Mohamed Said, unaweza kuamini kwamba kwa kukwepa kujibu hoja za msingi unapata hifadhi ya muda, hapana unajidanganya...nakukumbusha kuwa hii ni JF...
you can run but you wont be able to hide! Mimi narudi kule kule kwa EAMWS...
EAMWS ilianzishwa na jumuiya ya Ismailia mwaka
1945 mjini Mombasa, Kenya na wakati tawi lake linaanzishwa hapa nchini kulitokea upinzani mkali kutoka kwa jumuiya ya Kiislaam iliyojulikana kama
Al Jamiatul Islamiyya ya Tanganyika iliyoanzishwa mwaka
1933 na unayopenda sana kuinukuu
Mohamed Said. Uhusiano huu mbaya ulileta uhasama mkubwa na kutolelewana baina ya hizi jumuiya mbili...sasa maswali kwako
Mohamed Said unayedai ulifanya utafiti wa muda mrefu na kuhoji mamia ya watu na viongozi mbalimbali;
- Je, jumuiya ya Ismailia iliyoiunda EAMWS iliwapokeaje waliokuwa viongozi na wanachama wa AMNUT?
- Je, kiongozi wa jumuiya ya Ismailia, AgaKhan, aliridhia hayo masalia ya AMNUT kuvamia jumuiya yake?
- Je, Aga Khan aliridhia malengo ya EAMWS, kubadilika na kujikita katika upinzani kwa kupambana na serikali?
- Je, wakati wa kuvunjwa EAMWS mwaka 1968, jumuiya ya Ismailia chini ya Aga Khan ilikuwa na msimamo gani?
- Je Mohamed Said katika utafiti wako, uliwahi kuuhoji uongozi wa Ismailia kuhusu kuvunjwa kwa chombo chao walichokiunda wenyewe?
- Na kama uliwahoji, nani hao uliowahoji na upi ulikuwa ni msimamo wao kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na serikali?
Mohamed Said, naamini majibu ya hayo maswali unayo kama kweli ulifanya utafiti wa muda mrefu kama unavyodai ingawa kwa upande mwingine inaonekana serikali haikuwa na tatizo lolote na
Aga Khan na sana sana ushirikiano ulizidi kujengeka na kuimarika hata baada ya
EAMWS kuvunjwa.
Inasemekana kabla ya serikali kuchukua hatua hiyo uongozi wa Ismailia ulikuwa unasononeka sana kwa vitendo vya kuingiliwa katika mipango yake na
masalia ya AMNUT na waliishukuru sana serikali kwa kuingilia kati.