Uchumi wa Bangladesh ni mkubwa kuliko uchumi wa taifa lolote Afrika

mkuu unataka kusema kwa uchumi wa mtu mojamoja Tanzania ina afadhali kuliko Bangladesh?

mbona hata tukiangalia hizo GDP per capita figures za tanzania na Bangladesh bado zinaonesha sisi ni maskini kuliko hao Bangladesh, sijaelewa hapo.
 
mkuu unataka kusema kwa uchumi wa mtu mojamoja Tanzania ina afadhali kuliko Bangladesh?

mbona hata tukiangalia hizo GDP per capita figures za tanzania na Bangladesh bado zinaonesha sisi ni maskini kuliko hao Bangladesh, sijaelewa hapo.
Sijajikita sana kulinganisha Bangladesh na Tanzania. Nimejikita kwenye heading ya kulinganisha Bangladesh na taifa lolote Afrika, na kuonesha uchumi mkubwa si lazima uwe uchumi mzuri, nchi inaweza kuwa na uchumi mkubwa kutokana na kuwa na watu masikini wengi.

Nimetoa uchumi wa Bangladesh kulinganisha na Seychelles kwa GDP per capita.

Main point, ukubwa wa uchumi si kipimo kizuri cha uzuri wa uchumi. Hata masikini wengi wakiwa pamoja wanatengeneza uchumi mkubwa na kugawana umasikini tu.

Tunavyoilinganisha Bangladesh na Afrika tuangalie angalau GDP per capita.

2021 figures.

Bangladesh $ 2458

Seychelles $ 14,653
Mauritius $ 9,106
South Africa $ 7,055
Botswana $6,805
Cape Verde $ 3,293
Ivory Coast $ 2,549

Kwa hivyo utaona licha ya Bangladesh kuwa na uchumi mkubwa , watu wa Bangladesh hawajaweza kufanya "uchumi" vizuri na kufaidika zaidi kutoka uchumi huo mkubwa kulinganisha na watu wa nchi nyingi za Afrika.

Kitu kingine unachobidi kuelewa ni kwamba, nchi inaweza kuwa na uchumi mkubwa, halafu huo uchumi mkubwa ukawa unachukuliwa na makampuni makubwa ya nje.

Hili ni tatizo kubwa Bangladesh. Tatizo linaloweza ku explain kwa nini Bangladesh on paper ina uchumi mkubwa sana, lakini maisha ya watu ni ya umasikini mkubwa.

Bangladesh wanatengeneza sana nguo na viatu. Kwa cheap labor. Sasa mauzo ya hivi viatu na nguo yanavyofanywa katika soko la dunia, hesabu zinaonesha hela nyingi zimeenda Bangladesh, wakati makampuni makubwa yana njia kemkem za kukwepa kodi na kuhakikisha hela zinabaki kwao, kama vile kununua malighafi na mitambo kutoka kwa international affiliates at inflated prices.

Hapo ndipo utaona nchi inaweza kuwa na uchumi mkubwa, halafu sehemu kubwa ya huo uchumi mkubwa inaenda nje, na wananchi wake wanabaki masikini tu.

Bangladesh na uchumi wake mkubwa imezidiwa mpaka na Ivory Coast (GDP per capita 2021) nchi ya Afrika ambayo imetoka kwenye vita muda si mrefu uliopita.
 
Mnashangaa nini wakati mada kama hizi hata watanzania hawawezi kuchangia na hiyo tu ni taswira tosha kwamba nchi ina watu wa namna gani.

Sasa nchi yenye watu kama hawa watawezaje kushindanishwa na Bangladesh ambayo watu wake hawakimbizi mwenge.
Wabongo lete mada ya ngono,wapo ma professor. Huko kwingine,usiwambie
 
Kwanini mnafuatilia vitu vinavyowajaza frustration..
!?
 
Kwanini mnafuatilia vitu vinavyowajaza frustration..
!?
Kwa sababu ni kwa kufuatilia vitu vinavyotujaza frustration tu ndivyo tunaweza kuondoa frustration.

Matatizo yakiwapo, hayamaliziki kwa sababu huyafuatilii.

Nyumba yako ikiwa inawaka moto, moto hauwezi kujizima wenyewe kwa sababu wewe huufuatilii.

Inakubidi ufuatilie matatizo, uyaelewe, ili uweze kuuyamaliza.
 
Sawa.
Mungu akubariki.
 
Tatizo ni hizi dini kuu mbili. Uislam na ukristo. Dini hizi ni wakala wa utumwa na umaskini. Kama waafrika ikitokea tukaacha na hizo imani, tutapiga hatua kubwa kimaendeleo maana akili zetu zote zimefungiwa hapo.
Huko bangladesh kuna dini gani
 
Ushamba ni mwingi bongo watu hawatake risk ya kufungua viwanda wao wanataka kwenda china kupiga picha basi wanaona wamepiga sana.

Ila nakuambia kuna vijana baadae hawa graduates jobless watakuja kupata idea ya kuunda viwanda vya nguo ,vyombo ,watafika mbali sana utajiri wa bongo ni dili za kusupply vitu kutoka nje kwa kufanya logistics..

Zile mashine za nguo zinauzwa china tena kibao ila hakuna mtu ananua ,kwanza wanaogopa operating costs ya viwanda wanataka mambo cheap sana ....Hii mitandao ndio ujinga kabisa mtu ili apost yupo Dubai, china , Marekani kufunga mzigo hapo ndio anaona ufahari.
 
Halafu kuna Wabangladesh zaidi ya 150 millions wanaishi nje ya Bangladesh...!

Ndo Nchi ambayo Kiongozi wa Nchi anaweza kusimama, na kuwaomba Raia waende nje ya Nchi wakatafute Maisha.

Kuna pengo kubwa mno la walionacho na wasionacho.
 
Ni kweli

Lakini ni nchi chafu, overpopulated na yenye masikini wengi sana
 
Watu mnashindwa kuendesha mradi wa Mwendokasi....-Magari tu..mtaweza kujenga viwanda..Afrika viongozi hawana maono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…