gombesugu, jaribu kupoa kidogo usije ukachemka. Baada ya hii post yako, sasa naweza kukiri kwa mbali kwamba naanza kukuelewa. Hata hivyo nina ombi kwako, tulia uipitie hii post yako na ikiwezekana uifanyie "
editing" pale itakapobidi, hii post inakuangusha...ama na wewe umeamua kuoga dimbwini na watoto? Ombi la pili, kama hutaudhika, jaribu kutumia kiswahili, hizi lugha za watu mtu akizidandia bila tahadhari, anaweza akapoteza kabisa maana ya ujumbe aliotaka kuufikisha. Mwisho natoa tu ushauri kuwa kabla ya ku"
post reply" jaribu kubonyeza "
preview post" usome uliyoyaandika na ukisharidhika kwamba hayana makosa yanayotokana na ama kwa kutokujua au kwa kukusudia, bonyeza "
submit". Ukifanya hivyo nitajitahidi nijibu mada kama ulivyoitoa hapo juu, asante...tuendelee.
Mag3,
Nilihisi kuwa ungekuwa wa awali kunijibu!ahaha!!
Mbona unaleta maneno ya kwenye kanga hapa jamvini Mzee wangu?
Naona wewe na Nguruvi3,mnajipa dhiki kubwa kwa kuwasaidia Waislamu na kuipunguzia mzigo Serikali hapo.
Nguruvi3,ati anatafutia vibarua/ajira Waislamu na wewe unataka kuanza kunisomesha mimi english literature na grammar. Kwa hicho kizungu chako cha enzi ya mkoloni naomba upumzike tu Mzee wangu. Kwani huna jamaa au wajukuu zako huko mkoani/kijijini kwenye asili yako wenye dhiki ya elimu?
Kwa ustaarabu,ulitakiwa unisamehe si unajua mimi ni kati ya wale wa Madrasa? Kwa uchechefu wa elimu yangu pia italazim umlaumu mwalimu wangu na sahib yangu wa miaka mingi Dr. Peter Breunig wa pale Univ of Frankfurt.
Nakufahamisha,hiyo english kwangu ni baadhi tu ya four International languages ambazo niko fluent ukiondoa kiswahili. Kila mojawapo ya hizo lugha nazungumza kwa lafidh/accent yenye ladha ya kutamanisha!ahaha!!
Mag3,nasikitika kuwa tangu nimejiunga hapa tayari ulijifanya ushanijua na kunishuku. Kwa dasturi zenu hizo mtapata tabu saana. Kila anayekubaliana na hoja za Sheikh Mohammed Said,mnajitahidi kumpa dhiki na madhila ya kila namna.
Nastaajabu,mbona huyo mnafiki mwenzio aliyejaribu kufurukuta kujibu,ameonyesha japo kwa ufedhuli kuwa ujumbe umemfika? Inakuwaje wewe jambo usolifahamu linakushughulisha na utoe kibri?
Watu wangapi hapa wanaandika "utumbo" na message zao zina typographical errors na makosa kadhaa lakini tunastahamiliana na kujaribu kufahamiana?
Au unafikiri kila mtu ana wakati wa kupoteza ili ashinde kutwa kwenye laptop na kujibizana na wewe?
Tafadhali Muheshimiwa Mag3,wewe ni mmojawapo wa wakubwa wetu hapa jamvini nami binafsi nakustahi saana na nilishakufahamisha mara kadhaa hapo awali.
Tuendelee na mnakasha.
Shukran.
Ps; Some people miss the message,because they're too busy looking for the mistakes!