Majibu ya tume lazima yaangukie hapa;
1. Vijana waliosababisha vurugu walitoka nchi jirani! Ipi? Haijulikani.
2. Vijana waliosababisha vurugu walihongwa fedha na wapinzani! Hizo fedha walihongwa lini, na kupitia njia gani? Haijulikani
3. Maandamano yalisimamiwa na TEC na Chadema! Wapi na kwa namna gani? Haijulikani.
Asiyejua aendako hapotei, kila kukicha afadhali ya jana. Mambo yashachacha hapa na hamna akili ya kuyachachua.
Wanasema huwezi kutatua tatizo kwa fikra zile zile zilizosababisha tatizo.
Hiyo Tume ya Uchunguzi inaongozwa na jaji, ila kwa bahati mbaya majaji wengi wa Tanzania ni kama policcm, hawaaminiki kabisaa. Hii inathibitishwa kupitia matendo ya yule mkuu wa iNEC ambaye ni jaji. Na kuna huyu mwingine sijui Msajili wa vyama vya siasa!!
Hivi haiwezekani kuomba usaidizi kwa majaji wa nchi zingine maana sisi ni kama hatuna??
Hakuna muunganiko mzuri wa vyombo vya ulinzi na usalama katika uwasilishaji wa taarifa na uchakati na haya ndio madhara yake kwa kiongozi wa nchi anakuwa na kauli tofauti tofauti za kupishana. Mungu atusaidie
Uongo hausaidii,
Waonyeshe hiyo miamala ya malipo.
Na wale waliouawa wakiwa manyumbani kwao, kama shehe Sharif Majini, wale vijana waliokuwa wanatazama mpira ndani ya nyumba, mtangazaji wa Cluods, na wengine wengi.. walilipwa pesa na nani kabla ya kuuliwa??
Ni ngumu sana kwa mwanamke kupangilia uwongo asijikanyage, wenye D2 tushajua hakuna tume hapo, ni watu wamepewa maelekezo ya nini cha kwenda kufanya na tumchafue nani
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.