Uchumi bado Umekaza? Vodacom yajiondoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Uchumi bado Umekaza? Vodacom yajiondoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Tujikumbushe udhamini wa miaka 3 uliotiwa saini mwaka 2019

TFF,Vodacom wasaini Mkataba wa Bilioni 9 kuidhamini Ligi Kuu​

August 23, 2019In : Ligi Kuu Tanzania Bara



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom wamesaini Mkataba wa miaka 3 wa Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mkataba huo unathamani ya shilingi bilioni 9 ambapo kila mwaka shilingi bilioni 3.

Ligi Kuu ya Tanzania Bara sasa itafahamika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
Rais wa TFF Wallace Karia akizungumza katika hafla ya utiaji saini amesema Udhamini huo utaleta matokeo chanya na watatoa ushirikiano kwa muda wote wa Mkataba.

Amesema Uendeshaji wa Mpira wa Miguu una gharama kubwa,wanawakaribisha Vodacom kushirikiana na wadhamini wengine.

Rais Karia ameongeza kuwa Kuongezeka kwa idadi ya timu kwenye mashindano ya CAF kufikia 4 ni kielelezo tosha cha kuimarika kwa Ligi Kuu.

Mkurugenzi wa Vodacom Hisham Hendi amesema ni furaha kubwa kuingia mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Hendi amesema Katika mipango yao ni kuona siku moja Watazamaji wanaoingia Uwanjani wanapata urahisi wa kununua tiketi kupitia huduma ya Mpesa.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ameipongeza TFF kwa hatua ya kusaini Mkataba na Kampuni ya Vodacom kudhamini Ligi Kuu.

Amesema Vodacom wameona uendeshaji bora wa TFF ambayo inaaminika na wanaingia katika moja ya Ligi Bora duniani.
Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika Makao Makuu ya Vodacom Plc source : TFF,Vodacom wasaini Mkataba wa Bilioni 9 kuidhamini Ligi Kuu – TFF
 
Jumatano, Mei 26, 2021

TFF na Azam Media zasaini udhamini wa Sh bilioni 225.6 kwa miaka 10 kurusha mechi live

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) na Azam Media zimesaini mkataba wa kihistoria wa udhamini wa kurusha matangazo ya Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Sh bilioni 225.6 kwa miaka 10, utakaomfanya bingwa wa msimu ujao kuondoka na kitika cha Sh milioni 500 kama bonasi.

Dau hilo ni kubwa ikilinganishwa na lile la miaka mitano iliyopita ambapo pande hizo mbili zilisaini mkataba kama huo wa Sh bilioni 23. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema tukio hilo limekuja baada ya Azam Media kushinda zabuni waliyokuwa wameitangaza tangu Aprili 2, mwaka huu.

“Tunawapongeza Azam Media kwa kushinda zabuni, kiwango hicho cha fedha ni ukijumlisha na kodi. Haijawahi kutokea mkataba kama huu katika historia ya soka letu.

Miaka ya karibuni ligi yetu imekuwa ikiimarika kwani tunashika nafasi ya nane Afrika,” alisema. Karia alisema mkataba huo ni kwa ajili ya TV tu na kwamba wanatarajia kupata na kituo kimoja cha redio kitakachoingia udhamini nao.

Alisema ana imani kuwa udhamini huo utavutia wachezaji wengi kuja kucheza soka nchini na ushindani kuongezeka. Rais huyo wa TFF alisema udhamini huo ni sehemu tu, kwani wanakusudia kupata wadhamini wengine kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo waliopo sasa, hivyo wanatarajia kupata fedha nyingine zaidi ya Sh bilioni 30. “Lazima timu zioneshe matumizi kila msimu ili kupata fedha hizo.

Kipaumbele muhimu kwa ajili ya fedha hizo ni kulipa wachezaji mishahara, usafiri na matibabu na sio usajili. Pia waamuzi watakuwa wanalipwa vizuri zaidi,” alisema. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando alichambua fedha hizo, akisema wamekubaliana asilimia 67 ya malipo ya kila msimu ziende moja kwa moja kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu.

Alisema msimu wa kwanza yaani ujao wa 2021/2022, Azam Media itatoa Sh bilioni 12 huku klabu zikipata Sh bilioni 8 na sehemu ya fedha zinazobakia zitasaidia maendeleo ya soka, TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB ).

“Fedha hizi zitakuwa zikiongezeka kila msimu na msimu wa mwisho wa mkataba yaani 2030/2031, Azam Media itatoa Sh bilioni 28 na wakati huo timu zote kwa ujumla zitapata Sh bilioni 19,”alisema Mhando. Alisema mbali na hayo, kutakuwa na bonasi kwa klabu hizo ili kufanya ligi iwe na ushindani mkubwa kwa kila nafasi ya msimamo wa ligi kila inapofikia tamati.

Mhando alifafanua kwa misimu mitatu ijayo yaani 2021/22 mpaka 2023/24, bingwa wa Ligi Kuu atapata bonsai ya Sh milioni 500 kwa msimu, mshindi wa pili Sh milioni 250, wa tatu Sh milioni 225 na nafasi ya nne Sh milioni 200. “Fedha hizo zitakuwa zikiongezeka kila msimu na ndio maana msimu wa 2028/29 mpaka 2030/31 bingwa atakuwa akipata Sh milioni 700, wa pili Sh milioni 325, nafasi ya tatu Sh milioni 275 na ya nne Sh milioni 250,” alisema.

Alisema bonasi hizo hazitaishia kwa timu nne pekee, bali kuanzia nafasi ya tano kuanzia msimu ujao atapata Sh milioni 65, ya sita Sh milioni 60, ya saba Sh milioni 55, ya nane Sh milioni 50, ya tisa Sh milioni 45, ya 10 Sh milioni 40, ya 11 Sh milioni 35, anayefuatia hadi ya 13 watapata Sh milioni 30, 25 na 20, ambapo pia timu zinazocheza mtoano zitapata Sh milioni 20.

Alisema anatamani kuona ligi ya Tanzania inashika nafasi ya tatu Afrika na kuongeza kuwa wamekusudia kuimarisha ubora wa matangazo yao kwa kuweka miundombinu ya taa katika baadhi ya viwanja ili kuonesha mechi za usiku na kufunga mbao za kidigitali za matangazo ya biashara viwanjani
 
Kampuni ya Mawasiliano Vodacom imelitaarifu Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania Kuwa haina nia ya kuendelea kuidhamini ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League ikitoa sababu ya mwenendo mbaya wa Biashara.

Ni uchumi? Bwana Bakhresa kayatoa kwenye uchumi upi mabilioni atakayoyaweka kwenye Mpira?
Si tulikuwa uchumi wa kati?? na walishirikiana na Mwendazake jiwe kuzuia Harakati za Lissu aliyetaka kuwaokoa? Na bado kila mtu ataonja dhambi alizofanya akiwa hai.
 
Kampuni ya Mawasiliano Vodacom imelitaarifu Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania Kuwa haina nia ya kuendelea kuidhamini ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League ikitoa sababu ya mwenendo mbaya wa Biashara....
Wana hasira za kubinywa kwa mabando yao waliyotaka kutuchinja nayo.
 
Sio vodacom tu Kampuni zote za simu zipo kwenye wakati mgumu sana.. biashara ya voice and sms service zimeshuka sana due to the likes of whatapp and telegram while bei ya data aka bundle ipo chini ukilinganisha na uwekezaji uliofanyika hasa kwenye 4G. Biashara inayofanya vzuri kwa mitandao ya simu ni mobile money tu.

So hili tulitegemea hasa baada ya vodacom kutangaza loss on it's 1st quota financial report.

While sisi tunafurahia bei za bundle kua chini huko kwao soon wataanza kupunguza wafanyakazi. Tigo wao wameona isiwe tabu wame exit the market, airtel wao wameamua kuuza minara ili kuweka vitabu vya hesabu sawa.

So before hatujaanza kulaumu we need to ask ourselves kwann hivi, then tutafte taarifa sahihi then from there tuna make a good judgement. Maana naona humu ndani watu wanatoa mapovu tu bila kua na taarifa sahihi.
 
Mwaka wao wa fedha uliopita vitabu vya mahesabu vinaonesha ilipata hasara kubwa baada ya kodi..Pengine ni namna ya kupunguza gharama ili mambo yakae sawa.
kwani kodi inalipwa na kampuni au walaji wa huduma?
 
Azam kazi kwako - pande hilo wewe tu.
 
TFF inaendeshwa kipumb.v sana..

Azam wamelipa haki za kuonesha mpira kwa miaka kumi in lumpsum bila kujal kuwa league yetu inakuwa kila mwaka..
Alaf Voda com ndio wajipendekeze na kutoa hela za bure huku Azam wakilamba hela za matangazo na subscription fee.. League jinga hiyo
Hawajawahi kulipa in lumpsum, na hawatalipa in lumpsum, hiyo pesa huwa ina tolewa kido kidogo, kulingana na makubaliano.huwezi kufikia hitimisho tu kuwa eti ligi yetu inakuwa kila mwaka, ligi iliyojaa ubabaishaji hivi, hili lilitegemewa tu inawezekana labda TFF, walimwambia ajaribu kuboresha mkataba wake wa udhamini inakuwaje zawadi ya mshindi wa kwanza apewe milioni 70!!, huku jamaa anatoa bonus ya milioni 500, kwa huyo mshindi?!!kifupi ligi ya bingo ni hasara tu.
 
Kampuni ya Mawasiliano Vodacom imelitaarifu Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania Kuwa haina nia ya kuendelea kuidhamini ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League ikitoa sababu ya mwenendo mbaya wa Biashara.

Ni uchumi? Bwana Bakhresa kayatoa kwenye uchumi upi mabilioni atakayoyaweka kwenye Mpira?
Hayatuhusu, vodacom majizi tu ya vifurushi halafu wanatueleza kitu gani
 
Ningekuwa karibu na raisi ningemshauri bakhresa awe na kampuni ya mawasiliano tanzania,alete mabasi,apewe miradi ya mwendo kasi,apewe bandari,apewe viwanja vya ndege na mpira sisi tukusanye kodi tu bora hata linchi limilikiwe na mtu asiye na chama
 
TFF inaendeshwa kipumb.v sana..

Azam wamelipa haki za kuonesha mpira kwa miaka kumi in lumpsum bila kujal kuwa league yetu inakuwa kila mwaka..
Alaf Voda com ndio wajipendekeze na kutoa hela za bure huku Azam wakilamba hela za matangazo na subscription fee.. League jinga hiyo
Una uhakika wamelipa hela yote ya miaka kumi mara moja? Nina mashaka na hilo maana kuna sehemu niliona watalipa kiasi fulani kila mwaka na kila mwaka watakuwa wakiongeza pesa wanayolipa ili mradi baada ya miaka kumi watakuwa wametimiza $100m. Pia kulipa lumpsum haimake business sense kwa Azam wala kwa TFF.
 
Ningekuwa karibu na raisi ningemshauri bakhresa awe na kampuni ya mawasiliano tanzania,alete mabasi,apewe miradi ya mwendo kasi,apewe bandari,apewe viwanja vya ndege na mpira sisi tukusanye kodi tu bora hata linchi limilikiwe na mtu asiye na chama
Nani alikwambia bhaharesa hana chama?na tangu lini raisi aka dectate business plans za mfanyabiashara yoyote?kwamba ukampe mwendokasi ht km haipo kwenye plans zake?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...JF never stop to amaze me
 
Juzi juzi tu
baada ya azam kazamisha TFF BILLION 225

Sahivi,
bei ya ving'amuz vya dish imepanda imepanda kufikia laki 2 (200,000) taslimu kwa kingamuz kimoja complete.

Tujiandae kwa bei mpya za vifurushi

[emoji23][emoji23]YAJAYO YANAFURAHISHA
 
ilikuwa lazima wajitoe , wa kurusha matangazo atoe bonas ya 500m ...just bonus nahisi azam aliamua kumfukuza voda mapema na voda kaona isiwe tabu , make ilikuwa lazima wapande dau utatoaje milion 80 alafu aongezewe bonus ya 500m
 
Juzi juzi tu
baada ya azam kazamisha TFF BILLION 225

Sahivi,
bei ya ving'amuz vya dish imepanda imepanda kufikia laki kwa kingamuz kimoja complete...
Hahahaha...kuna mtu hapo juu anataka tumpe miundo mbinu yote ss tukusanye kodi ili siku akipandisha gharama turudi humu kulialia...
 
Back
Top Bottom