Uchumi wa Bangladesh ni mkubwa kuliko uchumi wa taifa lolote Afrika

Uchumi wa Bangladesh ni mkubwa kuliko uchumi wa taifa lolote Afrika

Ukubwa wa uchumi maana yake nini?

Unaelewa kuwa nchi inaweza kuwa na uchumi mkubwa halafu bado ikawa masikini?

Yani nchi ina mamilioni ya masikini, ukijumlisha viuchumi vyao vyote vya dola moja moja ma nusu mpaka mbili kwa siku unapata uchumi mkubwa sana, lakini nchi nzima kiuchumi imejaa masikini tu. Ndiyo Bangladesh hiyo.

Yani hapo kinachofanya uchumi kuwa mkubwa ni wingi wa masikini tu wanaonunua unga robo kila siku.

Bangladesh ina masikini waliopita mstari, kwa viwango vya serikali yao wenyewe, ambao ni karibu nusu ya idadi ya Watanzania wote.

Sasa huo ni uchumi wa kujivunia?

Unajua kwamba kwa makadirio ya mwaka 2021, GDP per capita figure zilikuwa hivi.

Bangladesh $ 2,458
Seychelles $14,653

Unajua Seychelles iko Afrika?

Unaelewa GDP per capita ni nini?

Unaelewa kwamba unaweza kuwa na uchumi mkubwa kwa kuzaliana watu wengi tu, huku wote mkiwa mnaishi kwenye umasikini mbaya sana? Halafu mtu anaweza kuwa na uchumi mdogo unaomfanya awe tajiri sana?

Unaweza kutofautisha ukubwa wa uchumi na ufanisi wa uchumi japo kwa ngazi ya awali tu kwa kutumia GDP per capita figures kuona on average watu wana kipato gani?
mkuu unataka kusema kwa uchumi wa mtu mojamoja Tanzania ina afadhali kuliko Bangladesh?

mbona hata tukiangalia hizo GDP per capita figures za tanzania na Bangladesh bado zinaonesha sisi ni maskini kuliko hao Bangladesh, sijaelewa hapo.
 
mkuu unataka kusema kwa uchumi wa mtu mojamoja Tanzania ina afadhali kuliko Bangladesh?

mbona hata tukiangalia hizo GDP per capita figures za tanzania na Bangladesh bado zinaonesha sisi ni maskini kuliko hao Bangladesh, sijaelewa hapo.
Sijajikita sana kulinganisha Bangladesh na Tanzania. Nimejikita kwenye heading ya kulinganisha Bangladesh na taifa lolote Afrika, na kuonesha uchumi mkubwa si lazima uwe uchumi mzuri, nchi inaweza kuwa na uchumi mkubwa kutokana na kuwa na watu masikini wengi.

Nimetoa uchumi wa Bangladesh kulinganisha na Seychelles kwa GDP per capita.

Main point, ukubwa wa uchumi si kipimo kizuri cha uzuri wa uchumi. Hata masikini wengi wakiwa pamoja wanatengeneza uchumi mkubwa na kugawana umasikini tu.

Tunavyoilinganisha Bangladesh na Afrika tuangalie angalau GDP per capita.

2021 figures.

Bangladesh $ 2458

Seychelles $ 14,653
Mauritius $ 9,106
South Africa $ 7,055
Botswana $6,805
Cape Verde $ 3,293
Ivory Coast $ 2,549

Kwa hivyo utaona licha ya Bangladesh kuwa na uchumi mkubwa , watu wa Bangladesh hawajaweza kufanya "uchumi" vizuri na kufaidika zaidi kutoka uchumi huo mkubwa kulinganisha na watu wa nchi nyingi za Afrika.

Kitu kingine unachobidi kuelewa ni kwamba, nchi inaweza kuwa na uchumi mkubwa, halafu huo uchumi mkubwa ukawa unachukuliwa na makampuni makubwa ya nje.

Hili ni tatizo kubwa Bangladesh. Tatizo linaloweza ku explain kwa nini Bangladesh on paper ina uchumi mkubwa sana, lakini maisha ya watu ni ya umasikini mkubwa.

Bangladesh wanatengeneza sana nguo na viatu. Kwa cheap labor. Sasa mauzo ya hivi viatu na nguo yanavyofanywa katika soko la dunia, hesabu zinaonesha hela nyingi zimeenda Bangladesh, wakati makampuni makubwa yana njia kemkem za kukwepa kodi na kuhakikisha hela zinabaki kwao, kama vile kununua malighafi na mitambo kutoka kwa international affiliates at inflated prices.

Hapo ndipo utaona nchi inaweza kuwa na uchumi mkubwa, halafu sehemu kubwa ya huo uchumi mkubwa inaenda nje, na wananchi wake wanabaki masikini tu.

Bangladesh na uchumi wake mkubwa imezidiwa mpaka na Ivory Coast (GDP per capita 2021) nchi ya Afrika ambayo imetoka kwenye vita muda si mrefu uliopita.
 
Mnashangaa nini wakati mada kama hizi hata watanzania hawawezi kuchangia na hiyo tu ni taswira tosha kwamba nchi ina watu wa namna gani.

Sasa nchi yenye watu kama hawa watawezaje kushindanishwa na Bangladesh ambayo watu wake hawakimbizi mwenge.
Wabongo lete mada ya ngono,wapo ma professor. Huko kwingine,usiwambie
 
Kwanini mnafuatilia vitu vinavyowajaza frustration..
!?
 
Kwanini mnafuatilia vitu vinavyowajaza frustration..
!?
Kwa sababu ni kwa kufuatilia vitu vinavyotujaza frustration tu ndivyo tunaweza kuondoa frustration.

Matatizo yakiwapo, hayamaliziki kwa sababu huyafuatilii.

Nyumba yako ikiwa inawaka moto, moto hauwezi kujizima wenyewe kwa sababu wewe huufuatilii.

Inakubidi ufuatilie matatizo, uyaelewe, ili uweze kuuyamaliza.
 
Kwa sababu ni kwa kufuatilia vitu vinavyotujaza frustration tu ndivyo tunaweza kuondoa frustration.

Matatizo yakiwapo, hayamaliziki kwa sababu huyafuatilii.

Nyumba yako ikiwa inawaka moto, moto hauwezi kujizima wenyewe kwa sababu wewe huufuatilii.

Inakubidi ufuatilie matatizo, uyaelewe, ili uweze kuuyamaliza.
Sawa.
Mungu akubariki.
 
Tatizo ni hizi dini kuu mbili. Uislam na ukristo. Dini hizi ni wakala wa utumwa na umaskini. Kama waafrika ikitokea tukaacha na hizo imani, tutapiga hatua kubwa kimaendeleo maana akili zetu zote zimefungiwa hapo.
Huko bangladesh kuna dini gani
 
Tatizo biashara huku hatutaki na pia tunawapiga vita wafanyabiashara wetu na pia jamii haziamini kwenye kufanya na kumiliki biashara ya kutatua matatizo yetu sie twapenda sana hiki kiatu kimetoka ujerumani basi ndio kizuri hatutaki tutengeneze cha kwetu hakuna uchumi imara wa kuimport kila kitu lazima to encourage na kuwezesha uwanzishwaji wa SME na MME ndio tutakuwa kiuchumi pia tupunguze kodi kwenye vifaa vya ujasiria mali na uzalishaji yaani vile vya kuweza kujiajiri sio pump ya kumwagilia shamba bei juu mashine za kukata na kukunjia chuma bei juu hatutaweza kunyanyua watu wetu kiuchumi na tunatakiwa taasisi zetu za biashara na binafsi zifanye biashara nje ya mipaka zilete foreign currency.
Ushamba ni mwingi bongo watu hawatake risk ya kufungua viwanda wao wanataka kwenda china kupiga picha basi wanaona wamepiga sana.

Ila nakuambia kuna vijana baadae hawa graduates jobless watakuja kupata idea ya kuunda viwanda vya nguo ,vyombo ,watafika mbali sana utajiri wa bongo ni dili za kusupply vitu kutoka nje kwa kufanya logistics..

Zile mashine za nguo zinauzwa china tena kibao ila hakuna mtu ananua ,kwanza wanaogopa operating costs ya viwanda wanataka mambo cheap sana ....Hii mitandao ndio ujinga kabisa mtu ili apost yupo Dubai, china , Marekani kufunga mzigo hapo ndio anaona ufahari.
 
Halafu kuna Wabangladesh zaidi ya 150 millions wanaishi nje ya Bangladesh...!

Ndo Nchi ambayo Kiongozi wa Nchi anaweza kusimama, na kuwaomba Raia waende nje ya Nchi wakatafute Maisha.

Kuna pengo kubwa mno la walionacho na wasionacho.
 
Alietuloga kwa kweli hana huruma. South Africa, Nigeria Egypt wote wamezidiwa na Bangladesh

Afrika tuna matatizo gani. Nchi 54 wote tumefeli. Hata hizo za kaskazini (Arab countries) wamefeli. Uchumi wa Morocco, Egypt, Algeria, Tunisia, Libya hauendani na uhalisia. Wote tumefeli vibaya mno.

Hakuna nchi yenye matumaini Africa. Nchi za Asia nyingi Zika juu Sana. Nyingi zitakuwa developed countries miaka michache ijayo

Je, ni kweli tunaibiwa rasilimali au tumefeli tu. Tatizo nini?

Ni kweli

Lakini ni nchi chafu, overpopulated na yenye masikini wengi sana
 
Watu mnashindwa kuendesha mradi wa Mwendokasi....-Magari tu..mtaweza kujenga viwanda..Afrika viongozi hawana maono
 
Back
Top Bottom