Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mkuu JokaKuu nimemjibu hili suala akakaa kimya nikadhani ni mtu anayaelewa. Amelirudia akidhani ni point kubwa sana kumbe ni point ambayo huwezi kuamini huyu ndiye alikuwa mchumi anakaa na akina Mzee Mtei. Barubaru point hii ni ya mtoto wa mtaani asiyebahatika kukanya darsa.Acha kabisa!Barubaru,
..sasa mambo ya kusomesha watoto yameingiaje hapa??
..nani amekwambia wanawe Mwalimu hawajasoma, na hakuna aliyefika chuo kikuu?
..hivi unafikiri kila mzazi anayependa mwanawe afike chuo kikuu, anafanikiwa ktk lengo hilo?
..mimi namshukuru Mwalimu kwamba wakati wa utawala wake elimu ya Tanzania ilikuwa ni ya viwango.
..ilikuwa ukihitimu form 4, 6, University, kweli unakuwa umewiva kulingana na daraja ulilofikia siyo kama miaka hii.
..kuhusu mapigano mkoani Mara, wakati wa Mwalimu hali haikuwa mbaya kama sasa hivi. wakati wa Mwalimu hali ya usalama ilikuwa nzuri kuliko sasa hivi.
..wewe mwenyewe si ulikimbia kwenu Znz kuja kuishi na kusoma huku Tanganyika?? Sasa hata kwa hilo humshukuru hata kidogo Mwalimu Nyerere??
cc😡Jasusi, Mag3, Wickama, Kadogoo, Ritz, Nguruvi3
Anachotaka kusema hapa ni kuwa ukiwa profesa basi lazima watoto wako wawe maprofesa.
Anasahau kuwa learning inaambatana na mambo mengi sana.
Na wala haimanishi kuwa ukiwa na degree basi utakuwa umeelimika.
Sijui anamweka kundi gani Bill gate. Baba wa taifa la Zanzibar mh Okello alikuwa na degree ngapi?
Kuhusu mapigano Mara niliwahi kumuuliza anitajie nchi moja tu duniani ambayo haina mizozo au migogoro ya kijamii.
Nchi moja tu! hakuweza na narudia tena nchi moja tu. Kama hatataja basi akae kimya maana sina uhakika kama atakuwa anajua anaongelea nini.
Chuki ni kitu kibaya sana, kinaweza kukudhalilisha hata kama umevaa nguo.
Gharama za chuki ni mbaya kuliko kutembea mitaani uchi.