Uchumba wetu ulikufa sababu ya dini ni tofauti

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Leo pitapita yangu picha zilizopo kwenye digital camera kabla kuja smartphone kupiga picha nikaona picha ya mchumba wangu ambaye tulipendana sana.

Ulianza kubadilishwa na wazazi baada kujua mimi ni mla kitimoto na bia mbili za baridi.

Jibu nililo mpa "yani dini yangu yenyewe imenishinda kwenda kanisani jumapili niweze ya kwenu"

Mwisho tukaja kuachana na kupoteana kabisa.Hongera una watoto sasa sijui ni sheikh yupi!
 
Mshukuru Mungu wako uliepushiwa kitu kikubwa mno
 
Leo pitapita yangu picha zilizopo kwenye digital camera kabla kuja smartphone kupiga picha nikaona picha ya mchumba wangu ambaye tulipendana sana.

Ulianza kubadilishwa na wazazi baada kujua mimi ni mla kitimoto na bia mbili za baridi.

Jibu nililo mpa "yani dini yangu yenyewe imenishinda kwenda kanisani jumapili niweze ya kwenu"

Mwisho tukaja kuachana na kupoteana kabisa.Hongera una watoto sasa sijui ni sheikh yupi!

Hii imenikuta live, kuna mbuzi mmoja nlifahamiana naye kwa miaka kibao! Akijua fika nakula mbuzi katoliki nakushushia ile juice ya harusi ya Cana ya Galilaya!

Miaka kadhaa baadae ananiambia unajua wazee wanasema kama vipi hamia imani ya mwezi na nyota!

Nilimwambia tu…pita hivi maisha mema!
 
Ushauri wangu kwa vijana
Oa au olewa na mtu wa dini yako
Oa au olew na mtu wa kabila lako.
Daima utajanishukuru
Narudia
Oa au olewa na mtu wa dini yako
Oa au olewa na mtu wa kabila lako.
Utakuja nishukuru
Kuhusu dini naunga mkono watu waowane wa imani moja, lakini kuhusu Kabila hapana, kuna faida nyingi za kuchanganya Kabila kuliko hasara.

Hata ukisema uowe Kabila moja bado kuna koo huwezi kwenda kuowa zina matatizo.
 
Mkuu narudia tena
Oa au olewa na mtu wa dini yako
Oa au olewa na mtu wa kabila lako
Utakuja nishukuru. Leo sina muda wa kuandika sana ila kama unapata mtu wa kabila lako oa au olewa itakuepusha na ugomvi wa vyakula. Ugomvi wa tamaduni za kabila jingine. We mzaramo unaolewa na mmasai. Hapo kuna kana kamgogoro ka tamaduni pia misosi na mambo mengine. Si lazmishi mtu aoe au aolewe na kabila lake ila itakusaidia mbeleni amin
 
Tukubaliane tu kuna makabila bila kuyataja hayastarabika, watu wanapoowana kwa kuchanganya makabila inampa faida mmoja wapo kuadapt ustaarabu na kizazi chake kitastaarabika pia.

Wajinga Wawili wakiowana ni tatizo, na hili ndio tatizo linawakabiri Waarabu, wako wenyewe wana makabila yao kuna mabedui hawezi kuolewa na Kabila lingine, Sasa ikitokea uko Fulani ni wajinga basi ni kizazi chote.

Nioneshe Mwarabu gani uliyesoma naye alikuwa Kipanga darasani?
 
Binadamu tumeumbiwa ubinafsi. Kilamtu anaangalia kwake kwanza. Usiangalie kuchanganya wajinga na wenye akili maana we mwenyewe ukishajua mtu ni mjinga huwezi muoa au kuolewa nae.

Binadamu wote tunaangalia nyumban kwanza hayo mengine ni baadae.

Neno langu si sheria
 
Mkuu narudia tena
Oa au olewa na mtu wa dini yako
Oa au olewa na mtu wa kabila lako
Utakuja nishukuru. Leo sina muda wa kuandika sana ila kama unapata mtu wa kabila lako oa au olewa itakuepusha na ugomvi wa vyakula. Ugomvi wa tamaduni za kabila jingine. We mzaramo unaolewa na mmasai. Hapo kuna kana kamgogoro ka tamaduni pia misosi na mambo mengine. Si lazmishi mtu aoe au aolewe na kabila lake ila itakusaidia mbeleni amin
Hii ya kuhusu kabila ina sides mbili. Usihitimishe kwa kusema oa/ olewa na mtu wa kabila lako.
Mimi kama mtu niliyeoa mtu wa kabila tofauti kwa miaka 10 sasa ntakukatalia, tena kwa hoja thabiti. Habari za chakula, mila na desturi haijawahi kuwa sehem ya changamoto yetu.

Hata hivyo, kuna waliooa/olewa na watu wa makabila tofauti wanakabiliwa na changamoto za chakula, mila na desturi/ lugha n.k.

Ndio maana nasema, hii hoja ina ambiguity.
 
Binadamu tumeumbiwa ubinafsi. Kilamtu anaangalia kwake kwanza. Usiangalie kuchanganya wajinga na wenye akili maana we mwenyewe ukishajua mtu ni mjinga huwezi muoa au kuolewa nae.

Binadamu wote tunaangalia nyumban kwanza hayo mengine ni baadae.

Neno langu si sheria
Neno lako si sheria ndio maana makabila mengine mabinamu wanaowana kuweka strong bond kwenye ndoa.
 
Sema hamkupendana
Dini sio tatizo mkiridhiana
Mkuu nakumbuka enzi zangu niliwahi kuwa na ukaribu na mtoto wa watu tena walikuwa wa ile iman ya kaptula ndefu ila nilikuja jinasua huko na nikapata somo la oa dini yako oa labila lako kupunguza mizozo ndani ya familia. Baada ya hapo nimekuwa nikishaur sana vijana kuhusu haya mambo
 
Back
Top Bottom