Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si kweli! Hapa ndipo hoja ya Mag3 inapokuwa na nguvu sana.
Mag3 ameweka wazi jinsi Nyerere alivyokuja mwaka 1946 (kama mwaka ni sawa) na akauliza wakati huo Abdul alikuwa na sifa gani katika siasa?
Nyerere alikutana na Dosa Aziz kabla ya kukutana na Abdul. Kwa uchache alikuwa ameshaanza kufahamiana na wanamji
Ama kuendesha Benz kama hilo lilitokea basi kwa nyakati hizo ilikuwa ni heshima kwasababu Watanganyika wengi hawakumudu kiatu sembuse Benz. Sasa kuheshimiwa ikiwa ni pamoja na Nyerere hayo ni maneno yako kwasababu hakuna mahali pamenukuliwa akisema hayo. Tunaheshimu sana mawazo yako binafsi na si ya kihistoria.
Wazee wote waliopigania uhuru wa nchi hii wanapaswa kupewa heshima.
Hakuna mwenye heshima kubwa au ndogo, heshima ni heshima.
Jitihada za kumpandisha Abdul awe Rais wa TAA na TANU kisha Tanganyika haziwezi kuzaa matunda kwa werevu.
Abdul atabaki kuwa na mchango wake na kuheshimiwa kwa hilo.
Jitihada za kumdhalilisha Nyerere ili kusafisha nyota ya Abdul hazitazaa matunda asilani.
Nyerere atabaki kuwa kiongozi wa TAA,TANU, Rais wa kwanza wa Tanganyika huru, mwenyekiti wa kwanza wa CCM.
Na hapa umetusadia sana kutambua kuwa kumbe hata Abdul alifahamu kuwa ipo haja ya kuwa na mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha Watanganyika. Kidaha alikataa, Nyerere akakubali. Swali ni kuwa je, lengo la Abdul kuwaunganisha Watanganyika kwa kumtumia Nyerere lilifanikiwa au la?
Kwa bahati mbaya sana, historia unaisimulia kwa hisia kinyume na historia hiyo inavyotakiwa kusimuliwa!
Historia hutembea na huishi kwa fact na sio hisia!
Hata uwezo wakutafsiri hiyo hotuba mpaka leo tangu ilipowekwa hapa januari umeshindwa kijana?
Narudia tena kukusihi, itendee haki jf,
Elimu yote liyoipata katika uzi huu ninakushangaa isipokuwa na mafaa kwako!
Naamini kubeza kwa msomi huendana na hoja na sio makelele! sote tunapenda kunyonya elimu inayotolewa na Mohamed, lakini Mohamed si mtume, anapokosea na watu wakamkosoa basi tusiwaone hao wanaomkosoa ni wabaya kiasi cha wewe kuwashambulia wao binafsi badala ya hoja zao!Mimi nakesha hapa 24/7 na ikibid hata 365 kunyonya elimu kutoka kwa Moh Said na wengineo,na kuwabeza wengine wote wanaozuia na kukejeli elimu hii inayomwaga hapa bila tozo bila mashartii...
Huu mbini mie sijauelekeza kwako ni mahusisi kwa wanaukumbi ambao wanaofuatilia huu mnakasha.
Wewe endelea na porojo zako za mafaa.
Umekwisha...ha haa ha.
Kuna habari za kusikitisha ukumbini nadhani Mohamed Said, atatuelezea Inshaalah.
Wanajamvi,
Innalilah Wainnailaihy Rajuun.
Kwa Allah tumetoka na kwake ni marejeo yetu.
Bwana Ally Kleist Sykes amefariki dunia Nairobi.
Yericko Nyerere,
Kila siku nakuanbia wewe ni mtupu sana sana kwenye historia ya Tanganyika huna unachokijua kwenye AA, TAA, TANU, unachotakiwa upinde mgongo usomeshwe historia unajipunja mengi sana kutoka kwa Mohamed Said.
Hebu msome Nyerere mwenyewe hapa chini sijui wewe na Nyerere nani anasema kweli na nani muongo wapi Nyerere kasema walianzisha chama cha harakati za mwafrika...
Julius Nyerere
'"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.
Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.
Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?
Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).
Nadhani wewe ndiyo unatakiwa ufanye utafiti kabla ya kuandika hebu tuendelee kumsoma Nyerere mwenyewe hapa chini...
Julius Nyerere.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.
Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.
Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.
Hebu msome tena Nyerere hapa chini anavyoelezea harakati zake za kisiasa pamoja na wazee wetu ambao walikuwa na mahaba makubwa na Nyerere ingawa wewe unawaletea kejeli na dhihaka na kuwaita wazee wa vibarazani tu....
Julius Nyerere.
Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.
Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.
Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).
Mohamed Said, wala alazimishi umma wamuamini hata Nyerere mwenyewe anasema hebu msome hapa chini. hapa wanaukumbi tulizaneni mumsome vizuri Nyerere.
Julius Nyerere.
Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.
Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.
Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, "Twining (Twainingi) umekwisha!" (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!
Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!
Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.
Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.
Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.
Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.
Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee."'
Hizi picha za wazee wetu wakionyesha sura za bashasha pamoja na Nyerere, Sheikh Takadir kushoto kwa Nyerere kavaa kanzu na kofia kashika fimbo yake...
![]()
Hapa Wazee wapo uwanja wa ndege wakumuaga Nyerere akielekea UNO.
![]()
Wanajamvi,
Innalilah Wainnailaihy Rajuun.
Kwa Allah tumetoka na kwake ni marejeo yetu.
Bwana Ally Kleist Sykes amefariki dunia Nairobi.
Kadogoo,Jokakuu,
Chadema kupokea Takrima toka kwa kada wa CCM tafsiri yake nini? ni kichekesho kwa Chama kinachodai ni Wapinzani huku wanapokea Takrima toka kwa kada wa Chama tawala! Sabodo ni kada wa CCM au CDM? haingii akilini kada 1 kupenda vyama 2 tofauti! hapa kuna usiri fulani tunaomba akina Jokakuu watufichulie!
Ritz,Nashukuru kwa jibu lako murua.
Na Nyerere je asili yake ilikuwa wapi?
Hata mbunge wenu wa Chadema Mwanza Nyamagani Wenje ni Mtanzania mwenye asili ya Kenya.
Sabodo ni mwafrika au siyo mwafrika hapa ndiyo nataka kujua.
Barubaru,i
Hao wanajeshi je unajua wote walifukuzwa. Huyo wa Air force ngerengere alifukuzwa na wa china japo alikuwa mahiri sana kuongea kichina.Uliza utaelezwa.
Na hao wengine wote kama walipata degree basi wamepata degree zao baada ya baba yao kuondoka madarakani.Lakin jiulize je walisoma skuli gani za Sc na kama yupo aliyewahi kwenda High sch skuli gani?
Naomba uchunguze hilo kisha nikosoe kama nitakuwa nimenena uwongo
usitake niseme meng
Wanajamvi,
Innalilah Wainnailaihy Rajuun.
Kwa Allah tumetoka na kwake ni marejeo yetu.
Bwana Ally Kleist Sykes amefariki dunia Nairobi.
Wanajamvi,
Innalilah Wainnailaihy Rajuun.
Kwa Allah tumetoka na kwake ni marejeo yetu.
Bwana Ally Kleist Sykes amefariki dunia Nairobi.
Huu ni msiba wa kitaifa, kila mtanzania unamuhusu,
Hakika tumepoteza hazina kuu ya tunu ya uhuru wetu,
Alisimama kidete kupigania uhuru kwa jasho na damu!
Mungu amlaze pema peponi mpigania uhuru wa Tanganyika Mzee wetu Ally Klest Sykes!