Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Wickama,
AA wala TAA hawakupata kujiandikisha kama chama cha siasa.
Hawakuwa chama cha siasa katika mafaili bali kwenye matendo yao.
Haya matendo yao ya kisiasa ndiyo yalifanya Waingereza watoe
Government Circular No. 5 na 6 kuzuia Waafrika katika ajira za
serikali wasijiingize katika siasa.
Amefanikiwa kuzika hoja za Kipumbwi hadi atakapokutana na jamii ingine inayofyonza tu, hata hivyo lazima amejifunza jambo kubwa kuwa hadithi zake zinaji-contradict.
Amekata kata vipande vya vitabu ili kuuondoa umma katika katika hoja halisi aendelee kutaja majina ya watu bila logic za mtirirko wa matukio tukiambiwa ndiyo historia ya kweli.
Ameshindwa kutetea hoja za mapinduzi na hilo linabaki jeraha katika masimulizi yake.
Ninakuhakikishia hata rudia tena hadithi za Kipumbwi kama alivyokoma kuhusu ujio wa Nyerere, Sykes/Matola na AA.
Hili hatalijibu, nasi tunamwambia hoja za nyuma bado zinasimama kama zilivyo na zitaendelea kumwandama kama zimwi la Ibadan linavyomwandama kila uchao. Siku hizi Ibadan kimyaa! hataji hata katika sehemu alizohudhuria, ha ha ha ha
Hatalijibu kwasababu litamaliza ilm na wafyonzaji watazidi kuwa na wasisi.
Keshaondoa wasi wasi 200+K waliyokuwa nayo kuhusu maandiko yake isipokuwa wafyonzaji.
Mohamed, mapinduzi ya znz bado hujayatolea maelezo na sasa unaulizwa hilo hapo juu.
Ni kwamba ulikuwa hujui au?Mnayo kazi....huwa uongo wenu unawakost nyie zaidi.
Ni muhimu kuangalia namna huyo Rais wa Jamhuri ya muungano atakavyopatikana.
Itakuwa ni kituko kama rais atachaguliwa kwa kuangalia zamu za upande mmoja.
Ukweli unabaki kuwa wznz hawaonekani kujua wanataka nini.
Wakati tunaandaa taifa kwa awamu nyingine kama zilivyokuwa za miaka 50 iliyopita duru itashangaa sana kuukabidhi uongozi wa nchi kwa watu wasio na mapenzi na Watanganyika.
Hakuna sababu ya kupata kiongozi kwa kuangalia uzanzibar wake.
Hawa ni watu chini ya lakini tano kwasababu waliobaki wanaishi Tanganyika.
Ni kituko cha kutaka kupata kiongozi kwa kuangalia jina la sehemu.
Kuna ushahidi kuwa viongozi wa znz hasa waliberali hawataki Watanganyika.
Yanini basi wakabidhiwe uongozi wa nchi yetu?
Suala lingine ni kuangalia kati ya yale mambo 7 yaliyoamuliwa ni vipi Tanganyika itanufaika na gharamazake zitakuwaje kwa kugawana na wala si uwiano.
Tunasema si uwiano kwasababu znz ilikuwa na wajumbe sawa na Tanganyika na imepewa hadhi sawa kama Tanganyika katika majadiliano.
Sasa kwanini basi kusiwe na usawa katika mambo mengine?
Itanishangaza sana kama Watanganyika watakubali kubeba gharama kwasababu znz ni ndogo kieneo na idadi ya watu.
Ingekuwa hivyo wasingedai usawa wa tume.
Kuna mambo mengi sana ya kuangalia na kujiuliza. Kwa mfano wapi thamani za taifa zilijadiliwa.
Haiwezakani tume ije na mambo ambayo wananchi hawakupata fursa ya kuyajadili.
Lakini pia ni lazima tuangalie ni namna gani viongozi wamejiwekea kinga ili kuendelea na uhalifu kama tunaoushuhudia.
Haiwezekani Jaji mkuu ateuliwe na rais? Kwanini Jaji mkuu awajibike kwa Rais? Kwanini .
Halafu inabidi tutupie macho mambo mengi muhimu kama yahusuyo uchumi n.k.
Ujumbe wangu ni kuwa mchakato mzima ni wa ubabaishaji lakini katitka ubabaishaji huo ni makosa kukaa pembeni.
Tutaendelea kutoa mawazo na kusema tukitambua kuwa huu ni ubabaishaji
Hakuna kisicho na mwisho na wala hakuna dola iliyowahi kushinda nguvu za umma.
Jambo moja la muhimu ni kuweka itikadi za kisiasa, kidini na kikabila pembeni na kuaiangalia rasimu kama dira na urithi tutakaowaachia watoto wetu.
Tutangulize Utanganyika na pengine ni wakati sasa tuwaunge mkono wzn katika jitihada zao za kuondoka.
Hakika uwepo wao unaathiri sana nijadala yetu na katika athari hizo hakuna tunachopata kutoka kwao.
Hivyo tujikite kuijadili Tanganyika ya kesho, tuikinge na unyonywaji rahisi na tuijengee ramani ya kudumu.
Tusemezane
ha haa haa haaaa..... kama kuna Spinning, basi nipigwe ban...Mkuu Nguruvi3 heshima kwako...
Haiwezekani ukadai NCHI huru iliyo na mamlaka kamili halafu wakati huo huo uwe ndani ya kitu kinachoitwa Serikali ya Muungano.. hapa tunaweweseka tu pengine kwa kuogopa mzimu wa Mwalimu Nyerere utatushukia kwa hasira.
Suluhisho hapa ni kuwa na Zanzibar huru (kama wanavyotaka) na Tanganyika (Tanzania Bara au vyovyote vile tutakavyoiita) huru halafu tutafute namna nyingine ya kushirikiana nao kama majirani zetu. Lakini tusidanganyane kwa hili koti ya MUUNGANO ambalo kwa hakika sasa limepauka, limetoboka na halitutoshi tena!
Jee, umewahi kumsikia Mashado Plantan?
We sema usemalo,km unapinga au unasupport au una wazo jipya.Km hakuna tambaa.Utaingiliaje mazungumzo halafu uje na swali lisilohusika.
Nicholas; Nadhani nitahitaji some help here. Kuna mahali nilishawahi soma kama vile Sir Donald Cameron ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa hizi AA pamoja na indirect rule (though chiefs etc) kama mojawapo ya efforts zake kuwajenga waafrika na hata akakataa kuiunganisha tanganyika na kenya colony kuizuia tanganyika isimezwe na hilo colony. To be honest i need clarity kwa vile huwa inanichanganya naposoma juu ya AA--->TAA nani aliianzisha? kuna haja ya kutenga mwanzishaji na OFFICE bearers, unajua lolote? Au mimi nilielewa vibaya?
Mashado Plantan anahusika sana tena sana na uchochezi wa Mohamed Said, au ulikuwa hujui hilo?
OK; Baada ya salaam NADHANI,naona point ya Nicholas sasa. Kwa sababu siku zote serikali huwa inavitaka vyama kubaki kwenye yale mambo vilivyojiandikisha kufanya. Yaani, kama Yanga kesho hawawezi kuzuka na kusimamisha mbunge bila KUJIANDIKISHA kama chama cha SIASA. Hiyo Ban, itaendana na malengo ya kandikishwa TAA.
Una nyaraka nyingi za kina Sykes. Una mahali popote unapoweza kutuwekea humu JF;
1. Barua ya AA/TAA (before Nyerere)wakiomba rasmi kutambuliwa kama chama cha siasa kutoka mamlaka husika?
2. Una Malengo rasmi ambayo AA.....>TAA waliandikishwa nayo kwa registrar of associations wa Tangayika au yeyyote mwenye nayo atuwekee tujue walikuwa vipi? Na tuone ambayo political ni yapi? Sio general welfare!!!!
Kwa sababu bila kujiandikisha kama political party na chama kuwa na articles of association ambazo ni political, kauli za nani alisema/hakusema ni political party huku mtaani hazina pa kushika.Nadhani ndicho anachojaribu Nicholas kuweka across. Hebu tufate njia rasmi.
cc Nicholas, Yericko, Nguruvi
Umemaliza ...?Wala sihitaji jua hilo.Kwani si sehemu ya nilichokuwa naelezea.Ok.Sasa acha kupoteza muda jadili mada au chapa lapa.
OK; Baada ya salaam NADHANI,naona point ya Nicholas sasa. Kwa sababu siku zote serikali huwa inavitaka vyama kubaki kwenye yale mambo vilivyojiandikisha kufanya. Yaani, kama Yanga kesho hawawezi kuzuka na kusimamisha mbunge bila KUJIANDIKISHA kama chama cha SIASA. Hiyo Ban, itaendana na malengo ya kandikishwa TAA.
Una nyaraka nyingi za kina Sykes. Una mahali popote unapoweza kutuwekea humu JF;
1. Barua ya AA/TAA (before Nyerere)wakiomba rasmi kutambuliwa kama chama cha siasa kutoka mamlaka husika?
2. Una Malengo rasmi ambayo AA.....>TAA waliandikishwa nayo kwa registrar of associations wa Tangayika au yeyyote mwenye nayo atuwekee tujue walikuwa vipi? Na tuone ambayo political ni yapi? Sio general welfare!!!!
Kwa sababu bila kujiandikisha kama political party na chama kuwa na articles of association ambazo ni political, kauli za nani alisema/hakusema ni political party huku mtaani hazina pa kushika.Nadhani ndicho anachojaribu Nicholas kuweka across. Hebu tufate njia rasmi.
cc Nicholas, Yericko, Nguruvi
Hata waganga,wachawi, majambazi, watapeli na wahanga nao hupewa platform yakuzungumza...ni wewe tuu kuonyesha ubora w ahiyo paltform.....Si vyema kujjidanganya kwa hayo.Wengine waliojaaliwa hupima hadhira yao na kujua kuwa wamepewa kinachostahili au jambo limekuzwa kutokana na udhaifu wa hadhira.Tusemezane,
Katika majuma kama matatu yalopita nimekwenda Zanxibar
mara tatu na mara zote hizo nimepewa mialiko ya kuxungumza
mubashara kwenye radio.
Hii si dalili ya mtu anetafutwa kupopolewa.
Yericko,
Hapana haja ya kuhangaika sana.
Historia ya TANU ya wanajopo wa CCM ipo.
Historia iloandikwa na MS ipo.
Kila upande umeeleza historia yake.
Kwa nini wewe leo jasho likutoke kuikataa
historia yangu?
Tuuachie umma uamue nani mkweli na nani
muongo.
Haha mnachonifuarahisha waislam ni kupenda slightly twisted story.....mwishowe mnapotea kabisa.Hao wazee wako walisharidhika km wazee wa Bakwata..Salaam ndugu yangu WICKAMA,
Mwanzoni mwa harakati za kupigania uhuru kwa kipindi kirefu wakoloni walipiga marufuku vyama vyote vya siasa.Ilikuwa hauwezi kusajili chama cha siasa kwa msajili.TAA walitumia mbinu ya kufanya siasa kupitia TAA political subcommitee.Hili liko wazi sana lakini hasadi dhidi ya Sheikh Mohamed na historia ya wazee wake zimewafanya ukweli hamuoni.
Lakini si mmeishambiwa aminini historia yenu ya kupanga ya kivukoni, nasi tuacheni tumuamini Sheikh Mohamed atupe yale aloshuhudia na kusimuliwa na wazee wakee waliokuwa ndio moyo wa harakati za kudai uhuru.
Poleni sana.
Wickama,
Sina nyaraka hizo ulotaja.
Naona nduguyo ananitia kwenye makundi mabaya
ya wanga nk.
Wajua kinachonishangaza mie ni jinsi mnavyochomwa
na hii historia yetu.
Mbona historia yenu imetamalaki miaka na miaka na sie
hatujanyanyua hata jiwe kumpopoa mtu.
Shule zote historia isomweshayo ni hiyo ya Kivukoni sie tuliii
kama maji mtungini.
Aminini hiyo historia yenu hapana neno.
Hii nchi huru.