Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kwanini nimuondoe Sykes mmoja wa waasisi na wapigania uhuru wa taifa langu?

MM na Darwin,

Wale wanajopo wa Chuo Cha Kivukoni walitatizwa sana inaelekea na historia
ya ukoo mzima wa Sykes katika historia ya siasa katika Tanganyika kama vile
Nyerere mwenyewe alipotatizwa na ule mradi wa kuandika historia ya TANU pale
walipojaribu kuiandika mwaka 1962.

Na tatizo linakuja pale unapomtia Abdu.

Ukimtia Abdu katika historia ya uhuru wa Tanganyika inakubidi umtaje na baba
yake kwa sababu baba yake alikuwa muasisi wa African Association kama katibu
mwaka 1929.

Sasa ikiwa nia ni kumkweza Nyerere kama wewe ni mtu jasiri itakubidi na uandike
habari za Chief Burito Nyerere baba yake Nyerere kuonyesha kuwa wazee wa wakati
ule wote walikuwa hadhir katika kuwakusanya wananchi kuleta umoja.

Hii kwa mtafiti wa historia ya Tanganyika itakuwa kazi ngumu sana.

Mtafiti ambae atapenda kuandika historia ya uhuru kwa kuanza na Nyerere kwa ajili
hii ni lazima amtoe Abdu na asimtaje kabisa.

Kwa mimi kule kumleta Abdu katika maisha ya siasa ya Nyerere hii ikawa imewaleta
wazalendo wengi vijana waliokuwa katika harakati toka siku ile 1950 vijana walipokichukua
chama kutoka uongozi wa wazee akina Thomas Plantan.

Matokeo yake ndiyo leo tuko hapa JF.
 
Hujajibu swali ndugu yangu. Kighoma Malima alikuta uchakachuaji upi?
Uangalie kina cha maji kabla ya kuamua kujitosa mtoni.

Jikumbushe:

Heshima kwako Mag3, ebu simama kwenye hoja mkuu.

Mie ni Mkristo, lakini nikiri kuwa Mohamed Said kaeleza vizuri sana historia ya upande wake na sijaona hapa akiongea kwa dhihaka wala dharau, may be nina definition tofauti ya hayo, mambo mengi aliyoongea humu mie binafsi sikuwahi kuyasikia, tumesikiliza sana historia za upande mmoja kumhusu Nyererea na uhuru wa tanganyika, so ni afya pia kuwafahamu wahusika wengine na upande mwingine wa Nyerere, hili ni muhimu kwa kujua kwa usahihi kule tulipotoka.

Mohamed Saidi yeye ka-base kwa wazee wake wa Gerezani, tusimhukumu kwa kufanya hivyo kwa sababu may be ndio aliko na taarifa za kutosha na za uhakika zaidi, hayo ya mashujaa wengine sasa ni wajibu wako sasa kutuhabarisha ushujaa wao tu kistaarabu tu kwa kuonyesha ustahiki wa mchango wao kwa harakati za kisiasa za wakati ule, na pia kuonyesha ni kwa namna gani basi wazee wa Mohamed said hawastahili ushujaa aliowapa.

Naamini huu ni mjadala muhimu sana, jamii yoyote isiyojua ilipotoka ni jamii mfu, so kujua mabaya kwa mazuri yaliyopita ni muhimu sana kwa taifa lolote.
 
Hapo hujajibu swali, jibu kwanza halafu uliza. Hivi nani alisema jibu la swali ni swali.
Haya ndiyo matatizo ya kumeza ngano bila tafakuri. Ukibanwa kidogo huna pa kutokea.
Kama mwalimu anakimbia wewe mwanafunzi unapaswa kufanya nini?

Nguruvi3,

Zomba anakutosha mie kuingia ni ''over kill.''
Nakujibu kwa kuwa kwa hiyo ''mwalimu'' umenikusudia mie.

Kwa ajili hii nitakujibu.

Katika ukumbi huu sijaona mtu ambae anaweza kunifanya mimi
nioneshe visigino vyangu.

Na ngoja nikueleze Zomba wala si ''mwanafunzi'' kwa maana yako.
Zomba ni ''more than average.''

Wewe nimekusoma na ninamsoma Zomba.
Hujafikia hata kugusa ''intellect'' yake.

Kama kuna walimu unawajua waonyeshe post za Zomba na waambie
wazifanyie ''assessment'' kisha wape na zako.

Unajua sisi kuwa wakati huwa tunajizuia kwa ajili ya adabu ya mjadala
na uungwana hatupendi kukuambieni kweli ya nafsi zetu kuwa tunakuoeneni
vipi katika ufundi wa kuandika hata kupanga hoja.

Ndipo niliposema wakati fulani.

Tunao wengi humu lakini kwa kuwa chombo hakizami basi na tuendelee na
safari.
 
Ndugu zangu mmesahau kwamba "upumbavu ni kapaji"?
Kama idd amini alivamia kagera na kuwaua watanzania (waliokuwa wakiishi bukoba) ...je huyo anayesema vita vya kumshambulia amini vililengwa kwa sababu ni mwislamu...si wendawazimu huu?
Ni afadhali kuwa 'mjinga' ukielimishwa unaelimika na unakuwa 'mwerevu'...kuliko kuwa 'mpumbavu'....ama kweli upumbavu ni kipaji kama kilivyo kipaji cha ufupi. Mtu 'mfupi' hawezi kujirefusha.
Serikali inaona huu upotoshaji...kwa nini haitoi tamko la kukemea 'ngano' hizi za kizushi?
Kuna haja ya somo la historia kutiliwa mkazo huko mashuleni ...tangu shule ya msingi, sekondari, vyuoni nk
somo la uraia au elimu ya siasa ifundishwe kwa msisitizo, kuwafanya raia wa tanzania (hasa vijana ) kujua ukweli wa historia ya mapambano ya ukombozi kusini mwa afrika...
 
"Umedandia daladala la Tandika na wewe unakwenda Tegeta" = Courtesy Ritz.
 
Last edited by a moderator:
Nani mwingine alikuwepo wakati anakuambia hayo? au tukubali ni maneno yako kwa sababu wewe umesema, na kuwa kwa vile yalifanyika nje ya Msikiti?

MM,

Tulikuwa sisi wawili tu.
Hapana huna lazima ya kuniamini.

Ile kuwa pale msikitini ni njiani tulikutana na ndiyo
tukazungumza hapo.

Si kama nilitaja msikiti ili niaminike.
Ningelitaka shahidi wa kile nisemacho ningemleta Allah.

Ningeapa kwa jina lake Allah.
Hii ingetosha.
 
Una contacts RTD hawewezi kukutumia kwa post mpaka tusubiri utakapoenda TZ?

Halafu umesahau kuna mtu alitoa offer hapa kwahio wewe utakacholipia ni post tu ambayo haitafika hata 20$
Zomba,
Inakuwa rahisi kama niko Dar kwenda pale RTD na kuonana nao badala ya kuwapigia simu ukiwa Marekani eti wakutumie tape/cd huko Marekani. Nilishajaribu hapo awali haikuwezekana. Lakini nikiwa hapo uso kwa uso ni rahisi kupitisha deal.
 
Umekubali Yericko Nyerere kashindwa kutimiza ahadi mpaka sasa. Hivi RTD bado ipo? Si m pm Yericko Nyerere umpe hizo "contacts".

Hivi "RTD" bado ipo?

pssss, ikihitajika dollar 100 ntampa mimi haina haja ya kungoja mpaka uje nazo.

Hata kama RTD haipo (TBC inaitwa siku hizi) kwa sisi wa zamani RTD bado ipo. Yericko hatufahamiani, na concacts zangu hawafahamiani. It is a matter of personal diplomacy. Unaelewa?
 
Hujajibu swali ndugu yangu. Kighoma Malima alikuta uchakachuaji upi?
Uangalie kina cha maji kabla ya kuamua kujitosa mtoni.

Mkuu Nguruv3
Aliyeleta habari za Kigoma Malima na uchakachuaji wa elimu ni Tanzania Kwanza, mm nimeongezea maswali chini ya swali lako ili atujibu sote, rejea nyuma nisome vizuri mkuu.
 
Nguruvi3,

Zomba anakutosha mie kuingia ni ''over kill.''
Nakujibu kwa kuwa kwa hiyo ''mwalimu'' umenikusudia mie.

Kwa ajili hii nitakujibu.

Katika ukumbi huu sijaona mtu ambae anaweza kunifanya mimi
nioneshe visigino vyangu.

Na ngoja nikueleze Zomba wala si ''mwanafunzi'' kwa maana yako.
Zomba ni ''more than average.''

Wewe nimekusoma na ninamsoma Zomba.
Hujafikia hata kugusa ''intellect'' yake.

Kama kuna walimu unawajua waonyeshe post za Zomba na waambie
wazifanyie ''assessment'' kisha wape na zako.

Unajua sisi kuwa wakati huwa tunajizuia kwa ajili ya adabu ya mjadala
na uungwana hatupendi kukuambieni kweli ya nafsi zetu kuwa tunakuoeneni
vipi katika ufundi wa kuandika hata kupanga hoja.

Ndipo niliposema wakati fulani.

Tunao wengi humu lakini kwa kuwa chombo hakizami basi na tuendelee na
safari.
dah!
hii kali ya mwaka. zomba ni zaidi ya Nguruvi3 ????????????????????
 
Last edited by a moderator:
Zomba,
Inakuwa rahisi kama niko Dar kwenda pale RTD na kuonana nao badala ya kuwapigia simu ukiwa Marekani eti wakutumie tape/cd huko Marekani. Nilishajaribu hapo awali haikuwezekana. Lakini nikiwa hapo uso kwa uso ni rahisi kupitisha deal.

Inaonesha umejisahau kuwa tuko kwenye "dot com age", haina haja ya wao kukutumia "tape/cd" wanakurushia tu kupitia internet. Ongea nao, usihofu, halafu Mwambie Yericko Nyerere anipe contacts zake na mimi namrushia "equivalent" ya dollar 100 kwa Mpesa.

Dot com.
 
Last edited by a moderator:
Hata kama RTD haipo (TBC inaitwa siku hizi) kwa sisi wa zamani RTD bado ipo. Yericko hatufahamiani, na concacts zangu hawafahamiani. It is a matter of personal diplomacy. Unaelewa?

.......

Naelewa sana. Inaniwia vigumu kufahamu "mtoto" wa Nyerere, Yericko Nyerere kushindwa kupata hotuba ya Mzee wake.

Na hii ndio inawezekana kabisa ikawa ndio sababu yake/yenu ya kushangazwa ni vipi Mohamed Said ajuwe habari za wazee wake, mpaka inawafanya muwe mna-haha.

Mnasikitisha sana.
 
Darwin,

Hiyo clip haitowekwa hapa abadan kwa kuwa
ukweli umedhihiri.

Wameisikiliza na wamepigwa na radi ya saa
saba mchana jua kali.

Mimi nisingeweza kuzua uongo hata kidogo.

...........

Mohamed Said, wewe ni mtu mzima unapaswa kuwafundisha vijana werevu.

Madai ya Nyerere kumkana Abdul Wahid umayaleta wewe.
Tumekuomba ulete uthibitisho hukuleta kwasababu ima huna au unajua kuwa ni utunzi tu.

Jokakuu ameleta maandishi ya hotuba ambayo mimi niliisikia, na wewe umeshindwa, naruDia umeshindwa kukanusha kuwa yale hayakusemwa na Nyerere.

Sasa unataka ushahidi wa video clip ambao wewe uliyeleta mashtaka unapaswa kuleta.
Jukumu la kuthibirisha madai kwa mtuhumiwa lipo kwa mwendesha mashataka na hapa ni wewe.

HuweZi kuleta ushahidi wa maandishi au video bado unataka ''wawakilishi'' wa mtuhumiwa waleta ushahidi kwa mwendesha mashtaka. Mzee Said this is too low, absurd and anachronism.

Umeeleza kuhusu hotuba maarufu ya Waikela. Kama ilivyokuwa kwa hii unayotaka video, ya Waikela huna hata nukta kuthibitisha alichokisema zaidi ya maongezi katika chai unayoyaita utafiti.

Tumekuomba uthibitishe kama familia ya Sykes haikufuja na kunyang'anya nyumba iliyotolewa na D.Cameron.
Umeshindwa kukanusha ufisadi huo na badala yake unataka video ulioithibitisha kwa maandishi kuwa ndivyo Nyeere ilivyosema.

Tumekuuliza lini Jamiatul Islamiyya fil Tanganyika ilipigwa marufuku, huna ushahidi wa jinsi gani ilitoweka. Hayo huyaoni unadai video ya kile ulichokizusha kuhusu Nyerere.

Tumekuuliza wapi ushahidi wa namba za mitihani kutumika baada ya Kighoma Malima.
Huna na ni uongo na uzushi wa kimataifa. Hilo hulioni unachokiona ni video ya madai uliyotoa wewe mwenyewe

Mlolongo ni mrefu na hapa ninachotaka kukuambia ni kuwa usifundishe vijana kuwa wajanja wajinga.
Ni ngano yako ambayo kijana mmoja amesema Malima alichakachua. Tumemtaka athibitishe hana anachoweza kuandika hata mstari mmoja kwasababu tu ameshiba ngano isiyo na ushahidi na iliyoundwa kwa majina na mitaa ya kweli huku ikijazwa na hamira.

Katika vijana wako achilia mbali wewe mwenye dhamira ya upotoshaji hakuna anayeweza kusimama na kujenga hoja. Sasa unawafundisha badala ya kufikiri na kutafakari, watumie mbinu zako chafu na za kilaghai kudai video.
Kwa umri wako na heshima miongoni mwa jamii inayokusikiliza hili halihitaji wewe kusetiriwa bali kuambiwa ukweli.

Ukweli ni kuwa Mohamed Sadi Abdallah Mwekapopo Muyukwa Semitungo, muogope mwenyezi mungu maana hakuna jihadi ya fitna, farki, uzushi, uongo na uzandiki.
Zaidi ya hapo usiendelee kutuharibia vijana kwa kuwajaza ushujaa usiokuwepo kama si uzezeta.

Hii ni nchi ya Watanganyika, na wala usiuaminishe ulimwengu kuwa Ni wamanyema, Wazulu na Wanubi waliiokomboa hivyo wanapswa kupewa vyeo kwa kutumia jina la dini ya kiislam. Hilo sasa lipo wazi na ni wavivu wa fikra wasioliona.
Hakuna waziri, Daktari au Engineer wa kimanyema atakayeteuliwa bila sifa.
 
Darwin,

Hiyo clip haitowekwa hapa abadan kwa kuwa
ukweli umedhihiri.

Wameisikiliza na wamepigwa na radi ya saa
saba mchana jua kali.

Mimi nisingeweza kuzua uongo hata kidogo.
Kama ambavyo wewe hautoweka nakala halisi ya barua ya Ally Sykes kwenda kwa Keneth David Kaunda or vice versa!
 
Kama ambavyo wewe hautoweka nakala halisi ya barua ya Ally Sykes kwenda kwa Keneth David Kaunda or vice versa!

WC,

Ndugu yangu ikiwa sasa hapa ndipo tulipofika panatosha sana.
Hizo barua zipo na citation nimeweka katika rejea kwenye kitabu.

Lakini ikiwa akili yako inakutuma kuwa Ally Sykes na Kenneth
Kaunda hawakuwasiliana na mimi kisa hicho nimekitunga...

Ushauri wangu kwako ni huu.
Acha mjadala na mimi kuhusu historia ya uhuru.

Usipoteze muda wako kujadili kitu ambacho hakina ithbati.
Ukiendelea kunifatafata baada ya ushauri huu nitakupuuza.

Namaliza kwa kukupa hili moja tu.

Sykes Papers zinajumuisha nyaraka za TAA kwa ujumla wake,
TANU na barua za Nyerere kuanzia 1953.
 
Mohamed Said, wewe ni mtu mzima unapaswa kuwafundisha vijana werevu.

Madai ya Nyerere kumkana Abdul Wahid umayaleta wewe.
Tumekuomba ulete uthibitisho hukuleta kwasababu ima huna au unajua kuwa ni utunzi tu.

Jokakuu ameleta maandishi ya hotuba ambayo mimi niliisikia, na wewe umeshindwa, naruDia umeshindwa kukanusha kuwa yale hayakusemwa na Nyerere.

Sasa unataka ushahidi wa video clip ambao wewe uliyeleta mashtaka unapaswa kuleta.
Jukumu la kuthibirisha madai kwa mtuhumiwa lipo kwa mwendesha mashataka na hapa ni wewe.

HuweZi kuleta ushahidi wa maandishi au video bado unataka ''wawakilishi'' wa mtuhumiwa waleta ushahidi kwa mwendesha mashtaka. Mzee Said this is too low, absurd and anachronism.

Umeeleza kuhusu hotuba maarufu ya Waikela. Kama ilivyokuwa kwa hii unayotaka video, ya Waikela huna hata nukta kuthibitisha alichokisema zaidi ya maongezi katika chai unayoyaita utafiti.

Tumekuomba uthibitishe kama familia ya Sykes haikufuja na kunyang'anya nyumba iliyotolewa na D.Cameron.
Umeshindwa kukanusha ufisadi huo na badala yake unataka video ulioithibitisha kwa maandishi kuwa ndivyo Nyeere ilivyosema.

Tumekuuliza lini Jamiatul Islamiyya fil Tanganyika ilipigwa marufuku, huna ushahidi wa jinsi gani ilitoweka. Hayo huyaoni unadai video ya kile ulichokizusha kuhusu Nyerere.

Tumekuuliza wapi ushahidi wa namba za mitihani kutumika baada ya Kighoma Malima.
Huna na ni uongo na uzushi wa kimataifa. Hilo hulioni unachokiona ni video ya madai uliyotoa wewe mwenyewe

Mlolongo ni mrefu na hapa ninachotaka kukuambia ni kuwa usifundishe vijana kuwa wajanja wajinga.
Ni ngano yako ambayo kijana mmoja amesema Malima alichakachua. Tumemtaka athibitishe hana anachoweza kuandika hata mstari mmoja kwasababu tu ameshiba ngano isiyo na ushahidi na iliyoundwa kwa majina na mitaa ya kweli huku ikijazwa na hamira.

Katika vijana wako achilia mbali wewe mwenye dhamira ya upotoshaji hakuna anayeweza kusimama na kujenga hoja. Sasa unawafundisha badala ya kufikiri na kutafakari, watumie mbinu zako chafu na za kilaghai kudai video.
Kwa umri wako na heshima miongoni mwa jamii inayokusikiliza hili halihitaji wewe kusetiriwa bali kuambiwa ukweli.

Ukweli ni kuwa Mohamed Sadi Abdallah Mwekapopo Muyukwa Semitungo, muogope mwenyezi mungu maana hakuna jihadi ya fitna, farki, uzushi, uongo na uzandiki.
Zaidi ya hapo usiendelee kutuharibia vijana kwa kuwajaza ushujaa usiokuwepo kama si uzezeta.

Hii ni nchi ya Watanganyika, na wala usiuaminishe ulimwengu kuwa Ni wamanyema, Wazulu na Wanubi waliiokomboa hivyo wanapswa kupewa vyeo kwa kutumia jina la dini ya kiislam. Hilo sasa lipo wazi na ni wavivu wa fikra wasioliona.
Hakuna waziri, Daktari au Engineer wa kimanyema atakayeteuliwa bila sifa.

Nguruvi,

Umekosea tena kuandika majina yangu.
Usipate tabu nakurahishia kazi yako.

Kwenye hotuba ya kuaga Nyerere alimuadhimisha vizuri sana
Abdulwahid Sykes.

Nyerere akaeleza vipi uchaguzi wao ulivyokwenda na yeye juu
ya ugeni wake Dar es Salaam alimshinda mwenyeji wake na
kuchukua uongozi.

Wala nyumba ya TAA haukujengwa kwa kujitolea kila Jumapili
kama Abdu Sykes alivyoeleza na kuwa yeye akiwa mtoto alikuwa
akifuatana na baba yake kwenye ujenzi wa nyumba ile.

Abdu Sykes ni mwongo nyumba kajenga Gavana na itakuwa vyema
kama semina paper aloandika binti yake Daisy Aisha Sykes mwaka
1968 "The Life of Kleist Sykes" akisimamiwa na John Illife ikaondolewa
Maktaba ya Chuo Kikuu kwa kuwa ni kazi ya kugushi.

Hotuba ya Waikela kwa Nyerere "Moto wa Waislam" haikusomwa
katika mkutano wa EAMWS wala Waikela hakuwekwa kizuizini nk. nk.

Yote niliyoandika ni mambo ya kutunga tu hakuna ukweli wowote.

Kitabu changu lau kama kimepata reviews mbili Cambridge Journal
of African History hao waandishi John Illife na Jonathan Glassman ni
wapuuzi kama mimi.

Hawana maana yoyote.

Hiyo kunialika kwenye vyuo vyao US kuhadhir ni magumashi tupu
wamepoteza fedha zao zilizokuwa zinawawasha.

Historia ya uhuru ilishaandikwa na wasomi mabingwa wa TANU 1981
wakiongozwa na Dk. Mayanja Kiwanuka.

Naamini ubishi sasa umekwisha.
 
Kwa wajuvi wa historia ya Tanganyika naombeni mnifahamishe hawa watu walikuwa wenyeji wa wapi.

1] Dossa Aziz

2] Kasella Bantu

3] Dustan Omar

4] Denis Phombeah

5] John Rupia

6] Mwangosi
 
WC,

Ndugu yangu ikiwa sasa hapa ndipo tulipofika panatosha sana.
Hizo barua zipo na citation nimeweka katika rejea kwenye kitabu.

Lakini ikiwa akili yako inakutuma kuwa Ally Sykes na Kenneth
Kaunda hawakuwasiliana na mimi kisa hicho nimekitunga...

Ushauri wangu kwako ni huu.
Acha mjadala na mimi kuhusu historia ya uhuru.

Usipoteze muda wako kujadili kitu ambacho hakina ithbati.
Ukiendelea kunifatafata baada ya ushauri huu nitakupuuza.

Namaliza kwa kukupa hili moja tu.

Sykes Papers zinajumuisha nyaraka za TAA kwa ujumla wake,
TANU na barua za Nyerere kuanzia 1953.
Kama barua hizo zipo, onyesha angalau nakala moja tu. Unazificha za nini wakati kitabu chako ndicho chanzo cha yote haya? Sikuachii kabisa Mzee Mohamed hata kama utanipuuza!

Mwalimu alikupuuza wewe hivo sitoshangaa nawe ukipata mtu wa kupuuza. Madhara na madhila ya kitabu chako hiki na unayoendelea kuyahubiri kwa Waislam wenzako ndicho chanzo cha chokochoko zote hizi nchini.

Naapa tena, sikuachii hata kidogo.
 
Back
Top Bottom