Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Muheshimiwa Nguruvi3,

Nashukuru ndugu yangu. Naona kuna stalemate fulani ambayo nakhis inasababishwa na upande wenu ambao wewe binafsi ndo Kiongozi wao Mkuu.

Tangia lini nyinyi mkawa na hishma,mapenzi au kuwathamini WaZanzibary!? Au kwa sababu hapa mnaona kuna agendas na propagandas zenu,ndo mnaleta hayo machozi ya mamba na zile "hekima/ujanja wa Mwalimu"!?

Mimi binafsi kwa sasa nina majambo/vijishughuli vya kibaruani. Kwa hiyo takujibu kiduchu tu.

Binafsi najua yakuwa hizo mnazoita "hoja"/"maswali" yenu takriban yoote;pana persuasive evidences kwenye maandiko mengi ya Sheikh Mohammed kuwa yamejibiwa kiundani tena Kitaaluma.

Kwa kuwa mpaka sasa hapajaonekana/kuthibitishwa "Ugaidi,uchochezi na uhaini" na Yericko&Co dhidi ya Sheikh Mohammed...ni muhimu pia tukaangalia upande wa pili wa shilingi hiyohiyo!?

Nakuwekea maswali hapa chini kiduchu,tafadhali nakuombeni wewe binafsi na wafuasi wako mtupatie majibu ya kina. Baada ya hapo nitajaribu kumsihi Sheikh Mohammed akupeni majibu kwa yale mlotaka na kulazimisha ati mjibiwe upya.

  • Tunaomba Mwanakijiji aje hapa jamvini/au nyinyi wenzie kututhibitshia kwa kina,na ikiwezekana kutuonyesha nyaraka zozote alizonazo anazozijua;yakuwa Sheikh Mohammed ni Recruiter wa Muslim Brotherhood kwa hapo Tanzania na anadhaminiwa na "Kigogo fulani wa Shirika la Umma"...kama yeye Mwanakijji alivyodai/anavyodai!?
  • Tunahitaji pia huyo huyo Mwanakijiji au nyinyi mtuthibitishie yakuwa Sheikh Mohammed Said ni Member wa Muslim Brotherhood na ana mipango ya kuleta Islamic Sharia hapo Tanzania!?
  • Mag3,aombe radhi rasmi hapa jamvini aukupitia kwa The Big Show-Mwana Mtwara,kwa Family ya Muheshimiwa Marehemu Lawi Nangwanda Sijaona kwa usumbufu wowote walioupata kutokana na zile khabar za uongo na uchochezi alizotoa huyo Mag3!?
  • Yericko Nyerere au nyinyi mkiweza kumsaidia atuthibitshie yakuwa;Rais Jakaya Kikwete ni ndie anayemkingia kifua Sheikh Mohammed Said ili afanye/aendeleze "uchochezi" hapo nchini kama alivyodai hivi karibuni. Kwa kifupi hizi ni tuhuma nyingine nzito saana,ambazo huyu Yericko anaendelea kuleta bila ya kuhojiwa na yeyote hapa jamvini!?
  • Yericko Nyerere;atutajie uhusiano wake au alionao na maslahi gani anapata yeye binafsi kutoka pale Amerikan Embassy D'Salaam!? Na je maslahi hayo yana uhusiano wowote au malipo ya yeye kuja kufungua huu uzi hapa Jamvini/Jf!? Je kuna watu/kikundi kinamtumia kuleta mfarakano hapo nchini!?...maana yeye binafsi alishatuambia yakuwa maofisa kadhaa wa State Depart walikwenda kumtafuta nyumbani kwake Mbutu. Pia ametujuza yakuwa haohao wa-Amerika ndo wafadhili wakubwa wa kitabu chake cha Khadith za Kigaidi(ambacho sisi soote tumekiona hapa jamvini,na wala hakistahili kuitwa kitabu,lakini wa-Amerika pamoja na akili zao nyingi wameamua kuacha yoote lakini kukifadhili tu!?).
  • Je Yericko alikua na maslahi gani kwa Taifa pale alipobeba mikoba ya wale maofisa wa Ubalozi wa-Amerika kwenda nao Dodoma ili kushinikiza ile "Sharia ya Ugaidi" ipitishwe hapo, harakaharaka tena bila ya minyambuo ya kina na kitaaluma kutoka kwa Wabunge wala Serikali yetu maskini!?
Najua Muheshimiwa Nguruvi3;unapenda saana kutaja "mikoba ya Ibadan" ili kuwafurahisha wafuasi wako watiifu na kumtafir Sheikh Mohammed.

Je umeshawahi kujiuliza ile mikoba alobebeshwa Yericko ya wale State Depart Officials kwenda nao Dodoma ili ku-Lobby ile "Sharia ya Ugaidi" ilikua ina nini ndani yake/imebeba kipi!?

Kwa hiyo mara nyingi kabla hujaleta ile kebehi ya mikoba ya Ibadan hapa jamvini;jiul;ize je na ile "mikoba ya Chamwino/Dodoma" nayo ilibeba nini,au huyo Yericko alibebeshwa nini kwenda Chamwino!?

Wewe binafsi na Wanajamvi wengi tunajua,yakuwa huyo Yericko hana uwezo wala Ilm(tafadhali hapa sisemi kwa kumbeza asilan!),ya kujua kiundani au kujadili inner workings za State Depart and nature of Amerikan Foreign Policy and its intent!?...sasa alidhirika vipi na kwa lipi mpaka kufikia yeye kuwa-support na kuwabebeba mikoba yao wale Manguli wa Uharamia the so called State Depart officials/Strategists mpaka kule Dodoma kwenda "kuwapasua vichwa" Wabunge wetu dhaifu maskini za Mungu!?

Kwa kifupi Muheshimiwa Nguruvi3;kwetu sisi kama ni Watanzania wenzenu hivyo vitu nilokutajia pia vinatusumbua kichwa, na pia hivyo kwetu sisi ndio Ugaidi,Uchochezi na Uhaini mkubwa kwa Taifa letu changa...unless kama tuna khitilafu ya tafsir ya hivyo vitu yaani Ugaidi,Uchochezi na Uhaini,na kama ni hivyo italazim tufungue Thread nyingine ili kujadili yayo kwa kina!?

Natumai ndugu yetu Pain Killer na Wana Mbagala wenzie,watajitahidi kuwa na Sabra kwa hizi rabsha kiduchu hapa barzani/jamvini!

Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu kiduchu.

Ahsanta.

Cc;Shariff Ritz,Al Khalifa The Big Show,Sahib Al Maarifa Boko Haram,JokaKuu

Wanaukumbi,

Nguruvi3, na Yericko Nyerere, tupeni majibu kubeba mikoba ya Chamwino kwenda Dodoma kupitisha sheria ya ugaidi, mpaka mkaandika na kitabu cha ugaidi.
 
Last edited by a moderator:
Wewewewewewewewe
Wickama,
Kweli ni sahib wangu ahsante sana.

Basi ngoja nikupe kitu ni zaidi ya miaka 40 toka nimepiga ile nyimbo
''Things We Said Today'' lakini nakumbuka chords zake...

Opening G Minor, C Major, F kisha G.

Utamu uko kwenye hiyo opening kuna vamping kali sana ya George
Harrison.

Ahsante sana.

Sijui unatumia browser gani. Kuna moja wanaita SLIMBROWSER (mimi naitumia), hiyo ina facility ya ku-download moja kwa moja hizo video bila mzunguko wala maswali ya ku-register na ni fast. Jaribu ku-install uijaribu.

Good Luck
 
Wanakumbi,

Huyu hapa na katika wale ndugu zetu ambayo waongozwa na chuki dhidi ya Wazee wa Mzizima, hebu ngoja tudadavue bayana zake kiduchu.
Hapo juu ndugu yetu amekiri kuwa TANU kilikuwa chama cha Waislam, ha ha haaa, baada ya kukiri anajaribu kumtafutia nafasi Nyerere kuwa ndiyo aliifanya TANU kikawa na taswira ya kitaifa, wakati Nyerere kaanza siasa na wazee wa Dar es Salaam 1952, Wazee wa Dar es Salaam wameanza kufaamika kimataifa acha kitaifa wakati wa AA 1930 wakati Nyerere ana miaka 8 sembuse TANU soma chini hapa.
Kleist Sykes (1894 - 1949) was a Tanganyikan political activist. He helped formed the Tanganyika African Association.
Sykes was born in Pangani to father Sykes Mbuwane, a Zulu mercenary hired by the German Empire, and a Nyaturu mother. After his father died, Sykes moved with his godfather, Effendi Plantan, to Dar Es Salaam, and would later fight for the Germans in the First World War.[SUP][1][/SUP]
After the war, Sykes worked for the Tanganyika Railway. He met Dr. James Aggrey, Ghanaian teacher, who inspired Sykes to form the Tanganyika African Association (AA) in 1929, along with friends including Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu and Raikes Kusi. In the 1930s, AA members built the organization's headquarters at New Street, where the Tanganyika African National Union would later be created in 1954.[SUP][1][/SUP]
Sykes was the first African to join the Tanganyika Chamber of Commerce, and the second African to serve in colonial Dar es Salaam's Municipal Council.[SUP][1][/SUP]
Sykes had three sons, Abulwahid, Ally, and Abbas, who would also have prominent careers in Tanzania.[SUP][1][/SUP]
Wewe ndugu yangu ktk uraia una upeo mdogo sana...mtabaki kuwa careers tuu wa elimu.Mtu anaweza kupitisha script ktk generations zenu hata 6 bila nyie kuzijua, ila akaja kafir mmoja smart ktk vizazi akadecode scripts na matamshi mliyokaririshwa na akazijua na kuelewa alichoagizwa ,hata km ni kuwaua wote.Quran na Haddith zimekuwepo, na waislam wamezisoma na kuzikariri ili wahifashi,wamepewa motisha kuwa ndio dini ya kweli,na maandishi yae hayajawahi chokonolewa.Ila haichukui muda kwa kafiri kuvisoma hivyo vitabu na kuona shida nyingi sana ndani yake.Kuona vitu vingi vinavyopingana na Mungu wa Abrahamu.

Ulichoandika hakionyeshi popote kuwa waislam walishaifikisha TANU wala AA, TAA popote kimataifa.kupigana vita kama individual hakumaanishi kuwa taasisi uliyopo tayari imeshakuwa internationally recognised.Hakuna mahali panaonyesha hizo AA,au TAA au chochote kufanya kitu kimataifa.Na hii ni wazi hata Tanganyika yenyewe hakikuwa kimefika mahali...mikoa walikuwa na vyama vyao vya ushirika ambavyo ndivyo vilikuwa pia km vya kisiasa.

Soma hapa issue ya TANU mkoani kilimanjaro.Utaona jinsi hagi TANU na Nyerere walivyotumia hadi devide and rule na baadaye kuwahonga mangi wepesi ili TANU ikubalike ktk Mkoa wa Kilimanjaro.
[..............]Chaga people - Wikipedia, the free encyclopedia



Hapa chini unaelezea habari za uongo kabisa kutokana na fikra zako.

Nyerere asingeweza kufanya chochote alikuwa Mkirsto peke yake kama kungekuwa na udini asingeza hata kakaa pamoja na hawa wazee hebu msome chini hapa Nyerere mwenyewe.

Nadhani umeona Wazee walivyokuwa na mahaba na a Nyerere wakati wa harakati za uhuru.
Uongo upi sasa mbona mwenyewe unanithibitisha kwa quotes zako kuwa ni mkwel?My friend I know Islam and Muslims than you can ever imagine...Wazee wa kiislam wamekuwa wakitekwa kirahisi sana na kutumika sana,wengine kwa uzuri wengine kwa ubaya.Ni kuwavika kilemba cha ukoka na kuonyesha kuheshimu dini yao...Nyerere alikwenda mbali hadi kufuturu nao...kijana msomi mwenye akili ya kutisha,anayeweza ongea "Kikristu na Mzungu na kusikilizwa kwa heshima".Nyerere alishweza ongea na wazungu kwa ushawishi bila waongopa wala wabembeleza , wazee wa kiislam wasiojua utamaduni wa kizungu ni vipi wangemwacha? Wazungu wenyewe walimwamini Nyerere bila mpenda.Walimchukia ila walijua ni mwafrika pekee ambaye hawezi fanya ya maumau,wakaona ni bora zimwi likujualo kuliko hao akina sykes na wengine.Chama chao hakikua chama zaidi ya Kaumoja ka wazee wa kiislam ch akupigia soga.Hakikuwa kitu km Simba na Yanga...club ambazo hazijawa civilized kwa miaka yote.Sura tuionayo ni rangi tuu ya jitihada za watu wa mikoani.

Mahaba yapi unasema?Wale wazee walimwona msomi anaweza wawakilisha wasipoweza fika na kuwakilisha wazo la maana.Nyerere alikuwa akiwaelisha huku akishirikiana nao...na kufuata baadhi ya njia zao ili aweze kaa nao ,aliwashika wengi wa wale waliodhani anakaribia kuwa mwislam na hivyo kuupa heshima.I have seen it...nimekaa na waislam...nimesikia vilio vyao wanapokuta Vijana makini wanaofanya utendaji kwa ufanisi na kujua mambo...wengin huwa akili zao na roho zao huwatuma wajiulize kwanini sasa asiwe muislam km allah kamjalia ufahamu mkubwa...Mmoja niliwahi fanya nae kazi na nilimsaidia sana..mwishowe akaniambia,una elimu nzuri,unajua kazi yako, na allah,unajua maandiko vyema kwanini sasa uifuati dini yake?Nikaamulize kwanini usijiulize hilo swali kwa staili hiii."Hivi huyu mtu anamfuata Mungu gani aliyemsaidia kuwa na hivi vipawa?".Its only reasoning can be very wrong.
Wanakumbi huyu ndugu yetu sijui kaipata wapi kuwa wakati wa harakati za uhuru wa Tanganyika nusu ya Watanzania walikuwa hawajuhi kiswahili, kwa hiyo unataka kutuambia Nyerere alikuwa anajua kuongea lugha zote za Tanzania, ha ha haaa...nadhani wanaukumbi mmeona hoja dhahifu za huyu ndugu yetu. soma chini hapa harakati za TANU Tanga.
ILIKUWA ni huko Tanga tu katika historia ya Tanganyika kuwa dhana mpya katika siasa zaidi ya ule ubwana wa Wazungu uliongezwa katika uhusiano baina ya Waafrika na Waarabu. Dhana hii iliongezwa ndani ya mfumo wa siasa za Tanganyika ili kuwakinza Waafrika katika siasa. Hiki kilikuwa kitu ambacho Waafrika walikuwa hawajapambana nacho. Kwa zaidi ya karne moja walikuwa wamezoea ubwana wa Wazungu. Jimbo la Tanga lilibarikiwa na kuwa na Waafrika walioelimika sana. Waafrika hawa walikuwa kutoka kabila la Wabondei. UMCA ilikuwa imehama kutoka Zanzibar kwenda Magila katika Jimbo la Tanga mwaka 1875. Ukristo ulianzishwa na kustawi katika nchi ya Wabondei, na vivyo hivyo nafasi za elimu kwa watoto wa Wabondei. Katika lile wimbi la kuwania nafasi za elimu, watoto wengi wa Kiislamu walibatizwa. Ni jambo la kawaida miongoni mwa Wabondei kukuta majina kama Peter Saidi au John Ramadhani. Huu ni ukumbusho wa damu ya Kiislam katika Wabondei. Wabondei wengi walikwenda Makerere College na siasa za kizalendo zilipoanza baada ya Vita Kuu ya Pili, Wabondei walikuwa wamejaa katika utumishi wa serikali ya kikoloni. Gurudumu la historia ya Tanganyika likizungushwa na baadhi ya Wabondei, maarufu miongoni mwao wakiwa watu kama Martin Kayamba aliyejikomba sana kwa wakoloni, George Magembe mtu ambae huku alikuwa hayuko wala kule hayuko, hujui kama yupo na wazalendo au na wakoloni, Stephen Mhando; mzalendo mwenye msimamo mkali na na mdogo wake Peter.
Wabondei walikuwa ndiyo walimu, makarani, wakalimani mahakamani na maofisa wa ustawi wa jamii katika serikali ya kikoloni. Hili lilikuwa tabaka maalum la Waafrika, waliosomeshwa na wamishonari kuitumikia serikali ya kikoloni na katika kufanya hivyo kulitumikia Kanisa na Ukristo, uhusiano ambao ulikuwa wenye manufaa kwa pande zote mbili zilizokuwa zikishirikiana. Ilikuwa vigumu sana kwa Wabondei kutokana na upendeleo huo wasifikirie kwamba wana uhusiano maalum na Kanisa na serikali ya kikoloni. Hawa Waafrika wasomi kutoka shule za misheni na Makerere walikuwa watiifu kwa taasisi mbili zanye nguvu nchini, yaani serikali ya kikoloni na Kanisa. Kwa ajili hii basi, ilibakia kwa Wadigo Waislam wasiokuwa na elimu kama elimu ilivyokuwa ikiitikadiwa, kuunda TANU na kuongoza harakati za kudai uhuru.
Wamishionari waligundua kuwa Wadigo walikuwa wagumu sana kubatizwa na kuingizwa kwenye Ukristo kwa sababu ya imani yao thabiti katika Uislam. Kwa hiyo Wadigo hadi hii leo wamebakia kuwa kabila la Waislam. Baada ya kuukuta Uislamu umeimarika vyema katika pwani ya Tanga, wamishonari kwa kukataa kuhasimiana na Waislam, walianzisha misheni zao ndani zaidi mbali na pwani sehemu inayojulikana kama Misheni ya Magila. Hapa UMCA ilianzisha shule na hospitali. Wadigo walishikilia imani yao ya Kiislamu na wakabakia nyuma katika elimu kwa sababu ya kukataa kwao Ukristo. Kwa jili hii wakajinyima nafasi za kazi za madaraka katika seriklai ya kikoloni. Huku kuwapanga watu kwa tabaka kulikuwa na athari katika kuanzisha upinzani dhidi ya ukoloni kwa kuwa waliofadhiliwa na Kanisa walishindwa kupinga wakoloni kwa kuwa ukoloni na Ukristo walikuwa wamoja.
African Association huko Tanga ilikosa umoja baina ya wale walioitwa 'wasio na elimu na wasiojua kusoma' na wale wasomi ambao kutoka kwao wote hawa chama cha siasa kingeweza kuundwa. Waafrika wasomi, Wabondei waliunda vikundi vyao peke yao vya wasomi kutokana na juhudi za ofisa mmoja wa kikoloni. Vyama hivi vikijulikana kama Discussion Groups [SUP]167[/SUP] yaani, vikundi vya majadiliano, vilitarajiwa kutojihusisha na kisiasa na vilitiwa nguvu na serikali kuhimiza mijadala na kusoma vitabu. Katika muda wote wa uhai wa vikundi hivyo hawa wasomi wa Makerere walikuwa chini ya usimamizi wa afisa Mzungu.

African Association huko Tanga ilitawaliwa na watu wa mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na Kiafrika. Hawa walikuwa watu wenye elimu ndogo. Kundi hili halikuwa na mkabala mzuri na Wabondei wengi wao wakiwa Wakristo wenye elimu. Kundi hili lililokuwa na damu ya Kiarabu lilijiona bora kwa daraja kuliko Waafrika weusi. [SUP]168[/SUP] Kama hivi vikundi viwili muhimu vingeweza kuzikusanya pamoja nguvu tofauti zao, vingeweza kuunda umoja wa siasa wenye uwezo mkubwa sana kama ile kamati ndogo ya siasa ya TAA iliyoundwa huko Dar es Salaam. Muungano huu ungeweza kuongoza harakati za kudai uhuru huko na halikadhalika ungeweza kupata mafanikio makubwa kwa kuwashirikisha wananchi katika kudai haki zao. Lakini kama ilivyokuwa, hizi kambi mbili zilikuwa hasimu; kila upande ukijitenga mbali na umma; wengine walijiona bora kwa sababu ya rangi ya ngozi yao na wengine walijiona bora kwa sababu ya elimu yao.
Gavana Edward Twining alipounda Constitutional Development Committee mwaka 1949, na kukaribisha maoni na mapendekezo kutoka kwa raia, TAA Tanga ilijikuta haina uwezo wa kuandika waraka. Uongozi wa Waarabu katika African Association haukuwa na elimu, maarifa au ujuzi uliotakiwa kutayarisha na kuandika waraka kwa serikali. Wasomi wa Makerere katika vile vikundi vya majadiliano waliinyakua fursa hiyo na kuandika waraka ambao uliwakilishwa kwa Gavana Twining.[SUP]169[/SUP] Pamoja na ukweli kuwa waraka ule uliandikwa na Waafrika wenye elimu kubwa kwa wakati ule, kwa hakika waraka ulikuwa na upungufu ukilinganisha na ule ulioandikwa na kamati ndogo ya siasa ya TAA, Dar es Salaam.[SUP]170[/SUP]
Mwaka mmoja baadae, katika mwaka 1951 ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipozuru Tanganyika, kile kikundi cha majadiliano, ingawa si wawakilishi wa wananchi kikifanya kazi yake nje ya TAA, kiliwasilisha waraka kwa ujumbe huo kikionyesha kuwa wao wanawakilisha maoni ya Waafrika. Hili lilizusha mzozo baina ya wasomi wa Makerere na ule uongozi wa Waarabu katika TAA.[SUP]171[/SUP] Haya makundi mawili yalijikuta hayana kusudio au muelekeo wenye maana, kidogo kidogo yalisahaulika. Kule Tanga mara chache watu waliihusisha ofisi ya TAA na siasa. Ofisi ya TAA inakumbukwa na kuhusishwa na mahakama ambako Kadhi, Sheikh Ali bin Hemed alihukumu jamii ya Waislam kwa kutumia sharia.
Lakini Tanga iliibuka mwaka 1955 na kukabiliana na serikali ya kikoloni kupitia juhudi binafsi za kikundi cha wafanyabiashara wadogo wadogo katika soko la Ngamiani. Kikundi hiki kiliongozwa na kijana Peter Mhando, katibu wa zamani wa kile kikundi cha majadiliano cha wasomi wa Kibondei. Akikiongoza kikundi hiki ambacho kilikuwa na Waislam, alikuwa baharia mstaafu, Hamis Heri Ayemba. Hamis Heri alikuwa Mmanyema kutoka kabila la Wakusu wa Belgian Congo. Peter Mhando alikuwa akifanya kazi kama mhandisi katia Noran Industries- wanunuzi wa nazi na watengenezaji sabuni pale Tanga. Hamisi Heri alikuwa na umri wa katikati na katika ujana wake alikuwa baharia na alipata kusafiri chombo kimoja na Abeid Amani Karume, ambae baadae alikuja kuwa rais wa Zanzibar. Baada ya Vita Kuu ya Pili, Hamisi Heri alirudi kwao Tanga ili aanze biashara. Heri alikuwa mtu aliyejikuza na kujielimisha mwenyewe; na alikuwa amesafiri sana. Hamisi Heri alizungumza vizuri sana Kiingereza na Kiarabu. Katika miaka yake ya mwanzo katika biashara, alikuwa dalali. Heri aliwashangaza wateja wake kwa uhodari wake wa lugha mbali mbali, akinadi bei kwa Kihindi au Kiarabu, kutegemea utaifa wa watu waliokuwepo pale mnadani.
Harakati za kudai uhuru zilipoanza Heri alikuwa ametajirika na mmoja wa Waafrika wenye kuheshimiwa sana mjini Tanga. Mhando alipochoshwa na kile kikundi cha maji
Hapa hujaonyesha wapi wala kupinga hoja yangu kuwa kiswahili hakikuongelewa na watanzania kwa idadi ya hata kukaribia nusu.Na hakuna niliposema watu hawakujua kiswahili basi Nyerere aliongea Lugha zote.Kwani wakalimani walikuwepo wengi sana ktk wasomi wa eneo husika.Na Nyerere alifanikiwa kwa hilo,kushika mzawa na kumpa cheo hata kwa level ya kitaifa.

Sasa umezidi kuonyesha jinsi gani uislam ulivyowafanya wadigo watu wa hovyo .Hadi Leo wadigo ni wavivu,wachawi, watumwa..huwa wanatumikishwa hata na waarabu koko wasiojiweza hata kujikimu.Umezisi kuwafungua watu macho kwanini hadi leo wadigo ni watu wa hovyo.Kwako wewe ni mashujaa..Nyie ndio mnaandika historia kinyumenyume..Nashukuru kuniletea quote ya vitabu vya hovyo kabisa vya design ya mzee mohamed..maandiko yao yote yanaonyesha uduni na ujinga wa wadigo,inaonyesha jinsi gani wamanyema waliutumia uislam kutawala watu wa pwani kirahisi ..huyu jamaa ktk harakati za ukombozi anatajirika wengine wanakuwa duni....?

Wanawaita Wkristu wasomi kuwa ni wasaliti,ila na wewe kwa akili zako za ndege huwezi jiuliza hata leo nani mwenye akili timamu atajiunga na CUF?Wadigo wote wajinga kama ulivyoeleza ulitegemea wachague njia sahihi?Watu hukombolewa kwa "Elimu na uelewa wa mambo" na si kwa ujinga.Yote haya yalikuwa ni udini tuu.Wadigo kwao kuwa na muarabu ndio uzalendo kwa vile ni dini moja na master wa asili ktk fikra zao.

Nashukuru sana kwa hii quote...hii ndio diference kt ya waislam na makafiri..makafiri wapo too open na wanaelewa vitu...mwandishi uliye mquote ni mjinga na mpuuzi..kaandika kitu kinachom betray ktk lengo lake kubwa.

Hivi ndivyo vitu viwafanyavyo waislam kuwa nyuma ya Wakritsu..."Jua kweli n akweli ikuweke huru".Kadiri mnavyozidi kuongeza bidii,ndivyo mnapata surprises...one kafiri can ride many muslims intelectually.Nyerere alifanya....na .

Kiswahili kilisukumwa sana na wajerumani na ingawa maeneo waliyopita waarabu na watu wa pwani ktk utumwa ndipo palizungumzwa kiswahili.Ila hadi leo kuna watu hawaji kiswahili Arusha,Bukoba,manyara.Kondoa,Mbeya, na shinyanga,kilimanjaro, etc..Hembu rudi miaka 50.

Chini hapa angalia harakati za TANU Kenya
Mambo yalikuwa yanageuka dhidi ya Waingereza katika makoloni yake yote Afrika ya Mashariki. Wazalendo walikuwa wakifanya harakati zao na kuvuka mpaka mmoja wa nchi hadi mwingine bila matatizo. Ule wakati wa wao kusafiri kwa kificho na kufanya mikutano yao nyakati za usiku mafichoni ulikuwa umepita. TANU ilikuwa na nguvu ya sasa kuangali nje ya mipaka yake. Katika pwani ya Kenya katika mji wa Mombasa, kijana mmoja kutoka Moshi, Ismail Bayumi, aliyeajiriwa na Mombasa Municipal Council akivutika na mwenendo wa matukio ya kisiasa kama yalivyokuwa yakitokea katika Afrika Mashariki, aliwashawishi Watanganyika waliokuwa wakiishi na kufanya kazi Mombasa kuunda kile kilichokuja kujulikana kama Mombasa TANU Club. Sheria ya Kenya haikuwaruhusu Watanganyika kuunda chama cha siasa katika ardhi ya Kenya, kwa hiyo TANU Club ilisajiliwa kama chama cha starehe na ilikuwa na ofisi zake katika Barabara ya Lohana. Ismail Bayumi alichaguliwa rais wake wa kwanza. Lakini kwa hakika TANU Club ilifanya kazi kama chama cha siasa kwa niaba ya TANU, KANU na KADU kwa kiwango fulani. Wakati huo Jomo Kenyatta alikuwa Manyani akitumikia kifungo cha miaka saba gerezani kwa kuhusika na harakati za Mau Mau.
Tom Mboya aliitumia TANU Club kuifanyia kampeni KANU na kupigania kufunguliwa kwa Kenyatta kutoka gerezani. Kote nchini Kenya KANU ilikuwa ikiibuka kama chama cha wananchi wote. Wakati sera za KANU zilikuwa zile za mwelekeo wa kuwaunganisha wananchi wote dhidi ya ukoloni, KADU chini ya Ronald Ngala, kwa upande mwingine, ilikuwa na labda isemwe, ufahamu mfinyu, KADU ikifungamanisha sera zake na siasa za ukabila na utawala wa majimbo. Kwa hiyo KADU ilikuwa ikikusanya nguvu za upinzani wa makabila madogo dhidi ya KANU. KANU chini ya Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga na Tom Mboya, ilichukuliwa kuwa ni chama cha makabila mawili makubwa nchini Kenya, yaani Wakikuyu na Wajaluo ambayo yakiachiwa kutawala yatameza makabila madogo. Nchini Tanganyika ambako ushindani wa kikabila katika siasa haukuwepo, TANU Club ilijikuta kiitikadi inapenda kuwa karibu zaidi na KANU kuliko KADU.
TANU Club ilikuwa ikiandaa dansi katika Ukumbi wa Tononoka na dansi hizi zilikuja kupendwa sana na wanasiasa wa Kenya. Ilikuwa chini ya pazia la sherehe hizi katika Ukumbi wa Tononoka ndiyo wanasiasa wa Kenya na wale wa TANU Club walipata nafasi kupashana habari namna TANU ilivyokuwa ikiendelea nchini Tanganyika na nini TANU ingeweza kufanya huko Tanganyika ili kusaidia harakati za kudai uhuru nchini Kenya. Baada ya TANU Club kufanikiwa sana huko pwani uongozi wake uliamua kufungua tawi la TANU Club mjini Nairobi katika sehemu ya Pumwani. Tom Mboya na Ronald Ngala walikuwa mstari wa mbele katika sherehe zote za TANU Club, wakishiriki katika shuguli zake Mombasa na Nairobi.
Msukumo mkubwa wakati ule nchini Kenya ilikuwa kufanya kampeni ya nchi nzima kuwashinikiza Waingereza wamwachie huru Kenyatta aliyekuwa akichukuliwa na wananchi wote kama kiongozi na nguvu ya umoja wa Waafrika wa Kenya. Katika wimbi hili la kutaka Kenyatta afunguliwe kutoka gerazani, Tom Mboya alimdokeza Ismail Bayumi kuwa TANU ingeweza kusaidia katika kampeni hii ya kuwashinikiza Waingereza kumtoa Kenyatta kifungoni. Ismail alifikisha wazo hili makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam kwa kupitia mtu maalum aliyekuwa akiwasiliana na Tom Mboya na Nyerere kwa siri. TANU ilimtuma Bibi Titi Mohamed kwenda Kenya kuzitia shime harakati za kufunguliwa Kenyatta. Wazalendo nchini Kenya walikuwa wameshindwa kabisa kuwaingiza wanawake ndani ya KANU hivyo kuzinyima harakati za uhuru nguvu kubwa sana na ya kutegemewa ya akinamama. [SUP]175[/SUP] Huko Mombasa TANU Club ilifikiria kuwa kumleta Bibi Titi kuja Kenya kuifanyia kampeni KANU ilikuwa ni kitu kipya cha kuwahamasisha wanawake ndani ya KANU na kwa hiyo kuongeza nguvu mpya na kutia ari ya utaifa katika Kenya.

Bibi Titi alikuja Mombasa na kufanya mkutano Ukumbi wa Tononoka. Kwa kawaida kwa madhumuni ya kupata kibali mikutano hii ilikuwa inahesabiwa kama ni mikusanyiko ya kufanya sherehe siyo mikutano ya siasa na ilikuwa ikifanyika ndani. Lakini mkutano huu ulikuwa na umuhimu wake kwa sababu ya kuwako Bibi Titi Mohamed mjini Mombasa. Wengi walikuwa wamemsikia Bibi Titi lakini hawakuwa wamepata kumuona. Watu walijaa ndani ya ule ukumbi hadi nje kuzunguka viwanja vya Ukumbi wa Tononoka. Kwa kweli kwa hali yoyote mkutano ule usingeweza kuitwa kuwa ni mkutano wa wanachama wa TANU Club mjini Mombasa, au hata mkutano wa TANU Club Kenya nzima, kwa sababu wanachama wa KANU waliwazidi wanachama wa TANU Club kutoka Tanganyika.
Kenya ilikuwa bado haijaweza kumtoa hata mwanamke mmoja wa kiwango cha Bibi Titi. Kwa wakati ule kumwona mwanamke wa Kiislamu amesimama bila baibui akihutubia halaiki ya wanaume ilikuwa ni jambo la kushangaza sehemu za pwani, ambako wanawake walitembea huku wamejifunika mabaibui na hawakutakiwa hata kufanya kazi maofisini. Bibi Titi alifanya mikutano kule Mombasa na Nairobi akiwasisitizia watu wasikate tamaa wasimame pamoja hadi Kenyatta amefunguliwa kutoka gerezani. Habari za mikutano hii iliandikwa kwa mapana na marefu na magazeti ya Mombasa Times na Taifa Leo.
Miongoni mwa Wakenya kule pwani waliyofanya kazi karibu sana na TANU Club walikuwa Msanifu Kombo na Abdallah Ndovu Mwidau. Kombo na Mwidau kwa sababu ya mchango wao kwa KANU kupitia chama chenyewe na kupitia TANU Club wakaja kuwa na ushawishi mkubwa kwa Rais Kenyatta. Wazalendo hawa wawili baada ya uhuru wa Kenya wakawa watu wenye sauti kubwa kule pwani. Hakuna mtu kutoka pwani alikuwa anaweza kuteuliwa na kushika nafasi yoyote muhimu na Kenyatta bila Abdallah Mwidau na Msanifu Kombo kumuunga mkono. Mara tu baada ya kufunguliwa kutoka gerezani, Kenyatta alikwenda Mombasa kutoa shukrani zake kwa Msanifu Kombo, Abdallah Mwidau na TANU Club kwa msaada wao kwa KANU na kwa kufanya kampeni ya kufunguliwa kwake. Mkutano ulitayarishwa kule Tononoka na Kenyatta alikuja kutoa hotuba ya shukrani na kukutana na wanachama wa TANU Club.
.
Sioni sababu ya kuweka habari za TANU Kenya.Kwani TANU imezaliwa mikononi mwa Nyerere ambaye alishaweza teka fikra za Wazee,kwa kuwaonyesha uwezo wake binafsi, kwa kiasi cha kuwashawishi kuwa anao uwezo wanaouhitaji zaidi ya yeyote ktk dini na ukanda wao.Na hivyo TANU tayari ilikuw aikienda ktk terms za Nyerere.Hiyo ilikuwa Test ya Kwanza ya Nyerere Kabla ya kwenda kukutana na vipingamizi kule kilimanyaro,kule Bukoba,na Iringa(The Renegades)..Nyerere mwenyewe hakupenda sana kilimanjaro ya kisiasa na Nguvu.Hata alipokwenda Mnadi Mkapa Kilimanjaro(Uwanja wa Makumbusho pale mjini Moshi)...alionyesha na alionyesha wazi kuwa Kilimanjaro ni ya kudhibiti.
 
Ritz nikizidi kuelimisha ....TAA haikuanzishwa hata na waafrica ila waingereza km kiitu kilichoitwa ""Discussion forum for African opinion". Na hii inaweza kuwa sababu ya Nyerere kuigeuza kuwa chama cha Kisiasa na kuja na TANU.


Kwa kiasi fulani waislam wamekuwa too naive na kujikuta wakitaka jenga hoja za hila na upotoshaji ktk uhuru wa hii nchi.Nyerere alikuwa na vitu "cutting edge".Hotuba yake UN hata waingereza hawakuipenda ila member wengine walipoisikia tuu wakawa upande wa Nyerere.

Waingereza pia walimpenda nyerere kwa vile alibanwa kwa fikra na imani zake mwenyewe za usaha wa matabaka ya rangi.Hii iliwafanya wajihisi kuwa salama zaidi kwake.
 
Yericko/Wickama
Naona hili jambo limewakaa sana na kwa hakika naona wanajamvi wengi
wanataka kunisikia.

Bismillah:

[FONT=&]''The larger picture shows that the aim of the revolution was to overthrow patriotism in Zanzibaris which was opposed to Britain and Tanganyika under Mwalimu Nyerere.

In the eyes of the British at that time was that Zanzibar was already under the influence of Egypt under Gamal Abdel Nassir which would come to endanger the interest of Britain and its puppets in East Africa.

Sheikh Ali Muhsin was aware of this and that is why when he was being taken to jail he quickly sent someone to his Goan secretary to shred the paper which he had prepared for the Cabinet after his trip from Egypt.

The uncertainty by ZNP-ZPP leadership in the issue of security of Zanzibar wavering between dependence on Egypt and then coming back to Britain who did not want to believe that Zanzibar could be invaded by Tanganyika was the reason which made Zanzibar fall and could not rise up again until now.'' [/FONT]

Wanajamvi,
Wameyataka wenyewe kazi kwao.

Mzee MS; At last. sasa baada ya kukushukuru, twende na tamaduni za hii thread, tuwekee sherehe ya kujua source ya "the larger PICTURE" au kama ni mawazo yako pia kuwa specific kuwa NI YAKO.

Tutajadiliana baada ya hiyo sherehe.
 
Mzee MS; At last. sasa baada ya kukushukuru, twende na tamaduni za hii thread, tuwekee sherehe ya kujua source ya "the larger PICTURE" au kama ni mawazo yako pia kuwa specific kuwa NI YAKO.

Tutajadiliana baada ya hiyo sherehe.

Wickama,
Nimeacha kutoa source kwa makusudi.

Ntawaomba wanajamvi mnistahamilie kwa hilo katika maelezo yangu
yote kuhusu Zanzibar.

Ikiwa kitabu nitawaeleza In Sha Allah.
 
Sijui unatumia browser gani. Kuna moja wanaita SLIMBROWSER (mimi naitumia), hiyo ina facility ya ku-download moja kwa moja hizo video bila mzunguko wala maswali ya ku-register na ni fast. Jaribu ku-install uijaribu.

Good Luck
Wickama,
Ahsante sana.
 
And I thought Amir Jamal was Ismailiya. Nipe tuisheni.

And you "thought" Swai was a Lutheran? And "Ismailiya" are Lutherans, isn't it?

And that is your proof ya "uchochezi" wa Mohamed Said.
 
Wickama,
Nimeacha kutoa source kwa makusudi.

Ntawaomba wanajamvi mnistahamilie kwa hilo katika maelezo yangu
yote kuhusu Zanzibar.

Ikiwa kitabu nitawaeleza In Sha Allah.

Mkuu,

Unataka tujadili kwakutumia fumbo la imani?
 
Mohamed Said,
Hujajibu hoja yoyote

1. Ni nani alimuomba msaada mwenzake kati ya TANU na ASP?
2. Hujasema kama mapinduzi ni halali au ni haramu
3. Hujasema waliofanya kazi na Nyerere ni dhalimu wa uislam au ni wanampainduzi
3. Hujasema wazanzibar wanapshereheka mapinduzi wanasherehekea udhalm au mapinduzi halali.

Katika post niliyotuma awali nimeweka sawa maelezo yako na tafsiri ya kile kinachoweza kutokana na nayo.
Kwa kipande cha kitabu hujajibu hoja. Na badal yake umezidi kuleta hoja zingine za kutatanisha

Kama yupo yoyote katika jamvi aliyemwelewa Mohamed, basi maswali hayo atusadie.


Kama umeshindwa kuelewa,hebu kaa kando kidogo,
Give us some space to learn..!,
Hoja zako ziko ni childish,
Kama umeshaona hilo unalolidhania ni sahihi sawa baki nalo,au waambie jamaa zako si sahihi na watakuelewa na watayaacha hapa hapa,
Ila sasa usijichukulie jukumu la kutoa conclusion na kuwasemea watu humu ndani,kila mtu hapa ana upeo wake na uwezo wa kufikiria mambo,
Kama ulichokiwaza na kukiona wewe kiko hivyo basi ahalan wasalan,kichkue hicho na ubakie nacho,

Halali haramu ina nin hapa??

Tanu au Asp nani alimtaka mwenzake msaada kiaje na ili iweje hali ya kuwa hoja zinajieleza zenyewe??

Kusurvive au kufail kwa uislam na usultan kunakujaje tena??

Kama umepuuzwa kujibiwa,basi jua hoja zako ni za kipuuz kweli,

Na mpuuzi dawa yake ni kupuuzwa,kuwa na staha na weledi basi,elimu inayomwagwa hapa ni kubwa,litambue hilo...
 
Mohamed Said.
Twakufuatilia kwa utuvu wa hali ya juu sana kuhusu hilo darsa la zanzibar,
Na washaanza kuingiwa na kiwewe kwa sasa,tafadhwali tafadhwali tumekaa kitako hapa kunyonya ilm hiyo,
Masalaam...
 
Last edited by a moderator:
Wickama,
Nimeacha kutoa source kwa makusudi.

Ntawaomba wanajamvi mnistahamilie kwa hilo katika maelezo yangu
yote kuhusu Zanzibar.

Ikiwa kitabu nitawaeleza In Sha Allah.

Sawa sheikh; Sawa utatuwekea especially kitabu na papers kwa jinsi unavyojieleza. Yabidi basi hata utushukuru na Nguruvi japo kwa vi-LIKE. Bila maswali yetu kukubana ungebembelezwa lini na Prishaz!!!! hahahahahah.



hebu tuliza roho bwana. Nina kibano kwa sasa.

Bee Gees - Night Fever (Video) - YouTube
 
Kama umeshindwa kuelewa,hebu kaa kando kidogo,
Give us some space to learn..!,
Hoja zako ziko ni childish,
Kama umeshaona hilo unalolidhania ni sahihi sawa baki nalo,au waambie jamaa zako si sahihi na watakuelewa na watayaacha hapa hapa,
Ila sasa usijichukulie jukumu la kutoa conclusion na kuwasemea watu humu ndani,kila mtu hapa ana upeo wake na uwezo wa kufikiria mambo,
Kama ulichokiwaza na kukiona wewe kiko hivyo basi ahalan wasalan,kichkue hicho na ubakie nacho,

Halali haramu ina nin hapa??

Tanu au Asp nani alimtaka mwenzake msaada kiaje na ili iweje hali ya kuwa hoja zinajieleza zenyewe??

Kusurvive au kufail kwa uislam na usultan kunakujaje tena??

Kama umepuuzwa kujibiwa,basi jua hoja zako ni za kipuuz kweli,

Na mpuuzi dawa yake ni kupuuzwa,kuwa na staha na weledi basi,elimu inayomwagwa hapa ni kubwa,litambue hilo...
Mkuu, hivi ni kweli kuwa mbunge wetu Murji kakamatwa?
 
Ritz nikizidi kuelimisha ....TAA haikuanzishwa hata na waafrica ila waingereza km kiitu kilichoitwa ""Discussion forum for African opinion". Na hii inaweza kuwa sababu ya Nyerere kuigeuza kuwa chama cha Kisiasa na kuja na TANU.


Kwa kiasi fulani waislam wamekuwa too naive na kujikuta wakitaka jenga hoja za hila na upotoshaji ktk uhuru wa hii nchi.Nyerere alikuwa na vitu "cutting edge".Hotuba yake UN hata waingereza hawakuipenda ila member wengine walipoisikia tuu wakawa upande wa Nyerere.

Waingereza pia walimpenda nyerere kwa vile alibanwa kwa fikra na imani zake mwenyewe za usaha wa matabaka ya rangi.Hii iliwafanya wajihisi kuwa salama zaidi kwake.
Wanaukumbi huyu ndugu yetu naona bado anaendelea na porojo zake kuhusu historia ya Tanganyika na harakati za kutafuta uhuru.
Ritz nikizidi kuelimisha ....TAA haikuanzishwa hata na waafrica ila waingereza km kiitu kilichoitwa ""Discussion forum for African opinion". Na hii inaweza kuwa sababu ya Nyerere kuigeuza kuwa chama cha Kisiasa na kuja na TANU.
Wanaukumbi hapa juu tunamsoma ndugu yetu anatuambia TAA Haikuanzishwa na waafrika lakini hasemi ilianzishwa na na nani tusiandikie mate na wino upo hapa chini tumsome Nyerere mwenyewe.
Julius Kambarage Nyerere"Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere  Chuo Kikuu  nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia  nikiwa Makerere  akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association".
https://www.jamiiforums.com/member.php?u=34266Wanaukumbi nadhani ingekuwa vyema huyo jamaa yetu angetuambia TAA imeundwa na kina nani atutajie na majina yao, hebu tumsome tena huyu jamaa yetu hapa chini.
Kwa kiasi fulani waislam wamekuwa too naive na kujikuta wakitaka jenga hoja za hila na upotoshaji ktk uhuru wa hii nchi.Nyerere alikuwa na vitu "cutting edge".Hotuba yake UN hata waingereza hawakuipenda ila member wengine walipoisikia tuu wakawa upande wa Nyerere.
Wanaukumbi hapa juu ndugu yetu anajaribu kumuwekea Nyerere maneno mdomoni kuhusu Waingereza hebu hapa chini tumsome Nyerere mwenyewe anavyowaelezea Waingereza amabao tunaambiwa walikuwa upande wake.
Julius Kambarage Nyerere
"Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine  mpya (United Nations Organisation  UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.


Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana? Nikasema inawezekana. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara."
https://www.jamiiforums.com/member.php?u=34266Wanaukumbi nadhani tumeona tofauti ya maneno ya ndugu yetu na maneno ya Nyerere.
gombesugu, THE BIG SHOW,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom