Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Niliwahi sema wazi kuwa TANU ni chama cha kiislam(chama cha wasilam wa Dar) ambacho kilibahatika mpata Nyerere ambaye alikifanya kikawa na taswira ya kitaifa bila kuua usilam..Wengi hawakuelewa sana
Nyerere ali struggle sana kuweza balance udini uliokuwa unaibuka kila mara,....hao waislam na uzao wa km akina Ritz bado wana ndoto ya kuifanya CCM kurudi ktk dyanamics za TANU.
Vitabu vingi vya hovyo vimeandikwa kwa vile watu wana papara na hawaangalii vitu kiuhasilia,wangeweza kuwa na point za kweli na muhimu ktk historia.
"Badala ya kusema Waislam pekee ndio wameleta uhuru, wangesema islam iliplay role kubwa ktk siasa za TANU".Hata leo wangepewa CCM yao.Kwani ktk uhuru ingekuwa TAA /TANU ya kiislam ya dar..basi isinge vuka kibaha na isiengekaa ivuke kibaa.Kwanini iende na vipi ingevuka wakati tayari zaidi ya Nusu ya watanzania walikuwa hawajui kiswahili,na uslam ulipiti anjia za watumwa? waislam wengine ni wale waliotaka uganga na uchawi ndio waliiigia dini.
Wanakumbi,
Huyu hapa na katika wale ndugu zetu ambayo waongozwa na chuki dhidi ya Wazee wa Mzizima, hebu ngoja tudadavue bayana zake kiduchu.
Hapo juu ndugu yetu amekiri kuwa TANU kilikuwa chama cha Waislam, ha ha haaa, baada ya kukiri anajaribu kumtafutia nafasi Nyerere kuwa ndiyo aliifanya TANU kikawa na taswira ya kitaifa, wakati Nyerere kaanza siasa na wazee wa Dar es Salaam 1952, Wazee wa Dar es Salaam wameanza kufaamika kimataifa acha kitaifa wakati wa AA 1930 wakati Nyerere ana miaka 8 sembuse TANU soma chini hapa.Niliwahi sema wazi kuwa TANU ni chama cha kiislam(chama cha wasilam wa Dar) ambacho kilibahatika mpata Nyerere ambaye alikifanya kikawa na taswira ya kitaifa bila kuua usilam..Wengi hawakuelewa sana
Hapa chini unaelezea habari za uongo kabisa kutokana na fikra zako.Kleist Sykes (1894 - 1949) was a Tanganyikan political activist. He helped formed the Tanganyika African Association.
Sykes was born in Pangani to father Sykes Mbuwane, a Zulu mercenary hired by the German Empire, and a Nyaturu mother. After his father died, Sykes moved with his godfather, Effendi Plantan, to Dar Es Salaam, and would later fight for the Germans in the First World War.[SUP][1][/SUP]
After the war, Sykes worked for the Tanganyika Railway. He met Dr. James Aggrey, Ghanaian teacher, who inspired Sykes to form the Tanganyika African Association (AA) in 1929, along with friends including Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu and Raikes Kusi. In the 1930s, AA members built the organization's headquarters at New Street, where the Tanganyika African National Union would later be created in 1954.[SUP][1][/SUP]
Sykes was the first African to join the Tanganyika Chamber of Commerce, and the second African to serve in colonial Dar es Salaam's Municipal Council.[SUP][1][/SUP]
Sykes had three sons, Abulwahid, Ally, and Abbas, who would also have prominent careers in Tanzania.[SUP][1][/SUP]
Nyerere asingeweza kufanya chochote alikuwa Mkirsto peke yake kama kungekuwa na udini asingeza hata kakaa pamoja na hawa wazee hebu msome chini hapa Nyerere mwenyewe.Nyerere ali struggle sana kuweza balance udini uliokuwa unaibuka kila mara,....hao waislam na uzao wa km akina Ritz bado wana ndoto ya kuifanya CCM kurudi ktk dyanamics za TANU.
Nadhani umeona Wazee walivyokuwa na mahaba na a Nyerere wakati wa harakati za uhuru.Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.
Wanakumbi huyu ndugu yetu sijui kaipata wapi kuwa wakati wa harakati za uhuru wa Tanganyika nusu ya Watanzania walikuwa hawajuhi kiswahili, kwa hiyo unataka kutuambia Nyerere alikuwa anajua kuongea lugha zote za Tanzania, ha ha haaa...nadhani wanaukumbi mmeona hoja dhahifu za huyu ndugu yetu. soma chini hapa harakati za TANU Tanga."Badala ya kusema Waislam pekee ndio wameleta uhuru, wangesema islam iliplay role kubwa ktk siasa za TANU".Hata leo wangepewa CCM yao.Kwani ktk uhuru ingekuwa TAA /TANU ya kiislam ya dar..basi isinge vuka kibaha na isiengekaa ivuke kibaa.Kwanini iende na vipi ingevuka wakati tayari zaidi ya Nusu ya watanzania walikuwa hawajui kiswahili,na uslam ulipiti anjia za watumwa? waislam wengine ni wale waliotaka uganga na uchawi ndio waliiigia dini.
Chini hapa angalia harakati za TANU Kenya.ILIKUWA ni huko Tanga tu katika historia ya Tanganyika kuwa dhana mpya katika siasa zaidi ya ule ubwana wa Wazungu uliongezwa katika uhusiano baina ya Waafrika na Waarabu. Dhana hii iliongezwa ndani ya mfumo wa siasa za Tanganyika ili kuwakinza Waafrika katika siasa. Hiki kilikuwa kitu ambacho Waafrika walikuwa hawajapambana nacho. Kwa zaidi ya karne moja walikuwa wamezoea ubwana wa Wazungu. Jimbo la Tanga lilibarikiwa na kuwa na Waafrika walioelimika sana. Waafrika hawa walikuwa kutoka kabila la Wabondei. UMCA ilikuwa imehama kutoka Zanzibar kwenda Magila katika Jimbo la Tanga mwaka 1875. Ukristo ulianzishwa na kustawi katika nchi ya Wabondei, na vivyo hivyo nafasi za elimu kwa watoto wa Wabondei. Katika lile wimbi la kuwania nafasi za elimu, watoto wengi wa Kiislamu walibatizwa. Ni jambo la kawaida miongoni mwa Wabondei kukuta majina kama Peter Saidi au John Ramadhani. Huu ni ukumbusho wa damu ya Kiislam katika Wabondei. Wabondei wengi walikwenda Makerere College na siasa za kizalendo zilipoanza baada ya Vita Kuu ya Pili, Wabondei walikuwa wamejaa katika utumishi wa serikali ya kikoloni. Gurudumu la historia ya Tanganyika likizungushwa na baadhi ya Wabondei, maarufu miongoni mwao wakiwa watu kama Martin Kayamba aliyejikomba sana kwa wakoloni, George Magembe mtu ambae huku alikuwa hayuko wala kule hayuko, hujui kama yupo na wazalendo au na wakoloni, Stephen Mhando; mzalendo mwenye msimamo mkali na na mdogo wake Peter.
Wabondei walikuwa ndiyo walimu, makarani, wakalimani mahakamani na maofisa wa ustawi wa jamii katika serikali ya kikoloni. Hili lilikuwa tabaka maalum la Waafrika, waliosomeshwa na wamishonari kuitumikia serikali ya kikoloni na katika kufanya hivyo kulitumikia Kanisa na Ukristo, uhusiano ambao ulikuwa wenye manufaa kwa pande zote mbili zilizokuwa zikishirikiana. Ilikuwa vigumu sana kwa Wabondei kutokana na upendeleo huo wasifikirie kwamba wana uhusiano maalum na Kanisa na serikali ya kikoloni. Hawa Waafrika wasomi kutoka shule za misheni na Makerere walikuwa watiifu kwa taasisi mbili zanye nguvu nchini, yaani serikali ya kikoloni na Kanisa. Kwa ajili hii basi, ilibakia kwa Wadigo Waislam wasiokuwa na elimu kama elimu ilivyokuwa ikiitikadiwa, kuunda TANU na kuongoza harakati za kudai uhuru.
Wamishionari waligundua kuwa Wadigo walikuwa wagumu sana kubatizwa na kuingizwa kwenye Ukristo kwa sababu ya imani yao thabiti katika Uislam. Kwa hiyo Wadigo hadi hii leo wamebakia kuwa kabila la Waislam. Baada ya kuukuta Uislamu umeimarika vyema katika pwani ya Tanga, wamishonari kwa kukataa kuhasimiana na Waislam, walianzisha misheni zao ndani zaidi mbali na pwani sehemu inayojulikana kama Misheni ya Magila. Hapa UMCA ilianzisha shule na hospitali. Wadigo walishikilia imani yao ya Kiislamu na wakabakia nyuma katika elimu kwa sababu ya kukataa kwao Ukristo. Kwa jili hii wakajinyima nafasi za kazi za madaraka katika seriklai ya kikoloni. Huku kuwapanga watu kwa tabaka kulikuwa na athari katika kuanzisha upinzani dhidi ya ukoloni kwa kuwa waliofadhiliwa na Kanisa walishindwa kupinga wakoloni kwa kuwa ukoloni na Ukristo walikuwa wamoja.
African Association huko Tanga ilikosa umoja baina ya wale walioitwa 'wasio na elimu na wasiojua kusoma' na wale wasomi ambao kutoka kwao wote hawa chama cha siasa kingeweza kuundwa. Waafrika wasomi, Wabondei waliunda vikundi vyao peke yao vya wasomi kutokana na juhudi za ofisa mmoja wa kikoloni. Vyama hivi vikijulikana kama Discussion Groups [SUP]167[/SUP] yaani, vikundi vya majadiliano, vilitarajiwa kutojihusisha na kisiasa na vilitiwa nguvu na serikali kuhimiza mijadala na kusoma vitabu. Katika muda wote wa uhai wa vikundi hivyo hawa wasomi wa Makerere walikuwa chini ya usimamizi wa afisa Mzungu.
African Association huko Tanga ilitawaliwa na watu wa mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na Kiafrika. Hawa walikuwa watu wenye elimu ndogo. Kundi hili halikuwa na mkabala mzuri na Wabondei wengi wao wakiwa Wakristo wenye elimu. Kundi hili lililokuwa na damu ya Kiarabu lilijiona bora kwa daraja kuliko Waafrika weusi. [SUP]168[/SUP] Kama hivi vikundi viwili muhimu vingeweza kuzikusanya pamoja nguvu tofauti zao, vingeweza kuunda umoja wa siasa wenye uwezo mkubwa sana kama ile kamati ndogo ya siasa ya TAA iliyoundwa huko Dar es Salaam. Muungano huu ungeweza kuongoza harakati za kudai uhuru huko na halikadhalika ungeweza kupata mafanikio makubwa kwa kuwashirikisha wananchi katika kudai haki zao. Lakini kama ilivyokuwa, hizi kambi mbili zilikuwa hasimu; kila upande ukijitenga mbali na umma; wengine walijiona bora kwa sababu ya rangi ya ngozi yao na wengine walijiona bora kwa sababu ya elimu yao.
Gavana Edward Twining alipounda Constitutional Development Committee mwaka 1949, na kukaribisha maoni na mapendekezo kutoka kwa raia, TAA Tanga ilijikuta haina uwezo wa kuandika waraka. Uongozi wa Waarabu katika African Association haukuwa na elimu, maarifa au ujuzi uliotakiwa kutayarisha na kuandika waraka kwa serikali. Wasomi wa Makerere katika vile vikundi vya majadiliano waliinyakua fursa hiyo na kuandika waraka ambao uliwakilishwa kwa Gavana Twining.[SUP]169[/SUP] Pamoja na ukweli kuwa waraka ule uliandikwa na Waafrika wenye elimu kubwa kwa wakati ule, kwa hakika waraka ulikuwa na upungufu ukilinganisha na ule ulioandikwa na kamati ndogo ya siasa ya TAA, Dar es Salaam.[SUP]170[/SUP]
Mwaka mmoja baadae, katika mwaka 1951 ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipozuru Tanganyika, kile kikundi cha majadiliano, ingawa si wawakilishi wa wananchi kikifanya kazi yake nje ya TAA, kiliwasilisha waraka kwa ujumbe huo kikionyesha kuwa wao wanawakilisha maoni ya Waafrika. Hili lilizusha mzozo baina ya wasomi wa Makerere na ule uongozi wa Waarabu katika TAA.[SUP]171[/SUP] Haya makundi mawili yalijikuta hayana kusudio au muelekeo wenye maana, kidogo kidogo yalisahaulika. Kule Tanga mara chache watu waliihusisha ofisi ya TAA na siasa. Ofisi ya TAA inakumbukwa na kuhusishwa na mahakama ambako Kadhi, Sheikh Ali bin Hemed alihukumu jamii ya Waislam kwa kutumia sharia.
Lakini Tanga iliibuka mwaka 1955 na kukabiliana na serikali ya kikoloni kupitia juhudi binafsi za kikundi cha wafanyabiashara wadogo wadogo katika soko la Ngamiani. Kikundi hiki kiliongozwa na kijana Peter Mhando, katibu wa zamani wa kile kikundi cha majadiliano cha wasomi wa Kibondei. Akikiongoza kikundi hiki ambacho kilikuwa na Waislam, alikuwa baharia mstaafu, Hamis Heri Ayemba. Hamis Heri alikuwa Mmanyema kutoka kabila la Wakusu wa Belgian Congo. Peter Mhando alikuwa akifanya kazi kama mhandisi katia Noran Industries- wanunuzi wa nazi na watengenezaji sabuni pale Tanga. Hamisi Heri alikuwa na umri wa katikati na katika ujana wake alikuwa baharia na alipata kusafiri chombo kimoja na Abeid Amani Karume, ambae baadae alikuja kuwa rais wa Zanzibar. Baada ya Vita Kuu ya Pili, Hamisi Heri alirudi kwao Tanga ili aanze biashara. Heri alikuwa mtu aliyejikuza na kujielimisha mwenyewe; na alikuwa amesafiri sana. Hamisi Heri alizungumza vizuri sana Kiingereza na Kiarabu. Katika miaka yake ya mwanzo katika biashara, alikuwa dalali. Heri aliwashangaza wateja wake kwa uhodari wake wa lugha mbali mbali, akinadi bei kwa Kihindi au Kiarabu, kutegemea utaifa wa watu waliokuwepo pale mnadani.
Harakati za kudai uhuru zilipoanza Heri alikuwa ametajirika na mmoja wa Waafrika wenye kuheshimiwa sana mjini Tanga. Mhando alipochoshwa na kile kikundi cha maji
Mambo yalikuwa yanageuka dhidi ya Waingereza katika makoloni yake yote Afrika ya Mashariki. Wazalendo walikuwa wakifanya harakati zao na kuvuka mpaka mmoja wa nchi hadi mwingine bila matatizo. Ule wakati wa wao kusafiri kwa kificho na kufanya mikutano yao nyakati za usiku mafichoni ulikuwa umepita. TANU ilikuwa na nguvu ya sasa kuangali nje ya mipaka yake. Katika pwani ya Kenya katika mji wa Mombasa, kijana mmoja kutoka Moshi, Ismail Bayumi, aliyeajiriwa na Mombasa Municipal Council akivutika na mwenendo wa matukio ya kisiasa kama yalivyokuwa yakitokea katika Afrika Mashariki, aliwashawishi Watanganyika waliokuwa wakiishi na kufanya kazi Mombasa kuunda kile kilichokuja kujulikana kama Mombasa TANU Club. Sheria ya Kenya haikuwaruhusu Watanganyika kuunda chama cha siasa katika ardhi ya Kenya, kwa hiyo TANU Club ilisajiliwa kama chama cha starehe na ilikuwa na ofisi zake katika Barabara ya Lohana. Ismail Bayumi alichaguliwa rais wake wa kwanza. Lakini kwa hakika TANU Club ilifanya kazi kama chama cha siasa kwa niaba ya TANU, KANU na KADU kwa kiwango fulani. Wakati huo Jomo Kenyatta alikuwa Manyani akitumikia kifungo cha miaka saba gerezani kwa kuhusika na harakati za Mau Mau.
Tom Mboya aliitumia TANU Club kuifanyia kampeni KANU na kupigania kufunguliwa kwa Kenyatta kutoka gerezani. Kote nchini Kenya KANU ilikuwa ikiibuka kama chama cha wananchi wote. Wakati sera za KANU zilikuwa zile za mwelekeo wa kuwaunganisha wananchi wote dhidi ya ukoloni, KADU chini ya Ronald Ngala, kwa upande mwingine, ilikuwa na labda isemwe, ufahamu mfinyu, KADU ikifungamanisha sera zake na siasa za ukabila na utawala wa majimbo. Kwa hiyo KADU ilikuwa ikikusanya nguvu za upinzani wa makabila madogo dhidi ya KANU. KANU chini ya Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga na Tom Mboya, ilichukuliwa kuwa ni chama cha makabila mawili makubwa nchini Kenya, yaani Wakikuyu na Wajaluo ambayo yakiachiwa kutawala yatameza makabila madogo. Nchini Tanganyika ambako ushindani wa kikabila katika siasa haukuwepo, TANU Club ilijikuta kiitikadi inapenda kuwa karibu zaidi na KANU kuliko KADU.
TANU Club ilikuwa ikiandaa dansi katika Ukumbi wa Tononoka na dansi hizi zilikuja kupendwa sana na wanasiasa wa Kenya. Ilikuwa chini ya pazia la sherehe hizi katika Ukumbi wa Tononoka ndiyo wanasiasa wa Kenya na wale wa TANU Club walipata nafasi kupashana habari namna TANU ilivyokuwa ikiendelea nchini Tanganyika na nini TANU ingeweza kufanya huko Tanganyika ili kusaidia harakati za kudai uhuru nchini Kenya. Baada ya TANU Club kufanikiwa sana huko pwani uongozi wake uliamua kufungua tawi la TANU Club mjini Nairobi katika sehemu ya Pumwani. Tom Mboya na Ronald Ngala walikuwa mstari wa mbele katika sherehe zote za TANU Club, wakishiriki katika shuguli zake Mombasa na Nairobi.
Msukumo mkubwa wakati ule nchini Kenya ilikuwa kufanya kampeni ya nchi nzima kuwashinikiza Waingereza wamwachie huru Kenyatta aliyekuwa akichukuliwa na wananchi wote kama kiongozi na nguvu ya umoja wa Waafrika wa Kenya. Katika wimbi hili la kutaka Kenyatta afunguliwe kutoka gerazani, Tom Mboya alimdokeza Ismail Bayumi kuwa TANU ingeweza kusaidia katika kampeni hii ya kuwashinikiza Waingereza kumtoa Kenyatta kifungoni. Ismail alifikisha wazo hili makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam kwa kupitia mtu maalum aliyekuwa akiwasiliana na Tom Mboya na Nyerere kwa siri. TANU ilimtuma Bibi Titi Mohamed kwenda Kenya kuzitia shime harakati za kufunguliwa Kenyatta. Wazalendo nchini Kenya walikuwa wameshindwa kabisa kuwaingiza wanawake ndani ya KANU hivyo kuzinyima harakati za uhuru nguvu kubwa sana na ya kutegemewa ya akinamama. [SUP]175[/SUP] Huko Mombasa TANU Club ilifikiria kuwa kumleta Bibi Titi kuja Kenya kuifanyia kampeni KANU ilikuwa ni kitu kipya cha kuwahamasisha wanawake ndani ya KANU na kwa hiyo kuongeza nguvu mpya na kutia ari ya utaifa katika Kenya.
Bibi Titi alikuja Mombasa na kufanya mkutano Ukumbi wa Tononoka. Kwa kawaida kwa madhumuni ya kupata kibali mikutano hii ilikuwa inahesabiwa kama ni mikusanyiko ya kufanya sherehe siyo mikutano ya siasa na ilikuwa ikifanyika ndani. Lakini mkutano huu ulikuwa na umuhimu wake kwa sababu ya kuwako Bibi Titi Mohamed mjini Mombasa. Wengi walikuwa wamemsikia Bibi Titi lakini hawakuwa wamepata kumuona. Watu walijaa ndani ya ule ukumbi hadi nje kuzunguka viwanja vya Ukumbi wa Tononoka. Kwa kweli kwa hali yoyote mkutano ule usingeweza kuitwa kuwa ni mkutano wa wanachama wa TANU Club mjini Mombasa, au hata mkutano wa TANU Club Kenya nzima, kwa sababu wanachama wa KANU waliwazidi wanachama wa TANU Club kutoka Tanganyika.
Kenya ilikuwa bado haijaweza kumtoa hata mwanamke mmoja wa kiwango cha Bibi Titi. Kwa wakati ule kumwona mwanamke wa Kiislamu amesimama bila baibui akihutubia halaiki ya wanaume ilikuwa ni jambo la kushangaza sehemu za pwani, ambako wanawake walitembea huku wamejifunika mabaibui na hawakutakiwa hata kufanya kazi maofisini. Bibi Titi alifanya mikutano kule Mombasa na Nairobi akiwasisitizia watu wasikate tamaa wasimame pamoja hadi Kenyatta amefunguliwa kutoka gerezani. Habari za mikutano hii iliandikwa kwa mapana na marefu na magazeti ya Mombasa Times na Taifa Leo.
Miongoni mwa Wakenya kule pwani waliyofanya kazi karibu sana na TANU Club walikuwa Msanifu Kombo na Abdallah Ndovu Mwidau. Kombo na Mwidau kwa sababu ya mchango wao kwa KANU kupitia chama chenyewe na kupitia TANU Club wakaja kuwa na ushawishi mkubwa kwa Rais Kenyatta. Wazalendo hawa wawili baada ya uhuru wa Kenya wakawa watu wenye sauti kubwa kule pwani. Hakuna mtu kutoka pwani alikuwa anaweza kuteuliwa na kushika nafasi yoyote muhimu na Kenyatta bila Abdallah Mwidau na Msanifu Kombo kumuunga mkono. Mara tu baada ya kufunguliwa kutoka gerezani, Kenyatta alikwenda Mombasa kutoa shukrani zake kwa Msanifu Kombo, Abdallah Mwidau na TANU Club kwa msaada wao kwa KANU na kwa kufanya kampeni ya kufunguliwa kwake. Mkutano ulitayarishwa kule Tononoka na Kenyatta alikuja kutoa hotuba ya shukrani na kukutana na wanachama wa TANU Club.