Aaah, Mwenyeezi Mungu awarehemu waliotangulia, nawaona hivi, Maalim Sakina nilikuwa sitoki kwake mtaa wa Pemba wakati wa darsa la Al-Marhum Al Faqir Ahmed Sheikh, maaruf "Sheikh Ahmed Polisi" na hapo ndipo nilipoonana kwa mara ya kwanza na Alhabib Mwinyi Baraka.
Tahia Mwenyeezi Mungu amlaze pema, nakumbuka kuna siku AlMarhum Sheikh Kassim bin Juma katokea kwake pale Mchikichi, sisi tumesimama nje Mchikichi na Lumumba miongoni mwetu alikuwepo Tahia na Amne (aliyekuja kuwa mkewe Marehem Mbaraka Mwinshehe, gwiji la mziki kutokea Morogoro,) Sheikh Kassim kama kawaida yake ya utani-utani na sauti yake ya juu akasema "Tahia na Amne kama hamkutazama jinsi mnavyokuwa warefu haraha haraka, itabidi watokee kina Unju bin Unuku wengine kuja kuwaoa nyinyi, hao wote wafupi kwenu" akimaanisha sisi.
Aaah, umenikumbusha mbali Maalim Mohamed, mitaa yangu hiyo. Furaha ilioje kuwasoma watu nnaewajuwa fika.
Zomba,
Umenikumbusha mbali sana na mimi.
Mkabala wa nyumba ya akina Tahia ni nyumba ya bibi yake Sagaf.
Sagaf alikuwa umri sawa na mimi.
Palikuwa mzee mmoja akipiga pasi barazani pale katika 1960s.
Huyu mzee alikuwa rafiki sana na baba yangu toka utoto wao.
Hawa wameona kila kitu katika harakati za uhuru.
Tahia ni umri wangu pia.
Tahia ananihadithia anasema yeye hakuchaguliwa kuingia form one.
Basi siku hiyo Abdu Sykes kapita kwao kamkuta kakaa barazani akamuuliza,
''We Tahiya wenzako wako shule we unafanya nini hapa?'
Akamjibu, ''Sikuchaguliwa.''
Basi Abdu Sykes akamchukua kwenye gari yake hadi Aga Khan Girls.
Unajua Abdu Sykes alikuwa kwenye board ya Aga Khan Education Committee
toka ukoloni.
Tahiya anasema deski lililetwa lilikotolewa akawekewa darasani akaanza kusoma.
Mambo mengine yakafuata baadae.
Na Sindbad sijuia kama ulipata kumjua ni marehemu sasa.
Yeye nyumba yao illikuwa Kipata na Livingstone ilipo Keys Hotel sasa.
Hapo hapo karibu na akina Sykes nyumba yao ya Kipata.
Yeye marehemu Abdu alimpeleka kusoma Technical College baada ya
Form Four.
Marehemu Sindbad akaja kuwa fundi hodari wa ofice machines.
Sindbad ni rika langu na nimeshezanae mpira Kidonge Chekundu.
Allah alimpa umbo zito lakini akicheza centre half vizuri sana depsite
of his size.
Tahiya tukielewana sana na kustahiana sana.
Wakati nafanya utafiti wa kitabu hiki cha Abdu Sykes nilifanya mahojianonae na kisha
na mama yake mkubwa Maalim Sakina.
Alfakir Ahmed mimi pia alikuwa sheikh wangu yeye mtu wa tarika na akimuhusudu sana
Mwinyibaraka.
Ile darsa kwa Mama Nuru naijua sana.
Wakati umepita sana.
Mwinyibaraka alikuwa na Sheikh Hassan bin Amir katika ile safari ya Misri 1964 iliyoleta
mpango wa Chuo Kikuu kilichomuuma roho Nyerere.
Ah! Umenirudisha mbali sana.
Siku ya Eid saa kumi na moja tushavalia na akina Tahia wameshavalia tunatoka kuja Mnazi
Mmoja.
Karagosi kalewa tembo!
Juma Mlevi.
Huyu Juma Mlevi alikuwa katika TANU Bantu Group na alihudhuria mkutano wa Kura Tatu
Tabora 1958.
Those girls were smashing.
Mashaallah.
Nasi tumevaaa ''dandy'' si mchezo.
We where kids so innocent...
Nina paper nilitoa Kenyatta University 2006 kuhusu maisha ya Sheikh Kassim.
Insha Allah iko siku nitaibandika hapa.
Utamuona Nyerere ndani ya Sheikh Kassim.