Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mkuu nikushukuru kwa uvumilivu wako wakunisibiri nimalize ibada yangu takatifu,
Naamu nimesoma hayo maandishi unayodai ni ya Nyerere na Mzee Malima ambayo yamo katika andishi liitwalo
"Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes".
Majibu ya Nyerere yanaonyesha wazi alikana madai ya waislamu tena alikana kwakutumia vinasaba vya picha ya wanaukombozi kabisa,
Lakini wewe umerudia wimbo huohuo ambao ulishakanwa!
Hiyo ndiyo ''art'' ya uandishi.
Sijarudia kipande kile bure.
Nimekirudia ili wasiojua wajue.
Nyerere kwa hakika amekana.
Hiki ni kitu muhimu sana.
Hii inawapa fursa wasomaji wa kitabu changu kutafakari.
Kipi kilipitika hadi akawa sasa Nyerere anashutumiwa kuwa hawapendi Waislam?
Waislam hawa ambao yeye mwenyewe kawasifia?
Katika kitabu changu nikachukulia kutoka hapo na kueleza matokeo yaliyotokea
baada ya uhuru kupatikana 1961.
Kipi kilisababisha Nyerere akawa mbali na Abdu.
Akawa mbali na Sheikh Hassan bin Amir.
Akawa mbali na Titi Mohamed
Akawa mbali na Dk. Michael Lugazia
Akawa mbali na Dk. Wilbard Mwanjisi.
Akawa mbali na Bilali Rehani Waikela.
Akawa mbali na Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Idd Tulio.
Akawa mbali, akawa mbali akawa mbali...
Uchambuzi huu ndiyo ulokifanya kitabu hiki kiwe kitabu cha maana na kipendwe.
Acha lugha hizo zisizofaa za ''narudia wimbo'' wewe unajadiliana na mimi.
Ritz alikuonya mapema sana kuhusu mimi.
Hukuzingatia.
Ulidhani anafanya maskhara.
Haya niloandika yamevuruga akili ya wasomi wakubwa sana.
Hawakutosheka na mawasiliano ya email na simu.
Wamenialika kwao tuzungumze uso kwa uso.
Hakuna radio kubwa duniani VOA, BBC, DW, Sauti ya Iran nk ambazo mimi sijafanya mahojiano.
Kila mtafiti katika ''Islam and Politics'' kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita hakamalishi utafiti wake sharti
aje Tanzania kunihoji.
Nakueleza haya si kwa nia ya kujisifu bali tupate kufahamiana.
Huenda ukawaidhika.
Ingia Radio Butiama ya ndugu yako Gunze sikiliza mahojiano yetu.
Hii radio iko Columbus Ohio, USA.
Imeanzishwa kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa.