A
Anonymous
Guest
Hapa Charambe Magengeni kuna baadhi ya Askari Polisi wa Kituo cha Maturubai wanaodaiwa kushirikiana na mgambo kuwakamata vijana wa mtaa wetu na kuwabambikia kesi. Inadaiwa kuwa vijana wasipotoa pesa, hufungwa pingu na kupelekwa Kituo cha Maturubai.
Baada ya kufikishwa kituoni, baadhi ya askari wanawapokea na kuwaweka pembeni, kisha kuwaambia watoe pesa ili waachiwe.
Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua kuchunguza malalamiko haya, kwa kuwa vitendo vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya askari na mgambo hao vinachafua taswira ya kituo hicho, licha ya huduma nzuri zinazotolewa na askari wengine.
Tunahisi kuwa baadhi ya askari wanatumia mgambo hao kuwaburuza vijana wa Mtaa wa Charambe Magengeni.