Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
-
- #15,121
Barubaru, wewe ni fundi sana wa kukimbia hoja.
Kwanza, ile ya Nyerere Mkuu Jasusi atakapoamka atakuja na zana, huwa sina shaka na maudhui yake. Tuliweke kiporo
Pili, nimekuuliza taifa moja tu duniani ambalo jamii zake hazina migogoro. Umekaa kimya.
Pengine unaunga mkono zile za Sharrif Ritz, endapo ni hivyo basi thibitisha ili tuendelee kuanzia hapo
Tatu, nimekuambia kuwa:
a) Zanzibar haina bajeti ya ulinzi na usalama tangu mwaka 1964. Kataa au kubali
b)Haina bajeti ya elimu ya juu tangia wakati huo. Kataa au kubali
c)Mishahara ya wastaafu inalipwa kutoka hazina Dar. Kataa au kubali
d) Mishahara ya SMZ inatoka Tanganyika. Kataa au kubali
e)Kwamba, wazanzibar hawajui gharama za huduma kama umeme. Kataa au kubali
f) Kwamba bajeti ya znz ni billion 630, mapato ni bilioni 120 pengo la bilioni 510 linazibwa na bajeti ya Tanganyika.
g)Kwamba ofisi ya makamu wa rais muungano inapewa hela tu(billion 32) kwa znz . Kataa au kubali
h) Kwamba znz inapata 7% ya mgao wa pato la taifa kwa kuchangia ''0'' katika pato hilo. Kataa au kubali
Sasa kama una hoja nyingine ya mgao, huu ni ukumbi iweke wazi. Hili la kusema kuna taarifa za siri si kweli.
Hoja ndizo hizo hapo juu. Ima ukabiliane nazo au ukunje jamvi kwa upande mmoja, upande mwingine ubaki ukisoma
Asante sana mkuu kwa hoja hizi mujarabu!