Nadhani ni hali ngumu ya maisha na uwezo mdogo wa kufikiri maana ilatela ukakasi sana yaani hata hospitali na maeneo mengine nyeti yamejaa mafremu, nadhani kama tungekuwa smart kama wenzetu huko walikoendelea tungewekeza kwenye nyumba nzuri za kuishi ingekuwa kitu cha msingi sana maana hali ya makazi yetu kwa ujumla ni duni sana lakini fremu kaliiiii, utakuta jamaa anakaa chumba kimoja mbavu za mbwa lakini salon anayofanya kazi nzuri kinoma kiasi kwamba akifika kazini kwake analala tu usingizi kwa jinsi palivyo bomba. Nadhani watu waelimishwe kujenga apartments nzuri za gharama nafuu inaweza kuwa suluhu ya TANZANIA YA FREMU aka tozonia