zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Ninachoshukuru Mungu nikuwa watu zaidi ya 35,000 wameona kwa macho yako uchochezi na uzandiki wa huyu Babu
Umeshindwa kuuonesha, uko wapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninachoshukuru Mungu nikuwa watu zaidi ya 35,000 wameona kwa macho yako uchochezi na uzandiki wa huyu Babu
Sumu yake ndio hatari. Na kama husda mzee huyu anaongoza kwa aliyoyaandika na anayoyahubiri kumhusu Mwalimu. Alitamani sana akina Sykes wawe maRais wa NCHI hii isiyo yao ya asili!
Ninachoshukuru Mungu nikuwa watu zaidi ya 35,000 wameona kwa macho yako uchochezi na uzandiki wa huyu Babu
uzuri wa hapa jukwaani kila kitu kipo wazi,kila hoja zinazoanishwa zipo wazi na watu wenye akili zao timamu wanapima,na wanajua ni kina nani wana hoja na kina nani wana viroja,,
chagua majina yote na matusi yote ya kuyasema,lakini katu hayawez batilisha ukweli ambao tayari umekwisha tamkwa na kuainishwa wazi wazi.
Zaid zaid watu wenye akili timamu wakisoma mawazo yenu huzid kuwapuuza na kuwadharau..
Mmefika hadi hatua ya kumvisha julius hadhi ya "utakatifu" ,,hakuna la kushangaza katika kauli zenu..
All in all ukweli ushafahamika,zingine mengine ni blah blah zenu tuh..
Hamtauweza ufuta ukweli huu.
Yericko Nyerere,
Hao watu 35,000 unadhani utawashikia akili, ngoja nikuambie kitu Mohamed Said nadhani ulikuwa humjui wala kuwahi kufanya naye munakasha nadhani kipindi hiki ndiyo mara ya kwanza.
Mohamed Said kafanya sana mijadala humu JF kipindi cha nyuma mwaka juzi wakati wa sherehe za uhuru wa Tanganyika kulikuwa na nyuzi zake mbili humu zilikuwa na wachangiaji wengi sana na yeye akindika makala za uhuru kwenye gazeti la Mwananchi watu walikuwa wanaligombania.
Hawa watu 35,000 kwa akili yako unadhani wamekufuata wewe.
Tafuta hizo nyuzi za Mohamed Said uone nyomi la watu wanavyozisoma. Nena Jamii Intelligence kuna uzi wake mmoja kaangalie wasomaji. Halafu wewe anzisha uzi wako wa historia ukae hata miezi mitatu uone nani atasumbuka kuufuatilia.
Mohamed Said na wewe ni sawa sawa kufananisha mlima Kilimanjaro na mlima Machemba wa Mwanza.
Yaleyale ya 'ngano'. Huyo mtoto aliyebebeshwa mimba hana jina? Huyo mkristo aliyependelewa hana jina?
Kwani nyie mmeshaoneshwa huo ushahidi au mnameza tu kila kitu mnachoambiwa kwa sababu kimetoka kwa shehe/ustaadh!?
Ni kweli kabisa. Mohamed said amejitahidi kwa kadri ya uwezo aliojaaliwa na muumba kutambulisha dhulma walizokuwa wanafanyiwa waislam huko Tanganyika. Na hili ni somo tosha sana watu kuweza kujifunza.
haiingii akilini hata siku moja katika waasisi wa TANU asiwemu Mzee Kawawa ambaye baadae alikuwa waziri mkuu wa pili wa Tanganyika, Bibi Titi Mohamed ambaye alikuwa Mwenyekiti wa umoja wa akina mama wa TANU, achilia mbali akina Jumbe Tambaza, Sheikh Ramia na Sheikh Takaridir na ndugu zangu wa mtaa wa Likoma pale kariakoo akina Mzee Mtemvu.
Je walisahaulika kwa bahati mbaya au kwa nia maalum ya kupotosha historia ya kweli ya uhuru wenu.
Mwenye akili na afikiri ...
Mbona unatoa ahadi ya kitisho?
Unaijua dhambi ya uasi? Kasome Kuruani na Biblia zote zimeeleza adhabu ya dhambi ya uasi kama ilivyomkumba Yuda
Hivi hii ligi ya kitoto mtaacha lini? Sasa kwani huu uzi kaanzisha nani? Mohamed Said au Yericko?
Mzee wenu mweyewe maji yamezidi unga, ngoma imekuwa nzito sana kwake!
Kimsingi mjadala umeshafungwa...ngoja tuwaache mkiendelea na ligi yenu ya watoto...
Acheni porojo. Ilunga hana ushahidi wowote. Ilipoonekana wanafunzi wa kiislam wamefeli kupita kawaida kwenye somo la Islamic Knowledge, mlichunguza na mkaona hitilafu, mkapeleka NECTA/baraza la mitihani, nao wakaona hitilafu katika mfumo uliobadilishwa wa ukokotoaji. matokeo yakakokolewa upya na majibu mapya yakatoka. Aliyehusika akachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Huo ndiyo tunaouita USHAHIDI. Siyo porojo za Ilunga.Huwa hatusemi kwa kukhisi, tunasema kwa ushahidi, kama ungependa kuuona mtafute Mzee wetu Ilunga akuoneshe, watu wamefunzwa na sio wa kupayukwa payukwa tu kama anyie, kutetea hoja ambazo hazina mashiko, kutete udhalimu ambao mnajua fika! narudi kusema yana mwisho na yapo karibu Insh Allah
Ni mtoto wa Nyerre Burito na Mogaya wa Nyang'ombe, wote wakazi wa Butiama kwa vizazi sita nyuma. Akina Sykes, Plantan?Unaijuwa asili ya Nyerere au unajisemea tu?
Ni mtoto wa Nyerre Burito na Mogaya wa Nyang'ombe, wote wakazi wa Butiama kwa vizazi sita nyuma. Akina Sykes, Plantan?
Butyama na Watyama wapo. Ni ukoo mkubwa tu ndani ya WAZANAKI. Vizazi vingi tu wako pale. Au nawe ni muathirika wa NGANO za Mtikila? Kama walihamia pale kama KABILA itakuwa ni miaka mingi sana kama makabila mengi mengine nchi hii. Akina Sykes hawakuja kama kabila. Hawakuja nchi hii wakiwa Waislam. Ni ujanja wa Wabondei na Wamanyema uliowaingiza kwenye Uislam. Unacheza na mabinti wa Kimanyema?Habari zako si za kweli na pia ukijisoma vizuri inabidi utueleze kabla ya hivyo "vizazi sita" ni wa asili ya wapi?. Uliza kama hujui.
Kuhusu kina Sykes na Plantan pitia kitabu hiki:
"The life and times of Abdulwahid Sykes (1924-1968): the untold story of the muslim struggle against British colonialism in Tanganyika" Kilichoandikwa na Mohamed Said.
Kinaelezea kwa kina historia yao. Jee, huo uzushi wako unaweza kuleta ushahidi kama uliopo wa kina Sykes? nakuhakikishia huwezi.
JF ndiyo sehemu ya kwanza ambayo wanaamini wapigania uhuru wa Tanganyika walikuwa 17 tu. Ukiwemo wewe Nguruvi3, Mag3, Mchambuzi, Yericko Nyerere,
Husda kitu kibaya sana.
KUna mambo ambayo ni factual:
TANU imeanzishwa mwaka 1954 - period. hatuzungumzii mtu alikuja na wazo lini.. mtu akiwa na wazo la kuoa binti fulani na mwaka fulani hatuanzi kuhesabu ndoa siku alipopata wazo na hata jina la mwenza wake. Ndoa huanza inapofungwa. Wanaotaka kusema TANU ilianzia Burma ni kuchezea maneno tu.
TANU ilipoanza kiongozi wake alikuwa Mwalimu Nyerere - wapo wanaotaka awe Sykes au mtu mwingine yeyote. Haliwezekani historia imeshaandikwa. Kusema kuwa kiongozi wa kwanza wa TANU alikuwa Nyerere siyo dharau wala kejeli kwa wengine waliokuwepo it is just a fact. Kwa mfano, huwezi kumuondoa John Okello kwenye Mapinduzi ya Zanzibar hata kama humtaki.
Waasisi wa TANU siyo kila mtu aliyekuwa mwanachama wa kwanza wa TANU au aliyeunga mkono TANU toka mwanzo. Unapozungumzia waasisi unazungumzia watu wale waliokaa chini na kuanzisha TANU. Wale waliokubaliana kuua TAA na kuunda TANU ndio waasisi. Marekani kwa mfano unapozungumzia Foounding Fathers unazungumzia wale wajumbe wa mkutano uliotangaza Azimio la Uhuru 1776. Marekani inawataja wale waliotia sahihi Azimio la Uhuru na walioandika Katiba ya Marekani (Framers of the Constitution) kama kundi kuu la Waasisi wa Marekani. Lakini Saba kati yao ndio wanajulikana sana kama Founding Fathers - George Washington, John Adams, Alexander Hamilton, Benjamin Franklin, John Jay, Thomas Jeffferson, na James Madison.
Kwa Tanzania unaweza kabisa kuweka orodha ya watu ambao tunaweza kuwaita Waasisi wa TANU (siyo waasisi wa Tanganyika) - hili ni lile kundi la viongozi wa TAA kukaa chini na kuivunja ili kuunda TANU. Majina yao yamewekwa hapo.
Kutoka hapo kuna kundi la Wapigania Uhuru ambao kwa ujumla wao tunaweza kuwaita Waasisi wa Tanganyika - Sasa hawa siyo wote walikuwa wanachama wa TANU au kama walikuwa wanachama wameingia baadaye. Katika kundi hilo wamo wale wote ambao walishiriki katika harakati za Uhuru kwa kutoa mchango wa aina mbalimbali ikiwemo kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi katika sehemu mbalimbali nchini. Hawa ndio unaweza kuwaita Mashujaa wa Uhuru.
Orodha hii ni tofauti na wale walioupinga Ukoloni - kabla ya Vita ya Majimaji kulikuwepo na juhudi za makabila mbalimblai kuupinga ukoloni sehemu mbalimbali nchini. Mashujaa wetu hawa ni wale wote waliopigana kumkataa Mjerumani na utawala wake sehemu zote na kwa namna zote ambapo anayejulikana kati yao zaidi ni Chief Mkwawa wa Wahehe na kina Nduna Songea wa Wangoni na wenzake walionyongwa pale Songea. Hawa wazee ndio waliotangulia wapigania uhuru ndio maana katika historia tuna kipindi kinaitwa "Anti-colonial movement " na Independence Struggle (harakati za uhuru).
Tatizo kubwa la maandishi ya Bw. Said kama nilivyoonesha katika ukosoaji wangu mara kwa mara ni kuwa amejaribu kupotosha historia akitumia lugha ya kuipotosha historia. Kwa mfano anaposema katika "kupigania uhuru tulipigana sisi" kwa makusudi anataka kuashiria (imply) kuwa ni wao peke yao walipigania uhuru - anajua akisema "na sisi tulipigania uhuru" atakuwa anazimua hoja yake.
Mimi matumaini yangu ni kuwa vijana wetu ambao wametusoma hapa katika mamia haya ya kurasa watakuwa wamejifunza siyo tu historia zaidi bali pia kufikiri kwa usahihi (critical thinking). Watakuwa wamejifunza kusikiliza hoja na kuzipima na hata kuzikataa bila kujali zinatolewa na nani au vipi. Ni matumaini yangu wale ambao walikuwa wanaamini tu kauli za Bw. Said sasa hivi wamejifunza kugungua mara moja anaposema vitu visivyo na msingi katika historia na pale ambapo anatupa simulizi zuri ambalo halina utata na pale ambapo anaweza hisia zake kwenye tukio na kulipa tafsiri kwa hisia zake siyo kwa historia ilivyo.
Nina uhakika mada hii imepunguza vya kutosha tu watu wanaoamini simulizi lake lisilo na msingi wa kanuni za historia.
Hoja yako nilishajadili kwa kirefu lakini mzee mwanakijiji akawapa somo zito zaidi ambalo wewe, zomba na mohamed said kwa pamoja mmeshindwa kujibu kwa hoja, na kwa mtazamo wangu na nadhani wa wengi humu, hoja hiyo ya mzee mwanakijiji per post number 3127 imefifisha hoja zenu za msingi juu ya suala husika. Kwa manufaa yenu, naomba niiweke tena hapa kwani nimewakumbusha vya kutosha lakini mmekuwa wakimbizi katika hilo. Mzee Mwanakijiji alisema hivi
zomba,
Baba ya Dully Sykes( huyu kijana aliyeimba "mimi na mabinti damdam") alikuwa rafiki yangu zamani. Alinisimulia mengi kuhusu familia hii. Namna walivyosilimu, namna walivyokuwa wakistarehe na mabinti wa Kimanyema hapo Kariakoo,..., namshangaa mzee wetu huyu Mohamed anavyokomaa na Uislam wa hawa jamaa. Hawakuwa Waislam kinamna anavyotaka mzee Mohamed tuamini. Uislam wao haukuwahi kuwagombanisha na Mwalimu.