Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Aisee wakimbizi wanatuvurugia nchi

Ponda mrundi
Kinana msomali
Farid-wa mashariki ya akina osama
Sasa kumbe Mohame Saidi naye mkimbizi ndo maana anatuchonanisha tuwe kama jamaa wa Goma, na Mbuji mayi!!! Lahaula kwata leo nimejuwa ......

Mkuu umewasahau na hawa mwl/Nyerere mtutsi ( Rwanda ) Mkapa m-makua ( mozabiqui ) Padri mstaafu wilbrod slaa m-masai ( Kenya )
 
Sijamhoji baba yangu.
Haya niliyoandika ni mambo ya wakati baba yangu akiishi katika zama hizo za 1920.

Mambo yanatokea anayaona kwa macho yake.
Mimi nikaja nikaishi katika nyakati hizo.

Bado unahitaji sauti na video ya umri mzima wa baba yangu na wangu?
Lakini kubwa wewe au yeyote yule hana lazima ya kuamini nilioyoandika katika kitabu changu.

Sihitaji kuthibitisha chochote kwa yeyote awaye yule.
Nithibitishe nini ili iwe nini na kutaka nini?

Kuwa baba yangu akimjua Abdu Sykes toka utoto na ujana wao walikuwa pamoja
pale Mtaa wa Kipata na walisoma darasa moja Al Jamiatul Islamiyya Muslim School?

Kuwa baba yangu alikuwa akijua kuwa Abdu alikuwa akaifanya mipango ya
kuunda TANU toka 1950 na akimdokeza mambo yalivyokuwa yanakwenda?

Kuwa baba yangu kajuana na Nyerere nyumbani kwa Abdu Mtaa wa Aggrey mwaka 1952?

Hivi vyote vilikuwa vitu vya kawaida sana.
Yote ni matokeo ya kawaida baina ya watu.

Laiti historia ingeliandikwa bila khiyana wala pasingekuwapo na haja ya kueleza historia hii.

Mimi hakika humu natoa mengi katika yale niliyoandika miaka mingi nyuma lakini sitoi katika Wikipedia.
Wikipedia hawana maandishi yangu.

Maandishi yangu yako kwenye mradi wa Dictionary of African Biographies (DAB), New York.
Huu ni mradi wa Oxford University Press, New York na Harvard.

Maandishi hayo siruhusiwi kuyachapa popote hadi mradi umekamilika.

Siko humu kutetea chochote kwani kitabu hicho kinasomwa sasa mwaka wa 15 si kitu kipya.
Bahati mbaya kwako kuwa wewe umekujakijua kitabu hiki leo.

Asante sana mkuu, majibu yako yanazidi kuzaa maswali tena yamsingi mpana.

1) Maandishi ya bluu: Hujamuhoji Baba yako na hukuona umuhimu hivyo Watanzania milioni 44.5 ulioamua kuwabadilishia historia yao tukuamini wewe tu kwa ngano zako bila ushahidi yakinifu?

2) Maandishi ya kijana: Kwa umri alioishi mzee wako, huyo alikuwa ni kiungo muhimu cha maboresho ya historia ya nchi yetu, lakini kwakuwa uliadhimiria kuibadili historia ya Uhuru wa nchi hii, USHAHIDI pekee wenye ushawishi ulikuwa ni wa video na sauti tu za mahojiano yako na yeye kuliko wewe kumlisha maneno mzee wawatu aliyefariki huku ukiamini hana uwezo tena wakuja kukukana hapa.

3) Maandishi mekundu: umejibu hivi, "Mambo yanatokea anayaona kwa macho yake.
Mimi nikaja nikaishi katika nyakati hizo."

Kwamjibu wa jibu hili ni kuwa ulikuwepo enzi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika mpaka Uhuru kamili, Sasa naomba ufafanuzi wa haya:

a) Ulishiriki kwa namna ipi vita vya ukombozi ambavyo WAISLAMU wamekuja kudhulumika na Hayati Mzee nyerere?
b) Wewew ni mmoja ya waislamu wapigania Uhuru waliodhulumika na Nyerere?
c) Katika mda wote huo ulioishi uliwahi kumuuliza Nyerere juu ya kero yako? naomba sauti au video.
 
Mohamed Said hakuna anayemjibu kwa hoja na ushahidi kama anavyofanya yeye.Wengi ni jazba na ukereketwa wa kidini.Kwa muda mrefu amekuwa akishambuliwa yeye binafsi na si kile anachosema.Bado tunaamini anachosema mpaka pale utakapoletwa ushahidi mwanana dhidi ya kile alichosema yeye.Ajabu vitabu vyake vinakubalika na wasomi wakubwa na kufundishwa vyuo vikuu vikubwa huko ulaya,vipi wewe usiyekuwa na hoja makini wala weledi ktk historia ya nchi hii utake tukuamini katika porojo zako? Eti alichoandika ni uchochezi,chako wewe ulichoandika nini,porojo?...uongo...? ...Uzushi..? au Ukereketwa wa dini...? pinga hoja kwa hoja si kulazimisha na kushawishi wengine kwa Mohamed Said ni mchochezi. Ukitaka kujua kama Mohamed Said ni great thinker pitia post zake zote alizowahi kutoa humu,pamoja na mijadala aliyowahi kufanya hapa JF.Utaona si mtu wa jazba wala maneno ya kashfa,japo wengi humkashifu yeye binafsi bila ya kujibu anachosema
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere;5435226]Nimesoma maandiko ya ndugu yangu Mohamed Said aliyoyaMAJIBU YA MOHAMED SAID:

quote_icon.png
By Mohamed Said
Kuhusu elimu ya Waislam itatubidi tuje katika njama za Nyerere kuhujumu chuo kikuu cha Kiislam kilichokuwa kijengwe Dar es Salaam mwaka 1968 na jinsi alivyotumia uongo na ghilba kuvunja EAMWS
na kuunda taasisi kibaraka BAKWATA
Mohamed Said;5430921]Mimi sijamtukana Nyerere siwezi kukosa adabu kiasi hicho.Laiti ningelimtukana hata hao rafiki zangu wanaonialika katika taasisi zao wangenidharau.

Jasusi:Ahaa! Kwa hiyo ni maoni au interpretation yako. In other words hamna direct quote ambapo Nyerere anasema anawachukia Waislamu? We are now getting somewhere
MohamedSaid;5431529]Inasemekana Nyerere hakutaka kuja kwenye mazishi ya Abdulwahid kwa kuwa wakati ule ndiyo kulikuwa na lile tatizo la EAMWS na masheikh walikuwa wakikamatwa nyakati za usiku na kutupwa jela. Usalama wa Taifa unasemekana ulimshauri Nyerere kwa usalama wake kutohudhuria mazishi yale kwa sababu mazishi ya Abdulwahid yatahudhuriwa na Waislam wengi.
Chuki za Waislam dhidi ya Nyerere kwa wakati ule zilikuwa juu sana. Rashid Kawawa aliyekuwa Makamo wa Rais alipopata habari zile kuwa Nyerere hatofika mazishini haraka alimwendea.........
...!!! ???
 
...!!! ???

Hahaha mkuu inasemekana semekana zimekuwa nyingi hana hoja naona anajikanyaga na hii nikutokana na hao anaowaandikia kutokuwa na uwezo wa kuhoji haya mambo kwa undani wao wanalishwa tu maneno
 
Mohamed Said hakuna anayemjibu kwa hoja na ushahidi kama anavyofanya yeye.Wengi ni jazba na ukereketwa wa kidini.Kwa muda mrefu amekuwa akishambuliwa yeye binafsi na si kile anachosema.Bado tunaamini anachosema mpaka pale utakapoletwa ushahidi mwanana dhidi ya kile alichosema yeye.Ajabu vitabu vyake vinakubalika na wasomi wakubwa na kufundishwa vyuo vikuu vikubwa huko ulaya,vipi wewe usiyekuwa na hoja makini wala weledi ktk historia ya nchi hii utake tukuamini katika porojo zako? Eti alichoandika ni uchochezi,chako wewe ulichoandika nini,porojo?...uongo...? ...Uzushi..? au Ukereketwa wa dini...? pinga hoja kwa hoja si kulazimisha na kushawishi wengine kwa Mohamed Said ni mchochezi. Ukitaka kujua kama Mohamed Said ni great thinker pitia post zake zote alizowahi kutoa humu,pamoja na mijadala aliyowahi kufanya hapa JF.Utaona si mtu wa jazba wala maneno ya kashfa,japo wengi humkashifu yeye binafsi bila ya kujibu anachosema

Mkuu anachofanya Mohamed Said, ni kujibu hoja bila matusi wala kejeli. Tena ni mvumilivu sana hakuna wa kupambana naye kwa hoja.
 
Last edited by a moderator:
Dada/Mama, JF ni jukwaa huru kama navuruga mjadala ripoti kwa Mods. Usinifunge mdomo naendelea kuchangia.

Nimekushauri kwa mafaa yako mkuu, ili unufaike na mjadala huu ni vema ungekuwa msomaji tu
 
Asante sana mkuu, majibu yako yanazidi kuzaa maswali tena yamsingi mpana.

1) Maandishi ya bluu: Hujamuhoji Baba yako na hukuona umuhimu hivyo Watanzania milioni 44.5 ulioamua kuwabadilishia historia yao tukuamini wewe tu kwa ngano zako bila ushahidi yakinifu?

2) Maandishi ya kijana: Kwa umri alioishi mzee wako, huyo alikuwa ni kiungo muhimu cha maboresho ya historia ya nchi yetu, lakini kwakuwa uliadhimiria kuibadili historia ya Uhuru wa nchi hii, USHAHIDI pekee wenye ushawishi ulikuwa ni wa video na sauti tu za mahojiano yako na yeye kuliko wewe kumlisha maneno mzee wawatu aliyefariki huku ukiamini hana uwezo tena wakuja kukukana hapa.

3) Maandishi mekundu: umejibu hivi, "Mambo yanatokea anayaona kwa macho yake.
Mimi nikaja nikaishi katika nyakati hizo."

Kwamjibu wa jibu hili ni kuwa ulikuwepo enzi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika mpaka Uhuru kamili, Sasa naomba ufafanuzi wa haya:

a) Ulishiriki kwa namna ipi vita vya ukombozi ambavyo WAISLAMU wamekuja kudhulumika na Hayati Mzee nyerere?
b) Wewew ni mmoja ya waislamu wapigania Uhuru waliodhulumika na Nyerere?
c) Katika mda wote huo ulioishi uliwahi kumuuliza Nyerere juu ya kero yako? naomba sauti au video.
Ndugu yangu usijitese bure.
Kitabu hiki wala si cha kujadili leo.

Kitabu kina miaka 15 leo.
Kwa hakika maswali yako mengine yanashangaza.

Nikupe video...

Usihangaike na hayo yote.

Hiki kitabu kinasomwa kama vinavyosomwa vitabu vingine.
Wasomi wanakisomesha kama wanavyosomesha vitabu vingine vya historia.

Hivi kubwa lipi khasa hadi hupati raha na kitabu hiki.
Nakushauri kisome kitabu na ukimaliza kipuuze na endelea na maisha yako.

Hiki kitabu kwa sasa ndiyo "authority" katika historia ya TANU.
Kimekuwa hivyo kwa kuwa kitabu kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni na
utangulizi kuandikwa na Nyerere hakikukidhi haja.
 
Mkuu anachofanya Mohamed Said, ni kujibu hoja bila matusi wala kejeli. Tena ni mvumilivu sana hakuna wa kupambana naye kwa hoja.

Mkuu pevuka ndugu, ni hoja ipi aliyojibu mpaka tukaimaliza?

Tangu tuanza mjadala huu ndugu Mohamed hajajibu hoja yoyote na kuimaliza, anaziachia njiani ama anazikwepa kabisa!

Sasa ni hoja ipi uliyoileta hapa na akaijibu zaidi ya ukimsifu tu?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu anachofanya Mohamed Said, ni kujibu hoja bila matusi wala kejeli. Tena ni mvumilivu sana hakuna wa kupambana naye kwa hoja.

Ahsante sana ndugu yangu.
Mwalimu wangu wa madras Sheikh Haruna Mungu amrehemu akitufunza adabu ya mnakasha. Akisema jibu swali huku umetulia na chunga heshima wa yule unayejadiliananae. Akisema watu watauhukumu Uislam kwa kukuangalia wewe.

Haya ndiyo mafunzo yetu.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu usijitese bure.
Kitabu hiki wala si cha kujadili leo.

Kitabu kina miaka 15 leo.
Kwa hakika maswali yako mengine yanashangaza.

Nikupe video...

Usihangaike na hayo yote.

Hiki kitabu kinasomwa kama vinavyosomwa vitabu vingine.
Wasomi wanakisomesha kama wanavyosomesha vitabu vingine vya historia.

Hivi kubwa lipi khasa hadi hupati raha na kitabu hiki.
Nakushauri kisome kitabu na ukimaliza kipuuze na endelea na maisha yako.

Hiki kitabu kwa sasa ndiyo "authority" katika historia ya TANU.
Kimekuwa hivyo kwa kuwa kitabu kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni na
utangulizi kuandikwa na Nyerere hakikukidhi haja.

Mkuu wangu Mohamed Said, kitabu chako hata kama kilitungwa/kuandikwa miaka 300 iliyopita na umefanya mijadala zaidi ya milioni, bado hatuzuiliwi kuendeleza mjadala huu kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho!

Jaa kwenye mjadala, usiukimbie kwa hoja nyepesi hivyo mkuu wangu!
 
Nimekushauri kwa mafaa yako mkuu, ili unufaike na mjadala huu ni vema ungekuwa msomaji tu

Hakika Nyerere Yericko kaumia sana.
Abdulwahid aliishi na alikuwa rafiki mkubwa wa Nyerere.

Nyerere kaondoka nyumbani kwa Abdu Mtaa wa Stanley kwenda Musoma kumuoa Mama Maria.
Wameishi nyumba moja.

Mama yake Nyerere alikuwa shoga wa mama yake Abdu Bi Mluguru.
Wameishi kwa hisani kubwa sana hadi uhuru umepatikana.

Nyerere kakichukua chama mikononi mwa Abdu kwenye nyumba hiyo ofisi ya TANU ambayo
alijenga baba yake Abdu kati ya mwaka 1929 - 1933.

Hii ndiyo historia ya wazee wangu na ndiyo mazungumzo nikiyasikia wazee wangu wakizungumza.
Nakushauri hebu na wewe fanya utafiti lau mchache katika haya.
 
Ndugu yangu Mohamed Said nakwenda kanisani nikirudi nitasonga na wewe kwa faida ya watanzania wenzetu!
 
Mkuu wangu Mohamed Said, kitabu chako hata kama kilitungwa/kuandikwa miaka 300 iliyopita na umefanya mijadala zaidi ya milioni, bado hatuzuiliwi kuendeleza mjadala huu kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho!

Jaa kwenye mjadala, usiukimbie kwa hoja nyepesi hivyo mkuu wangu!

Umesema kweli haki ya kukizungumza lazima iwepo na kwangu ni faraja kubwa.
Mimi nakushauri endeleza mjadala lakini na wengine.

Mchango wangu mimi nishatoa.
Ni hicho kitabu.
 
Wakuu kama takwimu zilizo tolewa na ndugu zetu hawa Waislaam niza kweli - basi kuna tatizo kubwa nchini mwetu!! Kuna haja ya kujitazama upya kama TAIFA, hili si jambo la kupuuzia hata kidogo..
 
Back
Top Bottom