Uchungu wa Polepole kuhusu Haki, Demokrasia na Utawala bora unatoka wapi?

Uchungu wa Polepole kuhusu Haki, Demokrasia na Utawala bora unatoka wapi?

MOVIE KALI
0A093231-ABB5-45E2-B65A-0E87C55E13AF.jpeg
 
Hivi karibuni ndugu Polepole baada ya kujiuzuru ubalozi ame-trend sana na kujipatia maujiko (umaarufu) kuwa ni mpigania haki, demokrasia na utawala Bora.

Swali la kujiuliza ni kweli Polepole ana uchungu na mpigania haki, demokrasia na utawala Bora???.

Hebu tujiulize maswali mengine haya tena.
1. Tundu Lissu alipopigwa risasi akipigania haki, Demokrasia na utawala Bora, ndugu Polepole aliwahi kumpa pole Lissu au hata kwenda kumsalimia akiwa hospitali kama ishara ya kumuunga mkono ??

2. Polepole akiwa kama mwenezi wa CCM mwaka 2017 wakati Tundu Lissu alipopigwa risasi, aliwahi kulaani kitendo hicho cha kinyama??? kuonyesha kuwa anakerwa na uvunjifu wa wazi wa haki, demokrasia na utawala Bora.

3. Wakati wa utawala wa kikatiri wa mwendazake, ambao haukuzingatia haki, demokrasia na utawala Bora, huku yeye Polepole akiwa mwenezi wa CCM, mbona hakuwahi kupinga au kulaani utawala ule wa kidikteta na mabavu uliokuwa unavunja haki, demokrasia na utawala Bora ????

4. Wakati wa utawala wa mwendazake mambo ya utekaji, kutesa na kuwaua watu ulishamiri, huku Polepole akiwa Mwenezi, mbona hatujasikia anayakemea kwa nguvu matendo hayo maovu ya kikatiri na kishenzi????. Na hata yalipoendelezwa na utawala wa sasa hadi yakazidi vipimo mbona alikuwa kimya siku zote hatukusikia kuyakemea???

5. Baadhi ya Mbuga za wanyama wamepewa waarabu, bandari kubwa wakapewa waarabu, mapori wakapewa waarabu, viwanja vya ndege wakapewa waarabu. Mbona hatujasikia polepole anapinga mambo haya ya hovyo na ya kuiangamiza taifa.???

6. N.k

Tuendelee kujiuliza maswali ni kweli Polepole ni mzalendo na mwenye uchungu wa nchi yake kama anavyojaribu kujinasibu????

Wakati tunaendelea kujiuliza maswali mengi haya haina maana kwamba mtawala wa sasa anafuata misingi ya haki, demokrasia na utawala Bora, bali yeye kamzidi hata mtangulizi wake kwa mambo ya hovyo tunayoyahoji. Pengine ni kwa sababu alikuwa ni sehemu ya uasisi wa matendo hayo maovu labda ndo sasa anaya-practice vizuri zaidi.
Kwanza mkuu tuweke record sawa


Slowly haongei kwa kulinganisha utawala... anachozungumzia ni mfumo ambao upo unavyo jaribu kubagaza taswira ya katiba ya C e o na mfumo wake... anachofanya ni kile kitu kinasemwa kumwaga oil! Gari limesafr mda mrefu sana linahitaji mabadiliko kwenye mwonekano wa washirika wake haseme kwa kulinganisha utawala na mm kimsingi kwa upande huo nakubaliana nae kujisahihisha ni jambo Zuri na lenye siha ndani yake..

Kama unataka tulinganishe inabidi sasa tuje kuona mazur ya the late na present ceO.. tuyachambua mabaya yap pia.. ndo tuje uhalali wa mifumo si mtu....
 
Kwanza mkuu tuweke record sawa


Slowly haongei kwa kulinganisha utawala... anachozungumzia ni mfumo ambao upo unavyo jaribu kubagaza taswira ya katiba ya C e o na mfumo wake... anachofanya ni kile kitu kinasemwa kumwaga oil! Gari limesafr mda mrefu sana linahitaji mabadiliko kwenye mwonekano wa washirika wake haseme kwa kulinganisha utawala na mm kimsingi kwa upande huo nakubaliana nae kujisahihisha ni jambo Zuri na lenye siha ndani yake..

Kama unataka tulinganishe inabidi sasa tuje kuona mazur ya the late na present ceO.. tuyachambua mabaya yap pia.. ndo tuje uhalali wa mifumo si mtu....
Uko sahihi. Tunachosema Polepole anatakiwa kuanika mabaya na kwa sasa kazi hiyo kaanza kuifanya. Press ya kwanza hakufunguka vizuri. Press ya pili na tatu naanza kumwelewa maana anafunguka vizuri. Tumuunge mkono.
 
Sawa hatukatai lkn saivi kakataa sasa we ulikuwa unatakaje kwahiyo ukinya bahati mby kitandan utaendelea kunya kisa Jana ulikunya dah asee sijui tulirogwq na nan tz
Kitu gani kipya ambacho Polepole anakisema ambacho tulikuwa hatuzijui??
 
Hii ni ujinga wa hali ya juu. Kujaribu kuhalalisha makosa ya sasa kwa sababu anayekosoa hakufanya hivyo kipindi kilichopita. Asilimia 90 ya viongozi wa sasa walikuwepo wakati wa Magufuli, mbona hawakuhoji? Samia alikuwa namba mbili, na kila kitu kinamangukia. Kuna viongozi wa dini na watanzania wengi tu hawakuhoji... huoni kuwa mmoja akiona enough is enough ni jambo zuri?
Hoja yetu ni kwamba Polepole hana jipya mbele ya umma.

Ni wale wale, wanagombania keki. Watanzania wanataka kusikia watu wanakemea utekaji, mauaji na kutesa watu. Si hivo tu, wanataka yakomeshwe. Sasa Polepole umemsikia anakemea hayo????
 
Sawa hatukatai lkn saivi kakataa sasa we ulikuwa unatakaje kwahiyo ukinya bahati mby kitandan utaendelea kunya kisa Jana ulikunya dah asee sijui tulirogwq na nan tz
Jibu hoja. Kama hujaielewa sema tukufafanulie
 
Sasa ni wakati wa kuongea
Mbona anaongea kwa kuogopa ogope mara sijui kiapo mara maadili ya viongozi. Si angenyamaza tu.

Watanzania hawataki wauaji, watekaji, na watesaji wa watu.
 
KWAHIYO UNATAKA WATU WAENDELEE KUTEKWA? OK, AU TUPE LIST YA WATU WANAOTAKIWA KUKEMEA UTEKAJI, TUPE LIST
Wewe umeona Polepole amekemea mauaji, watu kutekwa na maovu mengine?????
 
Shetani akibadilika kuwa malaika tunaungana naye kumpiga adui yetu.
CHADEMA hamna tofauti na wafuasi wa Dikteta Charles Taylor waliotahadharishwa kuhusu kumchagua dikteta ila wakajibu "Aliua baba yangu, aliua mama yangu ila nitamchagua".... iko wazi kuwa Polepole ni mhusika muhimu kwenye utawala wa kikatili wa awamu ya 5 huku CHADEMA mkiwa wahanga wakuu lakini mmeamua kupuuza. Mmesahau viongozi wenu walivyohukumiwa vifungo kwenye kesi ya Akwilina?
 
Ndiyo mana imeshaasisiwa na akina polepole ikawa ni mtindo wa maisha
Sijui anataka tumpongeze moja ya waasisi wa utekaji, na mauaji ya wakosoaji wa serikali.
 
Back
Top Bottom