Wild Card,
Nasema mmeshtushwa kwa sababu mnavyohangaika humu kujaribu
kuibomoa historia hiyo. Hivi nyie hamjiulizi kwa nini mimi sijapinga historia yenu wala sikuulizeni
mswali, wala situkani au kutumia lugha chafu na kali.
Hivi kweli hamjajiuliza kwa nini iwe hivyo?
Mimi sina neno ikiwa mtapenda kuamini kuwa TANU imeanzishwa na Nyerere
kutokea Musoma. Kwa kweli sina neno asilani wala sitakubughudhi kwa hilo.
Nachokuomba ni kuwa na wewe usinibughudhi mimi nikikuambia kuwa TANU
ni ''brain child'' ya Abdu Sykes.Tatizo liko wapi ndugu yangu?
Kuna tatizo kubwa sana Mohamed.
Kwanza hakuna anayataka kizazi kijacho kilishwe habari zisizo na ukweli tukarudi hapa tulipo sisi wazazi wao.
Pili, ni kweli kuna kushtuka pale ambapo habari za wazi zisizohitaji logic zinapokuwa skewed kwa interest
Tatu, umeshasema huko nyuma umeandika kupinga historia ya kivukoni na hivyo kusema hujapinga si kweli
Nne, hakuna anayesema hiyo ya kivukoni ina ukamilifu,zinazofanya kazi hapa ni fikra za kutafuta uhalisia.
Mohamed, historia ni somo lenye mantiki. Mantiki kubwa ya historia huongozwa na vitu,watu, matendo na nyakati.
Hivyo lazima vifuatane kwa mpangilio wa jinsi vilivyotokea kwa uhalisia na si jinsi vilivyopaswa kutokea kwa kuumba.
Nikiandika historia yako nikataja mihadhara uliofanya kama Northwestern, Cambridge, Nairobi, Johanessburg nikaacha kuandika Ibadan nitakuwa sijaikamilisha historia yako kwasababu nimeruka kitu, mtu (ambaye ni wewe), watu (wana Ibadan na balozi), tukio ambalo ni paper na wakati ambao ni siku na muda uliokuwepo.
Ndivyo ulivyofanya kwa K.Sykes, Nyerere, Sheikh Ameir, EAMWS kutaja kwa uchache.
K.Sykes umemtaja kama mwanzilishi pekee wakati alikuwepo Matola hivyo kuondoa mtu na muda. Hapo si historia
Ukamtaja Nyerere kuanza siasa alipokutana na Sykes, ukaacha historia yake kuanzia huko nyuma hata alipokuwa katika siasa kabla ya A.Sykes. Umeruka watu, vitendo na muda. Umekiuka kanuni za historia, ni utunzi si historia.
Na bado unaendelea kukiuka kanuni za uandishi wa historia. Unaposema A.Sykes ndiye brain child ya TANU, umeruka ukweli kuw mid 40s Nyerere alishakuwa katika siasa kama yeye, na Abdu alikuwa anatumia jina la familia.
Umesahau kuwa kuanzia K.sykes hadi A.Sykes hakukuwa na katiba ya kisiasa, na kwamba katiba imeandikwa Nyerere alipotia mguu. Umeruka tukio,muda na wahusika. Hapo ni utunzi si historia.
Ukasahau kuwa brain child Abdul na baba yake hawakufanya mageuzi ya haraka kwa miaka 21 hadi alipokja mtu akafanya mageuzi ya kisiasa na harakati kwa miaka chini ya 10.
Hakufanya mwenyewe lakini historia inasema he was a force to be reckoned with. Unapoacha sentesi hiyo unakiuka mwongozo wa histora na kubaki na utunzi.
Imani kuwa historia imeshtua watu ni grandiosity, kilichoshtua watu ni mispresentation of facts, falsification, severe hyperbole iliyotengenezwa katika kasha la imani ili kumfunga mwanadamu asitumie akili zake kwa kuogopa kufanya hivyo ni kumhalifu mwenyezi mungu.
Wengine hatutaki watoto wetu wakaingia katika mtego huo ndiyo maana tupo hapa kuweka sawa na wala si kubomoa kwasababu facts zinabobomoa historia yako mwenyewe. Unaposhindwa kusema watu wa Kipumbwi waliandaliwa vipi, wakaenda vipi kwa amri ya nani na kwanini, na ipi ni nafasi yao katika historia ni facts zinabomoa historia yako.
Na hakika kama ulivyonena facts zimebomoa sana utunzi huu wa historia. Mtu aliyesoma kitabu chako miaka 15 iliyopita leo anajiuliza kukisoma tena, na kwa bahati mbaya akikisoma atakapofika ukurasa wa mwisho atakitoa kwa wauza vitumbua wafungie bidhaa zao.
Unapomwambia mtoto au mjukuu wa A.H.Mwinyi au Nassor Moyo kuwa baba yake ni dhwalimu kwa kufanya mapinduzi na kushirikiana na kufar Nyerere, wakati huo huo Mzee Mwinyi au Moyo wakihimiza watoto na wajukuu wao walinde mapinduzi ni kuwadhihaki, kudhihaki fikra na kuwakashf kama si kuwatusi.
Je, tukae kimya uchanganye na watoto wetu pia! not on our watch sir!