Mohamed, mnakasha ulishafungwa nami niliaga. Kinachonirudisha ni kauli zako ambazo hazina chembe za uungwana.
Mohamed Said;5587272]Nyerere ameandika hadi anakwenda hospitali akiandika...
Au hujui?
Mimi sijui kwasababu hukuwahi kutuambia mazungumzo ya Kighoma Malima na Nyerere yaliishaje baada ya kuonyeshwa picha za waislam.
Sijui kwasababu Prof Othman alipomuuliza mwalimu swali la yeye kujibu tuhuma hukutueleza mazungumzo yaliishaje.
Tunachojua wote hao ni marehemu na kama kawaida yako hukawii kuwawekea marehemu maneno.
Jinala mtu lishapata R.I.P. Mohamed anapata cha kusema.
'Kuhusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Historia...
Mie sitakupa jibu hebu wewe nenda pale kaulize kwa nini mko kimya sasamwaka wa 15 hamjaandika kitabu kujibu ''ngano'' za Mohamed Said.Au ukipenda waulize mbona hamkufanya ''review'' ya kitabu chake?
Mohamed, wasomi huandika vitabu kuamsha fikra, hawaandiki kujibu vitabu.Inawezekana baada ya kugundua kuwa hujui Nyerere alifika lini Dar kwa mara ya kwanza hawakuona sababu ya review
Au we hapa JF ndiyo unaona umefika huna tena safari?Ushatua mizigo yako.Unataka kutamba kwa kuuliza swali JF...
Pangekuwa hapana maana usingekuwa hapa JF.Ni wapi pengine watu wamewahi kubinya hadi ukashindwa kupumua?Ni wapi pengine umewahi kukiri mapungufu?
Sifa kubwa ya kitabu chochote cha kisomi ni kuja na habari mpya iliyokuwa haijulikani.
Habari mpya katika kitabu changu ilikuwa ''Islam and Politics in Colonial Tanganyika.''
Habari mpya ni kama ile ya Nyerere kutanguliza ''mzimu'' wake Dar es Salaam mwaka 1946 halafu akaja mwenyewe mwaka 1952?
Ni ile ya Nyerere kwenda sokoni akiwa hana hela? Ni ile ya Nyerere kununuliwa sarawili pale kariakoo!
Au hili pia hulijui?
Wewe ni JF, JF, JF...
JF ni kioboko au hili pia hujui? Ni wapi ambapo umewahi kuulizwa jambo au hoja ukashindwa kujibu?
Ni JF palipodhihirisha uzushi wa namba za mitihani na kuanzia siku ile hadi leo na milele madai yako kuhusu Malima kuanzisha namba za mitihani ni mwiko! umekoma1 na tumekomesha uzushi kwa vizazi vijavyo at least
Ni JF ndipo ulipoambiwa wait a minute Nyerere hakuanza siasa baada ya kuonana na Sykes, in fact alianza siasa miaka 6 kabla ya kukutana na Sykes na miaka 6 kabla hujazaliwa!
Ni JF palipoweka wazi na wewe kukiri kwa mdomo wako kuwa shirika la Marknoll lilichanga ticket ya Nyerere kwenda UNO kama walivyochanga wazee wako. Hujawahi kuulizwa kitu kama hicho Havard, Cambridge, University of Yemeni au Oxford.
Ni JF ndipo ulipokiri kwa mara ya kwanza katika miaka 15 ya uwepo wa ngano hii tamu.
Ni JF ambapo umeshindwa kuthibitisha madai yako kwa vidhibiti na kubaki kujinukuu kama ushahidi.
Pale uliposhikwa kunako ulinukuu maandishi ya Sivalon halafu ukasema umefanya utafiti.
Ni JF ambapo umeshindwa kutetea hoja za EAMWS na hilo linabaki kuwa donda kwasababu kila utakapotia mguu tutakata uthibitisho wa kina na mntiki kuhusu ushiriki wa kanisa na Nyerere.
Ni JF ambapo hukuthubutu kujibu hoja nzito na majibu yako yamekuwa kumkata kiburi kwa matusi.
Ni JF ambapo umepewa darsa la ilm ya dini kuhusu udhaifu wa kudhani Uislam ni barghashia au kanzu.
Ni JF umelazimika kuwaheshimu wapigania uhuru unaochukia majina yao.
Ni JF ambapo madai yako yamenyumbuliwa na kuonekana dhaifu hata wafuasi wako wengi wamekiri kulishwa ngano.
Ni JF ambapo mtu haonewi wala hahurumiwi, hayapendwi maandishi zinapendwa hoja.
Mohamed Said Salum Abdallah Muyukwa Semtaungo, umeshindwa kutetea hoja, umeshindwa kujibu maswali na umeonyesha upotofu wa hali ya juu.
Narudia tena kukuambia wewe peke yako huniwezi wewe njoo na wenzako 20
au na zaidi mimi nitakuwa peke yangu.Sifanyi maskhara.Mjikusanye kama mnavyojikusanya JF...
Wala hawahitajiki 20, mmoja tu anatosha.
Umeshindwa kujibu hoja kwa kichwa unakata vipande vya kitabu halafu unasema watu wenye vichwa vyao wajikusanye!!
Ungekuwa na uwezo usingekimbia maswali, usingezusha uongo na usingekiri yale yaliyowekwa bayana tena bila utafiti.
Nani atakuweza wewe bingwa wa ''inasemekana'' bingwa wa kusingizia marehemu na mtaalam wa chuki na farki.
Wewe peke yako huniwezi.Kuna mtu hapa jamvini alikuonya akakuambia, ''Huyu mume mkubwa humuwezi.''
Sheikh Mohamed, hata beberu naye ni mume kama alivyo jogoo.
Lakini unaweza kuwa mume wa mtu kutegemea na uwezo wake wa kufikiri.
Mohamed Said,hatuhitaji mume wala mke, shemeji au binamu tunahitaji ujibu hoja, maswali na utetee ngano.
Hapa hatuli ngano wala mashudu tunataka substance.
Usiughilibu umma na wewe ni tatizo kwa jamii kabla ya tatizo lenyewe.
Masalam sheikh nakutakia mchana mwema inshallah, na shughuli njema, mwenyezi mungu akujaze hekima, akuepushe na uzushi na aulinde ulimi wako inshallah. Wasalimie ndugu hapo kariakoo, nadhani joto sana sasa!
Asalaam alyakum