Uchungu wa Polepole kuhusu Haki, Demokrasia na Utawala bora unatoka wapi?

Hivi karibuni ndugu Polepole baada ya kujiuzuru ubalozi ame-trend sana na kujipatia maujiko (umaarufu) kuwa ni mpigania haki, demokrasia na utawala Bora.

Swali la kujiuliza ni kweli Polepole ana uchungu na mpigania haki, demokrasia na utawala Bora???.

Hebu tujiulize maswali mengine haya tena.
1. Tundu Lissu alipopigwa risasi akipigania haki, Demokrasia na utawala Bora, ndugu Polepole aliwahi kumpa pole Lissu au hata kwenda kumsalimia akiwa hospitali kama ishara ya kumuunga mkono ??

2. Polepole akiwa kama mwenezi wa CCM mwaka 2017 wakati Tundu Lissu alipopigwa risasi, aliwahi kulaani kitendo hicho cha kinyama??? kuonyesha kuwa anakerwa na uvunjifu wa wazi wa haki, demokrasia na utawala Bora.

3. Wakati wa utawala wa kikatiri wa mwendazake, ambao haukuzingatia haki, demokrasia na utawala Bora, huku yeye Polepole akiwa mwenezi wa CCM, mbona hakuwahi kupinga au kulaani utawala ule wa kidikteta na mabavu uliokuwa unavunja haki, demokrasia na utawala Bora ????

4. Wakati wa utawala wa mwendazake mambo ya utekaji, kutesa na kuwaua watu ulishamiri, huku Polepole akiwa Mwenezi, mbona hatujasikia anayakemea kwa nguvu matendo hayo maovu ya kikatiri na kishenzi????. Na hata yalipoendelezwa na utawala wa sasa hadi yakazidi vipimo mbona alikuwa kimya siku zote hatukusikia kuyakemea???

5. Baadhi ya Mbuga za wanyama wamepewa waarabu, bandari kubwa wakapewa waarabu, mapori wakapewa waarabu, viwanja vya ndege wakapewa waarabu. Mbona hatujasikia polepole anapinga mambo haya ya hovyo na ya kuiangamiza taifa.???

6. N.k

Tuendelee kujiuliza maswali ni kweli Polepole ni mzalendo na mwenye uchungu wa nchi yake kama anavyojaribu kujinasibu????

Wakati tunaendelea kujiuliza maswali mengi haya haina maana kwamba mtawala wa sasa anafuata misingi ya haki, demokrasia na utawala Bora, bali yeye kamzidi hata mtangulizi wake kwa mambo ya hovyo tunayoyahoji. Pengine ni kwa sababu alikuwa ni sehemu ya uasisi wa matendo hayo maovu labda ndo sasa anaya-practice vizuri zaidi.
Polepole ameokoka , mwache Mtumishi wa Mungu
 
Ila yeye hajasema hayo, ndiyo maana sisi tunashangaa. Kwamba mmoja wa waasisi wa mbinu ya utekaji, kuua na kusingizia watu makesii ya kipuuzi, leo hii analalamikia genge lake.

Akikiri mbele ya umma tutamsamehe.
 
Hivi mtu anakatazwa kujirudi?
 
Mimi naona ni vita vyake na uraisi wa Samia tu. Haoneshi hata chembe ya kujuta kwa yaliyofanyika wakati akiwa sehemu ya watawala.
 
Ila yeye hajasema hayo, ndiyo maana sisi tunashangaa. Kwamba mmoja wa waasisi wa mbinu ya utekaji, kuua na kusingizia watu makesii ya kipuuzi, leo hii analalamikia genge lake.

Akikiri mbele ya umma tutamsamehe.
Hilo la yeye kuasisi mbinu za utekaji na kuua una ushahidi nayo??
 
Hana sifa,kwanza ajisafishe kwa brashi ya chuma,kwa magadi soda.
Pili akae nje ya siasa kwa miaka isiopungua mitano.
Ni kweli hatujaona akijisafisha uchafu wake. Tunachoshuhudia ni kupambania fursa ya madaraka, yeye na genge lake la mwendazake regime.

Sisi tunataka mtu anayechukizwa na utekaji, utesaji, mauaji na ubambikaji kesi za kishenzi dhidi ya watu wanaokosoa serikali.
 
Hilo la yeye kuasisi mbinu za utekaji na kuua una ushahidi nayo??
Yes. Regime ya mwendazake na yeye Polepole akiwa msemaji wa mwendazake ndo waliasisi utekaji, mauaji na utekaji wa watu waliokuwa wanakosoa serikali yake.

Makamu wa mwezandake huwezi kumtenganisha na huo uchafu. Ilikuwa team moja.
 
Mimi naona ni vita vyake na uraisi wa Samia tu. Haoneshi hata chembe ya kujuta kwa yaliyofanyika wakati akiwa sehemu ya watawala.
Polepole anafikiri watanzania ni wajinga na kwamba ni wasahaurifu.
 
Back
Top Bottom