Uchumi wa mwanamke unapoimarika waweza hatarisha ndoa?

Unayosema yote hayo ni sawa.
Lakini ukiingia kwenye ndoa na ukaleta hayo mambo ndoa utabaki kuishangaa na kutoa milio.
na mwanamke ni mwepesi sana kuchoka huo usawa kwenye kuhudumia familia labda huko ulaya huku bongo utaishia kutukana ndoa
Si tumemsikia hata Zari the boss lady anavyoalalamika? Na Yule ana hela sasa sembuse hawa akina Ashura wa Mbagala Maji Matitu
 
Hii imebami kwenye theory Tu, uhalisia uko hivi the moment Mke wako anapokuzidi pesa Tu umekwishaaa
 
1. Kuhusu "Yeye ndiye kichwa, kwa hivyo lazima alipe 100%":

Huwezi kutumia sifa yake mwanaume kujenga himaya yako na kumwacha azame kwenye deni, kisha kudai anawajibika kwa kila kitu huku wewe ukiweka 100% ya faida. Hiyo si ndoa; hiyo ni ulaghai.


2. Kuhusu "Wewe si type yangu":

"Alikuwa 'type' yako alipokuwa akienda benki kusaini karatasi za mkopo kwa ajili ya biashara yako na ada ya shule ya watoto wako. Sasa kwa kuwa akaunti ya benki imejaa, 'type' yake ilibadilika ghafla?"


3. Kuhusu "Zawadi" dhidi ya Mtaji:

Mtaji unaotolewa kujenga biashara inayolisha familia ni uwekezaji katika ubia. Huwezi kuondoka na matunda huku ukimwacha.
 
Kama jamaa ana roho ngumu achukue ushauri wa Kibaharia. Kwakuwa pesa ya mke inatosha kulipa bills za familia na kusomesha machalii, basi mwamba anatakiwa akimbie familia akajipange na maisha yake kwanza.

Hii itamfanya jamaa ashughulike na kulipa madeni yote anayodaiwa na kipato cha ziada aweke akiba mpaka atakapomaliza deni. Kwa namna hii itamlazimu mwanamke kutumia kipato chake kuhudumia familia wakati mwamba anajipanga kujiinua upya kiuchumi.

Baada ya kukaa sawa jamaa, arudi apige tukio la kuhakikisha wanagawana hasara (kuvunja ndoa na kugawana mali) na asirudi nyuma tena zaidi ya kuangalia maisha yake na vifaranga vyake.
 
1 WAKORINTHO 13
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
 
Si tumemsikia hata Zari the boss lady anavyoalalamika? Na Yule ana hela sasa sembuse hawa akina Ashura wa Mbagala Maji Matitu
Yaani hawa wavulana wasipoelewa nature kwa mwanamke ikoje watateseka sana.
Mfano kuna minister mmoja kaolewa na wakili huwezi amini Jana tunaangalia yanga day mara paap kapiga simu!!!!!
Eeenh fulani unajua kama sabuni zimeisha???? halafu usisahau kupitia vitu si unajua watoto wanaenda shule lazima wale??!!!!! jamaa alikubali bila shida mama akaulizwa uko wapi akajibu alipo plus akaomba na hela atumiwe anunue wine jamaa akatuma 50.
Alikata simu tukamuuliza bibi wewe vp??? na uwaziri huo bili uliyotumia hapa kubwa inazidi hata ulivyoomba?????
Tukajibiwa nyie si mnalea hao wanaume!!!!,,, cheo changu hakihusiani na ndoa yangu mimi kupata cheo sio sababu ya kuacha kuhudumiwa natoa hela nikijisikia.
 
Typical 100% women behaviour. Huu ni ukweli ambao Wanaume Lialia hawataki kuukubali wanaishia kutukana Tu.

Wanawake hawana shida Sisi Wanaume ndio tunashida kutokuwaelewa.
Kwa sababu hiyo, Mimi wake zangu wapo kwa hili ya kunihudumia na domestic responsibilities, hela Natafuta mwenyewe Maana hata akizitafuta kwangu Hazina faida. I have always to remain as a King, sio unataka umwami na majukumu hutaki kufanya🤣🤣
 
Mumeo ana hasara
Mwanamke asiyekuhurumia hafai hata kidogo kukaa naye

Na uzuri red flag hua zipo mwanzoni ila tunachagua kuvumilia matokeo yake ndoa inabaki ni jela ambayo huwezi kutoka
 
Mumeo ana hasara
Mwanamke asiyekuhurumia hafai hata kidogo kukaa naye

Na uzuri red flag hua zipo mwanzoni ila tunachagua kuvumilia matokeo yake ndoa inabaki ni jela ambayo huwezi kutoka
Na kama ulijichanganya ndio hutoki tena Maana kila ukitaka kufanya maamuzi unaona hasara ni kubwa kuliko faida, unaamua kuugulia ndani kwa ndani, hujafikisha hata miaka 55 unakufa🤣🤣
 
Kabisa na huu ukweli ukieleweka ndoa zitasimama imara.
 
Mwanamke anapokuwa na kipato, anapata uhuru zaidi wa kufanya maamuzi na kuvumilia mambo machache yasiyofaa. Lakini kama kuna upendo, heshima na maelewano, kipato chake kinaweza kuimarisha ndoa badala ya kuiharibu.
 
Wanawake wabinafsi sana
 
Rafiki yangu alioa mwaka 2022 mwezi wa6,mke alikuwa hana kazi akamtupia mtaji wa kueleweka biashara ikazaa maradufu.
Mume alikuwa mwajiriwa so alikuwa na mikopo kadhaa katika hali ya kujiendeleza ikiwa ni pamoja na mkopo wa ujenzi na aliomfungulia mkewe biashara.
Mara ghafla wife kabadilika , mara hoo wife hamskilizi mume, mara ooh utaniambia nini?
Ukishajua kuwa tabia ya mkeo ipo hivyo, na kwamba uchumi wake binafsi ukikuwa atakutosa usimpe mtaji wala kumfungulia biashara ya maana. Mfungulie mishe ndogo ndogo kama ufugaji kuku au ng'ombe kadhaa wa maziwa.

Kama biashara ni kubwa iwe yako, ajiri wafanyakazi huyo mke awe mmoja wa waajiriwa wako unaowalipa mishahara, asiwe mmiliki.

Ni upuuzi ukope mkopo mkubwa umpe, biashara yake istawi, anakuzidi kipato, halafu uwe unapambana na marejesho mwenyewe huku ukihudumia familia 100%.. Utumwa mwingine ni wa kujitakia
 
Mumeo ana hasara
Mwanamke asiyekuhurumia hafai hata kidogo kukaa naye

Na uzuri red flag hua zipo mwanzoni ila tunachagua kuvumilia matokeo yake ndoa inabaki ni jela ambayo huwezi kutoka

Mume wangu hana hasara hiyo.
Nimeolewa na mwanaume na si mvulana........
Mwanaume anayetimiza majukumu yake ya kiume na mimi niko kutimiza majukumu yangu kama mke katika ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…