Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nguruvi3,

..hawaweki chochote ktk chungu.

..mkurugenzi wa tra Znz alisema kinachokusanywa Znz kinabaki na kutumika huko huko.
 
Last edited by a moderator:
Wana Baraza na Ndugu zangu katika Mnakasha huu..
Sina shaka kuwa jina la field marshal John Okelo si geni masikioni penu. Historia inayofundishwa darasani haimtaji kabisa mtu huyu. Nilitaka nami kumpuuza tu, lakini nimepitia pahala pameandikwa jambo zito na la kutisha likimwelezea Okelo pamoja na Baba wa Taifa. Tafadhalini sana, kwa wale wanaoweza kutupa historia ya huyu bwana na kugusa yafuatayo watusaidie ili niweze kukileta kwenu hiki kinachoniduwaza hapa..
1. Huyu John Okelo alikuwa ni nani?
2. Alihusikaje na siasa za Zanzibar?
3. Alipata wapi suport ktk utendaji wake?
4. Alifaidika vipi na mapinduzi aliyoyasimamia?
5. Alikuwa raia wa wapi?
6. Alikwenda wapi baada ya mapinduzi?
7. Yu hai hata sasa au alikwishatangulia mbele ya hak?
8. Kwanini historia rasmi ktk maskuli haimtambui kama inavyomtambua Karume na wengine?
9. Kwanini John Okelo hajawekwa kama msingi wa mapinduzi ya zanzibar?
Kwenu wana jamvi.
C.C Mohamed Said, Yericko Nyerere, Ritz, Gombesugu, Jokakuu, Mag3, Bigshow na wote humu..
 
Nguruvi3,

..hawaweki chochote ktk chungu.

..mkurugenzi wa tra Znz alisema kinachokusanywa Znz kinabaki na kutumika huko huko.

Umefika wakati sasa wakuwaamsha watanganyika wajue kuwa mtoto tuliyembeba amepanda na viwembe mgongoni, anatuchanja tumshushe haraka iwezekanavyo!
 
Last edited by a moderator:
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere,

Kila siku siku zote napenda kukushauri pinda mgongo ufundishwe na wajuvi wa historia kama Mohamed Said, hebu angalia unavyojichanganya hapa na hii historia yako kwa faida ya Wanaukumbi ngoja ni dadavue kiduchu bayana zako.

Wanaukumbi hapa tunaambia Sheikh Issa kazaliwa mwaka 1846 halafu amekutana na Askofu Maranda mwaka 1948 kwa hiyo tunaona Sheikh Issa alikuwa tayari na umri wa miaka 102. mtu mwenye umri huu anaweza kweli kufanya harakati za siasa mfano mdogo tu Nelson Mandela saizi ana umri wa miaka 94.

Nje ya kuhudumu katika uislamu, alikuwa ni mvuvi aliyevua pamoja na Ally Ramadhan mwekahazina wa kwanza wa AA,
Wanaukumbi hapa tena Yericko anajichanganya tena, AA iliundwa mwaka 1929 tukiangalia mwaka huo Sheikh Issa atakuwa na umri wa miaka 83, kweli umri huu mtu anaweza kuwa na nguvu ya kuvua samaki.

Wanaukumbi hapa tena Yericko anajichanganya mwaka 1954 Sheikh Issa alikuwa na umri wa miaka 108, ha haa ha, hebu hapa chini tumsome Nyerere mwenyewe kwenye hotuba yake ya kuanga wewe unasema habari za mwaka 1954 Nyerere mwenywe anasema habari za mwaka 1952, ha haa haa, hizi bayana zina tashtit.

Julius Nyerere.'"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Julius Nyerere"Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.
Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.


Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake""!
Huyu Sheikh Issa ameishi vipi vyote kuanzia AA, TAA. TANU, CCM maana ujasema alifariki lini.
 
 

Nguruvi umenisikitisha sana kwa jinsi unavyo wazungumzia wa Znz yani wewe unaposema sasa hivi hakuna tena "cold war" kwahiyo unataka kutuaminisha kwamba Nyerere na Karume walituunganisha kutokana na "cold war" hayo sio maneno sahihi kwa wa znz kwahiyo wazazibar walitumika kama beleshi ujenzi ukiisha linawekwa stoo na hizo cc uliowataja nikuulize unajua maana ya neno kafir? mkubwa wacha chuki na waznz haya maneno kwamba waznz ni tegemezi angeyazungumza baba yako wa taifa sio wewe nakusikitikia sana tuendelee na mnakasha. ahsante
 
Mkuu mzee wangu Mohamed, unamaana gani unaposema nyinyi?
ana maanisha wao wazee wao ndo wamiliki wa historia, sisi wazee wetu si sehemu ya histori, mtu wa ajabu kabisa huyu mzee. ubinafsi ndo nguzo kuu ya huyu mzee.
 

Wanajamvi,
Nimgeliweza kueleza mgogoro mzima wa Sheikh Hassan bin Amir na Nyerere
sheikh akiwa sasa anaongoza taasisi iliyoitwa Daawat Islamiyya (Wito kwa
Waislam) yeye akiwa Mwenyekiti na Schneider Abdillah Plantan akiwa katibu.

Lakini kwa kuwa Sheikh Hassan ametukanwa hapa ninajizuia kwa ajili ya kuhifadhi
heshma ya kiongozi wetu ambaye wengi wanamuitikadi kuwa alikuwa walii.
 
 
ana maanisha wao wazee wao ndo wamiliki wa historia, sisi wazee wetu si sehemu ya histori, mtu wa ajabu kabisa huyu mzee. ubinafsi ndo nguzo kuu ya huyu mzee.

Zumbemkuu,
Katika hii historia ya kuasisi TANU na historia ya Nyerere katikia TANU pale
New Street hakika wazee wangu hawana mfanowe.

Ikiwa huu unaona ni ubinafsi ni bahati mbaya.
 

Jokakuu hivi unaposema muungano leo hata ukivunjika watanganyika hamna shida hivi hatakama ni hiyo ruzuku inayotoka Tanzania bara unataka kuniambia nchi za nje hazichangii halafu leo hii nchi nchi za nje zikigoma kutoa pesa kuchangia bajeti serikali povu linawatoka na hii yote inaonyesha hata serikali ya watanganyika ni tegemezi kwahiyo punguzeni chuki wakuu asanteni.
 
Last edited by a moderator:

Unajifanya mjuvi ilihali hujui kitu,

Unaleta kejeli na matusi mwisho unaomba kupewa darasa?

Nakujuza kuwa mzee wetu Shehe Issa Bin Amir amefariki 26 januari 1953 akiwa na umri wa miaka 107!



Hoja zingine zote naomba uzijibu kwa swali hili,

1) Je Mwalimu Cesil Matola alikuwa na Umri gani 1929 wakati anakuwa rais wa KWANZA wa AA?

2) Ally Ramadhan alikuwa na umri gani wakati anachaguliwa kuwa Muweka hazina wa kwanza wa AA?

3) Klest Sykes alikuwa na umri gani wakati anachaguliwa kuwa katibu mkuu wa AA?

Ukijibu haya naomba jibu na hili:

Je unadhani Shehe Issa Bin Amir alikuwa na umri gani mpaka viongozi wa AA wakamheshimu na kutumia hekima zake?!

Tumia akili unayofundwa kila siku hapa jf
 
Zumbemkuu,
Katika hii historia ya kuasisi TANU na historia ya Nyerere katikia TANU pale
New Street hakika wazee wangu hawana mfanowe.

Ikiwa huu unaona ni ubinafsi ni bahati mbaya.
na iwe hivyo mkuu, babu yangu kule lushoto alitembea kwa miguu umbali mrefu, toka mlalo hadi Tanga mjini katika harakati za kudai uhuru leo useme wazee wako wa new street ndo waliotuletea uhuru........!!!!!
 

Sawa MS; Baada ya heshima yako, i will give you the benefit of the doubt. Ila one thing which must be told ni kuwa he errored kukataa kuwa kwenye cabinet. He missed the opportunity ya kuchangia kurekebisha au kusaidia from a vantage point. Kwa MAONI yangu huwa ni rahisi kusaidia ukiwa ndani ya mfumo kama cabinet. The point iam making ni kuwa KK amesaidia sana masuala ua university ya pale Morogoro kwa vile alikuwa na hiyo vantage point. In life vita siyo silaha tuuuu, ni pamoja na STRATEGY. Shukran MS.
 
Zumbemkuu,
Katika hii historia ya kuasisi TANU na historia ya Nyerere katikia TANU pale
New Street hakika wazee wangu hawana mfanowe.

Ikiwa huu unaona ni ubinafsi ni bahati mbaya.

Ukiwa mbinafsi na mbora mimi kamwe huwezi kuandika historia ya nchi inayohusu makabila zaidi ya 120 na inayohusi imani zaidi ya tano nchini!

Utabaki na kikundi cha wanafiki na wafitini tu ndio wataokuunga mkono!
 
na iwe hivyo mkuu, babu yangu kule lushoto alitembea kwa miguu umbali mrefu, toka mlalo hadi Tanga mjini katika harakati za kudai uhuru leo useme wazee wako wa new street ndo waliotuletea uhuru........!!!!!

Zumbe; Uko sawa kabisa ndugu yangu. Kuna maradhi mapya ya kudhani kuwa mikoani kulikuwa na magodoro tuu. Vichwa vyote vilikuwa kwenye familia moja. Ndio historia inayopigiwa debe hapa. Uko sawa kabisa. Hela ambazo hawa WAJANJA walizokuwa wanachota toka WANACHAMA wa mikoani (wanaita Matawi) wala hazisemwi. Ukiangalia kama Dar walipigana hata kajivita na wakoloni HAMNA, kama Dar hata wali-harass wauza watumwa HAMNA, au labda Dar wali-support vita kama Majimaji, HAMNA. Mkwawa kapigana jamaa wananunua samaki ferry. Leo ndio wanaosema eti wazee wetu mikoani walikuwa bongolala!!!!! Ila jamaa yao mmoja tuuu. Wabasema kua uyaone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…