DM,
Ndiyo maana historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika inawatisha.
Wakaona salama iko katika kutengezeza historia mbadala na rasmi
ili wawaondoe Waislam na mchango wao.
Utaeleza vipi Abdu Sykes kumleta Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA?
Utaeleza vipi Abdu na Dossa kumpeleka Nyerere kwa Mufti Sheikh Hassan
bin Amir?
Utaelezaje Sheikh Suleiman Takadir kuwa ndiyo mwenye dhamana ya
kumtambulisha Nyerere kwa wananchi kwenye mikutano ya mwanzo ya
TANU pale Mnazi Mmoja?
Utaeleza vipi Idd Tosiri na Idd Faiz kumchukua Nyerere mguu kwa mguu
hadi Bagamoyo kwenda kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramia?
Utaeleza vipi kuja kwa Ali Mnjale na Salum Mpunga Dar es salaam mwaka
1955 kuja kumtaka Nyerere aende Jimbo la Kusini kuzima fitna za Kanisa
Katoliki lililokuwa likitisha waumini wake wasijiunge na TANU?
Na vipi iwe Rajab Diwani na Ali Mwinyi Tambwe ndiyo wafuatane na Nyerere
kwenda Jimbo la Kusini kuzima fitna ile?
Utaeleza vipi, utaeleza vipi, utaeleza vipi....?