Son...
Ahsante sana kwa picha hizi.
Nimeweza kuwatambua baadhi ya watu ambao si mashuhuri kwa wengi
ukimtoa Nyerere na Kambona.
Huyo kushoto mrefu kupita wote ni Said Ali Maswanya.
Nyuma yake mkono wake Maswanya wa kushoto ni Masha Bilali.
Masha Bilali alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU baada ya kuaisisiwa
mkutano ambao waliohdhuria walikuwa takriban watu 20 au zaidi kidogo.
Pembeni mwa Maswanya ni Chinyama Kaume na kushotoni kwake ni Kamuzu
Banda ndani ya suti vipande vitatu na kofia.
Pembeni ni Nyerere na Kambona.
Hapo ni New Street ofisi ya TANU ile iliyojengwa na African Association.
Sheikh MS,
Wallahi we ni Mwanahistoria! hakuna shaka hii ni Taaluma yako na unaonekana unaipenda sana Taaluma yako hongera kwa hilo!
Umemtaja Kamuzu Banda, jee, kwanini alikuja kuwa adui mkubwa wa Nyerere? naomba kujua kama Almarhum Sheikh Hassan Bin Amir alikuwa na Watoto na kama wako hai! na baada ya Sheikh kuhamishwa nchini ni nani aliyekuwa Mufti baada yake?
