Uchunguzi: Jinsi watu wanavyoporwa mali zao baada ya mechi kumalizika Uwanja wa Taifa, huku Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikitumbua macho

Tatizo polisi wa maeneo yale wanaogop hilo kundi ni kubwa sana wakikamata au kujeruhi mwenzao hao polisi wenyewe kwenye kota zao wataonabcha mtema kuni au polisi yeyote akija pita anga zao wanamaliza wale wameshakubuhu polisi hawawaambii kitu.
Hao hao vibaka maeneo ya kota kule hawagusi walishaambiw kabisa fanyeni hukoooo hapa kama mnataka kukaa siku haribuni.
Basi wanalindana kwa style hiyo
Ni aibu sana kwa jeshi la Polisi kuwa na askari wanaowaogopa vibaka duni kama hawa wa keko , RPC wa Temeke ajiuzulu
 
" Nitasema Kweli daima fitna kwangu mwiko "

Zikiwa zimesalia dk 30 mpira kumalizika vijana wezi , vibaka na majambazi kutoka Keko Magurumbasi , Keko Mwanga , Keko torori , keko machungwa na baadhi kutoka Chang'ombe husogea karibu na uwanja wa Taifa , wengi hujikusanya kwenye njia panda ya Taifa kwenye maghorofa ya jeshi karibu kabisa na ofisi za Takukuru Wilaya ya Temeke , wakiwa na visu , bisibisi na mapanga , hii haijalishi kama itakuwa jioni ama usiku ( japo kwa usiku hali huwa mbaya zaidi )

Eneo hili limezungukwa na maghorofa ya Jwtz pande zote , na kwa kiasi kuna maghorofa ya NHC , hatua chache kutoka hapo ni Shule ya msingi Mgulani na kambi kubwa ya Jeshi la polisi inayoanzia Kilwa road , eneo hili pia linapakana na chuo kikuu cha DUCE na kambi kubwa sana ya JKT ambako ndio kuna shule ya Sekondari ya Jitegemee , hili si eneo la vibaka wajinga wa kutoka keko kutamba , lakini kwa sasa hali ni kinyume chake , vibaka wanatamba bila wasiwasi wowote ule .

Baada ya mechi kumalizika mtu yeyote mwenye kitu chochote cha thamani iwe pochi , simu , saa au hata cheni akifika eneo hili huporwa , mara kadhaa magari huvunjwa vioo na watu huporwa mali zao huku waporaji wakikimbia kuelekea Keko machungwa kwa kupita katikati ya maghorofa ya jeshi huku wanajeshi na familia zao wakiangalia kwa macho bila kutoa msaada wowote , waporaji na vibaka hawa wakishapora na kujeruhi hupita pia katikati ya Bar ya Inferno na kukimbilia bondeni kupitia Gesti ya Lyimo na kwenda kujificha uwanja wa mpira wa Keko Juu ambao ni mali ya ccm na ambao uko karibu na kota za polisi za Mchomba line , haya yanatendwa huku vyombo vyote vya dola vikiangalia kwa macho bila kuchukua hatua zozote , tena kwa miaka mingi , njia zote wanazopita vibaka hawa polisi wanazifahamu vizuri lakini hawachukui hatua zozote , Askari au mwanajeshi anayeweza kupinga hoja yangu hii ajitokeze hadharani , yanayotendwa na vibaka hawa mbele ya maeneo ya jeshi ni aibu kwa Polisi Mkoa wa Temeke ambao wengi wanajazana Uwanjani wa Taifa ili kutafuta rushwa ya kujikimu na kuwaacha raia wakiumia bila sababu mitaani .

Natoa wito kwa wote wanaoenda Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya Simba na Yanga na kufikiria kurudi kwa kupitia njia hii basi WAJILINDE WENYEWE , tena wajihami kwa silaha nzito wakiweza , lakini kama wakitegemea ulinzi wa jeshi la polisi wasije wakalia na kusaga meno.

Uchunguzi wetu huu ni endelevu na utaendelea tena kwa kuangalia usalama wa washabiki wa soka wanaopitia Mandela road , wanaoelekea Mtoni kupitia Uhasibu na wale wanaoelekea Temeke kupitia Wailes .

Naomba kuwasilisha
Ungesema Chadema wanakusanyika angalau polisi wangejua pakuanzia lakini vibaka hawadhuru kura.
 
Hata hivyo mpira ni uwakala wa shetani acha shetani akishirikiana na serikali ya kishetani waendeleze hujuma kwa hawa wanadamu wasiojua mpira Mungu kaukataa
Simu yenyewe unayotumia ni Wakala wa Shetani pia.
 
Ishu ni kuwa hao vibaka wnakuja kuwafanyizia ubaya huko kota kwao yaani wanaiba chochote watakachokuta nje sasa hao askari nao huwa wanawalinda kishkaji ili vibaka hao wasiwaharibie ishu ni kuwa askari akikamata au kuwachomea hao vibaka wa maeneo hayo hao hao vibaka wanaletaka venzao wa mbali na kuja kuwaibia au kuwafanyia chochote ambacho askari anapata hasara
Ni aibu sana kwa jeshi la Polisi kuwa na askari wanaowaogopa vibaka duni kama hawa wa keko , RPC wa Temeke ajiuzulu
 
Hata hivyo mpira ni uwakala wa shetani acha shetani akishirikiana na serikali ya kishetani waendeleze hujuma kwa hawa wanadamu wasiojua mpira Mungu kaukataa
Nakubaliana na wewe kuwa mpira unaweza kuwa ni uwakala wa shetani endapo:
1. utaleta hasira: na hii ipo sana kama timu pendwa imefungwa.
2. utaleta chuki: endapo refa katoa penalty iliyoonekana sio halali.
na mengine kama husda, lugha mbaya za matusi n.k. hivyo ni vyema wapenzi wa mpira wasiruhusu kutawaliwa na hivyo vitu, kwani mtakuwa mnamtumikia shetani, au kama huwezi kuviacha, basi wachana na mpira kabisa. Mungu hataki tutawaliwe na vya duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu mmoja kaporwa simu 3 na kupigwa visu zadi ya kumi , tunaendelea kufuatilia
 
" Nitasema Kweli daima fitna kwangu mwiko "

Zikiwa zimesalia dk 30 mpira kumalizika vijana wezi , vibaka na majambazi kutoka Keko Magurumbasi , Keko Mwanga , Keko torori , keko machungwa na baadhi kutoka Chang'ombe husogea karibu na uwanja wa Taifa , wengi hujikusanya kwenye njia panda ya Taifa kwenye maghorofa ya jeshi karibu kabisa na ofisi za Takukuru Wilaya ya Temeke , wakiwa na visu , bisibisi na mapanga , hii haijalishi kama itakuwa jioni ama usiku ( japo kwa usiku hali huwa mbaya zaidi )

Eneo hili limezungukwa na maghorofa ya Jwtz pande zote , na kwa kiasi kuna maghorofa ya NHC , hatua chache kutoka hapo ni Shule ya msingi Mgulani na kambi kubwa ya Jeshi la polisi inayoanzia Kilwa road , eneo hili pia linapakana na chuo kikuu cha DUCE na kambi kubwa sana ya JKT ambako ndio kuna shule ya Sekondari ya Jitegemee , hili si eneo la vibaka wajinga wa kutoka keko kutamba , lakini kwa sasa hali ni kinyume chake , vibaka wanatamba bila wasiwasi wowote ule .

Baada ya mechi kumalizika mtu yeyote mwenye kitu chochote cha thamani iwe pochi , simu , saa au hata cheni akifika eneo hili huporwa , mara kadhaa magari huvunjwa vioo na watu huporwa mali zao huku waporaji wakikimbia kuelekea Keko machungwa kwa kupita katikati ya maghorofa ya jeshi huku wanajeshi na familia zao wakiangalia kwa macho bila kutoa msaada wowote , waporaji na vibaka hawa wakishapora na kujeruhi hupita pia katikati ya Bar ya Inferno na kukimbilia bondeni kupitia Gesti ya Lyimo na kwenda kujificha uwanja wa mpira wa Keko Juu ambao ni mali ya ccm na ambao uko karibu na kota za polisi za Mchomba line , haya yanatendwa huku vyombo vyote vya dola vikiangalia kwa macho bila kuchukua hatua zozote , tena kwa miaka mingi , njia zote wanazopita vibaka hawa polisi wanazifahamu vizuri lakini hawachukui hatua zozote , Askari au mwanajeshi anayeweza kupinga hoja yangu hii ajitokeze hadharani , yanayotendwa na vibaka hawa mbele ya maeneo ya jeshi ni aibu kwa Polisi Mkoa wa Temeke ambao wengi wanajazana Uwanjani wa Taifa ili kutafuta rushwa ya kujikimu na kuwaacha raia wakiumia bila sababu mitaani .

Natoa wito kwa wote wanaoenda Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya Simba na Yanga na kufikiria kurudi kwa kupitia njia hii basi WAJILINDE WENYEWE , tena wajihami kwa silaha nzito wakiweza , lakini kama wakitegemea ulinzi wa jeshi la polisi wasije wakalia na kusaga meno.

Uchunguzi wetu huu ni endelevu na utaendelea tena kwa kuangalia usalama wa washabiki wa soka wanaopitia Mandela road , wanaoelekea Mtoni kupitia Uhasibu na wale wanaoelekea Temeke kupitia Wailes .

Naomba kuwasilisha
Maeneo hayo nikawaida sana na kila siku polisi wanaambiwa,mpaka siku afe mtu ndiyo hatua zitachukuliwa
 
Back
Top Bottom