Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Asante kwa maelezo murua kabisa ndugu yangu Mag3. Nipo hapa tangu siku ya kwanza kabisa ya mnakasha huu, jina la Okelo halijapata nafasi kabisa. Umenisaidia kujua pa kuanzia, barikiwa sana kaka.. Ningefurahi sana kama ungepata nafasi ya kuyajibu maswali yote kwenye swalh langu msingi, kipengele hadi kipengele..
Timothy Peter Thomas, Okello ametajwa sana humu, just do your homework and you will find all the answers.
 
Last edited by a moderator:
Jasusi,

Kwanza niliweka nia nikuwekee hapa ukukmbini watu wote kutoka Tanzania waliopitia Carleton University lakin nimepata ushauri toka kwa wengi nisiweke hapa lakin kama utapenda naweza nikaku PM wote uangalie kama Huyo Anna yupo.

Lakin unapoandika kitu hakikisha kuwa una yakini nacho kama mimi ninavyoyakinisha. Kumbuka kuwa enzi hizo ili mtu aende CHUO KIKUU ilimpasa kwanza amalize Form four na kisha aende form six na kisha apite JKT. au apitie Adult chances ambazo nina hakika yeye hajapita huko.Sa

Sasa hebu dadavua kidogo kuwa je aifanikiwa kupata maksi za kutosha kwenda form six. je alisoma skuli gani na JKT alipitia wapi kama huu msema kweli?

Nitakuongezea moja hapo yule mtoto wake uliyesema alikwenda Airforce China. Je unajua kuwa alikuwa form four akaenda kusomea kozi ya urubani ambazo colifications zake zilihitaji form six. Na wote aliokuwa nao walikuwa form six yeye pekee ndio alikuwa form four? Na alikuja baada e alishindwa masomo hayo. Je nae alipitishwa kinamna hiyo au ... Je nalo hili unalikataa?

Kwa kuwa najua mengi sana kwa sababu nilikuwa karibu na familia hiyo nilipokuwa Tz. napenda kukwambia Nyerere alipenda sana vijana wake wasome lakin ...

Nilichokubainishia hapa alipenda watoto wa wengine wapite njia sahihi yeye wake walipita njia za mkato japo wengi hawakufanikiwa kufika. Ndio maana tunasema hakuwa mwadilifu.

Kuhusu PhD yangu isikutie khofu kwani nimeipata kihalali kabisa toka Mtendeni skuli Dar, Tambaza, Ilboru, JKT Ruvu, UDSM(Tz). Carleton Univ(Can), Na Sofia Univ (Jpn).tafuta tu jina la Dr Hamza Yousuf Al-Naamaniy

Tuendelee na mnakasha kwani tutaingilia siri za ndani za familia hii ambazo si vizuri kuzianika hapa.

Pole sana

Barubaru,
Sasa unachobisha ni nini? Nimesema Anna alisoma Canada na nilimtembelea kule. That is a fact. So did Madaraka. Wewe kauli yako ni kwamba Nyerere hakusomesha wanae. Uwongo. Mimi nimemaliza form 4 Aga Khan mwaka 1967. Sikuchaguliwa kwenda form 5 kwa sababu ya jeuri yangu. Nikaondoka kwenda Marekani ambako nimesoma Howard University hapa Washington. D.C. Sasa unajaribu kusema nini? Kuna mdogo wangu naye alimaliza form 4 akaja kusoma University of Maryland. Sasa hapo kwako issue ni nini? Unasema unajua mengi sana juu ya familia hiyo lakini unachoandika hapa ni uwongo na ngano za vijiweni. Ndio maana nikakukumbusha kuwa mtu wa Phd unahitaji kuwa mbobeaji kwenye utafiti na unachoandika hakikisha kina mantiki. Hayo ya vijiweni waachie wenyewe. Nina marafiki wengi tu enzi hizo air force waliochukuliwa jeshini baada ya form 4 na kwenda kusoma Canada. Sasa sijui hapo unataka kusema nini. Hata marehemu Ditopile, huyu alikuwa class mate wangu, alijiunga jeshini baada ya kumaliza form 4 pale Aga Khan kwa hiyo sioni ajabu kwa John Nyerere kujiunga na jeshi baada ya form 4. Ni wengi tu waliofanya hivyo.
 
Ukisha kuwa kiongozi wa umma hakuna cha Private life tena! ndio maana aliyekuwa Rais wa Marekani Clinton habari zake za kumpapasa papasa Dada Lewinsky ziliwekwa hadharani na dunia nzima tukapashwa! mwangalie Beliskoni wa Italy!

Sawa Kadogoo; Mimi nilikuwa nafata kile nachoona dunia sasa inakifanya. Uingereza waandishi (mapaparazi wameeshaambiwa wawaache WATOTO WA MAREHEMU DIANA WAISHI KIBINAFSI. Clinton kweli anachambuliwa na hata mpenzi wake uliyemtaja, Lakini MWANAYE, yaani CHELSEA Clinton anapewa stahiki ya maisha yake kama mtu binafsi. Mabinti wa Obama hali kadhalika. Watoto sio wanasiasa. Labda mtu kama Makongoro tumkwae humu JF kwa siasa zake sio za babaake. Isitoshe Kadogoo, kama mwanao leo unamwambia "shule imepatikana kenya..... unaondoka kesho kwenda kusoma". Yeye muda wa kukuchimba wewe kama mzazi kuhakiki kuwa mipango yote ya kumtafutia shule ni halali au haramu ataianza vipi? Ndiyo maana nikaona atalaumiwa asiyestahili lawama. Ila kama wewe unaona ni tija wanachokifanya Jasusi na mwenzie kuchimbua undani wa watoto wa Julius sina hoja juu yako. Ulikuwa ushauri tuu.
 
Ndugu yangu Jasusi

Mimi ningekuomba hiyo mada ya Mwalimu Nyerere na familia yake muiache,

Inatuondoa katika uwepo nakutufanya tutake kuongea kitu!

Tutulie kwenye lengo la uzi huu

Nimekusikia, na nimemsikia Wickhama. Nilitaka tu kuondoa upotoshaji kuwa Nyerere hakusomesha wanae. That is all.
Uwongo ukiachwa utamalaki watu wanaanza kuamini kuwa ni kweli. Siwezi kukaa kimya wakati sifa za Nyerere zinapitishwa kwenye mahandaki ya matope. Nitanyamaza.
 
Barubaru,
Sasa unachobisha ni nini? Nimesema Anna alisoma Canada na nilimtembelea kule. That is a fact. So did Madaraka. Wewe kauli yako ni kwamba Nyerere hakusomesha wanae. Uwongo. Mimi nimemaliza form 4 Aga Khan mwaka 1967. Sikuchaguliwa kwenda form 5 kwa sababu ya jeuri yangu. Nikaondoka kwenda Marekani ambako nimesoma Howard University hapa Washington. D.C. Sasa unajaribu kusema nini? Kuna mdogo wangu naye alimaliza form 4 akaja kusoma University of Maryland. Sasa hapo kwako issue ni nini? Unasema unajua mengi sana juu ya familia hiyo lakini unachoandika hapa ni uwongo na ngano za vijiweni. Ndio maana nikakukumbusha kuwa mtu wa Phd unahitaji kuwa mbobeaji kwenye utafiti na unachoandika hakikisha kina mantiki. Hayo ya vijiweni waachie wenyewe. Nina marafiki wengi tu enzi hizo air force waliochukuliwa jeshini baada ya form 4 na kwenda kusoma Canada. Sasa sijui hapo unataka kusema nini. Hata marehemu Ditopile, huyu alikuwa class mate wangu, alijiunga jeshini baada ya kumaliza form 4 pale Aga Khan kwa hiyo sioni ajabu kwa John Nyerere kujiunga na jeshi baada ya form 4. Ni wengi tu waliofanya hivyo.

Wengi sana TZ wamemaliza form four, wakasomea kilimo (cert-diploma-BSc and then MSc and finally PhD) nawajuwa baadhi.
 
Nimekusikia, na nimemsikia Wickhama. Nilitaka tu kuondoa upotoshaji kuwa Nyerere hakusomesha wanae. That is all.
Uwongo ukiachwa utamalaki watu wanaanza kuamini kuwa ni kweli. Siwezi kukaa kimya wakati sifa za Nyerere zinapitishwa kwenye mahandaki ya matope. Nitanyamaza.

To be honest with you Jasusi; Nimesomea SUA na one of my very respected Professors pale, watoto wake pamoja kuwa alijitahidi kuwaanzishia international school Moshi, they all (2) dropped out of school. Mzazi humpi MTOTO IQ. Wewe unamzaa na kumlea. Siku zote mtu atajipanga pale ambapo IQ yake inastahili.

Yet lazima ieleweke kuwa DISCOVERERS wakubwa wengi kabisa anzia kama Einstein, Newton, hadi kina Bill Gates Hamna GRADUATE. Geographers kama akina Ibn Batuta, ramani zao hadi leo zinawashangaza watu kwa accuracy japo zimepishana hundreds of years na za Google maps. In the final analysis ni kile Mwenyezi Mungu alichokijaalia kwa hao unaowalea.

Shukran kwa maneno yako mema.
 
Zumbemkuu,
Ikiwa babu yetu alifanya juhudi hizo hilo ni jambo zuri na yeye anastahili sifa
kama wanazopata wote waliopigania uhuru.

Mzee MS; Vipi sheikh?..... Kijeshi wanasema ume-retreat!!!!!!!!!! Haki ya Mungu let me laugh hahahahahah. Umeamua kuponyesha bawa? Huyu bwana kaja vibaya? You have made my day MS... Aise huu mnakasha, sina hamu. Zumbe ulitakiwa kuja mapema, unanidai japo....... tende bwana.....hahahahahah.

Ngoja ni-copy haraka;
Nguruvi, Mag3, Kadogoo, Jasusi, Sheikh Farid
 
JokaKuu!
Ninachofahamu mimi kutoka kwako ni kuwa unajaribu kuwaonyesha wana ukumbi hasara za Muungano kwa Watanganyika na athari zake mbaya ikiwemo ukwamishaji wa "maendeleo" ya Mtanganyika kama vile Kusini.

Umetuonyesha huko nyuma pia kuwa upo mstari wa mbele katika kuwazindusha Watanganyika kuhusu hasara wanazozipata kutokana na Muungano.Ulitufahamisha vilevile kuwa Watanganyika wamechelewa katika kuzidai haki zao zinazohodhiwa na Muungano.

Unaweza kutuelezea ni sababu zipi unafikiria zilimchelewesha Mtanganyika kuzinduka katika kudai haki yake? Ni matumaini yangu kuwa kuelewa kwa Mtanganyika wapi alijikwaa kutakuja kumsaidia sana mbeleni.
*Si lazima JokaKuu yoyote anaweza kujimwaga na kutupatia tathmini yake.
Sideeq,

..nitajibu swali nililo-highlight with blue.

..kwanza, kuna suala la wa-Tgk kuwa na imani kubwa juu ya Mwalimu Nyerere, CCM, na watawala.

..pili,ni elimu ndogo waliyonayo wa-Tgk wengi ambapo hawatafiti kuhusu kinachoendelea ktk maisha yao, muungano ukiwa suala moja wapo.

..tatu, ni umasikini uliotamalaki miongoni mwa wa-Tgk. wengi wanakimbizana na shida zao za kila siku kujaribu kujikimu, sasa muungano ni jambo la mwisho kwao kujishughulisha nalo.

..nne, kuna wako wa-Tgk ambao wamelelewa ktk imani kwamba Afrika ni moja. Hawa ni ma-Pan Africanist ambao wako radhi kuvumilia vitimbi vya kila aina toka kwa wa-Znz ilimradi wasivunje "mwiko" walioachiwa na Mwalimu Nyerere.

..binafsi nilianza kuchunguza muungano baada ya kuwasikia wa-Znz wakilalamika. baada ya kufanya uchunguzi wangu nikagundua kwamba wa-Tgk ndiyo wanaowafadhili na kuwahifadhi wa-Znz kupitia muungano huu.

..kwa muda mrefu hoja za Znz zimekuwa ni maneno-maneno tu bila kutoa ushahidi wa data. kwani unafikiri nini kilimzuia Barubaru kuleta data nilizotoa hapa wakati yeye ndiye wa kwanza kusema kuna kitu kinaitwa Joint Finance Commission ya serikali ya muungano??

..wa-Tanganyika hatuzungumzi kwamba wa-Znz inainyonya Tgk na kuishia hapo, bali tunakwenda ndani zaidi na kunukuu ripoti mbalimbali za kitaalamu kama ushahidi wa madai yetu.

cc: nambokola, Wickama, gombesugu, SHEIKH FARID, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
To be honest with you Jasusi; Nimesomea SUA na one of my very respected Professors pale, watoto wake pamoja kuwa alijitahidi kuwaanzishia international school Moshi, they all (2) dropped out of school. Mzazi humpi MTOTO IQ. Wewe unamzaa na kumlea. Siku zote mtu atajipanga pale ambapo IQ yake inastahili.

Yet lazima ieleweke kuwa DISCOVERERS wakubwa wengi kabisa anzia kama Einstein, Newton, hadi kina Bill Gates Hamna GRADUATE. Geographers kama akina Ibn Batuta, ramani zao hadi leo zinawashangaza watu kwa accuracy japo zimepishana hundreds of years na za Google maps. In the final analysis ni kile Mwenyezi Mungu alichokijaalia kwa hao unaowalea.

Shukran kwa maneno yako mema.

Hivi kwako wewe GRADUATE ni nini mpaka mtu atimize vigezo gani? huwezi kusema Ibn Battuta siyo GRADUATE.
 
Mzee MS; Vipi sheikh?..... Kijeshi wanasema ume-retreat!!!!!!!!!! Haki ya Mungu let me laugh hahahahahah. Umeamua kuponyesha bawa? Huyu bwana kaja vibaya? You have made my day MS... Aise huu mnakasha, sina hamu. Zumbe ulitakiwa kuja mapema, unanidai japo....... tende bwana.....hahahahahah.

Ngoja ni-copy haraka;
Nguruvi, Mag3, Kadogoo, Jasusi, Sheikh Farid

Wickama,
Nitakuwa sina uadilifu ikiwa mimi naandika historia ya wazee wangu
naeleza makubwa walofanya katika kupigania uhuru halafu aje mtu
mwingine na yeye aeleze historia kama ya kwangu kisha mie nimpinge.

Siku zote nikisema na nyie andikieni historia za huko makwenu ili ijulikane
badala ya kunipinga.

Hii ya kutembea kwa miguu mwaka 1950 kutoka Usambaa hadi Tanga mie
nimeipenda sana nimefananisha na ile historia ya Mzee Said Chamwenyewe
aliyekuwa anapandabaiskleli kutoka Dar es Salaam hadi Rufiji akiuza kadi za
TANU.

Huu ni mwanzo mzuri.
 
Mohamed Said,

Hawa jamaa zetu wanadhani wewe upo humu ukumbini kufanya ubishi kutafuta ushindi siku zote mie napenda kukuita wewe "Teachable mind" hata siku moja haupingi jambo la mtu kuhusu historia yake wala wazee wake kuhusu TANU.

Wewe unatumia lugha "Soft spoken" kufundishia historia ya wazee wako ambao wametoa mchango wao katika kutafuta uhuru wa Tanganyika, unakuja na data na facts za kutosha siyo maneno matupu kulielezea jambo, anapokuja mtu na historia ya wazee wake kutoka maeneo mengine wanadhani wewe utawapinga na kuwatukana

Hapo ndiyo tunaona tofauti yao na wewe wanategemea wewe utawaletea kejeli na dhihaka dhidi ya hizo habari za wazee wao kinyume chake unawaunga mkono kitu ambacho hawakukitegemea.
 
Last edited by a moderator:
Sideeq,

..nitajibu swali nililo-highlight with blue.

..kwanza, kuna suala la wa-Tgk kuwa na imani kubwa juu ya Mwalimu Nyerere, CCM, na watawala.

..pili,ni elimu ndogo waliyonayo wa-Tgk wengi ambapo hawatafiti kuhusu kinachoendelea ktk maisha yao, muungano ukiwa suala moja wapo.

..tatu, ni umasikini uliotamalaki miongoni mwa wa-Tgk. wengi wanakimbizana na shida zao za kila siku kujaribu kujikimu, sasa muungano ni jambo la mwisho kwao kujishughulisha nalo.

..nne, kuna wako wa-Tgk ambao wamelelewa ktk imani kwamba Afrika ni moja. Hawa ni ma-Pan Africanist ambao wako radhi kuvumilia vitimbi vya kila aina toka kwa wa-Znz ilimradi wasivunje "mwiko" walioachiwa na Mwalimu Nyerere.

..binafsi nilianza kuchunguza muungano baada ya kuwasikia wa-Znz wakilalamika. baada ya kufanya uchunguzi wangu nikagundua kwamba wa-Tgk ndiyo wanaowafadhili na kuwahifadhi wa-Znz kupitia muungano huu.

..kwa muda mrefu hoja za Znz zimekuwa ni maneno-maneno tu bila kutoa ushahidi wa data. kwani unafikiri nini kilimzuia Barubaru kuleta data nilizotoa hapa wakati yeye ndiye wa kwanza kusema kuna kitu kinaitwa Joint Finance Commission ya serikali ya muungano??

..wa-Tanganyika hatuzungumzi kwamba wa-Znz inainyonya Tgk na kuishia hapo, bali tunakwenda ndani zaidi na kunukuu ripoti mbalimbali za kitaalamu kama ushahidi wa madai yetu.

cc: nambokola, Wickama, gombesugu, SHEIKH FARID, Nguruvi3
Pamoja na hayo yote aliyoeleza mkuu JokaKuu ninayoafikiana naye kabisa nichangie kwa uchache makundi nyuma ya muungano.

1.Kundi la kwanza la Watanganyika wanaokimbiza mkate wa siku(Joka kalieleza vema)
2. Kundi la Pan Africanism, hili linaamini kuwa sisi ni wamoja na kwamba nguvu yetu itatokana na umoja wetu

3. Wenye weledi, hawa wanaelewa lakini kwasababu zao za kisiasa wameamua tu kutoeleza ukweli
4. Kundi la wale wenye weledi lakini halikujua kuwa kuna tatizo. Hili ndilo kundi linalokua kwa kasi kubwa!

5. Ni kundi la wazanzibar wenye misimamo mikali na wanaotumia sheria kuwabagua Watanganyika
6. Kundi la wazanzibar wasema hovyo! wasio na maono na wasikiliza hadithi bila ushahidi au maarifa

Mwanafunzi wa chuo kikuu au chuo cha elimu ya juu na hata vya elimu ya kati wengi wanafahamu kuwa wanakopeshwa fedha kwa masomo kutoka katika kodi za baba na mama zao ili wadogo zao nao wapate fursa siku za usoni.
Kitu walichokuwa hawaelewi ni kuwa kodi hizo za wazazi wao zinawaosomesha wazanzibar bure bila kurudishwa.

Kundi la 5 ndilo limeanzisha kizai zai. Kila waliposema mafuta si ya muungano akili za Watanganyika ziligonga na kujiuliza hivi kipi ni cha muungano na kipi sicho! Hapo kundi la 3 wakaona hakuna sababu za ukimya wakaanza kufunguka

Kundi la 5 lilipoweka sheria za kumzuia Mtanganyika asipate ajira, kundi la 3, 4 likajiuliza,hivi inakuwaje wao wasome tena bure wachukue ajira za Watanganyika si kwa sifa bali kwa uzanzibar wao! kwanini Mtanganyika asipate fursa kwa Utanganyika wake kule visiwani?

Kundi hili ndilo limeweaka sheria za kumbagua Mtanganyika katika mambo ya umiliki wa ardhi. Matanganyika anajiuliza iweje wao waje tu kuishi bila kubaguliwa lakini Mtanganyika kwao ni adui namba moja!

Kundi lililoharibu kila kitu kwa wznz ni kundi la 6. Hili limeeneza uongo kama vile Watanganyika kuwanyonya, znz kuwa Dubai, kwamba Watanganyika wana mtaji wao BoT,mapato yote ya TRA yanaishia bara.
Linaendelea na hadithi, ni lazima Rais awe wa zamu, na kuwa znz ni nchi huru sawa na Tanganyika kwa kila kitu.

Uongo ukazidi znz inachangia sawa na Tanganyika na hivyo kila mapato lazima yagawanywe sawa.
Kundi hili ndilo limewazindua Watanganyika sana. Watanganyika wamefanya utafiti na fikra za tuhuma hizo na kila mara wameona madudu. Mathalan, Barubaru amesema Mgawanyo wa mapato unasimimiwa na joint commisision.

Imegundulika kuwa katika mapato ya taifa znz inachangia sifuri maana hiyo bilioni 24 ni nominal haifiki hazina.
Hata hivy0 katika 1498 bilioni hilo ni tone la maji baharini.

Sasa kila jambo limekuwa linaangaliwa kwa makini. Ndiyo maana watu wanajua bilioni 32 zimekwenda znz bila sababu, kwamba kodi zao zinalipa wastaafu wa znz, hata usafiri wa viongozi wa wao ni wa kodi zetu.
Limewazindua kwa kujiuliza kwanini wao watumie umeme bure na kulipiwa na mkulima wa Kipera Moorogoro

Kundi hili ndilo limefunua macho na kuhoji kwanini basi Tanganyika imwage bilioni 3.6 kwa chuo na wala si kujenga chuo Tanganyika kwa Watanganyika?

Kwahiyo kundi la 6 limewaunganisha Watanganyika wa kundi la 2,3,4 kwa nguvu sana ndio maana wanataka wznz waondoke kwa amani.

Ili ni kuonyesha ujinga wa kundi la 6,wao wamedai znz ni nchi na mbia wa muungan hivyo tume ya Warioba iwe na wajumbe 15 kila upande bila kujali eneo au idadi ya watu. Haraka haraka hii ni hoja ya maana sana!!

Tatizo ni kuwa ikitoka rasimu Watanganyika watahoji wapi 50/50?
Hakuna jambo litakaloangaliwa kwa udogo wa nchi au population kwa mantiki kuwa znz kama nchi na mbia wa muungano ilikuwa na 50% katika tume, vipi wakati wa kugawana majukumu ikimbilie udogo na idadi ya watu ili hali ilitumia udogo huo huo na idadi ya watu kupata 50%

Zaidi ya hapo Watanganyika watajiuliza endapo tumeamua kushirikiana katika mambo ABCD Tanganyika itafaidika na nini.
Hii maana yake ni kuwa jambo lisilo na manufaa kwa Tanganyika hilo halina maana na liachwe.

Hakuna sababu ya kutoa ulinzi na usalama kwa watu wa taifa jingine. Wakitaka basi 50% iwekwe mezani kitu ambacho ni kituko na kichekesho.

Kama 50% haiwezeakani kwasababu wao ni wachache kwa idadi na eneo, basi tunadhani tukutane EAC ambako kuna Burundi na Rwanda wenye haki zote kama wanachama!
 
Wickama,
Nitakuwa sina uadilifu ikiwa mimi naandika historia ya wazee wangu
naeleza makubwa walofanya katika kupigania uhuru halafu aje mtu
mwingine na yeye aeleze historia kama ya kwangu kisha mie nimpinge.

Siku zote nikisema na nyie andikieni historia za huko makwenu ili ijulikane
badala ya kunipinga.
Hakuna mtu anakupinga Mohamed, watu wanaweka rekodi sawa, wanaonyesha upotoshaji, wanafafanua uongo na wanaunga mkono pale penye hoja. Hili tumelisema sana tangu mnakasha uanze.

Nani alipinga kuwa K.Sykes hakuwa katibu wa AA? Lakini yeye ni miongoni mwa waanzilishi wa AA si yeye mwanzilishi peke yake akawa katibu, kuyasema hayo tatizo lipo wapi?

Unaposema watu wanakupinga unajaribu kutueleza habari tulizokuwa tunahisi na labda nikung'ate sikio( kwa sauti ya chini sana). Wanajamvi wanasema hivi kule ulikokuwa umezoea kusema bila kuambiwa no! iko hivi au kupewa hoja mbadala siyo hapa JF.
Eti wanasema ulizoea kulisha watu, hapa wanatafuna. wanaomeza wachache. eti hawakubali smlulizi la 15 tena! wanasema kwa kiinglishi enough is enough,let us save the generation from intellectual abuse.

Nakubalina na Wickama, siku hizi hatusikii tena tambo za mihadhara kwenye mavyuo vikuu! halafu unakubali historia ya Zumbemkuu1 jambo jema hili inshallah.
 
Wanajamvi,
kuna habari za kufuja mali za EAMWS, mnajua zilisababisha nini na zilifanywa na nani?

Abdul Wahid na Sheikh Amir kuna mahali wanakutana katika chama nje ya TAA na TANU.
Mnajua ni wapi na ni nani kiongozi wa taasisi hiyo?

CC Zumbemkuu, Mag3, JokaKuu, Shariff Ritz, al maarufu Gombesugu, Jasusi, Wickama
 
Sideeq,

..nitajibu swali nililo-highlight with blue.

..kwanza, kuna suala la wa-Tgk kuwa na imani kubwa juu ya Mwalimu Nyerere, CCM, na watawala.

..pili,ni elimu ndogo waliyonayo wa-Tgk wengi ambapo hawatafiti kuhusu kinachoendelea ktk maisha yao, muungano ukiwa suala moja wapo.

..tatu, ni umasikini uliotamalaki miongoni mwa wa-Tgk. wengi wanakimbizana na shida zao za kila siku kujaribu kujikimu, sasa muungano ni jambo la mwisho kwao kujishughulisha nalo.

..nne, kuna wako wa-Tgk ambao wamelelewa ktk imani kwamba Afrika ni moja. Hawa ni ma-Pan Africanist ambao wako radhi kuvumilia vitimbi vya kila aina toka kwa wa-Znz ilimradi wasivunje "mwiko" walioachiwa na Mwalimu Nyerere.

..binafsi nilianza kuchunguza muungano baada ya kuwasikia wa-Znz wakilalamika. baada ya kufanya uchunguzi wangu nikagundua kwamba wa-Tgk ndiyo wanaowafadhili na kuwahifadhi wa-Znz kupitia muungano huu.
Shukran kwa tathmini JokaKuu!

Nilivyoelewa mimi ni kuwa namba mbili mpaka nne zinarudi kwenye tatizo uliloliweka namba moja.
Tatizo ni lilelile tu halafu kutokea hapo mtu anaweza kutiririka.

Ninakubali kusahihishwa.
 
Wanajamvi,
kuna habari za kufuja mali za EAMWS, mnajua zilisababisha nini na zilifanywa na nani?

Abdul Wahid na Sheikh Amir kuna mahali wanakutana katika chama nje ya TAA na TANU.
Mnajua ni wapi na ni nani kiongozi wa taasisi hiyo?

CC Zumbemkuu, Mag3, JokaKuu, Shariff Ritz, al maarufu Gombesugu, Jasusi, Wickama

Tupe darsa kuhusu hizo habari Aly habib Nguruvi3,
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi,
kuna habari za kufuja mali za EAMWS, mnajua zilisababisha nini na zilifanywa na nani?

Abdul Wahid na Sheikh Amir kuna mahali wanakutana katika chama nje ya TAA na TANU.
Mnajua ni wapi na ni nani kiongozi wa taasisi hiyo?

CC Zumbemkuu, Mag3, JokaKuu, Shariff Ritz, al maarufu Gombesugu, Jasusi, Wickama

Juhudi za Kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiislamu chini ya EAMWS, 1964

APRILI 1964 ujumbe wa hali ya juu wa EAMWS ndani yake wakiwemo Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Omari Abdallah, Tewa Said Tewa, Katibu wa EAMWS Abdul-Aziz Khaki na mzee wa TANU Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; Makisi Mbwana, Issa Mtambo, Omari Muhaji na Saleh Masasi waliondoka kwenda ziara ya nchi za Waislamu kutafuta msaada wa kujenga Chuo Kikuu cha Kiislamu na kuanzisha uhusiano na nchi za Kiislam.

Gamal Abdel Nasser alifurahishwa sana na ujumbe wa Tanganyika kiasi kwamba ingawa alikuwa katika matayarisho ya mapokezi ya Waziri Mkuu wa Urusi Kruschev, na ingawa ujumbe wa EAMWS ulikuwa wa kidini zaidi kuliko wa kiserikali, alikutana na ujumbe ule akaupatia ofisi, huduma za simu, na makatibu muhtasi ili waweze kutayarisha mipango yao kwa serikali ya Misri bila shida. Halikadhalika alimuagiza makamu wake Sharbasy afanye makubaliano na EAMWS kwa niaba yake.

Serikali ya Misri ilikubali kugharamia ujenzi wa chuo hicho. Mkataba wa makubaliano ukatiwa sahihi mjini Cairo kati ya Tewa Said Tewa kwa niaba ya EAMWS na Makamu wa Rais wa Misri, Sharbasy kwa niaba ya serikali yake.

Serikali ya Misri iliahidi kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam ambacho kitamilikiwa na kuendeshwa na EAMWS. Gharama ya mradi mzima uliuwa pauni milioni hamsini na tano za Ki-Misri.

Baada ya kukamilisha kazi ile ujumbe ule uliondoka Cairo kuelekea Makka kufanya ibada ya hija. Baada ya kumaliza hija wajumbe wanne walirudi nyumbani na Tewa, Aziz Khaki, Sayyid Omar Abdallah wakaendelea na safari kwenda Aman, Jordan ambako walifanya mazungumzo na Mufti na Waziri wa Aukaf.

Kutokea hapo ujumbe ulikwenda Kuwait ambako ulikutana na Sheikh wa Kuwait kisha ukaenda Bhaghdad, Iraq na kukutana na rais wake, Abdisalama Arifek.

Kutoka hapo ujumbe ulielekea Beirut, Lebabon ambako ulifanya mazungumzo na viongozi wa harakati za Kiislam. Baada ya kutoka Beirut ujumbe ule ulirudi tena Cairo kwa ajili ya kukamilisha makubaliano ya kujenga Chuo Kikuu.

Tarehe 20 Mei, 1964 ujumbe ulirejea Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa EAMWS na Waislamu kwa ujumla. Mkutano wa Halmashauri Kuu ya EAMWS ukaitishwa na Tewa Said Tewa akatoa taarifa yake kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Kiislamu. Siku ya pili Tewa akaitisha mkutano na waandishi wa habari na kutoa habari za kufurahisha za kujengwa kwa Chuo Kikuu Cha Kiislamu kwa vyombo vya habari na kwa Waislamu kwa ujumla.

Kwa mafanikio haya Tewa akawa amejichimbia kaburi. Matokea haya yalijaza hofu kwa viongozi wa Kanisa. Kampeni za chinichini dhidi ya Tewa binafsi na uongozi mzima wa EAMWS zilianza.

Mara baada ya ujumbe wa EAMWS kurudi kutoka ziara yake, Nyerere alifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na Tewa Said Tewa, Mwenyekiti wa EAMWS upande wa Tanzania akajikuta nje ya serikali.

Nyerere akamteua Tewa balozi wa Tanzania katika Jamuhuri ya Watu wa China. Mwezi Januari, 1965 Tewa alikwenda China kuanza kazi yake mpya. Inasemekana uteuzi wa wa Tewa kwenda China ulisababishwa na juhudi zake za kutaka kuwaunganisha Waislam kuwa kitu kimoja chini ya jumuiya moja yenye nguvu. Wakati ule ile mipango iliyopitishwa na mkutano wa Waislamu mwaka 1962 ilikuwa ikitekelezwa vyema, shule zilikuwa zimejengwa Ilala, Kigogo na Kurasini, Dar es Salaam; shule zilikuwa zimejengwa Ruvu na Maneromango. Shule hii ya Maneromango ilikuwa na umuhimu wa pekee kwa sababu hii ndiyo ilikuwa shule ya kwanza ya Waislamu kujengwa Uzaramo. Shule za upili zilikuwa zikijengwa Dar es Salaam, Kinondoni na Moshi, Kibohehe. EAMWS ilikuwa vilevile imetiliana mkataba wa makubaliano na serikali ya Misri kuipa scholarship thelathini na tano kila mwaka kwa wanafunzi wa Kiislamu kusoma Misri. EAMWS ilikuwa imejenga shule, misikiti, shule za ufundi na hosteli kwa ajili ya wanafunzi katika sehemu nyingi za Afrika ya Mashariki. Kwa hakika EAMWS ilikuwa ikifanya mambo ya maendeleo kwa Waislamu.

Uganda Tanzania Kenya
Shule 77 70 28
Misikiti 67 53 29
Shule za Ufundi 3 - -
Hosteli 1 - -
Chanzo: Utafiti
Baada ya Tewa kuondoka Bibi Titi Mohamed akachaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa tawi la EAMWS la Tanzania ili kuongeza nguvu makao makuu kwa kuwa mwenyekiti hakuwepo. Kutokuwepo kwa Tewa nchini kulileta ombwe ambalo ilibidi lijazwe. Ghafla palizuka uvumi kuwa Sheikh Abdallah Chaurembo alikuwa achukue uongozi wa EAMWS. Inasemekana nia yake ilikuwa ni kwanza kupata urais wa EAMWS na kisha achaguliwe kuwa Mufti wa Tanzania. 35 Uvumi huu ulidumu kwa karibu mwaka mzima hadi pale Tewa aliporudi kutoka Peking baada ya kujiuzulu ubalozi kuja kugombea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965. Aliporudi Tewa alihojiwa na waandishi wa habari kuhusu uvumi ule na yeye jibu lake lilikuwa kuwa Muislamu yeyote mwenye sifa ya maadili mema ana haki ya kugombea nafasi yoyote katika uongozi wa EAMWS. Neno alilolitumia Tewa katika kumueleza mtu ambaye angeweza kuwaongoza Waislamu lilikuwa takwa, neno la Kiarabu kueleza mtu mcha-mungu.

Nikuanzia katika matukio haya ndipo tunaweza sasa kuanza kuchunguza jinsi Nyerere akiitumia serikali alivyoanza kuuhujumu umoja wa Waislamu kwa kutumia njama, hujuma za dhahiri na za kificho, magendo na kueneza uongo dhidi ya uongozi wa EAMWS, ambao ulionekana ni tishio kwa utawala wake. Wakati ule serikali nzima ilikuwa mikononi mwa Wakristo. Ukiwatoa Wazanzibari waliokuwa katika serikali ya muungano - Aboud M. Maalim, Waziri wa Biashara na Viwanda; Aboud Jumbe, Waziri Nchi; A.M. Babu, Waziri wa Ardhi, Makazi na Maji; Hasnu Makame, Waziri wa Habari na Utalii; Rashid Kawawa ambae alikuwa mtu wa karibu sana na Nyerere, waziri Muislamu katika baraza la mawaziri kumi na tano alikuwa Said Ali Maswanya, Waziri wa Mambo ya Ndani. Hali kama hii ya Wakristo kushika nyadhifa takriban zote za serikali ilikuja vipi? Jibu la swali hili linapatikana katika historia ya Tanganyika wakati wamisionari wa kwanza walipowasili nchini kuja 'kulistaarabisha bara jeusi' na halikadhalika katika historia ya TANU .

'Mgogoro' wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) wa Mwaka wa 1968
Uchochezi wa 'Mgogoro' wa BAKWATA

Kutokana na katiba ya mwaka wa 1957 lengo kuu la EAMWS ilikuwa ni 'kuutangaza Uislamu katika Afrika ya Mashariki'. EAMWS yenyewe ilikuwa ikijigamba kuwa uti wake wa mgongo ilikuwa ni tabligh, yaani utangazaji wa dini. Jumuiya hii iliyoanzishwa mwaka 1933 ilikuwa ya Waislamu wa mataifa yote katika uanachama na katika uongozi wake.

Katika uhai wake wa miaka thelathini na tano EAMWS ilijiweka mbali sana na siasa. Jumuiya hii ilishughulikia kuutetea na kuueneza Uislamu katika Afrika ya Mashariki. Lakini baada ya kutokea maasi ya Tanganyika Rifles mwaka 1964 yaliyopelekea viongozi wengi wa Kiislamu kuwekwa kizuizini, EAMWS ikawa imepoteza mwelekeo wake na kudhoofika. Baadhi ya matawi yaliyokuwa katika majimbo yakafungwa kwa woga na kukosa viongozi thabiti na kwa matawi mengine yalifungwa kwa sababu viongozi wake walikuwa wakichimbwa chinichini na serikali. Waislamu wengi walihisi vitisho vya serikali kwa hiyo waliogopa kuchukua uongozi wa EAMWS. Wengi waliogopa kuitumikia EAMWS kwa kuwa walihisi ofisi za jumuiya hiyo zilikuwa zikichukuliwa na serikali kama vituo vya upinzani dhidi yake. Kwa zaidi ya miaka mitatu toka ule mkutano wa mwaka 1963, EAMWS haikuweza kufanya mkutano wowote.

EAMWS ilipokuja kuitisha mkutano wake wa mwaka mjini Arusha mwaka 1966 kikajitokeza kikundi kutoka upande wa Tanzania kikidai EAMWS ijigawe, kila nchi iwe na mamlaka yake na ijitegemee yenyewe, yaani Tanzania, Kenya na Uganda zote ziwe mbalimbali. Kikundi hiki kilichokuwa kikidai utengano vilevile kikadai kuwa katiba ya EAMWS nayo iwe ya 'kizalendo'.

Hii ilikuwa na maana kuwa uongozi itabidi uifanyie katiba marekebisho ili kuiwezesha Tanzania kuwa huru ndani ya EAMWS. Wajumbe waliokuwa wanaona mbali kutoka Tanzania na wengine kutoka Kenya na Uganda, na kwa hakika mkutano mzima kwa ujumla walipinga kitendo hicho, wakidai kuwa kwa kufanya hivyo Waislamu wa Tanzania watakuwa wametengwa na umma wa Kiislamu wa Afrika ya Mashariki. Jambo hili likitokea, si tu litakuwa limewadhoofisha Waislam wa Tanzania peke yao, bali Waislamu wa Afrika ya Mashariki nzima. Wajumbe wa Kenya na Uganda walikuwa wanatambua kuwa kulikuwa na shinikizo kubwa kutoka serikali ya Tanzania kwa Watanzania kujitoa kutoka EAMWS. Halikadhalika ilikuwa inafahamika kuwa wajumbe wa Tanzania walikuwa wakifanya kazi chini ya shinikizo kali kutoka serikali ya Nyerere.

Haikuwa siri sana kuwa baadhi ya viongozi wa EAMWS walikuwa kisirisiri wakiandamwa na serikali. Lakini mkutano ule haukuzungumzia matatizo haya kwa kuwa hayo yalichukuwaliwa kama matatizo ya ndani ya nchi. Hata hivyo kwa ule moyo wa Kiislamu wa kuhurumiana, wajumbe wa Kenya na Uganda kwa faragha walionesha masikitiko yao kwa Tewa kuhusu ile hali iliyokuwa ikiwakabili Waislamu wa Tanzania. Wajumbe walipokuwa wakiondoka kurejea makwao, ilikuwa wazi kuwa serikali ya Tanzania ilikuwa ikiingilia kati EAMWS kiasi cha kuifanya jumuiya hiyo ishindwe kufanya kazi yake vyema na kupitisha maamuzi yake. Hali hii ilijidhihirisha wazi pale kwa kipindi kizima cha mkutano, makachero wa serikali walikuwa wamejitokeza kwa wingi mjini Arusha.

Haukupita muda ikadhihirika kuwa serikali ilikuwa imepania kuivunja EAMWS kwa kuwatumia Waislamu wachache walioteuliwa kwa kazi hiyo. Lengo likiwa ni kuanzisha taasisi mpya ambayo serikali itaweza kuiamuru. Ieleweke hapa kuwa kama ilivyokwisha elezwa hapo nyuma, serikali nzima ya Tanzania ilikuwa mikononi mwa Wakristo na watendaji hawa walikuwa wapo chini ya Kanisa. Hii ilikuwa na maana kuwa kilichotakiwa kuwepo ilikuwa taasisi ya Kiislamu ambayo Kanisa itaweza kuiamuru. Hii ilikuwa ni jambo lazima lifanyike ili kuwadhibiti Waislamu kama nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya siasa. Baada ya kuelewa hali hii ndipo sasa tunaweza kuuangalia kile kilichoitwa 'mgogoro' wa EAMWS ambao ulidumu kwa miezi mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968.

Ili tuweze kuuelewa vyema kisa kizima cha 'mgogoro' ni muhimu kwanza kuelewa chanzo chake, hadhi za wahusika wakuu na nafasi zao katika 'mgogoro' ule. Mwisho, ni muhimu kuweka bayana na kuchambua nafasi ya Julius Nyerere, serikali yake, chama cha TANU na vyombo vya dola katika 'mgogoro' ule. Hii itasaidia kuelewa kama kweli ulikuwepo 'mgogoro' katika EAMWS, au 'mgogoro' ulibambukizwa na watu katika TANU, serikali na ndani ya Waislamu wenyewe ili kuwadhoofisha Waislamu kwa nia ya kuwa usije Uislamu ukawa na nguvu katika Tanzania hivyo kuwawezesha Waislamu kushika madaraka ya nchi.

Mwaka wa 1967 Mwalimu Julius Nyerere alitangaza Azimio la Arusha hatua ambayo iliitia Tanzania katika siasa ya ujamaa. Sera hii mpya ya uchumi ilipokelewa vyema na wananchi. Mtu ambae hata alikuwa hajulikani, tena mwalimu wa shule ya msingi akijulikana kwa jina la Adam Nasibu ambae alikuwa katibu wa Bukoba wa EAMWS, alichukua nafasi hii kwa kuongoza maandamano hadi ofisi ya TANU ya Mkoa kumuunga mkono Mwalimu Nyerere na sera yake mpya ya uchumi ya Azimio la Arusha. Adam Nasibu inasemekana kuwa alisema ujamaa ni sawa na mafundisho ya Qur'an Tukufu. Adam Nasibu hakuishia hapo alikwenda mbele zaidi na kutoa 'miongozo kwa viongozi wote wa Kiislamu wa Bukoba akifafanua Azimio la Arusha'. Wasiokuwa Waislam walimuona Adam Nasibu kama Muislam mwenye mwamko mzuri wa kimaendeleo, na kwa kuwa yeye alikuwa ni kiongozi wa EAMWS, kuunga kwake mkono Azimio la Arusha kulionekana kama kitendo rasmi cha jumuiya hiyo kuunga mkono sera hiyo. Lakini kabla ya yeye kufanya haya, hakuna mtu aliyemjua mwalimu huyu wa shule kama mwanasiasa licha ya kuwa msomi mwenye uwezo wa kuchambua mambo.

Katika hali ya kawaida, uongozi wa EAMWS pale makao makuu Dar es Salaam ungelikasirishwa kidogo na kitendo cha Adam Nasibu cha ushabiki wa siasa. Lakini uongozi wa EAMWS haukumuonya kiongozi wake wa Bukoba kuhusu jambo lile ambalo dhahiri halikuwa la kupendeza katika jumuiya. Bila shaka uongozi wa EAMWS ulichelea kuwa kwa kufanya hivyo wangelionekana si uzalendo, hasa ukiichukulia jinsi wananchi walivyohamasika na Azimio la Arusha. Hata hivyo Waislamu siku zote ndiyo waliokuwa mbele katika kuongoza siasa. Makao Makuu walibaki kimya kama vile hakuna kilichotokea.

Tofauti na mwaka wa 1963 wakati Nyerere alipojaribu kufanya mapinduzi dhidi ya uongozi wa EAMWS, mwaka wa 1967 hali ya mambo yalikuwa yamebadilika sana yakimwendea Nyerere vyema. Serikali ilikuwa imedhibiti vyombo vyote vya habari ukiondoa gazeti la The Tanganyika Standard ambalo bado lilikuwa chini ya Lonrho. Nyerere alikuwa amemuweka Martin Kiama kama mkurugenzi wa radio ya taifa, na Benjamin William Mkapa kama mhariri wa magazeti mawili ya TANU, The Nationalist na Uhuru. Adam Nasibu aliandikwa katika magazeti na habari zake kutangazwa katika radio kwa ajili ya kitendo chake, hasa kuhusu yale maneno aliyosema kuwa ujamaa ni sawa na mafundisho ya Qur'an.

Katika hali ya mambo kama yalivyokuwa wakati ule hasa jinsi uhasama ilivyokuwapo baina ya serikali na Waislam, baadhi ya Waislam walimuona Adam Nasibu kama kibaraka anaetafuta umaarufu wa bure kwa kujipendekeza kwa TANU, Nyerere na serikali yake. Juu ya haya yote kile kitendo cha katibu wa Bukoba wa EAMWS kitakuja kuwaathiri vibaya jumuiya hiyo na uongozi wake wote pamoja na Mufti Sheikh Hassan Bin Amir.

Kwa wengine Adam Nasibu alionekana kama mzalendo na Muislamu mwenye 'uoni wa mbali'. Kwa ajili hii basi serikali ikamuona kama kiongozi wa baadae ambayo ingeweza kumtegemea wakati wa shida. Uongozi wa EAMWS makao makuu ukaonekana haupo pamoja na wananchi, wala haujali shida zao na uko mbali sana na sera za serikali. Lakini kwa hakika EAMWS kama taasisi ya dini isingeliweza kujitokeza na kuunga mkono Azimio la Arusha kwa kuwa hayo yalikuwa mambo ya siasa. Kwa kufanya hivyo ingelikuwa inakwenda kinyume na msimamo wake wa kutojiingiza katika siasa. Kwa zaidi ya robo karne toka iasisiwe EAMWS ilikuwa imejiweka mbali sana na mambo ya siasa ikishughulika na masuala ya Uislamu tu. Hata hivyo kuwa nje ya Azimio la Arusha kukaonekana kama kitendo cha kukosa uzalendo na kutoa picha kuwa jumuiya hiyo ilikuwa haijali maendeleo na ustawi wa watu wa Tanzania. Mambo yakawa yamevurugika zaidi kwa kuwa rais wa EAMWS, Tewa Said na makamo wake Bibi Titi Mohamed walikuwa katika baraza la mawaziri la Nyerere na wakapoteza nyadhifa zao za ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1965. Kwa ajili hii basi serikali ikawa inaeneza propaganda kuwa kwa kuwa Tewa na Bibi Titi walikuwa katika uongozi wa juu wa EAMWS, walikuwa wanatumia nafasi zao kujijengea himaya mpya kutoka kwa Waislamu dhidi ya Nyerere. Viongozi hawa ikawa lazima washughulikiwe na kuangamizwa. Mtu wa kufanya kazi hii hakuwa mwingine ila Adam Nasibu katibu wa EAMWS Bukoba, mwalimu wa shule ya msingi ambae elimu yake wala haikuwa kubwa. Adam Nasibu alikuwa tayari keshafanikiwa kufanya mapinduzi dhidi ya rais wa EAMWS, Tewa Said Tewa. Kutokana na vitendo vyake alikuwa ameidhihirishia serikali kuwa yeye angeweza kuwa mtumishi bora kwa dola kuliko ule uongozi wa EAMWS uliokuwa pale makao makuu Dar es Salaam ambao ulikuwa ukionekana umechoka.
 
Mohamed Said,

Hawa jamaa zetu wanadhani wewe upo humu ukumbini kufanya ubishi kutafuta ushindi siku zote mie napenda kukuita wewe "Teachable mind" hata siku moja haupingi jambo la mtu kuhusu historia yake wala wazee wake kuhusu TANU.

Wewe unatumia lugha "Soft spoken" kufundishia historia ya wazee wako ambao wametoa mchango wao katika kutafuta uhuru wa Tanganyika, unakuja na data na facts za kutosha siyo maneno matupu kulielezea jambo, anapokuja mtu na historia ya wazee wake kutoka maeneo mengine wanadhani wewe utawapinga na kuwatukana

Hapo ndiyo tunaona tofauti yao na wewe wanategemea wewe utawaletea kejeli na dhihaka dhidi ya hizo habari za wazee wao kinyume chake unawaunga mkono kitu ambacho hawakukitegemea.
yaani mnavyojichanganya, huu mnakasha utawaumbua sana,
sasa kama ni historia ya wazee wenu kwanini mnataka upendeleo waonekane wao ndo bora zaidi kuliko wazee wengine?
 
Wanajamvi,
kuna habari za kufuja mali za EAMWS, mnajua zilisababisha nini na zilifanywa na nani?

Abdul Wahid na Sheikh Amir kuna mahali wanakutana katika chama nje ya TAA na TANU.
Mnajua ni wapi na ni nani kiongozi wa taasisi hiyo?

CC Zumbemkuu, Mag3, JokaKuu, Shariff Ritz, al maarufu Gombesugu, Jasusi, Wickama
tupe nondo mkuu.
 
yaani mnavyojichanganya, huu mnakasha utawaumbua sana,
sasa kama ni historia ya wazee wenu kwanini mnataka upendeleo waonekane wao ndo bora zaidi kuliko wazee wengine?

Wewe ndiyo unajichanganya wapi tumesema tunataka upendeleo tutake upendeleo kwa nani hili iweje.

Mohamed Said anaelezea historia ya Wazee wetu nyie roho zinawauma hakuna sehemu yeyote ambayo mmelazimishwa kuikubali.

Ndiyo maana mkashauriwa na nyie andikeni historia ya wazee wenu.
 
Back
Top Bottom