Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Shariff Ritz,

Unajua mtu asomjua ndugu yetu Nguruvi3,anaweza akapatwa na hamaki nyingi!ahaha!!

Yeye ni bingwa wa PR na Propaganda, nafikiri alisomea Russia enzi ile ya USSR/Communism!?ahaha!!

Lakini mimi sitaki leo "kumchokoza" saana,ndugu yangu wa Kicheba,asije kuninyima lile "pakacha letu"!ahaha!!

Halafu pia nimekumbuka,yakuwa ni juzi tu nimetoka kumtaka radhi Muheshimiwa Nguruvi3!

Mpe salaam ndugu yetu Maulaga. Alifika Kilwa amepatwa na huzuni nyingi alipoona ile "Misikiti mikubwa" ya pale. Ati alijiuliza mbona majina ya Wajenzi/Wafanyakazi hakuyaona,aliona tu majina ya Wasimamizi wa ujenzi!?

Mjulishe na siku nyingine akatembelee na pale Bagamoyo,Zanzibar na kwingineko kwingi mno, ili akajionee na yale Makanisa makubwa mno yaso mfano, nao pia hawajaandika nani walokua wafanyakazi. Lakini tunaona tu majina ya Makasisi wa Kizungu walosimamia ujenzi ule!?....Watu weusi wana taabu nyingi hapa duniani!ahaha!!

Ahsanta Al Akhiy.
 

Al Akhiy gombesugu,

Tafikisha salaam Inshaalah kwa ndugu yetu maulanga.
 
Last edited by a moderator:
Hivi mumesoma vizuri nilichoandika? Mbona nimemnukuu Mohamed na Ziddy kila mara.
Halafu kuna sehemu nimefanya connection kama sehemu ya analysis. Ndivyo wenye weledi wasiolishwa ngano, wasiokubali fitna, urongo na uzushi wanavyofanya, yaani lazima mtu atumie akili.

Kwahiyo someni vizuri mtaona si kila mahali lazima iwekwe link, kuna njia nyingi za kuandika.

Ninawashangaa sana akina Ritz, Gombesugu na Sideeq. Eti leo mnaomba ushahidi. Hivi si kituko hiki !
Mumueshindwa kumwambia Mohamed alete ushahidi na mnafahamu hivyo mnaoomba wangu.
Hivi mumesahau kuwa kitabu kizima na paper za Mohamed zimejaa ''INASEMESEKANA, INAWEZEKANA, ILISEMWA'' hayo hamyaoni.

Nitapiga mfupa, Mwambie Mohamed ajibu hoja. Shariff samahani kama kwa kukujibu nimekuudhi ni siku nyingi sana sijajibu hoja zako.
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Nahisi umepata kiji-glass japo kiduchu W'end hii,kwa hiyo nakusihi upande kitandani kuyaa halafu tutazungumza kesho ndugu yangu kwa ustaarabu!?

Niwie radhi Muungwana kama umekereka na kauli yangu hii nyepesi kwako.

Ahsanta.

Cc;Ritz
 
nguruvi nimekusoma na bado nakusoma, kwanza nikushukuru kwa Darsa matata sana unalotupatia humu pamoja na wachangiaji wengine hususan Jasusi Mag3 nanreen WildCard Nyambala Mzee Mwanakijiji na wengineo,msichoke kutoa darasa juu ya upotoshaji wa makusudi,kuhusu mzee wetu MS najua vema kuwa huwa hajibu hoja hata anapoulizwa swali,hili linatoa picha sisi wenyewe kuchekecha makapi na ngano.Narudia tena Asante kwa darsa,endelea kupiga mipini
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3,

Wala ujaniudhi ndugu yangu hii minakasha ndiyo ugonjwa wangu hata kama hatukubaliani katika hoja zetu bado tutakuwa wamoja wote ni Watanzania.

Kila mmoja atabaki kuwa na misimamo yeke kuhusu haya tunayojadili nadhani unajua mimi na wewe tulivyo.

Tusemezane...pumzika w/end hii mambo mengi.
 
Last edited by a moderator:

Prishaz,

Mbona unatutenga pamoja kuwa hatupo kwenye orodha yako hakuna ulichojifunza japo kiduchu kutoka kwa Ritz, gombesugu, ha haa haaa.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu hatuna haja ya kugombea fito wakati tunajenga banda moja( Hakuna Mungu wa mkristo au Muislam ) sote tunaabudu Mungu mmoja na zaidi ukiangalia Ismail ambae ni mtoto wa mjakazi kwa sara ndo baba wa uislam na huo ni uzao wa ibrahim someni maandiko matakatifu
 
Sheikh Mohammed, na wanajamvi
Asalaam alaykum Al Akhiy
nimewahi kusikia mwalimu nyerere (a.k.a baba wa taifa )na wale wazee waliwahi kufunga saum siku zile za mapambano ya uhuru jee sheikh unaweza kutupa kisa chake kiduchu
.natanguliza samahani kwa uchechefu wangu huu


Ahsanta.
Bcc; Ritz
 
Prishaz,

Mbona unatutenga pamoja kuwa hatupo kwenye orodha yako hakuna ulichojifunza japo kiduchu kutoka kwa Ritz, gombesugu, ha haa haaa.

Ritz niwie radhi natumia kamchina ndio nikataja wachache lkn nikaongeza na wengineo,najifunza kwa kila mmoja wewe ukiwamo pamoja kunichekesha wakati mwingine ila gombesugu nampongeza sana kwa uungwana wa uandishi wake anavutia kusoma.
 
Last edited by a moderator:

Gombesugu; Kwanza una-over-react. Pili nilikuwa na-react na swali la muulizaji. Tatu, nilimwambia kitu kilichowahi kusemwa humu JF kuwa UDSM hawatoi kitabu cha mzee MS kama reference. Nne sina nitakachofaidi kuuchukia uislamu. Tano, hayo unayoyasema siyo ya kweli na ni matayarisho yako kama siku zote ili unitusi. Go ahead haitakuwa umeanza leo.
 


4.,unasema huna utakachofaidi ukiukana uislam?
Hueleweki,una-kihate kitu unachojinasibisha kukipenda?haingii akilin hata kidogo..
Tatizo umeacha kuzungumza hoja,
 

Gombesugu; Vita ni akili sio misuli pia yake. Ukijua udhaifu wa adui yako inakusaidia kupanga jinsi ya kupamabana naye. Naposema psychology hapa ni kwamba mshindani wako akishajua;

1. hakuna umoja katika nyie (kila siku ni vita baina yenu)
2. hakuna nidhamu baina yenu (kila siku ni kutukanana na viongozi wa dini zenu hadharani na kwenye media)
3. hakuna upangaji wa malengo mama (ni kelele za sisi, sisi, sisi.......)

anakuwa na mwanya wa kujua akutibulie wapi.

Shukran
 

Sidique; Nilivyomwelewa Nguruvi, na mimi pia hii paper ya Dr Ziddy nilishaisoma, hailekelekei kwamba sheikh aliwapa fair hearing TANU kama unavyomrai Nguruvi. Jaribu kuisoma hiyo paper. Hakuna mahali sheikh amehudhuria na kutoa Faatiha kwenye mikutano ya TANU, ila alifanya hivyo kila mara kwa mikutano ya wanafunzi wake ambayo ilikuwa pinzani kwa TANU ndipo hadi akaonywa na huyo rafiki yake ambaye ni Mkomoro. Hii ilikuwa punde baada ya kurudi toka kutafuta hiyo university kule Egypt. Jaribu kupata hiyo paper, la sivyo hamtaelewana na Nguruvi anaongelea nini.
 

Gombesugu; Turkey ni 90% moslems. Saudia haitofautiani na namba hiyo, tena yapita. Lakini Saudia walijikomboa toka kwa waturuki. Angola hali kadhalika. German na Poland Jee? iwavyo vyovyote vile hoja na ushauri niliompa Uthman bado una mashiko.

Samahani kwa uchefuchefu wangu
 
Kuongea na Mkristu juu ya mfumo kristu Tanzania ni sawa na kuopngea na Mbuzi au ng'ombe unadhani atakusikia?Dawa kubwa ni action since action speaks more than words@all Christians in this Christian Forum!
 
Wickama, kuna wale ambao wamesoma paper ya Ziddy na wanaelewa kile alichokieleza.
Kinachofanyika ni jitihada za makusudi kabisa za kuficha baadhi ya ukweli ilimradi usije haribu mambo mengine.

Kuna wale ambao hawajaisoma paper wanabisha tu kwasababu basi kasema flani huyo ni mpinzani.
Kuna wale waliosoma na kwabahati mbaya wamesoma kama riwaya bila chembe ya fikra, hawa ndio waporomosha mitusi

Narudia tena, katika yote ninayoeleza nimewanukuu Mohamed Said na Issa Ziddy.
Hakuna mahali nimenukuu Nyerere au mtu mwingine.Kinachoshangaza watu hawawezi kutetea kile kilichoandikwa na ''waislam'' lakini ni wepesi sana wa kupiga nderemo na vifijo kwa kile wanachokisikia tu kwavile kinamhusu asiye mwislam.

Ziddy anasema kuwa kulikuwa na ugomvi wa KISIASA kati ya Mufti Amir na wanafunzi wake.
Mmoja wao alikuwa ni Sheikh Cahurembo. Tunajua mufti Amir alikuwa mwanachama wa TANU achilia mbali AA na TAA.
Alikuwa katika TAA sub Political committee (Mohamed).
Swali ni kuwa kulikuwa na ugomvi gani wa Kisiasa? na tuna uhakika haukuhusu TANU. Ni upi huo?

Pili, Ziddy anasema Sheikh Amir alirudi na pound milioni 55 za ahadi kutoka Misri ili kujenga Chuo kikuu.
Katika safari hiyo aliandamana na Tew S Tewa ambaye alikuwa waziri katika serikali ya Nyerere.

Kwa kutumia akili za kawaida kabisa zisizomhitaji Mohamed kwa wenzetu wasoma riwaya, haiwezekani Nyerere aruhusu afisa wake aende kwenye ziara asioijua wala kuitaka.
Swali ni kuwa, kama Nyerere hakutaka chuo kikuu akina Tewa walikwenda kama mawaziri kwa idhini ya nani?

Tatu, Tunajua kuwa kiwanja kilichokuwa kijengwe chuo kikuu ni kile cha Chang'ombe.
Kiwanja hicho kina mgogoro wa kuuzwa baina ya waislam. Na wala serikali haijawahi kuingilia kati mauzo yake.
Swali ni kuwa, Nyerere na ukatoliki wanahusika vipi na vurugu za kiwanja hicho ambacho kimeuzwa na kununuliwa na waislam wenyewe kwa wenyewe?

Nne, Sheikh Amir aliporudi alionywa na sheikh Comorian kuacha mawaidha ya kisiasa na kubadili mwelekeo.
Je, ni kwanini sheikh Comorian alimkanya mwasisi wa TANU asiendelee na siasa ili hali ni siasa hizo zilifanyika misikitini kuikomboa nchi.Kuna mawaidha gani yaliyokuwa ya hatari ambayo Comorian aliona si muafaka kuendelea nayo.

Tano, Sheikh Amir alipewa nafasi ya kuwa katika serikali kama kiongozi tena baraza la mawaziri.
Alikataa kwasababu hakupenda siasa na alitamani kuendeleza mambo ya dini.
Swali, je, sheikh Comoriana alipomuonya asiendelee na mawaidha ya siasa, ilikuwa ni mawaidha gani na kwanini alikuwa na mawaidha ya siasa ili hali alikataa kuendelea na siasa?
Je,kulikuwa na jambo gani alililokuwa analifanya vichochoroni linalofanana na siasa na wala si siasa ile ya Nyerere kumtaka kuwa waziri?

Sita, Mikoa mitatu ya Tanga, Bukoba na Iringa ilipojitoa EAMWS sheikh Amir alijaribu kusuluhisha.
Moja ya madai yao ni kuwa na uwazi wa matumizi ya fedha makao makuu ambako Shikh Amir alikuwa kinara.
Kwanini mikoa hiyo ilitilia shaka na kuweka sharti la uwazi wa fedha makao makuu na kwa sheikh ambaye anaitwa Walii leo hii?

Saba, Kwavile EAMWS ilianza katika miaka ya 1945 na makao makuu yakiwa Mombasa, na kwavile ''ilipigwa'' marufuku na Nyerere wa Tanganyika(Mohamed), swali ni kuwa kwanini basi ilikufa huko makao makuu baada ya kuzuiwa Tanganyika?

Nane, Kwavile famililia ya Sykes ilikuwa na mkono katika uanzishwaji wa Dawaiya fi Tanganyika na Al-jamiyyatu Islamiyya fi Tanganyika na kwa vile sheikh Amir alikuwa mwanachama wake na kuna nyakati Abdul alikuwa katibu wa moja ya hizo taasisi, swali, ni akina nani waanzilishi wa AMNUT na je hawakuwa na uhusiano na Mwalimu wao Amir?

Nimewasamehe watakaotanguliza matusi kama mzee wetu, nawashukuru watakaona busara na kuacha hekima itamalaki.

Khair Inshallah naendelea kunya glasi ya maji ya ndimu na asali kama alivyonena Gombesugu. Lau kana haitalate afueni nitapata kikombe cha shurbati cha Shariff Ritz!

Nitatulia mavune yakiondoka lakini sitatulia nikiona uongo, upotoshaji na uzandiki kwa miaka mingine 15 ukitamalaki, never!!
 
Ndugu yangu gombesugu, hukuwa na sababu yoyote ya kupitisha ujumbe huu kwa mkuu wangu Ritz! mtindo huu anautumia sana mzee wetu Mohamed anapotaka kuwapelekea ujumbe watu wake aliowaweka kwenye ile "list" yake, sasa sijui na wewe ndugu yangu umeniweka kwenye "list" yako kama ile ya mzee wangu Mohamed? Kwa ufupi nilipoandika mambo ya Kilwa kisiwani sikuwa na kusudi lolote baya dhidi ya uislam na miskiti, nilitaka kuonesha jinsi ambavyo historia isivyorekodiwa sawa kwa watendaji wote! sina chuki na uislam kwani ni mfumo wa maisha na imani ambayo mtu hawezi kuiondoa hata kama haipendi!wala siwezi kulinganisha uovu bianafsi wawaovu kwa kuangalia dini zao kwani hawafanyi hivyo kwa kufuata matakwa ya imani zao. Nimewahi kuwashuhudia majambazi na wauaji wakubwa wakitoa sadaka maalum makanisani huku wakishangiliwa na waumini wa dini husika! Yale mapiramid kule Misiri yalijengwa na watumwa ambao majina yao hayajaandikwa popote, nani aliijenga Roman empire? nani aliisimamisha Ottoman empire? nani alijenge "great wall" kule China? je wote wamrekodiwa kwa uzito sawa? nani leo anawatetea? je tunayafahamu majina yao, je walikuwa na majina? au walijulikana kwa namba?
 
4.,unasema huna utakachofaidi ukiukana uislam?
Hueleweki,una-kihate kitu unachojinasibisha kukipenda?haingii akilin hata kidogo..
Tatizo umeacha kuzungumza hoja,
Mkuu THE BIG SHOW, pole sana ndugu yangu na usumbufu mlioupata huko Mtwara, kwa vyovyote serikali imepata ujumbe hata kama itaendelea na ukaidi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…