Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
sawa kabisa,hakuna matata mm,,
lakini yeye hakuishia kuchukua yale aliyoambiwa na wazee wake tuh kisha akakaa chini na kuandika,la hasha usipotoshe mzee mwanakijiji,tafadhali muogope mungu wako,,
moh said kafanya utaifit,kama muandishi lazima ukae chini ufanye literature review,na katika posts zilizopita huku kaonesha lists kubwa ya vitabu vya heshima na kuaminika ambavyo yeye amevipitia katika kuusaka na kuuthibitisha ukweli kuongezea na yale ambayo kaambiwa na wazee wake,,
well,mimi ninachokiona hapa ni kwamba watu mmejiandaa kuupinga ukweli kwa gharama zozote zile ikibid,sasa tujiulize,kwani tatizo ni nini??
Kama mtu kajaribu kuandika alchokindika na kuyasema yale ambayo ameyasema,wengine kama hawaamin kwani wamelazimishwa kuyakubali??
Na kama wanaona au mnaona anapotosha,je nani kawakataza na nyinyi kukaa chini kuandika yale mnayoyajua ili kuja kuepusha vizazi vyenu kuja kupotoka na hiki alichokiandika ndug moh said??
Ukweli huu kwa sasa hauwez kufutika eti tuh kwa kuwa nyinyi hamtaki au hamkubali,ni wakati wenu sasa nanyiny kukaa chini na kukiandika kile mnachohis kina ukweli na uhalisia mzee mwanakijiji,,
lakin katika hili la ndug moh said sisi tushajitangazia ushindi tayari,siyo siri ametufungua macho sana,yani turudi tena katika upotofu hali ya kuwa ukweli ushatubainikia??
Hilo haliwezekan,hamtatukamata tena..
victory won..!!
Sawa, kwani tatizo ni kutangaza ushindi. Hapa hatuko kwenye mechi kama ni ushindi basi chukueni (sijui wewe na nani). Lakini hapa tuko kwenye kupima hoja kisomi. Unaposema "M. Said amefanya utafiti" una uhakika? utafiti gani? Hivi unajua kanuni za kufanya utafiti wa kihistoria? Kwenda na kunukuu watu kuthibitisha dhana yako (hypothesis) unafikiri ndio 'utafiti'. Kukusanya taarifa, picha na kuziwekea tafsriri ndio unaamini ni utafiti? I hope sivyo wanafundishi kwenye hivi vyuo vyetu kuwa ukikusanya taarifa (data) - hata bila kujali umekusanya vipi au sample yako ipi - inatosha kukufanya uitwe mtafiti.
M. Said hajaandika kitabu cha historia, hajafanya utafiti wa kihistoria na kazi yake haikubaliki kuitwa ya kihistoria wala kupewa heshima ya kuwa imefanyiwa utafiti wa kutosha. Ni simulizi ambalo kwa kweli unaweza kuliita 'semi-fiction' yaani katumia matukio ya kweli kuweka chumvi ya porojo. Bahati mbaya watu kama wewe wameshindwa kutofautisha ukweli na porojo.