Sheikh Mohammed Said,nimekusoma kwa makini saana tangia mwanzo wa thread hii yoote. Nimeona na kukubali ustadi na umahiri na jitihada zako katika kuweka historia kwa mujibu unavyoifahamu. Pamoja na makosa madogo madogo lakini nakubaliana na wewe kwa mengi ulosema. Na mintaarafu ya mjadala huu kufunguliwa ilikua ni juu ya uchochezi unaofanya hapo na ati kutaka kuhatarisha amani. Si kweli japo hii pia kama ulivyosema mara kadhaa haizuii wengine kufikiria watakavyo.
Haya malumbano ni hakika hayatakwisha hata miaka kadhaa. Maana kila mtu ana perception,stereotype na prejudice tafauti kutokana na mila na dasturi alizotoka. Ndo maana japo woote mnahisi mnazungumza lugha moja kiswahili lakini muafaka ni mdogo mno. Kwa mfano mambo kadhaa ya kashfa,kejeli na tashtit upatazo humu na kulalama lakini hao wanaokutolea ati hawajui kuwa wametukana!? Nakusifu saana kwa sabra ilokujaa na hiyo ndio tamaduni na dasturi ya msomi wa kikweli.
Kwa ufupi pamoja na hayo yoote mintaaraf ya bayana yangu hii kukuomba ujitoe rasmi kwenye kilingi hiki na ufungue kilingi kingine kwa mafundisho yako ya historia humuhumu JF....labda ukiite Baraza ya Mohammed Said!?ahahah!! Insha Allah wale tutakaokutaka tutakufuata huko na nina hakika itakua ni wengi mno. Maana hapa nahisi ni marudio tu na yule Yericko Nyerere alotoa hiyo mada ya shutuma naona amekua mchangiaji mdogo mno shughuli kawaaachia wenzie!?
Sisi wengine tushapitia saana hizo historia za wazungu miaka kadhaa mpaka zatutia kizunguzungu,ndo maana ni muhimu pia tuwape nafasi kina sie/wenzetu ili nao watupe habari. Matokeo yake uinakua udini,kashfa,jazba na malumbano yaso maana! Najua ni rahisi saana mzungu yeyote hata kama ni mpuuzi kuandika historia ya Tanganyika na kukubalika,hasa pale anapotia mbwembwe kama vile Bwana Nyerere alikutana na mtu fulani kwenye cossy pub/restaurant fulani hapa city centre Mzizima na alikua amevalia suti ya rangi kijivu!ahaha!!....inakua rahisi watu kumuelewa kwa sababu tayari maarifa na akili zetu zina hamu na shauku za myth za kihali fulani! Leo unapokuja wewe Sheikh Mohammed kueleza habari huku ukitaja mitaa ya kariakoo na unakunywa togwa na vitumbua hata kama ni za kweli lakini itakua ngumu mno ku-penetrate kwenye skull ya watanganyika wenzio!....Japo hao hao unaowaeleza inawezekana wakati ndo kwanza walikua Kwimba,Magu, Tandahimba au ngara wakinywa mataputapu na kutafuna senene/panzi!....Hii ndo faida/hasara mojawapo walotuachia wazungu! Na hapa ni hao hao wazungu ndo wanaofaidi na kuneemeka! Wametufanzia mengi saana machafu,leo wametuacha na hasama na kutoaminiana pita kiasi!
Kwa kumalizia Sheikh Mohammed natumai utalikubali ombi langu na kufungua thread/kibaraza chengine ili na sisi wengine tuweze kukuuliza masuala ya kina na labda Insha Allah tujadiliane na kufahamiana.
Mabwana Ritz,The Big Show,Kadogoo,Barubaru na wengine wengi Insha Allah Mola tawalipa fadhila zenu kwa kuwa na Sheikh Mohammed katika mjadala huu.
Mabwana Jasusi,Jokakuu,Nguruvi,Mag3 na Mwanakijiji,mmefanya jambo zuri saana kumhoji Sheikh Mohammed Said kwa kina japo wakati mwengine lugha zilikhitilafiana na ikakurubisha jazba na kejeli kadhaa. Lakini haina neno ndo mambo ya mijadala kama hii. Nina hakika nyinyi ni watu wazima na hishma nyingi saana na hikma zisizo mipaka. Natoa shauri huu mjadala ufungwe maana unakwenda nje ya mintaaraf ilofanywa uanzishwe!? Ndio maana mnaishia kuzungushana kwa maswali na majibu yaleyale na hatimae tunaendea kwenye mambo ya slavery. Haya mambo ya slavery ni very complex subject,kama wapo watakao ili tuzumgumzie masuala kama haya na kuelimishana na kujadiliana kwa undani basi ifunguliwe thread nyingine. Nami Insha Allah japo kwa uchechefu lakini tajitahidi kuchangia maana ni mojawapo ya fani yangu. Kwa mfano kuanza kuitana walowezi,wakati hao unaowaita walowezi wana zaidi ya karne hapo Tanganyika...nafikiri tujaribu kupendana na kuelezana kwa njia nzuri kama ilivyokua enzi za mababu zetu!
Kwa ufupi inastaajabisha kama Serikali imekiona na kukiachia kitabu au vitabu vya Mohammed Said vitambe takribani miaka kadhaa na hata Bwana Nyerere mwenyewe nae hakuona haja ya kujibu,sasa huo uchochezi unatokea wapi!? Maana nafahamu kuwa vitabu vilivyoonekana hatari kama cha Prof. Njozi The Killings of Mwembechai, si tuliona havikuchua hata duru vikafungiwa!? Serikali za awamu kadhaa wamekikuta na kukiacha hiki kitabu ni kweli hwakuona au hawauoni huo uchochezi wa kuhatarisha amani ya nchi kama alivyodai Bwana Yericko Nyerere alipoanzusha mada!?
Njia nzuri na ya kuthibitisha hizo tuhuma dhidi ya Sheikh Mohammed,wanataaluma kama kina Prof Mushi na kama kuna wengine humu wajitolee kuandika kitabu kingine na kuzidi kutufumbua macho soote! Maana tangia hii thread ifunguliwe kuna mambo kadhaa alosema na kutujuza Sheikh Mohammed,kwa ufupi ni kukusanya yoote iwe ushahidi dhidi yake kwenye hicho kitabu kingine. Naye Sheikh Mohammed au mwengine siku yoyote atatokea aidha kupinga kitabu hicho na kuandika kingine,kwa utaratibu huo sisi tusojua ndo tutazidi kufahamu. Kwa mfano mdogo tu angalia JF Kennedy ana biography zaidi ya nne
na kutoka kwa critics wa kila upande.
Tutumie vyema haki yetu ya kujadili na kufahamisha!