Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Muheshimiwa Nguruvi3,
Nashukuru ndugu yangu. Naona kuna stalemate fulani ambayo nakhis inasababishwa na upande wenu ambao wewe binafsi ndo Kiongozi wao Mkuu.
Tangia lini nyinyi mkawa na hishma,mapenzi au kuwathamini WaZanzibary!? Au kwa sababu hapa mnaona kuna agendas na propagandas zenu,ndo mnaleta hayo machozi ya mamba na zile "hekima/ujanja wa Mwalimu"!?
Mimi binafsi kwa sasa nina majambo/vijishughuli vya kibaruani. Kwa hiyo takujibu kiduchu tu.
Binafsi najua yakuwa hizo mnazoita "hoja"/"maswali" yenu takriban yoote;pana persuasive evidences kwenye maandiko mengi ya Sheikh Mohammed kuwa yamejibiwa kiundani tena Kitaaluma.
Kwa kuwa mpaka sasa hapajaonekana/kuthibitishwa "Ugaidi,uchochezi na uhaini" na Yericko&Co dhidi ya Sheikh Mohammed...ni muhimu pia tukaangalia upande wa pili wa shilingi hiyohiyo!?
Nakuwekea maswali hapa chini kiduchu,tafadhali nakuombeni wewe binafsi na wafuasi wako mtupatie majibu ya kina. Baada ya hapo nitajaribu kumsihi Sheikh Mohammed akupeni majibu kwa yale mlotaka na kulazimisha ati mjibiwe upya.
Najua Muheshimiwa Nguruvi3;unapenda saana kutaja "mikoba ya Ibadan" ili kuwafurahisha wafuasi wako watiifu na kumtafir Sheikh Mohammed.
- Tunaomba Mwanakijiji aje hapa jamvini/au nyinyi wenzie kututhibitshia kwa kina,na ikiwezekana kutuonyesha nyaraka zozote alizonazo anazozijua;yakuwa Sheikh Mohammed ni Recruiter wa Muslim Brotherhood kwa hapo Tanzania na anadhaminiwa na "Kigogo fulani wa Shirika la Umma"...kama yeye Mwanakijji alivyodai/anavyodai!?
- Tunahitaji pia huyo huyo Mwanakijiji au nyinyi mtuthibitishie yakuwa Sheikh Mohammed Said ni Member wa Muslim Brotherhood na ana mipango ya kuleta Islamic Sharia hapo Tanzania!?
- Mag3,aombe radhi rasmi hapa jamvini aukupitia kwa The Big Show-Mwana Mtwara,kwa Family ya Muheshimiwa Marehemu Lawi Nangwanda Sijaona kwa usumbufu wowote walioupata kutokana na zile khabar za uongo na uchochezi alizotoa huyo Mag3!?
- Yericko Nyerere au nyinyi mkiweza kumsaidia atuthibitshie yakuwa;Rais Jakaya Kikwete ni ndie anayemkingia kifua Sheikh Mohammed Said ili afanye/aendeleze "uchochezi" hapo nchini kama alivyodai hivi karibuni. Kwa kifupi hizi ni tuhuma nyingine nzito saana,ambazo huyu Yericko anaendelea kuleta bila ya kuhojiwa na yeyote hapa jamvini!?
- Yericko Nyerere;atutajie uhusiano wake au alionao na maslahi gani anapata yeye binafsi kutoka pale Amerikan Embassy D'Salaam!? Na je maslahi hayo yana uhusiano wowote au malipo ya yeye kuja kufungua huu uzi hapa Jamvini/Jf!? Je kuna watu/kikundi kinamtumia kuleta mfarakano hapo nchini!?...maana yeye binafsi alishatuambia yakuwa maofisa kadhaa wa State Depart walikwenda kumtafuta nyumbani kwake Mbutu. Pia ametujuza yakuwa haohao wa-Amerika ndo wafadhili wakubwa wa kitabu chake cha Khadith za Kigaidi(ambacho sisi soote tumekiona hapa jamvini,na wala hakistahili kuitwa kitabu,lakini wa-Amerika pamoja na akili zao nyingi wameamua kuacha yoote lakini kukifadhili tu!?).
- Je Yericko alikua na maslahi gani kwa Taifa pale alipobeba mikoba ya wale maofisa wa Ubalozi wa-Amerika kwenda nao Dodoma ili kushinikiza ile "Sharia ya Ugaidi" ipitishwe hapo, harakaharaka tena bila ya minyambuo ya kina na kitaaluma kutoka kwa Wabunge wala Serikali yetu maskini!?
Je umeshawahi kujiuliza ile mikoba alobebeshwa Yericko ya wale State Depart Officials kwenda nao Dodoma ili ku-Lobby ile "Sharia ya Ugaidi" ilikua ina nini ndani yake/imebeba kipi!?
Kwa hiyo mara nyingi kabla hujaleta ile kebehi ya mikoba ya Ibadan hapa jamvini;jiul;ize je na ile "mikoba ya Chamwino/Dodoma" nayo ilibeba nini,au huyo Yericko alibebeshwa nini kwenda Chamwino!?
Wewe binafsi na Wanajamvi wengi tunajua,yakuwa huyo Yericko hana uwezo wala Ilm(tafadhali hapa sisemi kwa kumbeza asilan!),ya kujua kiundani au kujadili inner workings za State Depart and nature of Amerikan Foreign Policy and its intent!?...sasa alidhirika vipi na kwa lipi mpaka kufikia yeye kuwa-support na kuwabebeba mikoba yao wale Manguli wa Uharamia the so called State Depart officials/Strategists mpaka kule Dodoma kwenda "kuwapasua vichwa" Wabunge wetu dhaifu maskini za Mungu!?
Kwa kifupi Muheshimiwa Nguruvi3;kwetu sisi kama ni Watanzania wenzenu hivyo vitu nilokutajia pia vinatusumbua kichwa, na pia hivyo kwetu sisi ndio Ugaidi,Uchochezi na Uhaini mkubwa kwa Taifa letu changa...unless kama tuna khitilafu ya tafsir ya hivyo vitu yaani Ugaidi,Uchochezi na Uhaini,na kama ni hivyo italazim tufungue Thread nyingine ili kujadili yayo kwa kina!?
Natumai ndugu yetu Pain Killer na Wana Mbagala wenzie,watajitahidi kuwa na Sabra kwa hizi rabsha kiduchu hapa barzani/jamvini!
Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu kiduchu.
Ahsanta.
Cc;Shariff Ritz,Al Khalifa The Big Show,Sahib Al Maarifa Boko Haram,JokaKuu
Wanaukumbi,
Nguruvi3, na Yericko Nyerere, tupeni majibu kubeba mikoba ya Chamwino kwenda Dodoma kupitisha sheria ya ugaidi, mpaka mkaandika na kitabu cha ugaidi.
Last edited by a moderator: