Uchunguzi: Ngono zembe inaharibu bahati na future

Uchunguzi: Ngono zembe inaharibu bahati na future

Duh huu mkuku

DU

Duh huu mkuki rohoni, aisee hii kitu ndo inaponza maisha yangu tangu nianze chuo hadi nimemaliza nimeshikwa na addiction ya dada poa, na hii tabia niliianzia chuo, addiction hii inakwendana na alcohol consumption, yaani nikishaonja tu alcohol lazima akili iende kwa dada poa, na nina experience ya kutembea na dada poa kwa miaka 6 , kitu kinachopelekea kutopata kazi wala deals za maana tofauti na wenzangu tuliokuwa tukiishi ghetto moja chuo, wenzangu hadi sa hivi wameajiriwa ila mimi , ilikuwa bado kidogo kupata ajira ila sijui nn kilitokea baada ya kuitwa interview nakupita zote, nilichokuja kugundua dada poa/ malaya wengi wana mikosi kutokana na nafsi zao kubeba nafsi nyingi ambazo baadhi ni chafu na safi pia, na wengi wanaenda kwa waganga wanapewa dawa za kunasa wateja / kugandwa na wateja, yaani ukimla tu siku moja lazima kila ukienda ilo eneo ile dawa yake inakuvuta umtafute yeye tu , yaani ata malaya awe ana sura mbaya lazima umfate yeye tu, na unapotembea naye nyota yako inachafuka maama tendo la ndoa uunganisha nafsi,na ukitembea nao wengi nafsi yako inakuwa haitulii na unaweza kujikuta unaoa malaya kwa sababu ya nafsi , na kuna malaya wengine wana nafsi za bahati , kuna kipindi nipo chuo kuna malaya nilikuwa nikilala naye tu nashangaa kesho yake nikienda chuo, mademu wananichangamkia kinoma hadi nikawa nashangaa iki ni nn? Ila nina experience kubwa sana na malaya na mambo yao ya nafsi, na vitu vingi vimenitokea kwa kutembea nao vingi vibaya kama kutumia kiasi kikubwa cha pesa, na iyo addiction nimeshindwa kuiacha kabisa , kila nikijaribu siwezi kabisa, yaani najiskia raha kutembea na malaya kuliko msichana wa kawaida,ila najitahidi niondokane nayo naamini iko siku itakwisha,
Mkuu, tatizo lako limewahi kunikumba mimi, nilijiingiza huko sikupata kazi miaka 10, ila niliweza kujitoa kwenye vifungo vya nafsi kwa maombi
 
Anaandika, Robert Heriel,
Kuhani katika Hekalu Jeusi.

Ukitaka bahati yako na mkondo wako wa pesa uanze kuyumba basi itakupasa uanze uzinzi au uasherati. Yaani hiyo ndiyo mbinu namba moja kabambe ya kujitia matatizoni.

Nafsi ya mtu huchafuliwa na uzinzi, yaani ili mtu awe mchafu basi itampasa awe mzinzi.
Uzinzi siyo tuu ni hatari kwa magonjwa hatari ya zinaa, bali pia ni hatari kwa magonjwa ya kuondoa kinga za kiroho.

Kikawaida binadamu akishaanza kufanya uzinzi ataanza kupoteza uwezo wake wa asili. Moja ya uwezo wa asili wa binadamu ni kuota ndoto zenye mantiki nyakati za usiku.

Binadamu kabla hajaanza ngono huota ndoto na anakuwa na uwezo wa kuzikumbuka kama siyo kuzitafsiri kabisa. Lakini akishaanza uzinzi ndoto hizo huanza kupungua na kupotea kabisa.

Huwezi ukawa mzinzi alafu ukaomba bahati au misaada ya kiroho kivyovyote vile. Hapo itakupasa ujitakase walau kwa siku zisizopungua tano ili uwe safi, kisha ndiyo ufanye mawasiliano na falme za rohoni.

Hata ukienda kwa waganga wa kienyeji kuna dawa ambazo ukipewa utaambiwa usikutane na mwanamke kwa siku kadhaa ili dawa zifanye kazi.

Au utaambiwa utembee na binti mdogo tena ikiwezekana ambaye ni bikra. Hapo ndipo kesi nyingi za ubakaji kwa watoto wadogo hujitokeza.

Vijana mnaoanza biashara, hasa hizi biashara za mitaji midogo chin ya milioni tano. Ukitaka biashara yako iende bila shida basi cha kwanza itakupasa ukae mbali na wanawake, acha ngono zembe.

Kama utashindwa ni akheri uoe kabisa, tena uoe mwanamke msafi mwenye maadili. Siyo uoe tena limalaya ambao litakuwa linafanya zinaa huko na kukuletea wewe mikosi.

Tunaposema mwanamke malaya au muasherati hafai kwa ndoa, na ikiwezekana kama umemuoa ukamfumania, basi itakupasa usijiulize mara mbilimbili, fukuza! Siyo kwa sababu tuu ya wivu wa kimapenzi. No! Bali ni pamoja na mambo ya kimaendeleo.

Hakuna familia zenye kufanya umalaya zikaendelea. Umalaya na umasikini vinapelekana bega kwa bega.

Mwanamke aliyefanya uzinzi au ngono anakuwa mchafu Kwa siku 14 wakati mwanaume anakuwa mchafu kwa siku 7.

Kama unamchongo unaousikilizia basi itakupasa ukae mbali na ngono zembe mpaka utiki. Lakini kama utajiingiza huko siyo ajabu pesa zako zikawa zinakuja lakini kila zikikaribia kuingia zinapeperuka. Yaani ni kama unanyang'anywa tonge mdomoni.

Umalaya ndiyo dhambi pekee ambayo mtu anaufanyia mwili wake. Dhambi zingine mtu hufanya nje ya mwili wake, yaani huwafanyia wengine. Ndiyo dhambi inayodhuru mwili na roho kwa haraka sana.

Ngono zinavuta mikosi, yaani unaweza pata pesa sasa hivi alafu hapohapo likatokea tatizo la kuitumia pesa uliyoipata nje ya mipango yako.

Namna pekee ambayo wazinzi wanaweza kuwa na bahati katika mambo yao ni kujiingiza kwenye ushirikina na ulozi. Ambapo itawapasa wagharamike kwa namna moja ama nyingine kusafisha nyota zao kwa kipindi cha muda fulani, huku wakiendelea na uchafu wao.

Sio rahisi umuone mtu anafanya uzinzi halafu mambo yake yanaenda bila ya kuwa mshirikina. Hiyo haiwezekaniki.

Biashara inahitaji usafi siyo tuu wa kimwili, bali pia usafi wa kiroho (mvuto) na kitu pekee kinachochafua mvuto wa kiroho ni zinaa.

Huwezi kuwa mzinzi halafu ukaenda kwenye project zako, mfano unamashamba ya mpunga au nyanya halafu uende ukiwa unafanya uchafu, lazima mambo yaharibike, au ufugaji. Kila kitu kina siri zake, aidha utumie madawa ya jadi ndiyo ufanikiwe lakini kumuomba Mungu asaidie miradi yao ilhali roho yako imechafuka huo ni uongo.

Kuna baadhi ya watu wanatabia ya kuingiza wanawake au malaya kwenye nyumba zao wanazoishi, ndugu zangu hivi kama umekosa akili kwa kiwango hicho, umeona haitoshi ulete wanawake waitie mikosi nyumba yako. Unafikiri guest house zilijengwa kwaajili gani.

Kama utashindwa kabisa ni bora mkafanyie kwenye vichaka, huko mbona fresh tuu kuliko kuingiza uchafu nyumbani kwako. Huo ni ukosefu wa maarifa.

Vijana kama unahitaji njia yako isiwe ngumu sana, yaani pesa zako zisije kwa mbinde basi unashauriwa acha ngono zembe. Na uliyenaye awe mwaminifu, na kamwe mtu asiyemwaminifu usijisumbue kumfundisha uaminifu au kumbembeleza, unabembeleza mtu anayeharibu mifumo ya maisha yako.

Usiponielewa, utanielewa katika mambo unayoyafanya, yaani kila ukifanyacho hakiendi, unafeli. Wakati wenzako chochote tunachogusa kitaenda kitake kisitake.

Ni yule kuhani

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
Uko sahihi sana mkuu...
 
Does this only apply to africans? Mbona wazungu wanazini sana na uasherati kuoitiliza na bado wao ndio wenye mihela hapa duniani? Mwengine juzi juzi tuu hapa kawa mfalme pamoja na roho mbaya ya mama yake lakini wapi, jamaa kaula.
Kuwa na hela nyingi sio baraka mkuu,unajua anayoyapitia pamoja na kuwa na hizo hela nyingi?unaweza kukuta halali usiku,utajuaje,unaweza kukuta maelewano ndani ya nyumba na mkewe ni sifuri kila mtu analala chumba chake,hawali pamoja,huyu akija sitting room mwingine anaondoka utajuaje,watoto wanaugua kila kukicha utajuaje,watoto wanakuwa walevi wafujaji wa pesa hawataki kusoma,wanageukia ushoga au usagaji utajuaje?wewe unabaki tu huku nje unaangalia kiwango cha pesa alichonacho ambacho hakimletei muhusika amani bali huzuni na mikosi...
 
Yaweza kuwa kwel ..yaweza kuwa uongooo.
Nishakuga sana muaminifuuu bila zinaaa na nishakua pia mzinzi ila SIJAWAHI KUONA TOFAUTI YA MAISHA YANGU. Hustle ni zile zile tuuu.

Zinaa yaweza punguza nguvu ya mtu kiroho yes i agree but sio guarantee ya kumfanya mtu asifanikiwe...i completelly object. Inategemeana tu na vile una mtazamo gani maana AONAVYO MTU NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO..

Ukiamin ngono inaleta mikosi sawaa, mikosi haitaacha kukuandama..

Ukiamini ngoni ni hitaji tu la kimwili la kiumbe kama mwanadamu kama vile kula na kunywa bas itakua hivyo kwako..maana KWA IMANI MTU HUAMINI HATA KUPATA.......

NA IMANI CHANZO CHAKE KUSIKIA.....
unasikia nini au una amini nini THAT IS UP TO YOU.

Ila kisicho kataliwa ni kwamba zinaa inakuweka kwenye risk kama magonjwa na matumizi makubwa ya kipato nje ya utaratibu pindi unaposhindwa kuwa makini..

Huu ni mtazamo wangu binafsi na it is working fine for me. Sijataka kuleta mifano ya "mbona huyu hivi, mbuyu yule vile"

Tumepew akili tuzitumie
Nakazia,na tukitoka kwenye papuchi tunaoga na magadi Ku neutralize
 
Does this only apply to africans? Mbona wazungu wanazini sana na uasherati kuoitiliza na bado wao ndio wenye mihela hapa duniani? Mwengine juzi juzi tuu hapa kawa mfalme pamoja na roho mbaya ya mama yake lakini wapi, jamaa kaula.

Nakazia; WAAFRICA TUNAJILAANI WENYEWE

kuna vitu vingi sana havina uhalisia ila tunalazimisha tu et ukifanya hivi yatakukuta hayaa na yanatukuta kweli kutokana na kupelekea kuamini hivyoo ila ukweli ni kwamba sio hivyo tunavyoamini

Unaona hapo ulaya/ng’ambo kuna vitoto vijana vina miaka 17-19 vinacheza mpira ligi tofauti tofauti vina mafanikio kinyama na havijaoa wala nini? Vina wachumba tu yaani alaf fresh tu sisi yaani tunajikandamiza kinoma yaani

Na mafanikio kwetu yanakuwa magumu kutokana na ujinga tulioamua kuuingiza akilini mwetu
 
Nakazia; WAAFRICA TUNAJILAANI WENYEWE

kuna vitu vingi sana havina uhalisia ila tunalazimisha tu et ukifanya hivi yatakukuta hayaa na yanatukuta kweli kutokana na kupelekea kuamini hivyoo ila ukweli ni kwamba sio hivyo tunavyoamini

Unaona hapo ulaya/ng’ambo kuna vitoto vijana vina miaka 17-19 vinacheza mpira ligi tofauti tofauti vina mafanikio kinyama na havijaoa wala nini? Vina wachumba tu yaani alaf fresh tu sisi yaani tunajikandamiza kinoma yaani

Na mafanikio kwetu yanakuwa magumu kutokana na ujinga tulioamua kuuingiza akilini mwetu
Yah...utumwa wa kifikra...mind slavery
 
Kuwa na hela nyingi sio baraka mkuu,unajua anayoyapitia pamoja na kuwa na hizo hela nyingi?unaweza kukuta halali usiku,utajuaje,unaweza kukuta maelewano ndani ya nyumba na mkewe ni sifuri kila mtu analala chumba chake,hawali pamoja,huyu akija sitting room mwingine anaondoka utajuaje,watoto wanaugua kila kukicha utajuaje,watoto wanakuwa walevi wafujaji wa pesa hawataki kusoma,wanageukia ushoga au usagaji utajuaje?wewe unabaki tu huku nje unaangalia kiwango cha pesa alichonacho ambacho hakimletei muhusika amani bali huzuni na mikosi...
Braza japo sikupingi ila naona hapa umeongea ASSUMPTIONS....pia haya mambo yanawakuta hata wasiokua wanafanya hizo zinaaa...

Hapa tunazungumzia mafanikio...na ni jambo la kupendeza hata kiroho watu kufanikiwa
 
Mbona mnauliza maswali ambayo keshayajibu!! Apo kwenye thread kasema utapoteza nguvu ya kiroho(means connection yako na mungu wako) labda kama utakua unategemea ushirikina na pia hata kwenye ushirikina pia kuna mashart yake unaweza ambiwa usilale na mwanamke ndani ya mwezi mpaka jambo lako likae sawa au ukambiwa kalale na mwanamke bikra ama mzee and etc... so kama mafanikio yako yanategemea KUPIGA GOTI NA KUMWOMBA MUNGU bas ogopa uzinzi ila kama unategemea ushirikina and etc bas fwata masharti utafanikiwa.

Binafsi naamini ivo pia maana hata hao WAZINZI&MALAYA hua maisha yao yanahusiana sana (Direct) na BAR/LODGE/POMBE/TATTOO and etc hasa vilevi na maranyingi wafanya bishara wanao husiana na hawa watu pia hawa watu wenyewe matatizo yao huyapeleka kwenye maeneo ya ushirikina ili kuwa solved na kuapata wateja zaidi na huko pia ni ulimwemgu mwingine na unamashart yake ya kuishi uko kwaiyo ukiwa mtu wa IBADA alafu ukajimix na hivi vitu pia hao wazinzi na uzinzi obviosly lazima mambo yako yatafail kos umetoka kwenye ulimwengu wako wa asili.

Mfano MALAYA kaenda kwa mganga kupata madawa ya kupata wateja wengi na wanogewe wakiwa kwake nawe ni mtu wa maombi unaamini katika mungu kuvuna zaidi mafanikio yako then ukaenda kwa uyo MAYALA alie zindikwa na mganga so yule MALAYA atakuvisha maagano yake ya uko kwa waganda na kwakua ushasaliti ulimwengu wako wa asili na umevamia ulimwengu wa watu wengine ile security ya kiroho inaweza kukutoka maana umevunja mashart yake pia so itakubidi na wewe uingie kwenye huo ulimwengu mwingine mojakwamoja ili upate mafanikio.

Unaruhusiwa kunisahihisha kama nimekosea.

#TUPEANEELIMU.
Daah!!! Mnajibebesha mizigo mizito sana wakuu kwa vitu ambavyo kwa asilimia kubwa mmeaminishwa tuuu na hamna elimu ya kutosha juu yake...

Binafsi nimekua na imani hiz kwa muda mrefu sana but homestly mantic yake sivyo kama ambayo tunaji surubu nayo...

Anyway kuishi ni vile mtu anaamua na inakua vile vile anavyoniaminisha
 
Mkuu kwenye imani yako je maandiko yameandikwa umfate mfalme suleiman?

#TUELIMISHANE.
Mbona huwa huwa tunahimizwa kumuiga suleman kwenye mambo mengi sana.Na maadam wameandikwa bas ndio tunapaswa kujifunza toka kwao
 
UKWELI MTUPU.

Any Adultery & Fonication destroys someone's spiritual life

Na ni kweli na hakika kuwa inaondoa Baraka zote za kiafya, kiakili na kiuchumi

Ukilala na Mwanamke Malaya, Ukifanya Punyeto na kuangalia Pornography tayari unaingia mahali pabaya sana na umeshakuwa adui wa Mungu muumba wako.
Basi Mungu ana maadui wengi sana kwa usawa huu...
 
Nawezaje dumisha nguvu zangu zakiroho kuwa karibu na MUNGU nakamwe nisifikilie zinaa ama ngono zembe kwa vijana maana unatubu then ukiingie insta ama twitter daa balaa tupu
 
Back
Top Bottom