Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Gwalihenzi, kuna usemi moja unasema hivi, "if facts dont fit your theory, change the facts". Toka mwanzoni kabisa katika maandishi yake, Mohamed Said alijua analenga nini na kwa watu gani. Research anayodai aliifanya haikuwa na nia ya kutafuta ukweli bali kuthibitisha yale anayodai alisimuliwa na watu ambao wameshatangulia mbele ya haki na anajua fika hatuwezi kuwahoji. Wote wale ambao wanahusika kwa namna moja au nyingine lakini bado wako hai, hathubutu kabisaa kuwanukuu wala kuwahoji, sababu? Njia ya muongo na mchochezi ni fupi sana.Mohamed, habari zako hazina uthibitisho hivyo haziaminiki! waambie wafuasi wako, mimi hapana.
Mohamed Said amepata mshtuko mkubwa sana baada kuwekewa pingamizi na wanajamvi wa JF ambao hawako tayari kumeza ngano zake na yaonekana kaamua kukesha humu JF kujitetea. Tatizo alilonalo ni kuwa anajaribu kujitetea kwa kutumia ushahidi wa maandiko yake yale yale ambayo yamemuumbua...makes no sense, does it?
Great spirits of leaders like Mwalimu will always encounter violent opposition from mediocre minds the likes of which we are witnessing here...fanatics driven by inferiority complex, jealousy, hatred and religious fundamentalism!
