Jasusi,
kilio changu,
Son of Alaska, ..wakati nakua, shina letu la CCM, yaani nyumba 10, lilijumuisha eneo la kanisa. ..Mwenyekiti wa shina, na mjumbe wetu wa nyumba 10, alikuwa ni Mzee wa Kiislamu. ..alikuwepo baba mmoja mtumishi wa kanisa, lakini ana tabia ya ulevi, na kumpiga mkewe. ..yule mama mke wa mtumishi wa kanisa siku nyingine mambo yakimzidia alikuwa anakimbilia kujisalimisha na kutafuta usuluhishi kwa mjumbe wa nyumba 10, yaani yule Mzee wa Kiislamu!! ..hiyo ndiyo Tanzania ambayo wengine tumekua tukiiona, sasa haya yanayotokea leo kwa kweli yanashangaza sana. WHAT HAPPENED TO US?? ..SHULENI tulikuwa hatuulizani dini madarasani, au mabwenini. siku za kuabudu zilikuwa ni Ijumaa, Jumamosi, na Jumapili. siku hizo wanafunzi walikuwa wanakwenda kuabudu na tukimaliza tunakuwa kitu kimoja tunapambana na MASOMO. ..nakumbuka nikisoma shule ya bweni, wakati wa mwezi wa RAMADHANI, Waislamu walikuwa wanapikiwa special diet kwa ajili ya futari na daku. sasa mtu anapodai serikali ilikuwa ikiwakwaza Waislamu kielimu kwa kweli nashindwa kumuelewa. ..MALUMBANO ya dini ipi ni bora au ya kweli, sikuwahi kuyasikia nikiwa shuleni. MIZOZO ya kidini kwamba upande mmoja unaonea upande mwingine nayo sikuisikia shuleni. This is a new thing to some of us.