Mzee Mwanakijiji
Ni hitimisho zuri na sahihi.
Yeyote atakayedai kuwa kuna dhulma dhidi ya waislam, hawezi kuleta ushahidi nje ya maandiko ya Moh Said, Njozi na vitabu vya akina Sivalon wanavyovitaja. Dhulma gani hiyo ambayo kuonekana kwake mpaka kwa vitabu tu? Tena vitabu vyenyewe vinmeandikwa "inasemekana..."
Kwenye maisha ya kawaida huku mtaani kila observation ina maelezo yake:
"Wahindi wengi wamefanikiwa biashara kwa sababu wana umoja na wanainuana kwenye mitaji".
"Fulani na fulani wana utajiri wa kurithi kutoka kwa babu yao ambaye alikuwa jambazi."
"Ukoo ule wanapenda shule na wamesoma sana"
"Wakinga, wapemba na Wachaga wanafanikiwa kibiashara"
"Wale jamaa hawathamini shule, wanapenda sana ufugaji na uwindaji"
Watu ninao wa-refer kwenye statements hizo wanaweza kuwa wa dini yoyote. Na sijawahi sikia kuwa fulani kafanikiwa kwa sababu ya ukristo wake au kashindwa maisha kwa sababu ya uislam wake.
Kwa kweli hakuna ushahidi wowote huku mtaani wa dhulma dhidi ya waislam. Shida na raha sote tunazipata. Waislam wanadhulmiwa kwenye maandiko tu ya Moh Said.