
Pengine unaunga mkono zile za Sharrif Ritz, endapo ni hivyo basi thibitisha ili tuendelee kuanzia hapo

Tatu, nimekuambia kuwa:
a) Zanzibar haina bajeti ya ulinzi na usalama tangu mwaka 1964. Kataa au kubali
b)Haina bajeti ya elimu ya juu tangia wakati huo. Kataa au kubali
c)Mishahara ya wastaafu inalipwa kutoka hazina Dar. Kataa au kubali
d) Mishahara ya SMZ inatoka Tanganyika. Kataa au kubali
e)Kwamba, wazanzibar hawajui gharama za huduma kama umeme. Kataa au kubali
f) Kwamba bajeti ya znz ni billion 630, mapato ni bilioni 120 pengo la bilioni 510 linazibwa na bajeti ya Tanganyika.
g)Kwamba ofisi ya makamu wa rais muungano inapewa hela tu(billion 32) kwa znz . Kataa au kubali
h) Kwamba znz inapata 7% ya mgao wa pato la taifa kwa kuchangia ''0'' katika pato hilo. Kataa au kubali

Sasa kama una hoja nyingine ya mgao, huu ni ukumbi iweke wazi. Hili la kusema kuna taarifa za siri si kweli.

Hoja ndizo hizo hapo juu. Ima ukabiliane nazo au ukunje jamvi kwa upande mmoja, upande mwingine ubaki ukisoma
 
Ritz, watu wanaoishi Misiri, Libya,Algeria na Morocco ni waafrika? Je nchi hizo ni zakiafrika? ili uwe muafrika nilazima utimize vigezo gani? Serikali ya nyerere iliwateua akina Brayson na Jamal kuwa mawaziri, je hawa walikuwa waafrika? je kunatofauti kuwa Mtanganyika/Mtanzania na kuwa Muafrika?
 
Kadogoo, kada ni mtu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…