Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nguruvi,

Nimekusoma.
Tubaki hapa hapa au tusonge mbele?
Acha hadithi ya Shylock muyahudi na kilo ya nyama, sema taarifa zako sio sahihi na ujitoe kwenye mnakasha baada ya kutuomba radhi. Kwa uongo huu nani ataendelea kukusoma na kukuamini?
 
Yote yanawezekana kwa uwezo wa Allah.Lakini ikiwa unatamani kitu kipya ni HIKI.usisite kuleta jibu kumsaidi Mundungus ambaye bado hajarudi. Sidhani kama hiyo mpya imeandikwa na Mohammed Said.Ikiwa ni yeye basi natanguliza kuomba samahani.
Sawa, hiyo iliandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema na anayejitambulisha kama Mwandishi Wetu, huyu anaweza akawa mtu yeyote yule, je umesoma na hii Nani kama Mwalimu Julius Nyerere? iliyoandikwa kwenye gazeti hilo hilo?
 
Mohamed,
Nina swali jingine la ziada. Usichoke na maswali yangu, tafadhali. Mara kadhaa umezungumzia Christian lobby, sasa sijui hii Christian lobby ni akina nani. Niliwahi kufanya kazi katika bunge la Marekani na malobbyist wote wakifahamika pale wanapokuja kukutana na wabunge. Utasikia huyu ni lobbyist wa farmers union, lobbyist wa jews, etc. etc. But you could identify them. Sasa wewe unazungumzia Christian lobby in Tanzania in the abstract. Can you at least put a name or a face on them? Kama ni akina Peter Kisumo, John Malecela, at least tujue hawa akina Christian lobby ni akina nani. Ni hilo tu.

Jasusi,

Taratibu hii Christian Lobby utaifahamu.
Subiri tumalize kisa cha Sheikh Malik.
 
Sikukuu na Udowe nyumba ipi? hapo kuna ya Alamarhum Sheikh Hashim bin Abdallah, usoni kwake kwa kina Moshi (nyumba imebomolewa siku nyingi sana), upande wa pili kwa kina Mwita (wapo) usoni pembeni yake kwa Sharrif. Hiyo ndiyo udoe na Sikukuu. Lete habari zako.
Ha ha haaaaa wafia dini utawajuwa tu. kwa taharifa yako mie nimeishi nyumba ya Sheikh Nurdin(kwa sasa ni marehemu)mtaa wa Udowe na sikukuu barabarani kabisaaa. Je unafahamu Sheikh Nurdin alitokea wapi hapa Tanganyika? Na je unafahamu baba yake ni nani? Musione watu tuko kimya mkaona kama hatujui hizo simulizi zenu za mitaa ya kariakoo...tukimwaga yetu hapa kwa hakika mtakimbia. ANGALIZO: mimi ni kijana ambae niko chini ya miaka 30 ki umri, so usiniulize maswali ya miaka ya 70 au 80 coz itakuwa lugha gongana.
 
Jasusi,

Nadhani nilipata kukugusia kuwa kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyoandika mapendekezo ya
katiba kwa Gavana Edward Twining.

Kamati hii iliundwa mwaka wa 1950.
Mapendekezo ya kamati hii yalizungumzwa katika mkutano wa kuasisi TANU 1954.

Yaliyokuwa katika mapendekezo yale ya Political Subcommittee hayana tofauti na yale TANU iliwasilisha
UNO 1955.

Na mengine mengi nikakueleza nikiamini utanielewa.

Kuna mengine sijayasema lakini kuhusu document hiyo nadhani unajua kuwa ilipotea na haionekani
popote.

Hiyo ''kunakili'' unasema wewe.
Mimi sijasema neno hilo.

Mimi sijasema uongo na ndiyo maana husema siku zote.
Nanyi andikeni huo ukweli tuusome.

Hivi unajua kama katika ile Political Subcommittee alikuwapo mwanasheria Earle Seaton kama mshauri
wa TAA toka 1950?

Unaijua style ya uandishi wa Seaton?
Unajua kuwa Seaton na Abdu walikuwa marafiki wakubwa?

Nadhani unatambua kwa nini nakudokeza haya.

Mzee Saidi nguli wa historia unayekumbuka hata mambo yanayoonwa kuwa yalikuwa insignificant au irrelevant mfano Nyerere alikuwa navaa nini, habari za kina Juma mlevi, Nyerere alilala wapi akiwa Tabora, swali

"Je unawakumbuka kwa majina ni wazee gani waliopewa jukumu la negotiations za uhuru na waingereza na walichaguliwa na nani na kwa nini?''
 
Ha ha haaaaa wafia dini utawajuwa tu. kwa taharifa yako mie nimeishi nyumba ya Sheikh Nurdin(kwa sasa ni marehemu)mtaa wa Udowe na sikukuu barabarani kabisaaa. Je unafahamu Sheikh Nurdin alitokea wapi hapa Tanganyika? Na je unafahamu baba yake ni nani? Musione watu tuko kimya mkaona kama hatujui hizo simulizi zenu za mitaa ya kariakoo...tukimwaga yetu hapa kwa hakika mtakimbia. ANGALIZO: mimi ni kijana ambae niko chini ya miaka 30 ki umri, so usiniulize maswali ya miaka ya 70 au 80 coz itakuwa lugha gongana.

BD,

Kwa Sheikh Nurdin nyumba yake ni Sikukuu na Kariakoo.
Huko Sikukuu na Udoe ni kwa Mzee Mwita.

Inawezekana ni siku nyingi unachanganya mitaa.
 
Sikukuu na Udowe nyumba ipi? hapo kuna ya Alamarhum Sheikh Hashim bin Abdallah, usoni kwake kwa kina Moshi (nyumba imebomolewa siku nyingi sana), upande wa pili kwa kina Mwita (wapo) usoni pembeni yake kwa Sharrif. Hiyo ndiyo udoe na Sikukuu. Lete habari zako.
Unahifahamu nyumba ya wakina Shefa? Na jee unamfahamu Ahmed Said mjukuu wa mzee Nurdin? Na je unamfahamu yule
Profesor wa chuokikuu ambae ni mtunzi au mwandishi mzuri sana wa vitabu ambae anaishi pale upanga jirani na msikiti?
Haya sasa lete habari zao kama kweli wewe ni mfia dini wa Kariakoo.
 
Mzee Saidi nguli wa historia unayekumbuka hata mambo yanayoonwa kuwa yalikuwa insignificant au irrelevant mfano Nyerere alikuwa navaa nini, habari za kina Juma mlevi, Nyerere alilala wapi akiwa Tabora, swali

"Je unawakumbuka kwa majina ni wazee gani waliopewa jukumu la negotiations za uhuru na waingereza na walichaguliwa na nani na kwa nini?''

Nyambala,

Sasa hii kitu gani sielewi nini azma yako.

Kuwa hujui unauliza kutaka kujua au unauliza
kunipima uwezo wangu?
 
Jasusi,

Mimi nimezaliwa karibia na Ikulu, karibia na uwanja wa golf, karibia na bahari.

Mwanza, Musoma, Shinyanga, Tanga, Bukoba, na kwingineko ni kuangaika tu na maisha.

Aaah, ninyi kumbe ni watoto wa Ocean Road? Wengine tulizaliwa kwenye changarawe kijijini.
 
Ha ha haaaaa wafia dini utawajuwa tu. kwa taharifa yako mie nimeishi nyumba ya Sheikh Nurdin(kwa sasa ni marehemu)mtaa wa Udowe na sikukuu barabarani kabisaaa. Je unafahamu Sheikh Nurdin alitokea wapi hapa Tanganyika? Na je unafahamu baba yake ni nani? Musione watu tuko kimya mkaona kama hatujui hizo simulizi zenu za mitaa ya kariakoo...tukimwaga yetu hapa kwa hakika mtakimbia. ANGALIZO: mimi ni kijana ambae niko chini ya miaka 30 ki umri, so usiniulize maswali ya miaka ya 70 au 80 coz itakuwa lugha gongana.

Ficha upumbavu wako hujui hata Sheikh Nurdin amefariki lini hujui Sheikh Nurdin alikuwa anakaa wapi halafu una umri wa chini miaka 30 ulingani hata na wajukuu wa Sheikh kwa umri wako huo humjui Sheikh.
 
BD,

Kwa Sheikh Nurdin nyumba yake ni Sikukuu na Kariakoo.
Huko Sikukuu na Udoe ni kwa Mzee Mwita.

Inawezekana ni siku nyingi unachanganya mitaa.
Siyo kweli, nyumba ya Sheikh Nurdin ipo mtaa wa udowe na sikukuu....mtaa wa kariakoo kuna nyumba ya wakina Malki na mzee Yasir jirani na plat pham....usiku vijana wanakesha sana wakiuza chipsi na juice za miwa. Nyumba ya wakina Malki kwa sasa imevunjwa na ina kesi mahakanani. Unamjua Kidusa na Amili?
 
eeeh, bwana eeh! nani kama Nyerere? I am a believer!
Ngoja niwawekee hii makala iliyoandikwa na Joseph Mihangwa katika gazeti la Raia Mwema toleo No. 156.

Uongozi nchini: Nani kama Mwalimu Julius Nyerere?

KINDUMBWENDUMBWE cha kugombea nafasi ya urais kinaendelea kuelekea tamati Oktoba 31, Watanzania watakapomchagua rais wa Jamhuri ya Muungano.

Uchaguzi huu unafanyika siku 17 tu tangu Watanzania waadhimishe siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 14, kuwakumbusha busara na ushupavu wa Mwalimu na makubwa aliyoyafanya katika kuongoza watu wake.

Kwa hiyo Watanzania wanakwenda kwenye vituo vya kupigia kura wakiwa na kumbukumbu hiyo na picha za wagombea ambao wanapaswa kupimwa kwa vigezo vya maadili ya kitaifa aliyoasisi Mwalimu.

Wapo wagombea makini wanaokiri umahiri na uadilifu wa Mwalimu Nyerere katika uongozi na kabla ya kampeni walikumbuka kwenda "kuhiji" kwenye kaburi lake huko Butiama; lakini wapo pia wale vichwa ngumu wanaojifanya kutotambua mchango wake nchini, Afrika na dunia nzima. Hawa ni wale waliogubikwa na upofu wa chuki kwa sababu tu Mwalimu alikuwa mwasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakasahau Taifa na utaifa.

Lakini hata kama watampima Mwalimu kwa vigezo vya CCM (ya sasa) alivyoiasisi, watakuwa hawamtendei haki, kwa sababu CCM ya sasa si ile CCM ya enzi za Mwalimu.

Kwa miaka 10 mfululizo siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imeadhimishwa kimya kimya nchini bila kutangazwa kwa marefu na mapana; wala hotuba zake kurejewa sawa sawa kwa sababu ya viongozi kuogopa kuumbuliwa na "mzimu" wa Mwalimu.

Ni "mzimu" huo wa Baba wa Taifa unaotufanya tujiulize swali hili kadri tunavyokaribia siku ya uchaguzi kumpata rais: "Nani kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Uongozi wa nchi yetu?

Hajatokea kiongozi Mtanzania mashuhuri kama Mwalimu Nyerere, ambaye ameweza kuheshimiwa na kila mtu katika Taifa, Afrika ikamtukuza, mataifa makubwa yakamheshimu na kumtetemekea hata kama hakuwa na umbo kubwa, jeshi kubwa wala utajiri binafsi au wa nchi.

Hapa nyumbani, walimwita "Mwalimu", si tu kwa sababu alikuwa mwalimu kwa fani, bali kwa kuwa pia alikuwa mwalimu wa kulielimisha Taifa kwa njia ya uongozi bora na uadilifu.

Jumuiya ya Kimataifa ilimheshimu Nyerere na kumtamani kiasi cha kumfananisha na watawala mashuhuri wa kale wa aina ya Mfalme Sulemani wa enzi za Biblia, Julius Kaisari wa Rumi ya kale na Richard wa pili wa Uingereza.

Akimkaribisha Mwalimu Ikulu ya Marekani mwaka 1977, Rais wa nchi hiyo enzi hizo, Jimmy Carter, alimsifia Mwalimu kama "mtawala mwandamizi, msoni, mwanafalsafa na mwandishi mahiri ambaye ameacha yote na kudharau vishawishi vya utajiri na raha kwa njia ya kujitoa mhanga kwa ajili ya watu wake".

Leo, tangu awamu ya pili hadi ya tatu ya uongozi wa nchi yetu, ni kiongozi gani ameweza kufumba macho utajiri umpite kando na kujitoa mhanga kwa ajili ya anaowaongoza?. Leo, utajiri unanunua uongozi na uongozi unanunua utajiri; viongozi wa leo ni sehemu ya tabaka la matajiri wakubwa nchini, tofauti na enzi za uongozi wa Mwalimu Nyerere. Kitendo cha kuhalalisha "takrima" katika kampeni za kupata viongozi ni ushahidi tosha kwamba masikini hataweza tena kupata uongozi nchini.

Hajatokea kiongozi Mtanzania, mashuhuri kama Mwalimu Nyerere aliyeweza kutema cheche za moto kutetea msimamo wake, msimamo wa nchi yake na dunia ya wanyonge na mataifa makubwa yakafyata mkia na kutii.

Akiwa na umri mdogo tu wa miaka 33 mwaka 1955, Mwalimu alihutubia Umoja wa Mataifa na kufanikiwa kuichanachana hoja ya Waingereza waliodai kwamba Watanganyika walikuwa hawajawa tayari kujitawala. Mwalimu na wenzake, walileta Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 kwa nguvu ya hoja.

Mwalimu alijulikana zaidi nje ya nchi kuliko Tanzania yenyewe kutokana na ukweli kwamba alikuwa mtetezi na msemeaji wa "uhuru wa kweli", haki za wanyonge na usawa wa mataifa yote makubwa kwa madogo.

Ni kwa sababu hii aliweka sharti kwa Tanganyika kujiunga na Jumuiya ya madola mwaka 1961, mpaka kwanza nchi ya Afrika Kusini [ya kibaguzi] ifukuzwe uanachama wa Jumuiya hiyo; na kweli ikawa hivyo.

Ni Mwalimu aliyevunja uhusiano na Uingereza kwa kuitambua Serikali ya kimabavu [UDI] ya Ian Smith wa Rhodesia; lakini akarejesha uhusiano huo baada ya Uingereza kusalimu amri kwa kuvunja uhusiano na Serikali ya kidhalimu ya Ian Smith.

Ni Mwalimu Nyerere aliyefungua milango kuunga mkono [kwa hali na mali] harakati za ukombozi barani Afrika hadi Bara lote likawa huru kinyume na matakwa ya mataifa makubwa. Ni Mwalimu Nyerere, kiongozi wa nchi masikini, aliyekuwa wa kwanza barani Afrika kuanzisha uhusiano wa nchi yake na nchi ya Kikomunisti ya China, wakati nchi nyingine zikihofu kukemewa na kambi kongwe ya Kibepari iliyokuwa na nguvu kubwa za kijeshi na za kiuchumi.

Tuambieni leo, ni kiongozi yupi nchini na Afrika, anayeweza kuikemea nchi kama Uingereza, Marekani, akasikilizwa, achilia mbali mashirika ya kifedha ya kimataifa, kama Benki ya Dunia (WB) na IMF?. Leo, Waziri Mkuu wa Uingereza ana uwezo, kama ilivyotokea 2004, kuwaita viongozi wa nchi za Kiafrika mjini London na "kuwahubiri" anavyotaka. Mkurugenzi wa WB au IMF, anaweza kumtuma rais wa Kiafrika akamletee "soda" dukani kama mtoto mdogo na akafanya hivyo mbio, kwa utii na nidhamu ya woga, huku watu wake wakiinamisha nyuso kwa haya kubwa. Haya yote yasingeweza kutokea enzi za Mwalimu kwa sababu hakupenda kuonewa yeye mwenyewe na pia wanyonge wote wa dunia hii.

Mfano mmoja ni mwaka 1982, wakati Mwalimu aliposhikana shati na IMF akipinga shinikizo la shirika hilo kwa Tanzania kuridhia masharti na sera za kurekebisha uchumi (SAPs), ikiwa ni pamoja na kupunguza thamani ya fedha yake.

Kwa kujiamini Mwalimu alisema: "Tanzania haipo tayari kupunguza thamani ya fedha yake kwa sababu tu huo ni utamaduni wa soko huria kwa matarajio ya ufumbuzi wa kila tatizo…Serikali yangu haipo tayari kutupa kando azma yake ya kutoa elimu bure kwa kila mtoto, tiba na maji safi na salama kwa wote… Wala hatupo tayari kushughulikia tatizo la upungufu (wa bidhaa) kwa kutegemea sera za fedha bila kuangalia athari zitakazoleta kwa masikini".

Edwin Mtei, waziri wa fedha wa wakati ule, ambaye pia alikuwa mtetezi mkubwa wa sera za IMF na WB alitofautiana na Mwalimu na hivyo akalazimika kujiuzulu.

Leo, sera za IMF na WB zimedumaza uchumi wetu na kujenga matabaka katika jamii na ufa kati ya walio nacho na wasio nacho unaongezeka kwa kasi ya kutisha; na vivyo hivyo ufa kati ya watawala na watawaliwa.

Hajatokea kiongozi Mtanzania, mashuhuri na shupavu kama Mwalimu Nyerere, aliyeonekana kuchukizwa dhahiri na rushwa na ufisadi ndani ya Serikali.

Kiongozi wa kwanza kuonja hasira ya Mwalimu baada tu ya Uhuru mwaka 1961, alikuwa waziri wa sheria wa enzi hizo, Chifu Abdallah Fundikira aliyetuhumiwa kupokea rushwa. Hivyo, alifukuzwa uwaziri sawia.


Mwaka 1981, Mwalimu hakuweza kumwonea haya waziri wa mawasiliano, Augustine Mwingira, ilipobainika kuwa alinunua ndege mbovu kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), kutoka kwa mfanyabiashara wa Kipalestina, George Hallack; na kwamba ndege hiyo haikustahili bei iliyonunuliwa. Alimfukuza kazi, pamoja na meneja mkuu wa ATC, Lawrence Mmasi. Magofu ya ndege hiyo yanaonekana hadi leo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.

Vivyo hivyo, mwaka huo, Mwalimu hakuweza kumvumilia Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Meli Tanzania (TSC) George Mbowe, ilipobainika kuwa alishiriki kumuuzia mfanyabiashara wa Kihindi, Akberali Rajpar, meli ya Shirika la Meli za Mwambao (TACOSHIL) – MV Jitegemee", kwa bei ya kutupa na kwa mazingira ya kutatanisha.

Mbowe na meneja mkuu wa shirika hilo, Gideon Tibesigwa, walifukuzwa kazi; ambapo Rajpar alitiwa kizuizini kwa kipindi kwa tuhuma za kuhujumu uchumi.

Na aliyekuwa meneja mkuu wa Shirika la Vifaa vya Elimu (TES), Gervas Chilipweli, na mdhibiti wake wa fedha, Mujibur Rahman, walipumzishwa kazi baada ya kugunduliwa kwa hujuma na ubadhirifu mkubwa wa fedha katika shirika hilo.

Katika kipindi hicho hicho, Mwalimu alimfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abdulnuru Suleimani, kutokana na malalamiko ya wananchi juu ya kukithiri kwa rushwa katika uongozi wa mkoa.

Leo, ni kiongozi gani mwenye ujasiri kama wa Mwalimu Nyerere, aliye tayari kusafisha nyumba yake kwa manufaa ya wanyonge na kuipatia heshima serikali yake?

Leo, licha ya Taarifa ya Tume ya Jaji Warioba kubaini mianya yote ya rushwa na wala rushwa, hakuna hatua zilizochukuliwa; mikataba yenye mizengwe imeendelea kutiwa sahihi (IPTL), mikataba ya madini na ubinafsishaji] na kufuja uchumi wa nchi; wakubwa wanajiuzia majumba ya Serikali kwa bei ya kutupa; na kwa yote hayo hakuna anayejali.

Angalia vioja hivi: kabla ya wageni kuwekeza katika sekta ya madini, kati ya 1990 – 94, sekta hiyo ilitoa ajira kwa zaidi ya vijana 400,000 na wachimbaji wadogo wadogo walichangia asilimia 15 ya pato la taifa. Leo, pamoja na sekta hiyo kukua kwa asilimia 400, sasa wawekezaji hao wanachangia asilimia 3.5 tu katika pato la Taifa. Mapato mengine yanakwenda wapi?.

Wakati huo huo, Serikali inapoteza dola milioni 20 (karibu bilioni 290) kwa mwaka kwa njia ya msamaha wa kodi (kwa mujibu wa TRA), kiasi kinachotosha kugharamia elimu yenye sifa kwa miaka mitano chini ya "Mpango wa Elimu kwa Wote" – (UPE). Tanzania inahitaji dola milioni 45 kwa mwaka kuboresha mfumo wake wa elimu.

Wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere tulikuwa na maadili ya uongozi na itikadi iliyo wazi; lakini leo, nchi haina maadili ya uongozi wala itikadi inayofahamika, huku Katiba ya nchi ikiuma na kupulizia juu ya mambo haya. Haya yote yasingeweza kuvumilika kwa Mwalimu Nyerere.

Hajatokea kiongozi Mtanzania kama Mwalimu Nyerere, mwenye kuongozwa na utaifa na uzalendo katika kuongoza, badala ya kuongozwa ukereketwa wa vyama vya siasa.

Ingawa Mwalimu alikuwa mwasisi wa mfumo wa chama kimoja nchini, aliona mapema udhaifu wa mfumo huo na pia wakati gani mfumo wa vyama vingi ungeweza kujitokeza.

Ni mwaka 1962 alipoliweka wazi jambo hili aliposema, kwamba Tanzania haikuhitaji mfumo wa vyama vingi kwa sababu hapakuwa na matabaka nchini; na kwamba "itakapotokea matabaka ya kijamii kuibuka nchini, hapo vyama vingi vya siasa vitaibuka, tupende tusipende".

Mwalimu alisema, kama hilo litatokea, itamaanisha kwamba TANU (CCM?) imeshindwa kuongoza.
Ni Mwalimu Nyerere aliyebaini kuwa CCM ambacho kinapashwa kuwa chama cha watu na chombo cha maendeleo, sasa kipo tu kwa ajili ya chaguzi za kisiasa, alisema: CCM kipo kwa sababu tu kinabebwa na Sheria inayozuia Upinzani…… Kukosekana kwa Upinzani kunakifanya chama kisinzie kwa kuamini kwamba kimeshika hatamu".

Alibaini ya kuwa CCM kiligeuka kuwa chama cha viongozi badala ya kuwa chama cha wanachama, na hivyo yalihitajika mabadiliko kukifanya kiwe karibu na watu.

Ni kwa sababu hii Mwalimu alianzisha mjadala juu ya mfumo wa vyama vingi, kwa mara ya kwanza Februari 1990, mjini Dar es Salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari; na mara ya pili Juni 26, 1990 mjini Mwanza, kwenye mkutano wa Umoja wa Vijana wa CCM. Ni Mwalimu Nyerere aliyebaini kwamba, mfumo wa vyama vingi haukwepeki; mengine yote ni ngonjera tupu.

Haijatokea kiongozi Mtanzania mwenye kuwa karibu na watu, mwenye kuishi maisha ya kawaida na uwezo wa kuwasiliana na watu moja kwa moja na kujenga imani kwao kama Mwalimu Nyerere.

Ni kiongozi yupi leo, aliye tayari kwenda vijijini kuchanganyika na watu shambani, akawafundisha kilimo bora na jinsi ya kupambana na malaria?

Mwalimu aliweza kufanya hivyo; lakini "shangingi" za viongozi wa leo zinaogopa tope kuwafikia wanaovuja jasho mashambani.

Kwa kifupi, Tanzania haijatoa kiongozi shupavu, mwadilifu na mahiri aina ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere. Hata kwa bara la Afrika, ni hayati Kwame Nkrumah wa Ghana pekee anayeweza kulinganishwa naye.

Tunapoelekea Oktoba 31, 2010, tuna kila sababu ya kujiuliza katika harakati za kujihakikishia uongozi bora: Nani kama Mwalimu Julius K. Nyerere?


Nani kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!
 
Ndugu, Mimi nimezaliwa kabla ya uhuru. Mama yangu Mkiristo na baba yangu Muislam. Nimefuatilia mnakasha huu, lakini nazidi kuchanganyikiwa. Naomba wachangiaji hapa ambao wengi mmedhihirisha uwezo wenu kwa hoja mtueleze kila mmoja kwa wakati wake suluisho la tatizo hili kati ya jamii yetu (Waislam na Waksrito). La sivyo mtaendelea na huu mtanange ambao hautakuwa na mwisho.

Mpaka sasa pande hizi mbili ni 2 parallel sides which will never meet.
For the sake of harmony in our up to now peaceful nation we need to reach a compromise.
Let us concentrate on the future and our well being.
 
Matola,

Nilitaka kukuonyesha ustaarabu lakini inonekana ustaarabu
unapouweka sipo unakuwa umeudhulumu.

Ukweli ni kuwa raia wa Afrika Kusini hawakuwa na ruksa ya
kuingia Tanzania.

Mohamed,
Na wale wafuasi wa ANC waliokuwa na kambi zao Morogoro si raia wa Afrika kusini?
 
Hili ni kweli kabisa.
Hapana. Hii si kweli kabisa. Kama wewe ni mtafiri mahiri ungejua kwamba Nyerere hakutaka Biafra ijitenge kwa madai ya kunyanyaswa na waislamu. Nyerere alichukua muda kuleta upatanishi kati ya Gowon na Ojuku na Gowon akawa mkaidi. Wakati huo Waibo wakiendelea kuuawa kama wanyama na Wahausa. There was a pogrom against the Ibos in Nigeria. Ila kwenu ninyi kama Muislamu anaua Wakristo siyo nongwa, inaonekana. Kuna thread humu aliianzisha William Malecela kuhusu Biafra. Itafute. Tulimpa somo kule. Kwa hiyo usidanganye watu kwamba Nyerere alitaka Biafra ijitenge kwa sababu hizo alizotaja mfumo.
 
Unaijua historia ya Kariakoo wewe? Unajua kuwa wakati wa Mjerumani Kariakoo haikuwepo? Unajua Kariakoo ilikuwa ni shamba tu la Mjerumani alilolinunua kutoka kwa Sultani? Kwa ufupi ni kuwa baada ya vita vya kwanza vya dunia Kariakoo ilikuja kuwa kituo cha kijeshi na baadaye makazi ya kwanza ya African Carrier Cops (kariakoo). Unajua baada ya Uingereza kuiasisi Tanganyika kwa nini iliitwa nchi ya Rangi Tatu? Unajua ni mwaka gani iliamuliwa na serikali ya wakati huo kuligawanya hilo shamba kuwa viwanja na kuwapa "natives"? Unajua "natives" wa kwanza Kariakoo walikuwa ni wa jamii ipi? Usichokijua ni kama usiku wa giza, pole sana.
Ritz, kuna misitu ambayo ukiingia unatakiwa uwe na zana hasa wala si visu vya kukatika mikate. Haya Ritz hebu tupe upande wa pili wa historia maana upande wa kwanza ndio huu.
 
Back
Top Bottom