Wamo humu kwenye nyuzi inaonesha umekurupuka hujaisoma, Jee, unamjuwa Tewa?
teh teh....kumbe mzee akibanwa kilio kinasikika upande mwingine wa dunia.....?huyu bwanyenye anayemtetea mzee inawezekana nae alichangia kiasi fulani kujenga ground za kutukuzwa uarabau.
Salaam ndugu yangu WICKAMA,
Mwanzoni mwa harakati za kupigania uhuru kwa kipindi kirefu wakoloni walipiga marufuku vyama vyote vya siasa.Ilikuwa hauwezi kusajili chama cha siasa kwa msajili.TAA walitumia mbinu ya kufanya siasa kupitia TAA political subcommitee.Hili liko wazi sana lakini hasadi dhidi ya Sheikh Mohamed na historia ya wazee wake zimewafanya ukweli hamuoni.
Lakini si mmeishambiwa aminini historia yenu ya kupanga ya kivukoni, nasi tuacheni tumuamini Sheikh Mohamed atupe yale aloshuhudia na kusimuliwa na wazee wakee waliokuwa ndio moyo wa harakati za kudai uhuru.
Poleni sana.
Hao wahusika wakuu ,kwanini wasidai kipindi hicho...?Walihofia kuwa wangeumbuliwa?Kuuna mabo mengi ya kuangali hata kam ani kwa kuhadithiwa ili kujenga credibility..Alihakikisha vipi kuwa hao jamaa hawakuwa wana jikuza kama wale wanajesh iwaliokuwa wapishi,madaktari na wengine ktk Vita ya Kagera wanavyojifagilia kuwa waliwachapa sana waganda hadi uganda..Ila wakibanwa wanasogea ktk kweli ,kwakusema wao waliganya kazi ya kwanza kumto aktk ardhi ya Tanzania,wengine wakapokea na kwenda watoa uganda...km huna huruma na uongo wao ukiwabana zaidi wanakwambia wao walikuwa wakipokea vitu walivyotuma raia kwa ajili ya wanajeshi.hadi hapo utaendelea amini chochote kirahisi?Yericko,
Mimi nina shaka kabisa kuwa wewe hijawa kufanya utafiti wowote ule na kuuweka katika maandishi ili wasomi waupitie ndio maana unauliza suala kama hilo nililo Bold.
Kumbuka kuwa Al habbib Mohamed said amefanya utafiti wa kihistoria tena ule wa mapokeo ya moja kwa moja ikiwemo kupata nyaraka na kupewa ufafanuzi wake kwa wahusika wakuu ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki wao binafsi katika mchakato wa kupatikana na uhuru wake.
Hao walishiriki aliowasema kuwa victims,kwa aliyoyaeleza kuhusu familia za Rupia,Sykes, Kyaruzi etc...hakuna walichokosa hata km wengine walipata zaidi ya walichosatahili,kwani hawakuwa mercenaries ,ambao baada ya kazi walipwe.Kama kweli umekisoma kitabu chake utabaini kuna mengi ameshuhudia mwenyewe na mengine amepata moja kwa moja toka kwa washiriki aliowaeleza kwa mapana na marefu mchango wao katika kupatikana kwa uhuru wenu.
Na kwa mchakato WAKO KWA KUANDIKA KITU hicho ungejikuta UNAINGIA KATIKA FUNGU LA WASOMI KWA KUJIBU UTAFITI WAKE KWA KUANDIKA KITABU CHAKO KUPINGANA NA KITABU CHAKE.
Mimi naamini kwa dhati kabisa Al Habib Mohamed Said atakupa msaada mkubwa sana katika hilo.
Huo ni ushauri wangu kwa wasomiTUNAAMINI KUWA UTAFITI UNAPINGWA KWA UTAFITI NA WALA SI BLA BLA AU MISTARI MIWILI AU MITATU KATIKA JF.
Ritz,
Huyu jamaa haijui historia ya TANU.
Angekuwa anaijua asingekuwa na mdomo wa kumkashifu Abdu Sykes.
Hata wale wasiompenda katika TANU hawakuthubutu kusema kuwa
TAA iilikuwa ajira yake kwani chama kikenda kwa fedha zake.
Shariff naishia hapa.
Ukawaambia kuwa Mapinduzi ni haram, na kwamba akina Mwinyi, Nasor Moyo, Jumbe, Kombo, Natepe, Karume, Salimn, Wakili wao ni makafir kwa kushirikiana na Nyerere?
Uliwaambia kuwa aliyemuondoa sultan ni wakipumbwi baada ya kulewa ndaza wakachukua jahazi na kwenda kwa sultan
Uliwaambia kuwa mauaji yaliyofanywa yalikuwa chini ya Kassim Hanga. Uliwaambia kuwa Okello ndio baba wa taifa lao.
Juzi tu Pemba sheikh kabondwa kwa kujiunga na CCM, wewe kaseme hayo mbele yao kama hujapopolewa.
Hata huko znz unakokwenda unaongea katika misikiti ya pembezoni.
Si umewahi kusema unafundisha, tulipofuatilia ni Thaqafa! wewe Mohamed kuna kidogo usichokimwagia hamira.
Lakini tulia kadri siku zinavyokwenda wale ambao baba na mama zao wametoa roho kuikomboa nchi yao ya znz na unawaita majina ya kashfa na dherue watakujibu, sijui ni kwa karatasi, spika au mawe.
Pole kwa mafuriko na kupitwa na mambo..nadhani ndiyo yatakuwa yamekuponza urukie kila mtu kwa kutojua.Au pengine ndio kule kutoitendea dini yenu haki,kila kitu hamchukui muda fikir huwa maniingiza halafu ikipata majibu yanayoumiza mnaanza jificha kuwa dini imetukanwa na excuse nyingine ya vilema.Yericko,
Naona bila ya kumtaja Gombesugu huna raha moyoni kijana!?
Mimi si niliaga yakuwa nitakua safari kwa wiki nzima!?...nimerejea nyumbani asubuhi hii lakini mafuriko ni mengi maeneo ya jirani zetu...na pia inalazim nipitie yalonipita hapa jamvini kiduchu.
Naona unapenda pale Nicholas anapotoa hisia zake,nakhis lazim atakua mtu wa Chadema mwenzio!?ahaha!!
Tutaongea na tuendelee na mnakasha.
Ahsanta.
Unatuthibitishiaje kuwa hiyo ndio historia ya kweli?
Lete uthibitisho nje ya maandiko yako wewe mwenyewe!
Yericko,
Kuna watu wameniomba nikupuuze.
Ungesaidia sana km ungesema lengo alo kukualika ni lipi?Na mwisho wake walikirank vipi kitabu chako?Wanajamvi,
Siku zote hulikumbusha jamvi kuwa mie "sikiri" bali husema.
Jingine.
Kuna mtu anasema ati sijaandika historia.
Akaangalie catalogue ya Library of Congress kitabu changu kiko
wapi.
Northwestern University wamenialika chuoni kwao kuzungumza
mwaka 2011.
Ajishauri kwanza hiki chuo nini sifa yao kuu?
Iweje wamualike mtu wa madrassa?
Hapo chini ulikuwa unafanya uchochezi Marekani ha haa haaa.
View attachment 97012
Ungesaidia sana km ungesema lengo alo kukualika ni lipi?Na mwisho wake walikirank vipi kitabu chako?
Wabongo na watu wa masharii ya kati wanatabia ya kuitw ana watu wa makundi yao ulaya ili wapatte palatform ya kujikuza na baadaye wapate uhalali wa kudanganya wapendavyo.
Hii ndio sababu...siwakubali Migiro,Salim A.Salim ,membe and the sort...hawa wote wana one thing in common..ni incompetent...ila bahati mbaya Migizo kakutwa na age ya dotokomu na propaganda zikiwa chini..tungesikia ni Hila za Marekani, mama asikae UN..kwani anawabana sana.
Kuna tatizo kubwa sana Mohamed.Wild Card,
Nasema mmeshtushwa kwa sababu mnavyohangaika humu kujaribu
kuibomoa historia hiyo. Hivi nyie hamjiulizi kwa nini mimi sijapinga historia yenu wala sikuulizeni
mswali, wala situkani au kutumia lugha chafu na kali.
Hivi kweli hamjajiuliza kwa nini iwe hivyo?
Mimi sina neno ikiwa mtapenda kuamini kuwa TANU imeanzishwa na Nyerere
kutokea Musoma. Kwa kweli sina neno asilani wala sitakubughudhi kwa hilo.
Nachokuomba ni kuwa na wewe usinibughudhi mimi nikikuambia kuwa TANU
ni ''brain child'' ya Abdu Sykes.Tatizo liko wapi ndugu yangu?
Naona hatujaelewana. Bora tuachie hapa. Kitabu hakina jibu la kama ASP walilazimishwa na TANU msaada. Ahsante bwana.
??? !!!
Wickama,
Hebu pumzika na hii:
We have seen many times that the question of Zanzibar revolution is associated with
"Arab slave trade."
The origin of this paradigm stems from not knowing the actual source of the revolution.
The most telling problem was to perceive that the revolution in Zanzibar had to take
place because of the oppressive regime of the Zanzibaris of Arab descent.
It was not necessary that the invasion of Zanzibar should take place.
It was a special plot by one country invading another and hiding that hideous fact which
gave Zanzibar sleepless nights for forty nine years.
Kuna tatizo kubwa sana Mohamed.
Kwanza hakuna anayataka kizazi kijacho kilishwe habari zisizo na ukweli tukarudi hapa tulipo sisi wazazi wao.
Pili, ni kweli kuna kushtuka pale ambapo habari za wazi zisizohitaji logic zinapokuwa skewed kwa interest
Tatu, umeshasema huko nyuma umeandika kupinga historia ya kivukoni na hivyo kusema hujapinga si kweli
Nne, hakuna anayesema hiyo ya kivukoni ina ukamilifu,zinazofanya kazi hapa ni fikra za kutafuta uhalisia.
Mohamed, historia ni somo lenye mantiki. Mantiki kubwa ya historia huongozwa na vitu,watu, matendo na nyakati.
Hivyo lazima vifuatane kwa mpangilio wa jinsi vilivyotokea kwa uhalisia na si jinsi vilivyopaswa kutokea kwa kuumba.
Nikiandika historia yako nikataja mihadhara uliofanya kama Northwestern, Cambridge, Nairobi, Johanessburg nikaacha kuandika Ibadan nitakuwa sijaikamilisha historia yako kwasababu nimeruka kitu, mtu (ambaye ni wewe), watu (wana Ibadan na balozi), tukio ambalo ni paper na wakati ambao ni siku na muda uliokuwepo.
Ndivyo ulivyofanya kwa K.Sykes, Nyerere, Sheikh Ameir, EAMWS kutaja kwa uchache.
K.Sykes umemtaja kama mwanzilishi pekee wakati alikuwepo Matola hivyo kuondoa mtu na muda. Hapo si historia
Ukamtaja Nyerere kuanza siasa alipokutana na Sykes, ukaacha historia yake kuanzia huko nyuma hata alipokuwa katika siasa kabla ya A.Sykes. Umeruka watu, vitendo na muda. Umekiuka kanuni za historia, ni utunzi si historia.
Na bado unaendelea kukiuka kanuni za uandishi wa historia. Unaposema A.Sykes ndiye brain child ya TANU, umeruka ukweli kuw mid 40s Nyerere alishakuwa katika siasa kama yeye, na Abdu alikuwa anatumia jina la familia.
Umesahau kuwa kuanzia K.sykes hadi A.Sykes hakukuwa na katiba ya kisiasa, na kwamba katiba imeandikwa Nyerere alipotia mguu. Umeruka tukio,muda na wahusika. Hapo ni utunzi si historia.
Ukasahau kuwa brain child Abdul na baba yake hawakufanya mageuzi ya haraka kwa miaka 21 hadi alipokja mtu akafanya mageuzi ya kisiasa na harakati kwa miaka chini ya 10.
Hakufanya mwenyewe lakini historia inasema he was a force to be reckoned with. Unapoacha sentesi hiyo unakiuka mwongozo wa histora na kubaki na utunzi.
Imani kuwa historia imeshtua watu ni grandiosity, kilichoshtua watu ni mispresentation of facts, falsification, severe hyperbole iliyotengenezwa katika kasha la imani ili kumfunga mwanadamu asitumie akili zake kwa kuogopa kufanya hivyo ni kumhalifu mwenyezi mungu.
Wengine hatutaki watoto wetu wakaingia katika mtego huo ndiyo maana tupo hapa kuweka sawa na wala si kubomoa kwasababu facts zinabobomoa historia yako mwenyewe. Unaposhindwa kusema watu wa Kipumbwi waliandaliwa vipi, wakaenda vipi kwa amri ya nani na kwanini, na ipi ni nafasi yao katika historia ni facts zinabomoa historia yako.
Na hakika kama ulivyonena facts zimebomoa sana utunzi huu wa historia. Mtu aliyesoma kitabu chako miaka 15 iliyopita leo anajiuliza kukisoma tena, na kwa bahati mbaya akikisoma atakapofika ukurasa wa mwisho atakitoa kwa wauza vitumbua wafungie bidhaa zao.
Unapomwambia mtoto au mjukuu wa A.H.Mwinyi au Nassor Moyo kuwa baba yake ni dhwalimu kwa kufanya mapinduzi na kushirikiana na kufar Nyerere, wakati huo huo Mzee Mwinyi au Moyo wakihimiza watoto na wajukuu wao walinde mapinduzi ni kuwadhihaki, kudhihaki fikra na kuwakashf kama si kuwatusi.
Je, tukae kimya uchanganye na watoto wetu pia! not on our watch sir!
Upande wa vijana wa kikristo sijui watakuwa wanakataa kulishwa nini,lakini kwa upande wa wale wa kiislamu tutakaowazaa ni wazi kuwa watakuwa hawataki kusikia uzushi kuwa Nyerere alikuwa akipigania umoja wa taifa la Tanzania na kwamba alikuwa akipinga udini.Vile vile baada ya kusoma historia halisi kutoka kwa akina Mohammed Saidi hawatakuwa na sababu ya kuamini eti mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni kwa ajili ya ukombozi wa Zanzibar.Kuna tatizo kubwa sana Mohamed.
Kwanza hakuna anayataka kizazi kijacho kilishwe habari zisizo na ukweli tukarudi hapa tulipo sisi wazazi wao
!
Naona hatujaelewana. Bora tuachie hapa. Kitabu hakina jibu la kama ASP walilazimishwa na TANU msaada. Ahsante bwana.
Mkuu gombesugu, sijui utapata lini muda ili uthibitishe tuhuma nzito ambazo umekuwa ukinimwagia mimi binafsi kwamba nimekuwa na ukashifu uislam hapa jamvini!Yericko,
Naona bila ya kumtaja Gombesugu huna raha moyoni kijana!?
Mimi si niliaga yakuwa nitakua safari kwa wiki nzima!?...nimerejea nyumbani asubuhi hii lakini mafuriko ni mengi maeneo ya jirani zetu...na pia inalazim nipitie yalonipita hapa jamvini kiduchu.
Naona unapenda pale Nicholas anapotoa hisia zake,nakhis lazim atakua mtu wa Chadema mwenzio!?ahaha!!
Tutaongea na tuendelee na mnakasha.
Ahsanta.