Sidique; Nilivyomwelewa Nguruvi, na mimi pia hii paper ya Dr Ziddy nilishaisoma, hailekelekei kwamba sheikh aliwapa fair hearing TANU kama unavyomrai Nguruvi. Jaribu kuisoma hiyo paper. Hakuna mahali sheikh amehudhuria na kutoa Faatiha kwenye mikutano ya TANU, ila alifanya hivyo kila mara kwa mikutano ya wanafunzi wake ambayo ilikuwa pinzani kwa TANU ndipo hadi akaonywa na huyo rafiki yake ambaye ni Mkomoro. Hii ilikuwa punde baada ya kurudi toka kutafuta hiyo university kule Egypt. Jaribu kupata hiyo paper, la sivyo hamtaelewana na Nguruvi anaongelea nini.
Wickama, kuna wale ambao wamesoma paper ya Ziddy na wanaelewa kile alichokieleza.
Kinachofanyika ni jitihada za makusudi kabisa za kuficha baadhi ya ukweli ilimradi usije haribu mambo mengine.
Kuna wale ambao hawajaisoma paper wanabisha tu kwasababu basi kasema flani huyo ni mpinzani.
Kuna wale waliosoma na kwabahati mbaya wamesoma kama riwaya bila chembe ya fikra, hawa ndio waporomosha mitusi
Narudia tena, katika yote ninayoeleza nimewanukuu Mohamed Said na Issa Ziddy.
Hakuna mahali nimenukuu Nyerere au mtu mwingine.Kinachoshangaza watu hawawezi kutetea kile kilichoandikwa na ''waislam'' lakini ni wepesi sana wa kupiga nderemo na vifijo kwa kile wanachokisikia tu kwavile kinamhusu asiye mwislam.
Ziddy anasema kuwa kulikuwa na ugomvi wa KISIASA kati ya Mufti Amir na wanafunzi wake.
Mmoja wao alikuwa ni Sheikh Cahurembo. Tunajua mufti Amir alikuwa mwanachama wa TANU achilia mbali AA na TAA.
Alikuwa katika TAA sub Political committee (Mohamed).
Swali ni kuwa kulikuwa na ugomvi gani wa Kisiasa? na tuna uhakika haukuhusu TANU. Ni upi huo?
Pili, Ziddy anasema Sheikh Amir alirudi na pound milioni 55 za ahadi kutoka Misri ili kujenga Chuo kikuu.
Katika safari hiyo aliandamana na Tew S Tewa ambaye alikuwa waziri katika serikali ya Nyerere.
Kwa kutumia akili za kawaida kabisa zisizomhitaji Mohamed kwa wenzetu wasoma riwaya, haiwezekani Nyerere aruhusu afisa wake aende kwenye ziara asioijua wala kuitaka.
Swali ni kuwa, kama Nyerere hakutaka chuo kikuu akina Tewa walikwenda kama mawaziri kwa idhini ya nani?
Tatu, Tunajua kuwa kiwanja kilichokuwa kijengwe chuo kikuu ni kile cha Chang'ombe.
Kiwanja hicho kina mgogoro wa kuuzwa baina ya waislam. Na wala serikali haijawahi kuingilia kati mauzo yake.
Swali ni kuwa, Nyerere na ukatoliki wanahusika vipi na vurugu za kiwanja hicho ambacho kimeuzwa na kununuliwa na waislam wenyewe kwa wenyewe?
Nne, Sheikh Amir aliporudi alionywa na sheikh Comorian kuacha mawaidha ya kisiasa na kubadili mwelekeo.
Je, ni kwanini sheikh Comorian alimkanya mwasisi wa TANU asiendelee na siasa ili hali ni siasa hizo zilifanyika misikitini kuikomboa nchi.Kuna mawaidha gani yaliyokuwa ya hatari ambayo Comorian aliona si muafaka kuendelea nayo.
Tano, Sheikh Amir alipewa nafasi ya kuwa katika serikali kama kiongozi tena baraza la mawaziri.
Alikataa kwasababu hakupenda siasa na alitamani kuendeleza mambo ya dini.
Swali, je, sheikh Comoriana alipomuonya asiendelee na mawaidha ya siasa, ilikuwa ni mawaidha gani na kwanini alikuwa na mawaidha ya siasa ili hali alikataa kuendelea na siasa?
Je,kulikuwa na jambo gani alililokuwa analifanya vichochoroni linalofanana na siasa na wala si siasa ile ya Nyerere kumtaka kuwa waziri?
Sita, Mikoa mitatu ya Tanga, Bukoba na Iringa ilipojitoa EAMWS sheikh Amir alijaribu kusuluhisha.
Moja ya madai yao ni kuwa na uwazi wa matumizi ya fedha makao makuu ambako Shikh Amir alikuwa kinara.
Kwanini mikoa hiyo ilitilia shaka na kuweka sharti la uwazi wa fedha makao makuu na kwa sheikh ambaye anaitwa Walii leo hii?
Saba, Kwavile EAMWS ilianza katika miaka ya 1945 na makao makuu yakiwa Mombasa, na kwavile ''ilipigwa'' marufuku na Nyerere wa Tanganyika(Mohamed), swali ni kuwa kwanini basi ilikufa huko makao makuu baada ya kuzuiwa Tanganyika?
Nane, Kwavile famililia ya Sykes ilikuwa na mkono katika uanzishwaji wa Dawaiya fi Tanganyika na Al-jamiyyatu Islamiyya fi Tanganyika na kwa vile sheikh Amir alikuwa mwanachama wake na kuna nyakati Abdul alikuwa katibu wa moja ya hizo taasisi, swali, ni akina nani waanzilishi wa AMNUT na je hawakuwa na uhusiano na Mwalimu wao Amir?
Nimewasamehe watakaotanguliza matusi kama mzee wetu, nawashukuru watakaona busara na kuacha hekima itamalaki.
Khair Inshallah naendelea kunya glasi ya maji ya ndimu na asali kama alivyonena Gombesugu. Lau kana haitalate afueni nitapata kikombe cha shurbati cha Shariff Ritz!
Nitatulia mavune yakiondoka lakini sitatulia nikiona uongo, upotoshaji na uzandiki kwa miaka mingine 15 ukitamalaki, never!!