Uchumi ni tatizo kubwa katika ndoa za Vijana

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,405
Reaction score
13,411
Jioni hii nimekaa room kwangu mara nasikia majirani (wake zao) wametoka kwenye mizunguko yao. Katika hii nyumba kuna wapangaji watatu wawili ni familia bachelor ni mimi tu.

Punde nasikia moja ya jirani yangu analalamika kwa mwenzie kua mmewe karudi kapiga msosi wote bila kujali kua yeye kala au hajala na yeye karudi ana njaa. Mbaya zaidi mwamba kapita na mboga zote (maharage) bibie karudi na mchele wa kupika jioni akitegemea kuna mboga. Kwa hasira bibie ana mpango wa kuanza kula mgahawani kama mbwai mbwai tu.

By the way mwamba namfahamu ni mtafutaji si kama anakaa nyumbani sema tu ni ndio harakati za kuungaunga, ila anajituma sana tu na hachagui kazi. Huenda alipitiwa tu ila mkewe kawaka balaa.

("Wanawake hawapendi safari, wanapenda asali"- Nikki wa Pili)
 
Mwanamke akitafuta halafu mwanaume akala roho zinawaumaga Sana sijui kwanini
 
Mwanamke akitafuta halafu mwanaume akala roho zinawaumaga Sana sijui kwanini
Pesa yao ni kama ina chapa toka BOT si kwa matumizi ya nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…