Mohamed Said, wewe ni mtu mzima unapaswa kuwafundisha vijana werevu.
Madai ya Nyerere kumkana Abdul Wahid umayaleta wewe.
Tumekuomba ulete uthibitisho hukuleta kwasababu ima huna au unajua kuwa ni utunzi tu.
Jokakuu ameleta maandishi ya hotuba ambayo mimi niliisikia, na wewe umeshindwa, naruDia umeshindwa kukanusha kuwa yale hayakusemwa na Nyerere.
Sasa unataka ushahidi wa video clip ambao wewe uliyeleta mashtaka unapaswa kuleta.
Jukumu la kuthibirisha madai kwa mtuhumiwa lipo kwa mwendesha mashataka na hapa ni wewe.
HuweZi kuleta ushahidi wa maandishi au video bado unataka ''wawakilishi'' wa mtuhumiwa waleta ushahidi kwa mwendesha mashtaka. Mzee Said this is too low, absurd and anachronism.
Umeeleza kuhusu hotuba maarufu ya Waikela. Kama ilivyokuwa kwa hii unayotaka video, ya Waikela huna hata nukta kuthibitisha alichokisema zaidi ya maongezi katika chai unayoyaita utafiti.
Tumekuomba uthibitishe kama familia ya Sykes haikufuja na kunyang'anya nyumba iliyotolewa na D.Cameron.
Umeshindwa kukanusha ufisadi huo na badala yake unataka video ulioithibitisha kwa maandishi kuwa ndivyo Nyeere ilivyosema.
Tumekuuliza lini Jamiatul Islamiyya fil Tanganyika ilipigwa marufuku, huna ushahidi wa jinsi gani ilitoweka. Hayo huyaoni unadai video ya kile ulichokizusha kuhusu Nyerere.
Tumekuuliza wapi ushahidi wa namba za mitihani kutumika baada ya Kighoma Malima.
Huna na ni uongo na uzushi wa kimataifa. Hilo hulioni unachokiona ni video ya madai uliyotoa wewe mwenyewe
Mlolongo ni mrefu na hapa ninachotaka kukuambia ni kuwa usifundishe vijana kuwa wajanja wajinga.
Ni ngano yako ambayo kijana mmoja amesema Malima alichakachua. Tumemtaka athibitishe hana anachoweza kuandika hata mstari mmoja kwasababu tu ameshiba ngano isiyo na ushahidi na iliyoundwa kwa majina na mitaa ya kweli huku ikijazwa na hamira.
Katika vijana wako achilia mbali wewe mwenye dhamira ya upotoshaji hakuna anayeweza kusimama na kujenga hoja. Sasa unawafundisha badala ya kufikiri na kutafakari, watumie mbinu zako chafu na za kilaghai kudai video.
Kwa umri wako na heshima miongoni mwa jamii inayokusikiliza hili halihitaji wewe kusetiriwa bali kuambiwa ukweli.
Ukweli ni kuwa Mohamed Sadi Abdallah Mwekapopo Muyukwa Semitungo, muogope mwenyezi mungu maana hakuna jihadi ya fitna, farki, uzushi, uongo na uzandiki.
Zaidi ya hapo usiendelee kutuharibia vijana kwa kuwajaza ushujaa usiokuwepo kama si uzezeta.
Hii ni nchi ya Watanganyika, na wala usiuaminishe ulimwengu kuwa Ni wamanyema, Wazulu na Wanubi waliiokomboa hivyo wanapswa kupewa vyeo kwa kutumia jina la dini ya kiislam. Hilo sasa lipo wazi na ni wavivu wa fikra wasioliona.
Hakuna waziri, Daktari au Engineer wa kimanyema atakayeteuliwa bila sifa.
Nguruvi,
Umekosea tena kuandika majina yangu.
Usipate tabu nakurahishia kazi yako.
Kwenye hotuba ya kuaga Nyerere alimuadhimisha vizuri sana
Abdulwahid Sykes.
Nyerere akaeleza vipi uchaguzi wao ulivyokwenda na yeye juu
ya ugeni wake Dar es Salaam alimshinda mwenyeji wake na
kuchukua uongozi.
Wala nyumba ya TAA haukujengwa kwa kujitolea kila Jumapili
kama Abdu Sykes alivyoeleza na kuwa yeye akiwa mtoto alikuwa
akifuatana na baba yake kwenye ujenzi wa nyumba ile.
Abdu Sykes ni mwongo nyumba kajenga Gavana na itakuwa vyema
kama semina paper aloandika binti yake Daisy Aisha Sykes mwaka
1968 "The Life of Kleist Sykes" akisimamiwa na John Illife ikaondolewa
Maktaba ya Chuo Kikuu kwa kuwa ni kazi ya kugushi.
Hotuba ya Waikela kwa Nyerere "Moto wa Waislam" haikusomwa
katika mkutano wa EAMWS wala Waikela hakuwekwa kizuizini nk. nk.
Yote niliyoandika ni mambo ya kutunga tu hakuna ukweli wowote.
Kitabu changu lau kama kimepata reviews mbili Cambridge Journal
of African History hao waandishi John Illife na Jonathan Glassman ni
wapuuzi kama mimi.
Hawana maana yoyote.
Hiyo kunialika kwenye vyuo vyao US kuhadhir ni magumashi tupu
wamepoteza fedha zao zilizokuwa zinawawasha.
Historia ya uhuru ilishaandikwa na wasomi mabingwa wa TANU 1981
wakiongozwa na Dk. Mayanja Kiwanuka.
Naamini ubishi sasa umekwisha.