Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mkuu wangu Mohamed Said kati ya mabandiko yako mengi pengine hili naweza kukubaliana na wewe.Sipingi kwamba Mwl Nyerere alikuwa hakosei hapana najua alikuwa na madhaifu yake mengi kama walivyo binadamu wote.Wakuu Ritz zomba Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Mchambuzi Mkandara... Tazameni kwa makini hiyo list ya madaktari utabaini wote ni wagalatia sasa nauliza swali rahisi sana Mwl Nyerere alikuwa akiwagandamiza wagalatia wenzake !.

Mkuu Ngongo,

Unauliza swali wakati jibu lipo wazi kila mmoja anaeleza madhira yake, alichofanya Mohamed Said kaeleza madhira yaliyowakumba wazee wake ambao ni waislam.

Ni kweli Kambarage aliwatosa hawa madaktari na wengine wakakimbia nchi, familia za hawa wazee wazalendo zipo mpaka sasa ndiyo wanajua madhira walioyofanyiwa wazee wao na Kambarage.

Lakini kwanye ili sidhani kama Nyerere atapata lawama kisa kawafanyia wakiristu wenzake.
 
Last edited by a moderator:
Huyo ndiye wa kwanza na ndiye alikuwa mweka hazina wa Jammiatul Islamiya na ndiye aliyefanya safari ya kwenda Tanga kuzileta fedha zilizomuwezesha nyerere kusafirishwa kwenda New York, bado tu huuoni umuhimu wake?

Zomba,

Hebu tujikumbushe:

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Idd Faiz Mafongo alihudhuria mkutano wa uzinduzi wa TANU katika Ukumbi wa Arnautoglu.

Haifahamiki kwa hakika hasa ni lini Idd Faiz alijiunga na TANU kwa sababu kadi yake ya kwanza ya uanachama ilipotea na akapewa
kadi nyingine iliyokuwa na namba 915 iliyotolewa tarehe 28 Agosti, 1954.

Lakini kwa kukisia tu kutokana na kadi ambayo Idd Faiz mwenyewe aliitoa kwa kaka yake Idd Tosiri ambayo ilikuwa kadi namba 25
na yenye saini yake kama afisa aliyetoa kadi hiyo, inaweza kuchukuliwa kwa uhakika kuwa Idd Faiz alikuwa miongoni mwa wale
watu wa mwanzo kabisa kuingia TANU na huenda akawa miongoni mwa wanachama ishirini wa mwanzo.

Ukichukua katika fikra ukweli kwamba Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya aliingizwa TANU na Mtemvu
katikati ya mwezi Agosti, 1955, huenda Ally Mwinyi kama katibu wa Al Jamiatul Islamiyya na Idd Faiz akiwa mweka hazina, wote
wawili waliingia TANU wakati mmoja.
 
Tufahamishe kwa nini Chifu Kidaha Makwaia, alifungwa na Wilbard Mwanjisi kwa nini alikimbia nchi.
Kwa kweli sijui lakini kumbukumbu za mahakama zipo. Mzee Mwanjisi ndugu na jamaa zake wapo.
 
Mzee Mohamed usihangaike na vitu "trivial" kama hivi hasa kwa hadhi yako ya sasa. Haya yamewakumba wengi wa DINI zote. Wewe ndie uliyekuwa unamtazama mzee huyo kwa dini yake, yeye alikuwa anakutazama kama "threat" kwa nafasi yake kwa sababu ya vyeti vyako vikali ulivyovipata ndani ya mfumokristo wa elimu bila kufelishwa!

Nisaidie zile KATIBA za TAA na TANU tafadhali.

WC,

Niwie radhi sina hizo katiba.
 
Mkuu Ritz ndiyo ushangae walioshindwana na Mwl Nyerere walikuwa wengi,watu wa makabila yote,watu wa dini zote Mohamed Said hakuliona hilo kaamua kuchagua kundi lake la wazee wa Gerezani kumbe wapo wahaya,wachagga,wapare,wanyakyusa,wapemba,wakristo,waislam na wengine wengi.

Mkuu Ngongo,

Unauliza swali wakati jibu lipo wazi kila mmoja anaeleza madhira yake, alichofanya Mohamed Said kaeleza madhira yaliyowakumba wazee wake ambao ni waislam.

Ni kweli Kambarage aliwatosa hawa madaktari na wengine wakakimbia nchi, familia za hawa wazee wazalendo zipo mpaka sasa ndiyo wanajua madhira walioyofanyiwa wazee wao na Kambarage.

Lakini kwanye ili sidhani kama Nyerere atapata lawama kisa kawafanyia wakiristu wenzake.
 
Last edited by a moderator:
Huyo ndiye wa kwanza na ndiye alikuwa mweka hazina wa Jammiatul Islamiya na ndiye aliyefanya safari ya kwenda Tanga kuzileta fedha zilizomuwezesha nyerere kusafirishwa kwenda New York, bado tu huuoni umuhimu wake?
Hilo tu? Kwa hiyo fisadi Rostam Aziz ni muhimu sana kwa URAIS wa Rais wetu JK?
 
Ritz,
Unawafahamu waweka hazina waliopita wangapi wa TANU? Kwa nini Idd Faiz pekee ndie akumbukwe? Kwa DINI yake?
WildCard,

Idd Faiz Mafongo ndiyo mweka hazina wa kwanza TANU na alihudhuria mkutano wa uzinduzi wa TANU katika ukumbi wa Arnautoglu.

Kaka yake na Idd Faiz, Idd Tosiri ambae alikuwa na kadi namba 25 ndiyo alikuwa afisa ambaye anatoa kadi za TANU.

Mwaka 1953 Idd Faiz alikuwa na umri wa miaka 43. Huyu ndiyo aliyempeleka Nyerere Bagamoyo kwa Sheikh Mohamed Ramia, pitia hotuba ya Nyerere hapo juu kuhusu safari yake ya kwenda Bagamoyo kufanyiwa dua.

Idd Faiz alikuwa akifuatana na Nyerere katika za awali za kuitangaza TANU, akihutubia mikutano jukwaa moja na Nyerere.

Huyu ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa pesa za kumpeleka Nyerere UNO. Kasafiri mpaka Tanga kukisanya michango tukuwekea picha yake.

Mkuu unawajua marais wa TAA waliyopita kabla ya Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Duh WildCard ha ha ha ha jamaa alikuwa busy kuandika habari za wazee wake wa Gerezani na kuiita historia ya uhuru wa Tanganyika.Na mimi naandika historia ya wazee wangu wa Arusha ambao Mwl Nyerere kawasahau kabisa.Nani anamkumbuka Mzee Maeda mwaafrika wa kwanza kujenga ghorofa Arusha mjini alikuwa akimpokea Nyerere na kumlaza hotelini mwake mikutano yote ya TAA/TANU ilifanyika nyumbani kwake wakoloni walimsumbua sana hadi kuyumbisha biashara zake za mabus na mahotel.Kasahaulika mzee wa watu kwasababu ya dini yake ya kikristo.

Acha utani Mzee Mohamed. Hauwezi kuandika HISTORIA ya TAA, TANU na NCHI yetu bila kupitia document muhimu kama hizi! Utakuwa umetudanganya sana. Ni aibu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz ndiyo ushangae walioshindwana na Mwl Nyerere walikuwa wengi,watu wa makabila yote,watu wa dini zote Mohamed Said hakuliona hilo kaamua kuchagua kundi lake la wazee wa Gerezani kumbe wapo wahaya,wachagga,wapare,wanyakyusa,wapemba,wakristo,waislam na wengine wengi.

Walioshidwa vipi?
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa nyerere mambo yalivurugika mpaka jeshi liliasi, zikatokea vurugu maarufu "tarehe 20" au hujuwi hilo? njaa tupu mpaka watu tukawa tunapanga foleni ili tupate sukari kilo moja kwa kaya kwa wiki nzima, kila mmoja hoi bina taabani
Neema za sasa ni kama ndoto na wakati wa Nyerere. Wadanganye wasiokuwepo wakati huo. Sokoni pamekauka, wakulima hawaruhusiwi kusafirisha hata nyanya zao, mageti kila barabara kuu za mikoani eti ya kuzuwia kipindupindu. Ukibeba kikapu mgambo wanakusimamisha kukuuliza umebeba nini, wakikuta una sukari zaidi ya kilo moja lazima ujieleze. Na rushwa hizi za wazi wazi ndio zikaanzia hapo. Unataka kusema nini wewe?

Wadanganye wasiokuwepo wakati huo au wewe umedanganywa kwa kuwa hukuwepo ukadanganyika. Kaeni muusome ukweli kwa Mohamed Said, wacheni kudanganywa na kuburuzwa kama misukule.
zomba,
naamini akili yako ni pana zaidi ya haya unayoyaandika hapa. Hebu ushughulishe ubongo wako kidogo tu.
 
Duh WildCard ha ha ha ha jamaa alikuwa busy kuandika habari za wazee wake wa Gerezani na kuiita historia ya uhuru wa Tanganyika.Na mimi naandika historia ya wazee wangu wa Arusha ambao Mwl Nyerere kawasahau kabisa.Nani anamkumbuka Mzee Maeda mwaafrika wa kwanza kujenga ghorofa Arusha mjini alikuwa akimpokea Nyerere na kumlaza hotelini mwake mikutano yote ya TAA/TANU ilifanyika nyumbani kwake wakoloni walimsumbua sana hadi kuyumbisha biashara zake za mabus na mahotel.Kasahaulika mzee wa watu kwasababu ya dini yake ya kikristo.
Mkuu Ngongo,
Ndiyo vizuri ukiandika hiyo historia ilikuwa mwaka gani?
 
Last edited by a moderator:
jasusi,

naona upo kama haupo, umepewa ofa ya kufunguwa nyuzi unajifanya hujaona? Hivi hutaki tupate darsa jingine tupanuwe mawazo?

Usigwae, ilmu ni rizki na hukujia pasipo wewe kutegemea na kupewa jukumu kama ulilopewa na mohamed said litaloweza kuwapatia wengine ilmu ukaiwacha fursa hiyo ni mfano wa mtu aliyepewa jukumu la kugawa sadaka akaingia nayo mitini na asiifikishe kwa wengi. Sitaki kuamini kama wewe unaweza kuingia na sadaka yetu "mitini".

zomba mzee wa hints..!

umenifurahisha sana mkuu,
jamaa anataka kukimbia na sadaka yetu sio??
Aje aimwage elimu yake hapa na sisi tufaidike,aache zake hizo..
 
Hoja yangu kuhusu ID nimeileta kwa sababu ya maelezo yako before

Ulizunguza hayo hapo juu kwa lengo la kuonyesha ni namna gani wewe ni mwandishi mahiri na jinsi kitabu chako kilivyo mahiri. Na hii si mara yako ya kwanza. Nilichochotaka kuweka sawa ni kuwa kuwa na kitabu katika library of congress si ujuvi wala ujuzi. Pili ni kuwa ili uwe member wa library of congress usiye raia wa marekani lazima upewe ID. Ambayo wewe huna period. And I can tell hujawahi hata kuingia mle maktabani. Otherwise kwa wamerekani ukiwa over 18 na una kitambulisho kilichotolewa na serikali ya Marekani mfano drivers licence u can access the library. Therefore it is not such a big deal kama ulivotaka kupotray. Ujumla wa hoja yangu ni kwamba hadithi zako si za kuaminika 100%. Umeshazoea kuhadhiri na kusikilizwa tu na si ku-debate.

N,

Ndugu yangu nimefika Library of Congress.
Ikiwa huamini basi.

Si jambo kubwa.
Mimi Allah kanifungulia dunia Alhamdulilah.

Nimetembea kwingi sana.

Mimi na kaka yangu sote tumezaliwa Kipata.
Yeye ni Prof. Ph D Genetics.

Iko siku tunakula dinner Cape Town na wake zetu.
Nikamwambia, ''Kaka from Kipata to Cape Town...''

Tuliangalia tulikotoka Kipata, Gerezani leo tuko Cape Town...

Ngoja nikuage na hii.

Nimewahi kuzuiwa Heathrow kuingia Uingereza kwa sababu tu passport yangu
ilikuwa imeingia nchi nyingi sana.

Walidhani mie Mzungu wa Unga...
Baada ya kujiridhisha wakaniachia.

Wewe inakutisha hiyo Washington DC kuwa sijaingia Library of Congress...

Nimefika hadi New York Columbia University kwenda kuona alikosoma shemeji yako...
Nilipokelewa na walimu wake na walinialika hadi nyumbani kwao New Jersey...

Mie si limbukeni nijisingizie nijikwaze...
Haya naeleze kukata kibri chenu.

Kwa kawaida sie huwa hatujinasibu.
 
Acha utani Mzee Mohamed. Hauwezi kuandika HISTORIA ya TAA, TANU na NCHI yetu bila kupitia document muhimu kama hizi! Utakuwa umetudanganya sana. Ni aibu.

WC,

Hapana ugomvi.
Hilo lichukulie utakavyo.
 
Ama Kwa Hakika Ndug Moh Said ni Bingwa na Mjuvi wa Minakasha..

uliaga na ukasema unaondoka wakaanza kulalamika na kukutaka urudi ya kwamba walikumis,,

sasa unazid kumwaga NONDO Wanaanza Kupata STRESS..!
 
Back
Top Bottom