31st October 2011...Sasa inanifanya niamini maneno ya
zomba (
my cousin) ameni PM na kuniambia hakuna cha
Mohamed Said wala Mwanakijiji wote hao ni system na wanawacheza shere. Ahsante
zomba kwa kunitanabahisha hayo, sasa sitopoteza usingizi wangu. Na nimeona ukweli.
Mohamed Said, nimekutetea sana na ni mwandishi mzuri sana, lakini kweli hukuwa unatetea Uislaam wala Waislaam,
unatetea na kuandika Historia ya wazee wako, na hata Uislaam unapoandikwa ndivyo sivyo hukuweza hata kutanabahi na japo kuuweka msimamo wako Kiislaam na wala kusema kweli hapo kuna kosa.
Nilichokitathmini, ni kuwa
unataka ieleweke kuwa Wamanyema na Wazulu ndio waliokuja kuwafungua macho wenyeji na wenyeji wote ni hamnapo hakunapo.
Naamini, Waislaam mlichokipanda ndio mnachokivuna. Mmeshindwa hata kuitetea aya ya Qur'an ilivyobandikwa ndivyo sivyo, mtaweza kuutetea Uislaam? Mtabaki kutetea wazee wenu, alifanya hivi walikuwa hivi wakawa vile, na hao wazee wenu kwa unafik wao ndio wakawapa msemo na nguvu watu kama kina Nyerere.